Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Tukubali kwamba hoja zimemalizika. Tunarudia yaleyale. Niwashukuru mleta mada, Yericko Nyerere na Mzee Mohamed Said kwa kujisimamia mwenyewe na kujibu yale alooweza kujibu. Nimshukuru pia kwa kukiri makosa na mapungufu ya kitabu chake. Kwa anadai kitabu kinaendelea kutolewa bila shaka kuna atakalofanya kurekebisha baadhi ya hoja mle hasa ya UDINI aloompakazia Mwalimu na wazee wake.
Nchi yetu itabaki bila DINI kama Mungu, Allah mwenyewe asivyo nayo. WATANZANIA kila mtu ataendelea kuabudu anavyoona inafaa bila ya kumbugudhi mwenzake. Tunapoongelea Taifa letu tusiingize DINI, KABILA ingawa vitu hivi vilikuwepo, vipo na vitaendelea kuwepo.
Watanganyika wote kabisa walipigania uhuru wa nchi yao. Historia isingeweza kuwaandika wote. Ambaye hakuandikwa sio kwamba ilidhamiriwa iwe hivo na yeyote. Hamuwezi kukaa na watu mkaunda CHAMA au UMOJA kwa madhumuni na malengo flani halafu ukataka wenzako wote wasahaulike kwa sababu ya DINI zao ambazo uliwakuta nazo. Haiingii akilini hata kidogo.
Kwa vyovyote vile tumeparurana katika mada hii. Tusameheane. Tubaki WATANZANIA. Hakuna aliyeshinda wala kushindwa. Wengi tuliowajadili humu wametangulia mbele ya haki. Hawakuyaandika karibu yote tulioyajadili na kubishana humu. Hakuna anayejua kwa uhakika kama wangepewa nafasi kama hii tuliopata wangeandika nini. Tumewalisha na kutafunisha maneno mengi tu. Hawakutaka kuonekana wanajikweza kwa kuandika HISTORIA walioitengeneza wenyewe.
Wild Card,
Wapi nimekiri makosa na upungufu wa kitabu changu?
Huu ndiyo ujanja wenu wa kumaliza mnakasha?
Haifai kabisa kutiliana maneno kinywani.
Ikiwa mnataka tumalize mnakasha na tumalize kiungwana.
Wala mimi sitakuulizeni kuhusu suala la ''uchochezi wangu.''
Nimekuwa hapa jamvini siku zote.
Wasikilizaji watatuhukumu.