Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Asante sana mkuu, wazo zuri na maswali hayo ni mazuri sana.
 
Last edited by a moderator:

Yericko,

Unaweza kuwa ni kweli siijjui historia ya machifu na ningependa kujifunza.
Inawezekana kweli pia nikahitaji msaada wa haraka.

Ila sifahamu kwa nini huo msaada uwe wa haraka.

Yericko unapoandika jitulize usimtazame yule unaekabiliananae.
Watazame wasikilizaji wale ndiyo muhimu.

Hawa ndiyo wapiga kura wako.

Huyu ''opponent'' ni mmoja hakushindi.
Jaribu kupata masikio ya wale wasikizaji wanaokusikilizeni.

Hawa ni wengi na ndiyo muhimu.

Jifunze kuandika kwa adabu.
 

Umepewa vitu vidogo tu vya Mkwawa unaanza matusi? Jee, ukianza kushushiwa nondo zenyewe utakuwaje?

Leo utatafuta pakutokea, hung'oki. Umemeza vyote; chambo, ndoano, chubwi na mshipi, pana pakuchomokea hapo?
 
Mag3,

Maswali yako ni ya msingi umeyaandika kiungwana yanaitaji majibu, mie binafsi na swali kwako kabla ya Nyerere kuitawala Tanzania. Tanganyika watu walikuwa hawaishi kwa upendo na amani.
 
Last edited by a moderator:
Hehee moja ya makosa unayoyafanya nikuamini na kutaka kila unaejadiliana hapa jf na wingine basi umtawale, jambo hilo hujajua uwa linakuondolea haiba sekunde hadi sekunde.

Kulazimisha adabu ilihali ipo nihukizo mbele za Mungu, hebu itangulizeweye kisha dai.

Juu ya kujifunza kuandika, nijambo linalo nifurahisha sana,ninaamini hata upewe na muumba miaka mingine 60 hutakuja kunifukia kwa uwezo wakuandika kwa nidhamu ya kimalenga
 

Jasusi hakika ni wengi wamesahauliwa na wamekwenda kaburini na kinyongo.
Mmojawapo ni Suleiman Masudi Mnonji.

Huyu Masudi Mnonji ndiye aliyemtia Lawi Sijaona katika siasa.
Nimefahamiana na mtoto wa Sijaona, Sijali kwa miaka mingi.

Kila ninapokutana humkumbusha, ''Sijali vipi mbona huandiki
maisha ya mzee tukamsoma?''

Jibu la Sijali ni lile lile siku zote, ''Nitaandika.''

Hebu kwa uchache kutana na Masudi Mnonji:

[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD] Southern Province, 1955[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
The TAA in Lindi was under the leadership of Suleiman Masudi Mnonji and Mohamed Waziri, President and Secretary and respectively. Mnonji was a tailor and Waziri was a draughtsman.

The TAA was formed belatedly in Lindi in 1953 at the time when the TAA leadership in Dar es Salaam was not only transforming the association into an open political party but was making arrangements to send a delegate to the United Nations to plead the cause of independence.

Masudi Mnonji had a fair amount of experience in politics. After World War Two, with his friend and fellow tradesman, Bakari Msham, he had tried to organise trade unions in different sisal estates in the Southern Province.

His efforts did not end there; he also organised cooks and washermen in Lindi to form their own organisation to fight for their rights. It was through his personal initiative that TAA came to be formed in Lindi and he offered his house at Makonde Street as its office.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Realising the importance of having educated leadership, Mnonji contacted Lawi Nangwanda Sijaona who was at that time living in Newala to come to Lindi and advise TAA on how to organize effectively.

Mnonji was a well-to-do African. He was the main supplier of government uniforms in the south.

Through this business he was able to own three houses in Lindi and when TAA was transformed to TANU he donated one of his houses as the first TANU office in Lindi, and probably the first in Southern Province.

Mnonji’s influence did not end there; one of his two wives, Bibi Zaituni Fadhili, was also involved in politics during the struggle.

Bibi Zaituni Fadhili and another woman, Bibi Shariffa bint Mzee, were among early women activists in Lindi.

Bibi Zaituni Fadhili died in 1995 as a serving member of parliament.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Masudu Mnonji baada ya uhuru kupatikana aliwekwa Kizuizini pamoja na Waislam wengine.
Ipo barua Mnonji alimwandikia Nyerere akiwa jela. Sijaona alikwenda jela kumtembelea Mnonji na Mzee Mnonji alimwomba Sijaona amwandikie barua kwa Nyerere.

Baadhi ya maneno katika barua hiyo Mnonji alimwambia Nyerere maneno haya:

''Ikiwa Muheshimiwa una ushahidi kuwa mimi nilikuwa napanga njama za kupindua serikali yako basi nakuomba nipeleke mahakamani nikajibu mashtaka. Lakini ikiwa hakuna ushahidi huo, nakuomba Muheshimiwa uniachie nirudi nyumbani kwangu.

Mwisho Muheshimiwa nakuomba utazame nyuma uangalie wewe na mimi tumetoka wapi.''
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Umepewa vitu vidogo tu vya Mkwawa unaanza matusi? Jee, ukianza kushushiwa nondo zenyewe utakuwaje?

Leo utatafuta pakutokea, hung'oki. Umemeza vyote; chambo, ndoano, chubwi na mshipi, pana pakuchomokea hapo?

kacheze chandimu hapa si mahala pako
 

mzee said naomba kumfahamu mzee LAWI NANGWANDA SIJAONA wa Mtwara na ushirki wake kwenye historia naamini nae ni mmoja kati ya wale wazee wakiislamu walioachwa na historia ya sasa juu ya uhuru wa Tanganyika.

Lakini kwenye maandishi yako sijapata kumuona!?

N.B
ninayo picha yake ila nashindwa kuiweka natumia simu yenye uwezo mdogo; labda nimuombe Mzee Mwanakijiji aiweke kwani nimeikuta kwenye ukuta wake wafacebook moja ya rafiki zake akiwa ame'tag
 
Last edited by a moderator:
Katika biography ya Muhammad Ali "The Greatest" kuna kisa anahadithia
fujo alizofanya Drew Bundini kwenye kupima uzito pambano na Sony Liston
Miami Beach Florida 1964.

Kweli Ali anasema nilimtuma Bundini tufanye "fujo" ya kupata "publicity"
magazeti na TV zitutoe.

Ali anasema Bundini kafanya vurugu iliyofurtu ada.
Akajuta.

"Kweli tuliandikwa sana lakini tulipigwa faini na boxing board."

Alipomuuliza Bundini akajibu, "Si ulisema tufanye fujo."

Ali anamaliza mkasa huu kwa kusema kuwa toka siku ile alimuogopa Bundini.
Sababu ni kuwa Bundini alikuwa mwehu.

Ali anasema mtu mzima yoyote lazima amuogope mwendawazimu.
 

Mkuu Moh, nilipo ona anazungumzia historia ya Mkwawa kwa kirefu bila ya kuzungumzia jina lake la ubatizo na alikuwa madhebu gani - ndio nikamwanzia mbali kwamba "nasikia Mkwawa alikuwa anajuwa kuandika na kusoma kiarabu" - amejibu ndio! Hii ina maana alikuwa anaelewa kila kitu, sasa kwa nini akulisema hilo, au ndio yanarudi yale yale ya kupidisha historia kwa kuondoa mambo muhimu ambayo yanaonekana yatawapa umaarufu watu/kudi fulani!!


Hata ili la kuanzisha historia ya Mkwawa kabla atujamaliza tuliyo anza nayo kwanza inashangaza kidogo, kuna jamaa walitaka alete vitu fulani fulani humu lakini naona hilo hakulitekeleza!


Wengi wetu humu tuna kiu ya kutaka kujua kiundani historia ya kweli kuhusu mababa/mababu zetu wanzilishi wa harakati za kupingana na ukoloni wa Kingereza, kuanzia kwenye miaka ya 1920s mpaka late 1950s, watajwe kwa majina yao, mchango wao na madhehebu yao - kama kuna baadhi ya wanaharakati walio shindwa kuelewana na Nyerere kwa sababu mbali mbali baada ya kukaribishwa kwenye kikundi chao, basi zielezwe sababu na ni nani alihusika kuwafuta kwenye historia ya nchi yetu na zitolewe sababu za msingi za kufanya mambo ya kiimla yanayo litia dosari historia ya Taifa letu, niliona juzi juzi hapa ndio JK alitumia uwanadamu kwa kuwakumbuka baadhi ya wanaharakati hawa kwa kuwatunuku nishani walio hai na wengine ambao wamekwisha tangulia mbele ya haki, sina shaka raia wema wataedelea kumpatia JK majina ya wale wote walio sahulika kuhusu harakati hizo.

Mimi nilikuwa nashauri historia kuhusu Mkwawa, Abushiri, Mangi Meli, Milambo, Rumanyika, Songea nk hayo tuachane nayo kwanza.
 

Kama ni wewe uliyeiandika mbona iko katika first person narrative? Au wewe ndie ulianzisha kampuni ya Sykes Sales Promotion? Au wewe ndie uliyeajiriwa na Colmore katika kampuni yake ya real estate? Au haujaisoma ile appendix?

Mwaikakagile kwa kuiweka kwenye appendix na sio kwenye main body ya text kunaashiria wazi kuwa yeye sie author bali ni documents ambazo ameambatanisha kuongezea uzito yale aliyoandika mwenyewe.

Na mwisho amesema wazi kuwa ameitoa kwenye gazeti la The East African la 16 Februari 2004. Kwa hali hiyo hata kama ni wewe ndie uliyeiandika (kitu ninachotia wasiwasi) basi mtu yeyote ambae angetaka kujua nani mwandishi wa hiyo obituary, angekukuta.

Ndio maana nasema una pretensions of grandeur na sense of victimhood. Kila wakati unahisi umeonewa hata pale ambapo sio.

Mimi natumia neno mmisheni kama vile wewe unavyotumia uislamu. Kugawa, kuonyesha tofauti.Kuonyesha kuwa kwa mtazamo wako mkristu bado ni yule wa mishen kota, adui na mbaya wa waislamu. Tofauti yangu na wewe, mimi natumia neno hili kuonyesha upuuzi wa hoja hiyo. Mmisheni katika ujumla wake hajawahi kuwa adui wa muislamu na vice versa.

Amandla......
 

Muhammad b.Khalfan al Barwani alikuwa mfanyabiashara mkubwa wa watumwa. Ni kweli alipigana na wajerumani lakini haikuwa katika kutetea uafrika au waafrika bali biashara yake. Mwaka 1890, shujaa huyu alikuwa tayari kuungana na wajerumani ili mradi wamwachie eneo la kutawala kama mdhalimu mwenzake Tippu Tip. Mwaka 1908 aliandika kitabu kinachoitwa " ndoto za Sheykh Ahmad" ambacho kilitafsiriwa na baadhi ya watu kama wito kwa muangano wa waislamu. Huyu, bila shaka, alikuwa muislamu kwanza na sidhani kama alijiona hata siku moja kama mwafrika. Kwa mtazamo wangu, kama alikuwa rafiki wa "Abdalah" Mkwawa basi ilikuwa marriage of convenience ya "adui wa adui yangu ni rafiki yangu". Unless tuambiwe kuwa "Abdalah" Mkwawa alipokuwa akipigana na wajerumani alikuwa anatetea uislamu wake na sio wahehe wake! Rumaliza akama alivyokuwa Tippu Tip hakuwa shujaa wa Afrika. Kwangu mimi, hakuwa na tofauti na wajerumani aliokuwa akipigana nao.

Amandla.....
 
KUna msemo wa kuwa unaweza kuwa "unatwanga maji kwenye kinu" au ni sawa "na kumpigia mbuzi gitaa". Kama watu wametusoma vya kutosha humu kuna mambo yako wazi kabisa kuhusu maandishi ya Bw. Mohammed Said. NIkiamua kujumlisha tu kwa ufupi ni kwamba:

1: Hakutaka kuandika kazi ya historia

Japo mara kwa mara ndugu yetu anapenda kuelezea maandishi yake kuwa ni kazi ya kihistoria ukweli ni kuwa - na tumefanikiwa kuuonesha mara kadhaa sasa - Bw. Said alitaka kuanzika simulizi (narrative) ya wazazi wake biila kujali USHAHIDI kihistoria. Sote katika utoto tumekaa na wazee wetu ambao wametusimulia mambo mengi - yawe ya uhuru au ya maisha ya kijijini - na yametupa mawazo fulani juu yetu sisi wenyewe. Kwa mfano, kuna watu ambao wanamchukia Nyerere kwa kuendesha kampeni ya Ujamaa Vijijini kwa sababu wazazi wao waliwasimulia jinsi hali ilivyokuwa mbaya. Wapo wengine ambao walijikuta wanamchukia Idi Amin kwa sababu wakati wanakua simulizi kubwa pale nyumbani lilikuwa ni chuki dhidi ya Idi Amin.

Sasa masimulizi hayo ya utotoni hata yakitoka kwa baba, babu, wajomba au shangazi hayawi historia kwa sababu wao wamesema. Yanakuwa historia kama yana ushahidi wa kihistoria. Bahati mbaya sana Bw. Said hajajali ushahidi wa kihistoria kwani ushahidi pekee ambao yeye kautumia ni ule wa kuthibitisha hoja yake. Kwa kufanya hivyo Bw. Said amefanya kosa kubwa sana katika uandishi wa historia - kuonesha historical bias. Sasa historical bias ni rahisi sana kuiona kwenye maandishi ya mtu.

Kitabu cha Bw. Said kinampa msomaji kile kinachojulikana kama revisionist history; yaani ameamua kutoka kwenye historia ilivyo na kuielea kwa misingi ya bias yake.

2. Bias kubwa ya Bw. Said naweza kusema inatokana na kile ambacho yeye anaamini ni nguvu yake - yaani wazee wake. Kwa kujaribu kuandika historia kwa kutumia wazee wake kama "the most reliable sources' na kushindwa kuwa huru kimawazo kusoma mawazo yanayopingana na wazee wake amejikuta anaandika historia kwa kutumia bias without any sense of objectivity. Kwa yeye anaamini hilo ni sawa kwa sababu "ni historia ya wazee wangu". Tatizo ni kuwa historia ya wazee wake haiwi historia kwa vile wamemsimulia yeye inakuwa historia kama inaangaliwa objectively. Hili ndio tatizo kubwa.

3. Kutokana na hayo mawili hapo juu maandishi ya Bw. Said yamejaa hisia zaidi kuliko ushahidi wa kihistoria. Hisia ambazo zinatokana na mapenzi ya mtoto kwa wazee wake, uchungu wa mjukuu kwa babu yake, na hisia ya fungamano la dini. Bw. Said ataamini yale yote anayoambbiwa na wazee wake bila kuyahoji kwani kuhoji ni kuwavunjia heshima, kuuliza ni kutokuwaamini. Mwanahistoria mzuri ni yule ambaye anahoji na kuuliza maswali. Bw. Said amekuwa mpokeaji wa majibu lakinibila kuuliza maswali wala kuwa tayari kutambua contradictions katika maelezo ya watu.

4. HIvyo Bw. Said kaandika kile nilichokipa jina la "histohisia" yaani historia inayoandikwa kutoka kwenye hisia. Bw. Said aliaminishwa toka utotoni kuwa wazee wake walionewa; pale mtaani alipokulia alizungukwa na watu ambao walimuaminisha kuwa Waislamu wameonewa na wazee wa Dar hususan wamefutwa katika historia. Aliambiwa adui aliyefanya hivi ni Julius Nyerere aliyekaribishwa na wazee wake na kufanyiwa kila aina ya ukarimu; akaambiwa kuwa alipoingia madarakani Nyerere aliwageuka Waislamu wa Dar na kuwatenga. Simulizi hili lilimgusa ndugu Said kiasi kwamba alijiapia mwenyewe kuwa akipata nafasi ya kuandika simulizi la wazee "wake" atafanya hivyo.

Maandishi yake basi na yeye mwenyewe ameshasema mara nyingi ni kutimiza ndoto ya kusimulia yaliyowakuta wazazi wake kwa kadiri walivyomwambia. Hakufanya juhudi zozote za kutaka kuhakikisha kama aliyoambiwa na wazee wake ni kweli na kama ni kweli basi kwa kiasi gani na je kuna maelezo mengine yanayoweza kuelezea aliyosimuliwa.

5. Kutokana na hilo la nne kwa makusudi kabisa na pasi ya kufikiria sana Bw. Said akaamua kufanya mambo mawili makubwa sana ambayo yanaharibu kabisa simulizi zake.

a. Kutosimulia wazee wengine ambao walishirikiana na wazee wake katika harakati za Uhuru pamoja na Baba wa Taifa. Na wazee hawa WOTE ni Wakristu. Kimsingi, Bw. Said amefanya exactly kile ambacho anamtuhumu Nyerere. Bw. Said anasema Nyerere aliacha historia iandikwe ikimuweka yeye kama 'peke yake' katika harakati za uhuru na kuwaacha wazee wa Kiislamu (hasemi wazee wengine); na yeye kwa makusudi ameamua kuandika historia ya wazee wa Kiislamu na kuwaacha wazee wengine! Lakini la kwake analihalalisha kuwa ni sawa kuandika 'historia' kwa kuangalia upande mmoja lakini ni makosa kwa waandishi wa historia ya Nyerere kuandika kwa upande mmoja!

b. Kutoka kwenye simulizi la historia aliyosimuliwa Bw. Said akaenda mbali zaidi na kuanza kuelezea kwa misingi ya kuonesha kuwa Wakristu nchini wananufaika na wamenufaika sana na uhuru kuliko Waislamu na hii imetokana na ukwlei kuwa Wakristu wamependelewa na Waislamu wametengwa. Simulizi lake basi limetoka kuwa la kihistoria na kuwa la kiharakati - sasa hili halina tatizo kabisa kama akisema awali kuwa ni suala la harakati.

6. Bw. Said amefanikiwa kupata wasikilizaji wengi na watu wengi wakimuamini kwa sababu wengi wa hawa hawana namna ya kujua mbinu anazotumia kujenga hoja. Ikumbukwe kuwa Bw. Said hajatumia mbinu za uandishi wa kihistoria ambao unaongozwa na historical method. Yeye kaandika kama alivyosmuliwa na alikusanya nyaraka na kuzipa tafsiri ya yeye anachoamini. Ukimsoma sana utaona ni jinsi gani anaandika kama ana uwezo wa kujua nia, hisia, na mawazo ya wahusika.

7. Kitabu chake maarufu kinachomzungumzia Abdul Sykes kwa kweli ni sehemu ndogo sana inahusiana na maisha ya Abdulwahid Sykes. NI kitabu ambacho kinaelezea kwa kirefu uwezo, ushawishi na uongozi wa Mwalimu Nyerere kati ya wazee wake Jijini Dar - Wakristu, Waislamu, Wahindi na Wapagani! Binafsi nilipokisoma kitabu hicho kwa kuangalia 'facts' peke yake nilikipenda mno kwani kinamuonesha Nyerere kwa mwanga mzuri sana. Ni pale tu Bw. Said anapoweka hisia zake ndipo unapoona utamu wa kitabu kufutika kwa sababu kwa kiasi kikubwa hisia zake hazina ushahidi wowote wa kuzithibitisha. Kwa mfano anaposema "ilisemwa" au "iliaminika" au "alidhaniwa" ni wazi kuwa hana namna yoyote ya kujua hisia hizo isipokuwa kwa kukisia - ndio maana naiita 'histohisia'.

Binafsi nashauri watu wote wanaopenda kujifunza tofauti ya historia na histohisia wakitafute kitabu hiki kwani kitawafundisha namna YA KUTOANDIKA HISTORIA.

MMM
 

Hii yote baada ya kusikia kuwa kumbe Mkwawa nae ni Abdallah.

pole kijana, fata nasaha za waliokutangulia, usiwe na kibri utafaidika, nakuasa pitia nyuzi yangu hii, ambayo labda wewe utaielewa, wengi walijidai hawaelewi: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/345499-watanzania-na-ubaguzi-wa-ujinga.html
 
Mag3,

Maswali yako ni ya msingi umeyaandika kiungwana yanaitaji majibu, mie binafsi na swali kwako kabla ya Nyerere kuitawala Tanzania. Tanganyika watu walikuwa hawaishi kwa upendo na amani.

Nyerere mwenyewe alikaribishwa kiuungwana na watu wa dar vijana kwa wazee, hilo anakiri nyerere mwenyewe, na hapo alikuwa hata ndoto ya kuwa atakuwa mtawala hana.

"Ninasema yote haya kwa shukrani kwa wazee. Jamaa hawa walikuwa watu wazima wa Dar es Salaam, na mimi kijana mdogo Mzanaki, na Kiswahili changu si kizuri sana – cha matatizo.

Nimekuja, natoka Ulaya, tena masomoni. Muda mfupi tu jamaa hawa wakaniamini haraka sana"

Hapo ninamnukuu bandiko la Yericko la post namba moja.

 

Na huyo huyo "Muhammad b.Khalfan al Barwani alikuwa mfanyabiashara mkubwa wa watumwa" ndiye rafiki yake mkubwa mtawala chifu Abdallah Mkwawa, walikuwa na nini in common?
 

MM,

Nime nimekusoma.
Lazima sisi kama binadamu tutakhitilafiana.

Wewe unakhitilafiana na mimi kama mimi nilivyokhitilafiana na kitabu
cha ''Historia ya TANU 1954 -1977'' kilichoandikwa na Chuo Cha Kivukoni.

Kitabu hiki hakikuwataja wazee wangu waliopigania uhuru wa Tanganyika.
Kitabu hakikumtaja Abdulwahid Sykes kilitosheka na Nyerere peke yake.

Sikufurahi.

Nikanyanyua kalamu nikawarejesha katika historia kupitia kitabu changu wale
wote waliosahauliwa.

Na wewe hujaridhika na kitabu changu kwa kuwaandika wazee wangu una
haki ya kuandika kitabu chako.

Hivi ndivyo usomi unavyokwenda.
Kila siku ni kutafuta kile ambacho hakikuwa kinafahamika na kukiweka hadharani.

From the known to the unknown.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…