Sasa huu udini wa leo wa kuwabagua Wakristu na kuwafanya maadui zenu nyinyi watoto mmeutoa wapi wakati historia inaonesha wazee wetu wote walikuwa wamoja - japo kulikuwa na kundi la wadini waliowachukia Wakristu tayari hata bila kufanyiwa jambo lolote na ndugu zao. Hii hali ya wewe kuwabagua wazee wa Kikristu katika simulizi lako ukatilia mkazo "wazee wako" tu huku ukitaka wengine nao waandike "wazee wao" wewe umetoa wapi? Kwanini usifuate mfano wa wazee wako waliokuwa wamoja?
Kwanini leo usiamue kufanya mihadi na Askofu Mkuu Pengo kufanya mazungumzo na kueleza uliyonayo moyoni? Au kwanini usiombe kwenda kutoa mhadhara wako kwenye Seminari pale Segerea na kujadiliana na Wasomi wengine?
MM,
Ni baada na Nyerere na Kanisa kuanza vita ya chinichini dhidi ya Uislam
ndipo mambo yakaanza kuvurugika.
Kanisa likapata hofu baada ya uhuru kwa kuona mipango ya maendele
ya Waislam chini ya EAMWS na uongozi wa Sheikh Hassan bin Amir.
Waislam wakaanza kujenga shule na wakaja na mradi wa
Chuo Kikuu chini ya EAMWS hapo ikawa sasa Kanisa linashinikiza
EAMWS ivunjwe kwa usalama wa Ukristo.
Nguvu ya Waislam katika vita dhidi ya ukoloni walikuwa wameishuhudia.
Walijua kwa umoja ule Uislam utaimarika Tanganyika.
Hapo ndipo Nyerere na Kanisa wakaanza kuvunja misingi iliyokuwa
ikiwapa nguvu Waislam.
Akaanza vita na masheikh, Baraza la Wazee wa TANU, EAMWS kisha
akaunda BAKWATA...
Haya nishayaeleza sana hapa jamvini.
Unasema nizungumze na Pengo.
Nizungumze na Pengo mimi kama nani.
Pengo mtu wa hadhi yake ni Mufti wa Bakwata si mimi.
Mimi Muislam wa kawaida tu hata msikitini siswal ''safal awal.''
Protokali gani itatumika mimi nizungumze na Pengo na nizungumze
na Pengo kitu gani?
Hata hivyo ahsante kwa kuninyanyua kiasi hicho.