Ndugu yangu Bukyanagandi, ni pigo kubwa sana kwa wanaotafuta "muujiza" ili kumpandisha Nyerere kutoka alipo "mwenyeheri" kumpeleka kwenye "mtakatifu". Muujiza walioutegemea ni kumfanya kuwa yeye ni "super hero" wa Tanganyika aliyeweza kuwakabili wakoloni peke yake na kuipatia Tanganyika Uhuru alioudai yeye pekee. Lingethibitishwa hiilo ni moja kwa moja linampa status Nyerere ya kuwa ni mfanya "miujiza" (miracles) ambao ni kigezo cha u "sainthood".
Ukweli anaouweka wazi Mohamed Said, unaharibu hicho kigezo na ni lazima wagalatia wampinge Mohamed Said kwa nguvu zote. Lakini ukweli ni ukweli haufutiki na muujiza uwe wa kweli basi, si wa kubuni.
Bukyanagandi nafahamu kuwa wewe si Muislaam kama ulivyojieleza katika moja ya post zako, lakini u katika wale waupendao ukweli na inashangaza kuona watu humu wanapinga lakini wanachokipinga hawakioneshi, iliyobaki wanarusha kila istihizai, kejeli, vijembe kwa kuwa tu wanadhani ndio wanafanya "character assassination", laiti angelikuja mmoja wao akasema, Mshume ni wa kabuni hakuwepo, Abdulwahid Sykes hajawahi kumweka Nyerere, Dossa Aziz hajatowa mchango wake katika harakati za kudai Uhuru na wengine wote aliowataja Mohamed Said, japo mmoja wao au habari yao moja wakaipinga, hapo ningewaelewa, lakini tazama na soma kwa makini hilo hukuti.
Ni maradhi tu yaliyomo mioyoni mwao, na kwa uhakika hayapunguwi yanazidi. Unajuwa adui yako kila unapofanikiwa yeye ndiyo huzidi kuumia? ndio hawa wanaopinga, mradi wapinge tu.