Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Utafiti wa mohammed said haujawatendea haki wapigania uhuru wengine ambao hawakuwa waislamu lakini hawakunufaika chochote baada ya uhuru.

wapo ambao kupata uhuru tu ilikuwa ni mafanikio kwao na hawakuhitaji ziada.

wapo ambao kwa kiwango chao cha elimu wakati wa kuunda serikali mpya wasingeweza kumudu changamoto mpya.

badala ya kuangalia wapigania uhuru tuangalie ukweli kwamba baraza la kwanza la mwalimu lilikuwa na waislamu wasomi wa kutosha kulinda maslahi ya waislamu ndani ya serikali.

Unaonesha kuwa umefanya utafiti wa kutosha kurusha shutuma kwa Mohamed Said, kwanini wewe ungoje Mohamed Said na wewe usiwatendee haki kwa kuandika habari zao kama alivyofanya kwa wazee wake Mohamed Said baada ya kuona kuwa hawajatendewa haki kutokuelezewa na historia ya kivukoni.

Huoni kuwa itakuwa vyema na utatusaidia na sisi kutupa elimu kama alivyotupa elimu Mohamed Said.
 
RONN,

mimi ningependa kukusaidia yafuatayo ikiwemo waTanganyika wote.

Kama umesoma mnakasha toka mwanzo mpaka mwisho utabaini kuwa kuna Historia mbili za wapigania uhuru wenu. Kuna wale waliotajwa katika kitabu cha Kivukoni na wapo katika tovuti ya CCM na wale waliotajwa na Mohamed Said ambao walisahaulika na tunawajua wengine ni maarufu sana kama akina Bibi TITI, Rashid Kawawa, Jumbe Tambaza, Sheikh Takadir, Sheikh Ramia, Mshume Kiate na akina Mtemvu.


Sasa cha msingi ni vijana wa Tanganyika sasa ni wakti muhimu kwenu kuvichukua vitabu hivyo viwili na kuanza kuvifanyia utafiti ili kutoa kitabu kimoja madhubuti chenye kuandika historia sahihi ya vuguvugu la uhuru wa Tanganyika.

Mimi naamini watu wengi bado wapo hai kama akina Mama Maria Nyerere na wengine ambao Mohamed Said amewataja katika kitabu chake ili kurahisisha utafiti wenu.

Siku zote tunaamini UTAFITI unapigwa kwa UTAFITI na si vinginevyo.


Mnakasha ulikuwa mzuri sana na tumejifunza mengi sana.

Wakuu tuwe makini na hili suala,

Hapa kuna mambo makuu mawili kwa historia ya nchi yetu!

Kwanza ni wapigania uhuru wa nchi yetu (mashujaa)

Pili kuna waasisi wa TANU.

Sasa sijui malalamiko yanasimama wapi?
 
Tumewalipa nini wapigania uhuru wafuatao.

1 Mkwawa
2. Mangi sina
3. Kimweri.
4. Kinjekitile.
5. Marealle.
6. Mirambo
7. mwakatumbula
8. Mandara
9 Na wengine.



Mohammed said anatudanganya kwamba uhuru wa Tanganyika ulianza kupiganwa mwaka 1929.

kuna machifu, watemi na watu wengi walipoteza maisha wakati wa mkoloni wakipigania uhuru, je wao hawana haki ya kudai familia zao zimenufanika vipi na uhuru au kudai fidia ya kupoteza babu zao kwenye vita hivyo???

Hawa ndio waasisi wa kupigania uhuru kamili wa Tanganyika
 
Wakuu tuwe makini na hili suala,

Hapa kuna mambo makuu mawili kwa historia ya nchi yetu!

Kwanza ni wapigania uhuru wa nchi yetu (mashujaa)

Pili kuna waasisi wa TANU.

Sasa sijui malalamiko yanasimama wapi?

Soma kichwa cha nyuzi yako hii halafu utajuwa malalamiko ni yepi na uzioneshe shutuma zako, naomba japo mstari mmoja wa kutoka kitabu cha Mohamed Said unaothibitisha shutuma zako.
 
Hakuna utafiki unaozungumzia mabaya tu huo ni uchochezi. Mohammed said hajawazungumzia wakristo wengi tu ambao walipata tatizo moja na walilopata waislamu. Lengo la utafiti huo lilikuwa moja kuonyesha mwalimu alikuwa mbaya lakini pia kwamba hakuna wakristo walipata mataizo ya aina moja na waliopata waislamu wakati wa mwalimu.

Kwa nini Maaskofu kama Macaurous wa Syprus alipofukuzwa na Mwalimu na wengine hakuwaeleza kwenye utafiti huo?

kwa nini kawaacha akina Johhn Malecella alipomwita na kmwambia ajiuzulu uwaziri mkuu hakugusia.

Lowassa alikutana na mkono wa Mwalimu pia hakugusia

na wengine wengi tu.

Nafikiri Kazimoto wewe ujawahi kufanya utafiti wowote. Ngoja nikusaidie kidogo.

Ili mtu uweze kufanya utafiti ni lazima ujue unataka kufanya utafiti wa Nini. Huwezi kufanya utafiti wa kila kitu.

Al Akhiy Mohamed Said alitaka kufanya utafiti wa Mchango wa wazee wake katika kupigania uhuru wa Tanganyika. Na hilo ameliweka wazi kila mtu analijua hilo. sasa asingeweza kwenda mpaka kwa hao mapadri au hata kwenda kwa chifu Rumanyika wa kule Bukoba. yeye amejikita zaidi kwa wazee wake wa Dar katika kupigania uhuru wa Tanganyika na reference yake kubwa ilikuwa Kijitabu cha Kivukoni ambacho kilisahau mchango wa wazee wake.

sasa na wewe unaweza chukua kijitabu cha Kivukoni kuhusu historia ya Uhuru wa Tanganyika na kile cha Mohamed Said kuangalia kama kuna watu wamesahaulika basi na wewe ukatoa kijitabu chako. Hiyo ni ruhsa kabisa kuliko kutoa shutuma na lugha za kejeli kwa al akhiy Mohamed Said kwa kazi yake nzuri.

Pole sana.
 
That is the big problem of Zomba, he is always a jack of all trades but master of non!

Raha sana kuona kuwa hata wewe umefaidika au hujapitia post namba 3186? ili utulize munkar wako.
 
Hawa ndio waasisi wa kupigania uhuru kamili wa Tanganyika

Yericko,

Nikubaliane nae kuwa historia ya nchi yetu inamapungufu na inahitaji masahihisho, lakini kwa hili la Mohamed si masahihisho bali ni upotoshaji mkubwa, Uchochezi na ni Uhaini kwa nchi. Kwa bahati mbaya bwana Mohamed Said histori anayoisimamia ameiakisi kuanzia miaka ya 1950+ tu,

Yericko.

Kama kweli ungekuwa muungwana ulitakiwa utuombe radhi wafuatiliaji wa mnakasha huu hasa PALE ULIPOSHINDWA KUTUTHIBITISHIA TUHUMA ZAKO ULIZOTOA DHIDI YA AL AKHIY MOHAMMED SAID.

Nafikiri sasa umekiri wazi kuwa kuna mambo mengi yalifichwa na MS ameyafichua tena kwa njia ya kisomi sana na wengi tumenufaika ikiwemo wewe mwenyewe.

Waswahili wanasema Bora uteleze mguu kuliko kuteleza ulimi.

Pole sana

 
Uzuri wa JF kama moderators hawajachakachuwa kila kitu kinakuwapo, soma ulichoandika na nilivyokujibu na kukupa darsa:

Uliandika hivi:



Nikakupa hint:



Hukunielewa kuwa nilikuwa nakusaidia kiuungwana, ndio maana nilikuwekea jina tu la Jimmy Cater bila maelezo, ili urejeshe kumbukumbu zako, ukajibu bila kufikiri:



Nikakupa darsa baada ya kuona kuwa kumbe huelewi unachokiandika na hata unaposaidiwa kwa kupewa hint bado unajifanya mjanja:



Nikakuta kwingine tena ulianza kupotosha kwa hili:


Nikaamuwa nikupe darsa lingine kwa kuwa huelewi unachokisema:



Sasa unarusha nini? vitu viko kinagaubaga.

Bado unatapatapa. Ritz aliandika kuwa Arafat alikutana na Moshe Dayan Camp David. That was the issue. That never happened. Sasa wewe unaniletea za Begin na Sadat, wapi na wapi? Ni yale yale eti Nyerere alikuwa anaenda sokoni Kariakoo bila kuwa na pesa mfukoni. Tumeshawazoea!
 
Kazimoto.

Nilipo underline. Nafikiri huko ni kumuhukumu Ahali yangu Mohamed Said, Kwani yeye ameandika Historia na mchango wa wazee wake katika kupigania uhuru wa Tanganyika. Na mara zote amekuwa akitoa changamoto kuwa kila mtu aandike historia ya wazee wake kama walishiriki kupigania uhuru wa Tanganyika. Hivyo na wewe au jamaa za hao uliobainsha wana nafasi kubwa kulinda historia zao na za jamii yao. Mfano mdogo tu PM wenu Pinda last few days alizindua historia ya kabila moja dogo sana kule kwao Katavi. Hivyo nafasi bado ipo changamkia.


Lakin vile vile kama utatumia utaratibu na lugha muafaka Mohamed Said anaweza kutupa mengi sana kuhusiana na hao kwani katika mnakasha huu alianza kubainisha kidogo kuhusu Mkwawa. Labda kwa hishma kubwa na taadhwima kubwa tuombe al Akhiy Mohamed Said atupe darsa kidogo kuhusu hao na michango yao sio tu katika kulinda himaya zao bali pia ukombozi wa Tanganyika.
Wasomi hujadili na kuchambua "historical fact" na sio hisia! na sio busara kutuambia kwamba Mohamed ameandika historia yaa wazee wake na hivyo na sisi tuandike historia ya wazee wetu, huo sio usomi.
 
Wasomi hujadili na kuchambua "historical fact" na sio hisia! na sio busara kutuambia kwamba Mohamed ameandika historia yaa wazee wake na hivyo na sisi tuandike historia ya wazee wetu, huo sio usomi.

Nakubaliana na wewe kabisa kuwa huo sio USOMI bali unaitwa UTAFITI.

Siku zote utafiti unajibiwa kwa UTAFITI na sio porojo wala kejeli. Sasa nafasi unayo nawe fanya utafiti utuletee paper yako ya kitaaluma.

Pole sana
 
Nakubaliana na wewe kabisa kuwa huo sio USOMI bali unaitwa UTAFITI.

Siku zote utafiti unajibiwa kwa UTAFITI na sio porojo wala kejeli. Sasa nafasi unayo nawe fanya utafiti utuletee paper yako ya kitaaluma.

Pole sana
Unaweka wapi mpaka kutenganisha usomi na utafiti? Kama kweli Mohamed Saidi alifanya utafiti kwa aliyoya andika mbona mpaka anaaga hapa jamvini hajaweka ushahidi wa kuthibitisha madai yake?
 
Zomba,

Hoja yako kuhusu list ya waasisi nimeijadili mara nyingi sana licha ya wewe kuendelea na hoja zako kwamba hiyo ni list ya kivukoni. Mimi nimejifunza hilo kupitia historia kwa kujisomea, tena iliyoandikwa miaka ya sitini wakati matukio yakiwa bado fresh, sio orodha zenu za kuchakachua mnazo tengeneza vijiweni karne ya 21. Hoja ya mzee mwanakijiji kwenye bandiko namba 3127 pia imewaweka sawa, lakini kama kawaida yenu, mnatimua mbio. Vinginevyo sioni kipya hapa zaidi ya muendelezo wa propaganda zisizo na maslahi kwetu kama taifa.
 
Unaweka wapi mpaka kutenganisha usomi na utafiti? Kama kweli Mohamed Saidi alifanya utafiti kwa aliyoya andika mbona mpaka anaaga hapa jamvini hajaweka ushahidi wa kuthibitisha madai yake?

Funguka kiakili na mara zote fikiri nje ya box.

Al Akhiy Mohamed Said (kama umesoma post ya kwanza ) ametuhumiwa kuwa yeye ni mchochezi , mpotoshaji na mhaini. sasa kilichotakiwa ni mtoa mada kuthibitisha tuhuma hizo. Na Mohamed Said alitakiwa kujibu tuhuma hizo.

Sijui nikusaidiaje hapo.

Nakupa pole
 
Funguka kiakili na mara zote fikiri nje ya box.

Al Akhiy Mohamed Said (kama umesoma post ya kwanza ) ametuhumiwa kuwa yeye ni mchochezi , mpotoshaji na mhaini. sasa kilichotakiwa ni mtoa mada kuthibitisha tuhuma hizo. Na Mohamed Said alitakiwa kujibu tuhuma hizo.

Sijui nikusaidiaje hapo.

Nakupa pole
Msaidie mpuuzi mwenzio Mohamedi Saidi kwa kufikiri na kuwadanganya kuwa juhudi na mapambano ya uhuru yalifanywa na wazee wake wakiislam na sio watanganyika wote kwa ujumla wao!
 
Back
Top Bottom