Uchimbaji wa maduka ya chini kwa ajili ya kuongeza sehemu ya maduka unatajwa kuwa chanzo cha kuporomoka kwa jengo kariakoo

Uchimbaji wa maduka ya chini kwa ajili ya kuongeza sehemu ya maduka unatajwa kuwa chanzo cha kuporomoka kwa jengo kariakoo

Kabla ya kuanza uchimbaji wa maduka chini, aliwasiliana na engeneer mkuu wa awali wa hilo jengo ili kupata ushauri?
Kwa mujibu wa mashuhuda, ghorofa hilo lilianguka ghafla saa tatu na dakika tano asubuhi wakati mafundi ujenzi walipokuwa kazini wakitoboa kwa ajili ya kuongeza sehemu ya maduka.

"Tulianza kusikia kelele za mtikisiko, kisha kwa ghafla jengo zima likaanguka. Wananchi wameshindwa kujiokoa na zoezi la ujenzi lilianza tangu jana hivyo angetaka urahisi angebomoa tu jengo lote," amesema mmoja wa mashuhuda, Harrison Shayo.

Mfanyabiashara mmoja ambaye hakujitambulisha kwa majina, ameeleza kuwa uchimbaji wa maduka ya chini ndio chanzo cha jengo la ghorofa kuporomoka katika eneo la Kariakoo, mtaa wa Congo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema hadi sasa mtu mmoja amefariki dunia na wengine 28 wameokolewa katika ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa Kariakoo jijini Dar es Salaam.​

Soma pia: Ghorofa limeporomoka Kariakoo asubuhi ya leo Novemba 16

View attachment 3153698
View attachment 3153756


Chanzo: Bongo FM, Mwananchi
 
Exactly, mimi kama kiongozi lazma ningetafuta kumjua mmiliki na straight away angepandishwa kizimbani. Sadly kwa utawala huu he will get away with it ila kwa kile chuma JPM alikuwa anakula mvua za kutosha.

Tamaa za kipuuzie kabisa hizo.
Hii ndio Bongo! Unakuta mmiliki ni mtoto wa mjini na ndio mfadhili wa chama - tycoon. Imeisha hiyo! Akili ya mtanzania anaijua aliyeiumba pekee.
Na hapo halijapita tetemeko la ardhi.
 
Shida sio kuchimba underground unasema? Wewe leo hii toa bati lako kisha mwaga zege juu then pandisha ukuta ili uwe na nyumba ya ghorofa halafu uone kama hilo jengo hamna siku litapasuka nyufa kama si kuwaua kabisa wanao.

Ninachomaanisha, kujenga ghorofa na kuweka basement sio shida bali inahitaji utalaamu sio ujanja ujanja, huwezi kujenga ghorofa la kawaida au lenye basement Kwa kutegemea mafundi wetu wa kitaa wa kuokotaokota ambao hawana zile deep technical skills za kufanya hizo design na kujenga.
 
Maboc wanaojenga magorofa kariako n wabahili sana Kwenye kununua material ,,mm n fundi welding Kuna bocc alinipakaa kazi za kuwekaa Dari Kwenye frem zakee zipo 20 ,kule darini anasema atakuwa anaweka mizigo ...mm km fundi nikamwambia hapa inabidi tutumie square pp nzito ya nchi 2x2 Kwa sbb yakuweza kuhimili uzito wa mizigo ..bocc ananiambia hzo n gharama sana weka square pp nchi 1x1 😔😔...nikamwambiaa c imara Sanaa na haziwezi kuhimili uzito wa mizigo maana frem n kubwa sana ,,akataka hzo hzo za 1x1 ,,,ss km mnavyojua mafundi hatuachagii kazi nikafanyaa kazi vzr tu nikamaliza frem zt na wapangaji wakaingiaaa,aiseee miezi 2 mingii matokeo boc aliyaonaa nilichomshauri mwanzo 😔😔...mwanaee mmoja ameponaa juzi japo c vzr maana alikuwa na frem pale ya vipodozi na akaenda jaza mizigo ya vipodozi kule darini ,cku amekaa zake anasuburi watejaaa darii lote lilimdondokeaa ..
Unawezakuta hata si bahili bali masharti ya ubosi wake huo ndiyo yanayomuendesha, mali zina siri nyingi sana.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
 
Back
Top Bottom