Uchimbaji wa maduka ya chini kwa ajili ya kuongeza sehemu ya maduka unatajwa kuwa chanzo cha kuporomoka kwa jengo kariakoo

Kabla ya kuanza uchimbaji wa maduka chini, aliwasiliana na engeneer mkuu wa awali wa hilo jengo ili kupata ushauri?
Labda aliona kutowasiliana nae ata save pesa.

Kwa watu wenye akili ilikua lazima atafutwe aliye sanifu hilo jengo mwanzoni, then kama ingefaa huyu injinia mpya wa sasa (if at all alitumika injinia) angezipitia design za kwanza na taarifa ya udongo (kama haipo angeshauri udongo upimwe) alafu ndio ashauri kama kwa design ya kwanza na hali halisi ya udongo project ingefaa au la!
 
Mimi kilichonishangaza ni mtu kwenda kuhutubia sehemu watu wapo ndani ya kifusi. Yaani nitabaki nashangaa tu.
Wewe huna cha maana hapo. Watu wanahutubia hata wakati wa vita msitari wa mbele kuwatia wapiganaji moyo. Sasa unachoshangaa sema ni ushamba na uelewa mdogo wako. Hongera Mheshimiwa kwa kufika eneo la tukio na kuongea na wananchi.
 
Hatuna haja ya kuzunguka mbuyu swali nikwamba mamlaka husika hawakuw na taarifa za hiyo michakato!?? Maana sidhani kama ni hilo jengo moja peke yake.
 
Silaumu yeyote,lakin mambo kama haya utakuta mamlaka zenye kuyazuia zinayachukuliaga pow halaf yakashatokea madhara ndo tunahaha huku watu washapoteza maisha au kuoata ulemavu wa kudumu.Kwa mfano mzuri uendeshaji wa vyombo vya moto barabaran ovyo unaogharimu maisha ya watu.Yaan likishatokea tukio utadhani ndo kwanza uzembe tumeuona.Vyombo vyenye mamlaka ya kudhibiti mambo yanaoweza sababisha maafa viaminiwe na kupewa uhuru kulingana taaluma zao, ili taifa lifaidike na elimu/mafunzo ya wataalam wa nchi yetu.
 
Kama ni kweli kilichoelezewa hapo juu ndiyo kilichokuwa kinafanyika na bila kufanya consultation..kwa kweli ni upumbavu mkubwa sana.
 
Exactly, mimi kama kiongozi lazma ningetafuta kumjua mmiliki na straight away angepandishwa kizimbani. Sadly kwa utawala huu he will get away with it ila kwa kile chuma JPM alikuwa anakula mvua za kutosha.

Tamaa za kipuuzie kabisa hizo.
Maisha ya kiumbe kinachoitwa mwanadamu yanathamani kubwa sana bila kujali status yake.. kwa kweli hili linahuzunisha mno! Kama mmiliki aliamua kufanya hivyo amekatili maisha ya nguvu kazi kubwa sana ya taifa hili, inachoma moyoni. HUZUNI SANAA
 
Haya jamani.fundi kaamua kusema UKWELI.apewe ULINZI
nadhani leo mmiliki wa hilo jengo hajalala na mkewe yupo mahabusu
 

Attachments

  • Screenshot_20241117-235352.png
    140 KB · Views: 3
  • Screenshot_20241117-235314.png
    144.9 KB · Views: 3
  • Screenshot_20241117-235252.png
    146.3 KB · Views: 3
  • Screenshot_20241117-235229.png
    421.8 KB · Views: 3
Tatizo watu wengi wanaamini miujiza na Mungu.

Hawajui au hawataki kuheshimu ukweli kwamba majengo yanafanya kazi kwa kanuni za kisayansi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…