Mag3,
Ni muhimu ikatambulika kwamba TAA ilizaliwa miaka zaidi ya 20 kabla ya TANU, wakatu huo Mwalimu akiwa hata hajabalee. Ni baadae sana ndio Mwalimu akaanza mahusiano na TAA, hasa baada ya viongozi wa TAA kumwona Nyerere kama ni mtu makini na mwenye ushawishi mkubwa katika suala zima la kudai uhuru wa Tanganyika. Hivyo viongozi wa TAA na Mwalimu wakaona kwamba wakishirikiana, kila upande utapata kile walichokuwa wanakitafuta.
Ikumbukwe pia kwamba TAA hakikuwa chama cha Siasa bali a Social Movement iliyokuwa ikipigania haki mbalimbali za watanganyika wakati wa Ukoloni. Umakini wa Mwalimu, hasa uliotokana na uwezo wake mkubwa wa kuunganisha watanganyika bila kujali dini, makabila na jinsia zao, uliwavutia sana viongozi wa TAA na ndipo wakakubali kufanya kazi na Mwalimu. Kila upande ukaleta assets zake muhimu mezani – kwa upande mmoja, Mwalimu akaleta his leadership abilities, Vision, Upeo wa kidunia kutokana na elimu yake Uingereza, Uwezo wa kujieleza, na uwezo wa kuunganisha watanganyika wa dini na makabila mbalimbali. Kwa upande mwingine, TAA nayo ikaleta uzoefu wake wa miaka zaidi ya 20 ya harakati za kudai haki na maslahi ya watu weusi na pia its large territorial base within Tanganyika chini ya wale viongozi kumi na sita ambao walikuwa ni wawakilishi wa TAA katika majimbo mbalimbali Tanganyika. Nyereer alikuja kuongezeka na kuwa mjumbe wa 17 katika mkutano mkuu wa TAA wa mwaka 1954 ambao ndio uliozaa TANU, lakini bado kama a political movement, sio chama cha Siasa.
Kuna mambo makuu matatu ya kuzingatia hapa: Kwanza ni muhimu tufahamu kwamba Nyerere alichaguliwa kuwa Rais wa kwanza wa TANU – TANU ikiwa as a Political Movement, sio Chama cha Siasa kwani ingawa TANU ilizaliwa mwaka 1954, bado hakikuwa Chama cha Siasa. TANU ilisajiliwa rasmi kama Chama Cha Siasa muda mfupi kabla ya Uhuru. Kwahiyo kuhoji jinsi gani Mwalimu alichaguliwa kuwa Rais wa kwanza wa TANU ni kuhoji mchakato jinsi gani VUGUVUGU LA KISIASA linajipatia viongozi wake, hivyo mjadala wa namna hiyo hauna manufaa yoyote kwetu.
Jambo la pili la kuzingatia ni kwamba – TAA kama a social movement kwa miaka zaidi ya 20 kabla ya kubadilika kuwa TANU, kilikuwa ni chombo chenye organizational culture yake, Siasa zake, makundi yake n.k, ambayo TANU ilikuja kuyarithi yote mwaka 1954. Katika hali hii, watu makini wanatakiwa kujikita zaidi katika kujadili jinsi gani Mwalimu Nyerere katika umri wa wakw mdogo na bila uzoefu wowote wa kisiasa na uongozi, aliweza kumudu misukosuko yote iliyotokana na sera ya mkoloni ya divide and rule, sera ya mkoloni to suppress dini moja dhidi ya nyingine au makabila Fulani Fulani dhidi ya mengine, na pia disruption zilizokuja baada ya mkoloni kuanzisha chama chake cha Siasa kama njia ya kuidhibiti TANU – Chama Cha UTP (United Tanganyika Party), ambacho kilifanya kila jitihada kuhakikisha kwamba TANU as a political movement hakigeuki kuwa chama cha Siasa;
Kwa kufanya haya, tutakuwa tunatendea haki historia ya nchi yetu na pia kuimarisha mshikamano wetu kama taifa, hasa kwa kutazama tunapoenda kuliko kujikita katika siasa za kujadili dini zetu, makabila yetu, na Ikulu yetu.