Uchimbaji wa maduka ya chini kwa ajili ya kuongeza sehemu ya maduka unatajwa kuwa chanzo cha kuporomoka kwa jengo kariakoo

Kabla ya kuanza uchimbaji wa maduka chini, aliwasiliana na engeneer mkuu wa awali wa hilo jengo ili kupata ushauri?
 
Exactly, mimi kama kiongozi lazma ningetafuta kumjua mmiliki na straight away angepandishwa kizimbani. Sadly kwa utawala huu he will get away with it ila kwa kile chuma JPM alikuwa anakula mvua za kutosha.

Tamaa za kipuuzie kabisa hizo.
Hii ndio Bongo! Unakuta mmiliki ni mtoto wa mjini na ndio mfadhili wa chama - tycoon. Imeisha hiyo! Akili ya mtanzania anaijua aliyeiumba pekee.
Na hapo halijapita tetemeko la ardhi.
 
Shida sio kuchimba underground unasema? Wewe leo hii toa bati lako kisha mwaga zege juu then pandisha ukuta ili uwe na nyumba ya ghorofa halafu uone kama hilo jengo hamna siku litapasuka nyufa kama si kuwaua kabisa wanao.

Ninachomaanisha, kujenga ghorofa na kuweka basement sio shida bali inahitaji utalaamu sio ujanja ujanja, huwezi kujenga ghorofa la kawaida au lenye basement Kwa kutegemea mafundi wetu wa kitaa wa kuokotaokota ambao hawana zile deep technical skills za kufanya hizo design na kujenga.
 
Unawezakuta hata si bahili bali masharti ya ubosi wake huo ndiyo yanayomuendesha, mali zina siri nyingi sana.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…