Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Ndiyo hapa najaribu kuufahamisha umma kuwa lipo tatizo
la dhulma katika jamii.

Jamii ikisha kubali ni rahisi kuishughulikia hiyo dhulma na
kuitokomeza.
 
Pasco,
Kuwa na subra kuna mwanabodi mmoja kasema ataweka tape tusikie sauti baada ya hapo ndiyo uandike hayo ya kuumbuliwa.

hayausiani ni hoja mbili tofauti
 
Last edited by a moderator:
Insha Allah nitakapomaliza na misikiti nitahadhir wazi
kiujivya jamii hatari inayotunyemelea kutokana na dhulma.
 

WildCard,

Usitumie fikra zako kuwasemea watu. Huu uzi mpaka saizi umesomwa na watu zaidi ya 20,000 hawa wote unawajua wanaofuatilia huu munakasha au umeamua kujifariji.
 
Last edited by a moderator:
Nyerere hakuwa amefanya lolote baya kwa Waislam wakati ule.

Ukweli ni kuwa mambo yakenda vizuri kabisa. TANU ikipata nguvu
kadri siku zilivyokwenda.

Lakini palikuwa na wasiwasi.

Ukoloni haukuwapiga sana Wakristo kama ulivyowapiga Waislam.

Wamishionari walikuwa wameshika elimu ambayo wakiitoa kwa
ubaguzi wakiwapendelea Wakristo.

Ikawa sasa wanauliza busara ya Abdu Sykes na wenzake kumweka
Mkatoliki kuongoza vita dhidi ya Waingereza.

Tatizo lilikuwa hili tu.

Lakini juu ya udhaifu wa Nyerere wa dini yake kuwa alizungukwa na
Waislam alikuwa anaungwa mkono na Mufti wa Tanganyika Sheikh
Hassan bin Amir.

Kisha marafiki zake vijana Abdu, Ally na Dossa walikuwa pamoja na
yeye bega kwa bega.

Kisha Baraza la Wazee wa TANU chini ya uenyekiti wa Sheikh Suleiman
Takadir lilikuwa nyuma yake.

Halafu hawa wote wenye kumuunga mkono ndiyo walikuwa wafadhili
wakubwa wa chama.

Katika hali kama hii Nyerere akawa na nguvu sana katika TANU.

Sasa achilia mbali "support" kutoka zawiyya za Sheikh Hassan bin Amir
huko mikoani na murid kote Tanganyika.

Achilia "support" ya akina Sheikh Mohamed Ramia, Sheikh Mohamed
Yusuf Badi kutoko Lindi, Sheikh Nurdin Hussein wa Lindi pia na wengine
wengi.

Hawa wapinzani wa Nyerere hawakufua dafu.

Mambo yalikwenda kiasi ilikuwa marufuku kwa Waislam kutoleana salaam
ya Kiislam maana "propagandists" akina Rashid Sisso na Abbas Bakis na
Bantu Group wakidai itawabagua Wakristo.

Haya yote wameyafanya Waislam wenyewe kwa mikono yao wenyewe.
Hii ndiyo historia ya wazee wangu na TANU.
 
Kwa hakika silalamiki.
Ila nachangia kile ninachojua kitaleta tija katika jamii.
 

Sasa huu udini wa leo wa kuwabagua Wakristu na kuwafanya maadui zenu nyinyi watoto mmeutoa wapi wakati historia inaonesha wazee wetu wote walikuwa wamoja - japo kulikuwa na kundi la wadini waliowachukia Wakristu tayari hata bila kufanyiwa jambo lolote na ndugu zao. Hii hali ya wewe kuwabagua wazee wa Kikristu katika simulizi lako ukatilia mkazo "wazee wako" tu huku ukitaka wengine nao waandike "wazee wao" wewe umetoa wapi? Kwanini usifuate mfano wa wazee wako waliokuwa wamoja?

Kwanini leo usiamue kufanya mihadi na Askofu Mkuu Pengo kufanya mazungumzo na kueleza uliyonayo moyoni? Au kwanini usiombe kwenda kutoa mhadhara wako kwenye Seminari pale Segerea na kujadiliana na Wasomi wengine?
 
Hayo yote ni ile "case" ya your word against mine kwa hiyo
hakuna tija sisi kulumbana nani kasema nini nani kasema
ilikuwa hivi.

Majina ya radicals nishaweka hapa zaidi ya mara mbili.
Alikuwa Sheikh Takadir, Mashado, Saleh Muhsin, Abdallah
Mohamed.

Hawa ni baadhi tu.
 
WildCard,

Usitumie fikra zako kuwasemea watu. Huu uzi mpaka saizi umesomwa na watu zaidi ya 20,000 hawa wote unawajua wanaofuatilia huu munakasha au umeamua kujifariji.
Naongelea watu kama wale waliochoma makanisa kule Mbagala na Zanzibar. Wengine hata kusoma na kuandika hawajui. Unaijua pia misikiti yetu ilivyo. Kama ipo misikiti yenye computer na internet na waumini wake wanapata access sijui itakuwa mingapi! Hao 20,000 wengi wao ni akina wewe na mimi.
 
Mambo yalivurugika Kanisa likapata hofu baada ya uhuru.

Waislam wakaanza kujenga shule na wakaja na mradi wa
Chuo Kikuu chini ya EAMWS hapo ikawa sasa Kanisa linashinikiza
EAMWS ivunjwe kwa usalama wa Ukristo.

Nguvu ya Waislam katika vita dhidi ya ukoloni walikuwa wameishuhudia.
Walijua kwa umoja ule Uislam utaimarika Tanganyika.

Hapo ndipo Nyerere na Kanisa wakaanza kuvunja misingi iliyokuwa
ikiwapa nguvu Waislam.

Akaanza vita na masheikh, Baraza la Wazee wa TANU, EAMWS kisha
akaunda BAKWATA...

Haya nishayaeleza sana hapa jamvini.
 

Mkuu hapa Mohamed hana nafasi yakupata uzima wa milele, sisi tudajitahidi kwa kazi moja tu ya kuwarudisha kundini wale waliopotoshwa na Mzee Mohamed Said kwa ngano zake!
 
(mihadhara yeye anafanya wazi wazi,na ulimwengu mzima,sembuse hapo segerea?
Keshasema yuko tayari kama mnampa mwaliko wa kuja kutoa darsa pindi pale mtapomuhitaji.
 
mkuu hapa mohamed hana nafasi yakupata uzima wa milele, sisi tudajitahidi kwa kazi moja tu ya kuwarudisha kundini wale waliopotoshwa na mzee mohamed said kwa ngano zake!

huwezi,na umechelewa sana,miaka 15 yote hiyo?

Unaweza kwenda kupiga marufuku huko ughaibuni maandiko hayo yasisomwe?thubutu..!
Huwez,ukiambiwa tupe makala zako wewe zinazoainisha ukweli unaopingana na wake utazitoa zipi??zile za kivukoni?
Shukuru tuh nafasi hii unayoipta hapa jf kuzungumza nae,na kujadiliana nae,lakini kivyovyote vile huwez kumfikia japo chembe kwa maarifa na uelewa,na ushukuru ya kwamba unanufaika kwa mengi kwa anayokueleza,msijitoe ufaham hapa.
 
Hiyo BAKWATA waliundiwa akina nani? Waislam vibaraka ambao walikuwa hawaioni dhulma ya kanisa na Mwalimu? Kwa nini BAKWATA bado ipo miaka kadhaa baada ya Mwalimu kuondoka madarakani na duniani. Jana ulihudhuria ile Maulid iliyoongozwa na Makamu wa Rais?
 

MM,

Ni baada na Nyerere na Kanisa kuanza vita ya chinichini dhidi ya Uislam
ndipo mambo yakaanza kuvurugika.

Kanisa likapata hofu baada ya uhuru kwa kuona mipango ya maendele
ya Waislam chini ya EAMWS na uongozi wa Sheikh Hassan bin Amir.

Waislam wakaanza kujenga shule na wakaja na mradi wa
Chuo Kikuu chini ya EAMWS hapo ikawa sasa Kanisa linashinikiza
EAMWS ivunjwe kwa usalama wa Ukristo.

Nguvu ya Waislam katika vita dhidi ya ukoloni walikuwa wameishuhudia.
Walijua kwa umoja ule Uislam utaimarika Tanganyika.

Hapo ndipo Nyerere na Kanisa wakaanza kuvunja misingi iliyokuwa
ikiwapa nguvu Waislam.

Akaanza vita na masheikh, Baraza la Wazee wa TANU, EAMWS kisha
akaunda BAKWATA...

Haya nishayaeleza sana hapa jamvini.

Unasema nizungumze na Pengo.
Nizungumze na Pengo mimi kama nani.

Pengo mtu wa hadhi yake ni Mufti wa Bakwata si mimi.
Mimi Muislam wa kawaida tu hata msikitini siswal ''safal awal.''

Protokali gani itatumika mimi nizungumze na Pengo na nizungumze
na Pengo kitu gani?

Hata hivyo ahsante kwa kuninyanyua kiasi hicho.
 

Unataka kuniambia Wakiristo ndiyo wameelimaka sana Tanzania. Sijui unaongelea Wakiristo wa wapi.

Unaweza kutupa idadi ya makanisa ambayo yana access ya internet kwa waumini wake.
 
Unataka kuniambia Wakiristo ndiyo wameelimaka sana Tanzania. Sijui unaongelea Wakiristo wa wapi.

Unaweza kutupa idadi ya makanisa ambayo yana access ya internet kwa waumini wake.
Sasa hapa unataka kupingana na mzee wetu Mohamed. Takwimu hizo nizitoe wapi wakati hata kanisani sijakanyaga miaka mingi tu. Sisumbuliwi na makanisa. Mimi na Mungu wangu asiye na DINI na Tanzania yangu tu.
 

Ndugu yangu, unaanza kukwepa kivuli chako mwenyewe?

Hebu rudia kusoma majibu yako yte kwenye thread kuu uone ulivyomdhalilisha Mwalimu Nyerere!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…