Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Yericko Nyerere,

Bado sana kwenye historia ya Tanganyika nakuuliza swali moja tu.

1) Manowari ya mamluki wa Kijerumani ilitia nanga Pangani mwaka gani?
 
Last edited by a moderator:
Haya ni maneno ya busara sana. Hakika Mohamed said sio tu mtaalamu wa historia pia ni mtu aliyebobea sana katika somo zima la Adab. Allah akubarik sana Mohamed Said.
 
Yericko Nyerere,

Bado sana kwenye historia ya Tanganyika nakuuliza swali moja tu.

1) Manowari ya mamluki wa Kijerumani ilitia nanga Pangani mwaka gani?

Swali lako bado sijalielewa, unamaanisha MAMLUKI wapi?

Wajerumani hawakuja kama mamluki bali walikuja kama walivyoitwa WAKOLONI

MAMLUKI ina maana moja tu kuu, nayo ni mtu asiyefahamika miongoni mwa watu mwenye kazi ya kijasusi tu!

Je unamaanisha ujio wao wa kwanza walitia nanga pale Pangani Tanga?

Kama ndivyo badi jibu langu ni ndio, na walikuta tayari Muarabu ashaweka himaya zake za kipagazi kwa maeneo ya pwani yote kama Kilwa, Pangani nk lakini hakuwa na udhibiti mkali wa himaya yake na wakatwaa
 
Last edited by a moderator:

Hiyo nimeipenda sana, mimi nilikuwa najuwa kuna Iphone tu kumbe na EyePhone zipo.

Ahsante.
 
Kweli wewe ni Bahr ya historia. Allah azidi kukubariki sana kwa darsa hili kwani tunajifunza mengi ambayo tulikuwa hatuyafahamu.
 

Mkuu matambiko ni mila za Makabila, kama ulivyo Uislam mila ya Ibrahim, ni mila tofauti ambazo haziwezi changamana, huwezi fanya matambiko ya kikabila na hapohapo ukasema wewe ni Muislam

Point ni kuwa Moh Said ana Wazee wake

Msome vizuri Mohamedi Said, na mwisho utakuja kugundua anatetea nini na kwa Maslahi ya nani, maana kama unafunika uso unaweza kudhani tuko kundi moja na Mzee Moh Said, nadhani FFox tongotongo lilimtoka na kujua Moh Said anatafuta nini kwa maslahi ya nani
hope na wewe soon utaelewa tu
 

Mamluki kutoka Msumbiji na sehemu zingine sijakuambia Wajerumani ndiyo mamluki.
 
Umechoka kulizungumzia hili jambo ambalo wewe umelipotosha?

Hapa shida ninayo iona ni kwamba ndugu Yeriko hutaki kukubaliana na Mohamed said kwamba wazee wake hawapo kwenya historia ya nchi hii hivyo historia imepotoshwa!
 

Kituko,

Naona unachanganya mambo hebu nipe ufafanuzi unaposema matambiko ni mila za makabila, kama ulivyo Uislam mila ya Ibrahim.

Matambiko yanafanywa na mila za makabila, ndiyo maana unaona watu wana dini zao lakini bado wanafanya matambiko ya mila zao kama Wamanyema walivyokuwa wanamfanyia Nyerere.
 
Last edited by a moderator:
Hizo ndio ngano wanazozifurahia sana mashabiki wako !!
 
Ritz, Sijui kama utaweza kupata majibu ya haya masuala yako. OK Tuvute subra
 
Imekua kosa kubwa kwa Mzee Mohamed Said kuandika historia ya wazee wake! Ajabu ya Rahmaan. Alafu ndo watu wanajiita wasomi na "Great Thinkers".


Yericko Nyerere, TBC wanasemaje? "Kesho haijafika tu" au ndo ilee "Tomorrow never comes"
 
Last edited by a moderator:

Contradictions kibao.
 

Mag3,

Ni muhimu ikatambulika kwamba TAA ilizaliwa miaka zaidi ya 20 kabla ya TANU, wakatu huo Mwalimu akiwa hata hajabalee. Ni baadae sana ndio Mwalimu akaanza mahusiano na TAA, hasa baada ya viongozi wa TAA kumwona Nyerere kama ni mtu makini na mwenye ushawishi mkubwa katika suala zima la kudai uhuru wa Tanganyika. Hivyo viongozi wa TAA na Mwalimu wakaona kwamba wakishirikiana, kila upande utapata kile walichokuwa wanakitafuta.

Ikumbukwe pia kwamba TAA hakikuwa chama cha Siasa bali a Social Movement iliyokuwa ikipigania haki mbalimbali za watanganyika wakati wa Ukoloni. Umakini wa Mwalimu, hasa uliotokana na uwezo wake mkubwa wa kuunganisha watanganyika bila kujali dini, makabila na jinsia zao, uliwavutia sana viongozi wa TAA na ndipo wakakubali kufanya kazi na Mwalimu. Kila upande ukaleta assets zake muhimu mezani – kwa upande mmoja, Mwalimu akaleta his leadership abilities, Vision, Upeo wa kidunia kutokana na elimu yake Uingereza, Uwezo wa kujieleza, na uwezo wa kuunganisha watanganyika wa dini na makabila mbalimbali. Kwa upande mwingine, TAA nayo ikaleta uzoefu wake wa miaka zaidi ya 20 ya harakati za kudai haki na maslahi ya watu weusi na pia its large territorial base within Tanganyika chini ya wale viongozi kumi na sita ambao walikuwa ni wawakilishi wa TAA katika majimbo mbalimbali Tanganyika. Nyereer alikuja kuongezeka na kuwa mjumbe wa 17 katika mkutano mkuu wa TAA wa mwaka 1954 ambao ndio uliozaa TANU, lakini bado kama a political movement, sio chama cha Siasa.

Kuna mambo makuu matatu ya kuzingatia hapa: Kwanza ni muhimu tufahamu kwamba Nyerere alichaguliwa kuwa Rais wa kwanza wa TANU – TANU ikiwa as a Political Movement, sio Chama cha Siasa kwani ingawa TANU ilizaliwa mwaka 1954, bado hakikuwa Chama cha Siasa. TANU ilisajiliwa rasmi kama Chama Cha Siasa muda mfupi kabla ya Uhuru. Kwahiyo kuhoji jinsi gani Mwalimu alichaguliwa kuwa Rais wa kwanza wa TANU ni kuhoji mchakato jinsi gani VUGUVUGU LA KISIASA linajipatia viongozi wake, hivyo mjadala wa namna hiyo hauna manufaa yoyote kwetu.

Jambo la pili la kuzingatia ni kwamba – TAA kama a social movement kwa miaka zaidi ya 20 kabla ya kubadilika kuwa TANU, kilikuwa ni chombo chenye organizational culture yake, Siasa zake, makundi yake n.k, ambayo TANU ilikuja kuyarithi yote mwaka 1954. Katika hali hii, watu makini wanatakiwa kujikita zaidi katika kujadili jinsi gani Mwalimu Nyerere katika umri wa wakw mdogo na bila uzoefu wowote wa kisiasa na uongozi, aliweza kumudu misukosuko yote iliyotokana na sera ya mkoloni ya divide and rule, sera ya mkoloni to suppress dini moja dhidi ya nyingine au makabila Fulani Fulani dhidi ya mengine, na pia disruption zilizokuja baada ya mkoloni kuanzisha chama chake cha Siasa kama njia ya kuidhibiti TANU – Chama Cha UTP (United Tanganyika Party), ambacho kilifanya kila jitihada kuhakikisha kwamba TANU as a political movement hakigeuki kuwa chama cha Siasa;

Kwa kufanya haya, tutakuwa tunatendea haki historia ya nchi yetu na pia kuimarisha mshikamano wetu kama taifa, hasa kwa kutazama tunapoenda kuliko kujikita katika siasa za kujadili dini zetu, makabila yetu, na Ikulu yetu.
 
Kama hayo yatafanywa kwa uadilifu mkubwa basi mtapata historia iliyojitosheleza. Tuombe heir
 
Funga domo lako we mjinga, kwanini humuulizi Ritz aliyelileta hilo!

Kama Ritz kaja kusema ovyo kuhusu Madrasa upo sahihi. La kama si hivyo msome Confucius. Anasema "A fool despises good counsel, but a wise man takes it to heart."
 
Last edited by a moderator:
Contradictions kibao.

Haujui historia ya nchi yako, bali utawala wenye maslahi yako, hilo ndio tatizo; ni aibu kwamba hauelewi TANU na TAA vyote havikuanza kama vyama vya siasa bali social movement (TAA), Political Movement (TANU); vinginevyo kuhusu jinsi gani na kwanini Mwalimu na TAA walikuja anza ushirikiano, hata kwa mtoto wa darasa la kwanza lazima atagundua kwamba hii ilitokana na ukweli kwamba Nyerere was a unique character katika mazingira ya wakati ule,

na baadae ilikuja bainika hivyo kwamba he was unique sio kwa Tanganyika tu bali dunia ya tatu kwa ujumla; vinginevyo uliyo highlight hapo juu kwamba ni contradictions, ni dhahiri kwamba hauna uthubutu wa kupambana na mimi kwa hoja, hauwezi jadiliana na mimi, wewe sio kiwango changu, kiwango chako ni cha kutetea madudu ya CCM ya awamu ya nne;
 
Historia kiboko sana hii. Mzee Mohamed hakuandika ni wapi Mwalimu alikuwa anajisaidia akibanwa na haja kubwa au ndogo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…