Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Zomba,

Chunguza kitu kimoja.

Kuna post naziweka hapa zina habari ambazo ningetegemea
ningeulizwa habari zaidi lakini naona kimya hawazigusi kitu
kama vile wanaziogopa.

Kwengine nikieleza habari hizo huwa kunakuja maswali mengi
ya kutaka kujua zaidi.

Humu ninachokiona ni maswali ya mtego kutaka kuumbua.

Nimegusia jinsi Lawi Sijaona alivyoitwa Lindi kutoka Newala
na Suleiman Masudi Mnonji.

Hii ilikuwa 1953.
Kisha nikaeleza jinsi Mnonji alivyounda TANU na wenzake.

Mwisho nikaeleza Nyerere alivyomfunga Mnonji baada ya
uhuru.

Mwisho nikaeleza barua ya masikitiko Mnonji aliyomwandikia
Nyerere kumwambia kuwa ikiwa yeye Nyerere ana ushahidi
wa yeye Mnonji kutaka kupindua serikali yake ampeleke
mahakamani akajibu mashtaka la hana basi amwache huru
arejee nyumbani kwake.

Mwisho wa barua Mnonji akamkumbusha Nyerere khisani
iliyokuwapo hapo nyuma kati yake na yeye.

Barua hii ilikuwa ''dictation'' Mnonji akimwambia Sijaona
jela na Sijaona akiandika.

Ile ilikuwa barua ya mkono ambayo Mnonji alimuomba
Sijaona ampe Nyerere.

Sijapata swali lolote katika mikasa kama hii na mfano wa
huu.
 

Asante sana Kaka Nguruvi3, na ndio maana mimi sikupenda sana mada kama ya Mkwawa na wengine ziingie humu kwani bado kuna viporo vingi havijajibiwa kwenye histohisia ya Mzee Mohamed ya 1950's

Nadhani Kaka Mohamedi hakulitendea haki kundi kubwa "lililosahahuliwa" kama kweli alikuwa na nia ya kulitetea kundi hilo kwa mujibu wa mabandiko yake,
Pilika za kugombea uhuru kwa upande wa Mzizima hazikuwa za Waislamu wala za Wazulu na Wamamnyema pekeyao, Waislamu, Wakristo, Wapagani na Waabudu Mizimu walishiriki kama Watanganyika bila kuangalia itikadi ya Imani zao wala makabila yao, tofauti na Mzee Mohamed anavyotaka kutuweka kwenye itikadi ya Kiimani na Kikabila

Baada ya Nyerere kusomewa Dua na Waislam pale kwa Tambaza, Kundi lingine lisilokuwa la Kiislamu lilimuita Nyerere na Kumfanyia Tambiko ambalo halikuwa la Kiislam(Hotuba ya Nyerere ya Kuaga 1985), Tambiko lilifanywa mbele ya hao Waislam (Tambaza at el) na wala (Waislam) hawakupinga kufanyika tambiko lililo kinyume na Uislam, kwa wale Waislam waliona kila iman inaplay part yake kwenye pilikpilka za kutafuta uhuru,

kwa Mohamedi kitendo cha kusomewa Dua ya Kiislamu ndio kinapewa kipaumbele lakini hilo la tambiko halimuhusu kwa sababu waliofanya hilo tambiko si wazee wake, yeye wazee wake ni wale Waislam wa Kizulu na Kimanyema. na hapo ndio unaweza kuona Mzee Mohamed ana Nia na Malengo gani kwenye hii Histohisia aliyoiandika na anayosimamia
 
Yericko,Mkwawa alikuwa Muislam.Waislam hatubatizwi tunazaliwa tayari ni Waislam.
Thanks 4 the info. mimi nilifikili Waislaam wanabatizwa kama sisi Wakristo, nilipo soma maelezo ya Mr.Zomba ndio nilielewa kiundani tofauti za ki-imani kati ya dini zetu mbili specifically mambo ya UBATIZO..
 
Yericko,

Mkwawa alikuwa Muislam.
Waislam hatubatizwi tunazaliwa tayari ni Waislam.
Hebu oneni hichi kituko!...jamani ni kweli Mungu yupo, ila hizi dini tumeletewa na wajanja wachache tu.

Wazungu walituletea ukristo

Waarabu walituletea uislaam....kabla ya waAfrica tulikuwa hatuna dini isipokuwa matambiko ya kimizimu tu.

Kweli wafia dini kazi mnayo.
 
Inaaminika na Mwalimu Nyerere amelithibitisha katika hotuba yake kuwa nyakati zingine walikwenda kutambika,

Swali la kujiuliza kwa wadau wote ni, Je walitambika Kikristu, Kiislamu ama kipagani/kijadi?

Tukipata jibu sasa tujenge hoja kwa dhana ya hoja ya udini ya Mohamed Said na waambata wao!
 

Yericko,

Mbona wewe kutwa ni vitisho tu?
Mnakasha hausafiri kwa vitisho.

Mnakasha unastawishwa kwa hoja.

Fika Makumbusho ya Mkwawa Kalenga kuna barua Mkwawa kawaandikia
Wajerumani mwaka 1896.

Barua hii Mkwawa kaanza kwa kusema, ''Bismillah Rahman Rahim.''
Huu ni ufunguo wa Muislam.

Mpagani haanzi mambo yake kwa maneno hayo.

Hayo mengine wala sina haja ya kujibu.
 

Tatizo siyo kukuweza tatizo kila unapotia mguu watu wameishapita huko ulichokiandika hapa kimedhirisha ulivyokuwa mtupu kwenye historia.
 

Nadhani tumejichokea.
Tunahitaji mapumziko.

Mnasemaje wana ukumbi?

Mnaona tija yoyote katika
mnakasha wa namni hii?

Hapa inatakiwa subra ya
Nabii Ayub.
 

Sasa naamini wazi kuwa historia huijui ndugu yangu, umebobea kidini zaidi!

Nakupa swali kisha jibu lake ndio ufunguo wako!

Mjerumani na Muarabu nani alitangulia kufika Tanganyika?
 

Yericko,
Bado una hamu.

Wewe kweli bado una uso wa kuzungumzia hotuba?
 
Nadhani tumejichokea.
Tunahitaji mapumziko.

Mnasemaje wana ukumbi?

Mnaona tija yoyote katika
mnakasha wa namni hii?

Hapa inatakiwa subra ya
Nabii Ayub.

Tatizo lako lilelile la asili la kukwepa hoja muhimu na kushangiilia kusifiwa na wasiojua historia
 

Kituko,

Alichofanya Mohamed Said ni kuandika.

"Historia iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza katika Tanganyika."

Pitia vizuri hiyo hotuba ya Nyerere anakuambia mwenyewe baada ya kumsomea dua wanamfanyia matambiko hao hao Wazee wa Dar es Salaam.

Matambiko ni mila za makabila wala siyo kitu kigeni.
 
Last edited by a moderator:

Wewe kinakushinda nini kuandika hayo ya waze wako wa kipagani aliyoyawacha Mohamed Said? mbona hukuuliza kwanini kitabu cha kivukoni kiliwaacha wote? mwenzako aliona wazee wake wapigania Uhuru hawakutajwa na kitabu cha kivukoni akaanza kuandika chake, wewe jee? hebu tueleze mzee wako yupi wakipagani alimweka nyerere nyumbani kwake? mzee wako yupi wa kipagani alimpelekea resheni nyerere nyumbani kwake? mzee wako yupi wa kipagani alikuwa akimpa lifti nyerere kumpeleka pugu? mzee wako yupi wa kipagani alikwenda kuchukuwa michango tanga ya kuchangia safari ya nyerere? mzee wako yupi wa kipagani alikuwa kwenye AA, TAA, TANU ambae kivukoni walimtaja na Mohamed Said hakumtaja?

Au hilo kundi la wazee wako walikuwa wakitambika tu?
 
Kuwarudisha maanayake ni kuuwaunganisha na waliopo si kuwatenga tena!

Alichokifanya Mohamed Said hakina tofauti na anachokilalamikia!

Ulichokifanya wewe ni kipi? vipi kuhusu Abushiri? maana zile za uso za knockout za Mkwawa nimeziona nikawa nashangilia, nangoja.
 
Lingekuwa jambo jema sana kama tutafanya hivyo,

Nitaajitahidi kuiweka vema na kila msomaji aone kwa macho yake ya nyama!
Hii ndiyo nafasi yako humu jamvini...ukitumwa u-fail hiki au kile ...usjiingize katika usiyoyajua!

*Wewe ni mtoto wa ngapi kwa julius nyerere?..hawa TBC hawa! wana "urasimu" kwelikweli.
 

Soma hotuba ya Nyerere hapo juu anakuambia Wazee wamemchukuwa wamemfanyia dua hao hao wazee wakamfanyia matambiko ya jadi. Kama unapingana na maneno ya mzee wako basi wewe ni NUNDA...Mzee wako anakiri Wazee wa Dar es Salaam kwanza wengine baadaye wewe bado utaki tu.
 
Umechoka kulizungumzia hili jambo ambalo wewe umelipotosha?

Mpaka sasa hujaonesha wapi limepotoshwa, hebu tupe nukuu japo ya sentensi moja tu ili uwe katika ukweli? ukishindwa ina maana wewe ndio umejaribu kupotosha lakini umeshindwa, ukakimbilia Iringa nako zikakunyeeshea, haafu leo una ubavu kweli hata wa kuandika? haya tunangoja.
 
Sasa naamini wazi kuwa historia huijui ndugu yangu, umebobea kidini zaidi!

Nakupa swali kisha jibu lake ndio ufunguo wako!

Mjerumani na Muarabu nani alitangulia kufika Tanganyika?

Naomba nikuulize, Wa"iraq"w unawajuwa? kama huwajui muulize Slaa katibu Mkuu wa chadema atakueleza ni watu gani hao. Ukipata jibu njoo utuhadithie.

Iraqw man
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…