Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Ndugu yangu, jibu hoja usikwepe, serikali hiyohiyo unayoilalamikia kuwa imewadhulumu, leo unaifuta makwa yayo?

Mkuu rudi kwenye mstari ujibu hoja, sio kurukaruka mjadala ndugu yangu.

Mimi si yule wa nipe nikupe.
Mimi silazimishwi kufanya jambo.

Mimi napenda mjadala wa kiungwana.
Mjadala wa kiungwana ni upi?

Mkifika mahali wote hamkubaliani mnatoka pale
mnakwenda mbele.

Hamuwi kama sahani ya santuri iliyokwama kwenye gramafoni.
 

Maswali haya nawaachia wengine wakujibu iwapo wataona yana maana.
 
Tukimaliza ya MOU tunarejea kwa matatizo yanayowasibu ndugu zetu wasomali namfumo wao wakiutawala, nitayaregelea maswali punde tu tukimaliza la moU

Kumbuka niwewe uliyetowa lawama za kwamba mfumo kristo na mou unafaidisha wakristu ukimtanguliza Nyerere kafara kwa madai yako kutuchochea watanzania.


Ngoja nikufahamishe kitu.

Mimi ni Muislam wa kawaida wala sina cheo Bakwata.
Wala si ''alim'' kuwa naweza nikafutu mas' ala.

Wala Rais Kikwete hanifahamu.

Swali hilo ungelipeleka Bakwata ndipo mahali pake.
 

Mkuu adolay,

Na mimi naomba nikuulize kuna ubaya wowote kumuita mtu yoyote kwa Professional yake hata kama kastaafu. Upadri ni taaluma kama taalumu zingine mpaka uende shule.

Katiba haijakataza kugombea lakini ni busara kutokugombea sababu Watanzania tumechanganyikana dini mbalimbali.

Nadhani nimejibu vyema.

Mkuu wewe ni mkiristo vipi unajishughulisha na mambo ya waislam tena umekwenda mbali zaidi mpaka Somalia.
 
Last edited by a moderator:
Mbona hoja zako Nyerere hazina mashiko wala mantiki? Bw Said anakupa kila kitu na ushahidi wewe unaropoka tu kihuni.Pia, kwa nini kuihusisha Somalia? Ni kwa sababu wataka kuonesha kuwa Waislamu ,naturally and inherently' hawasomi, hawapendi kusoma au hawawezi kuongoza Wizara au Idara za elimu? Umepata wapi dhana hiyo? Mbona hukuulizia juu ya nchi za Kiislamu zenye mifumo mizuri hata Wazungu huenda sasa kusoma huko, kama Emirates?
 

Mantiki ya maneno yako haya nikuwa, pale usipojibu hoja yaani ukikwepa, basi mimi nikubaliane na ngano zako!

Jambo hili sifalsa yangu mkuu,

Tujenge hoja na tushindane kwa hoja si imla!
 

Pole sana ndugu, usilolijua ni kama usiku wa giza!

Jaribu kuwa msomaji hapa utapata mang'amuzi ya nera!
 

mzee kwa porojo umetukuka, lol!.
 
Maswali haya nawaachia wengine wakujibu iwapo wataona yana maana.
Typically Mzee @ Mohamed Said. Haujawahi kujibu maswali kama haya hapo kabla na wala hautayajibu! Uislam wako ni ule wa Kariakoo kuelekea New Street.
 
"hiki kitabu ndio AUTHORITY katika historia ya TANU" naona sasa umeamua kututusi mchana kweupe
 
Pole sana ndugu, usilolijua ni kama usiku wa giza!

Jaribu kuwa msomaji hapa utapata mang'amuzi ya nera!

Wewe kila mtu akichambua hoja zako na kuziona hazina mashiko unamwambia ajaribu kuwa msomaji.

Watu wote wanafuatilia huu munakasha ndiyo wanapima hoja, Mohamed Said, kajishusha sana mpaka kufanya munakasha na wewe siyo kiwango chake.

Nakushauri tulizana vizuri kwa Mohamed Said, utavuna mengi ambayo hujawahi kukutana nayo kwenye anga za wasomi.

Hoja zako ni nyepesi sana ndugu yangu.

Kuwa na subira punguza jazba punguza viroja zama kwa Mohamed Said, utaibuka na elimu.
 
Last edited by a moderator:
Hahaaa daah wewe ndugu unanivunja mbavu sana, nikushukuru kwani umekuwa kitulizo tosha cha hasira yangu juu ya uposhaji wa Mohamed.
 
Last edited by a moderator:
Typically Mzee @ Mohamed Said. Haujawahi kujibu maswali kama haya hapo kabla na wala hautayajibu! Uislam wako ni ule wa Kariakoo kuelekea New Street.

Anakwamisha sana mjadala huu usisonge mbele kwa aina yake ya kukwepa hoja mhimu.
 

sikubali na kamwe sitaki fanya kazi hii hata kama nihongwe ujira mnono, roho yangu itanisuta nitaishi kwa tabu. Wewe umeweza hilo!
 
Last edited by a moderator:


Mkuu

1.Hujajibu swali hata moja narudia alikujibu vibaya ni nani, Dr slaa?

2. Unafahamu katiba ya wakatoliki? kama unaifahau elezea upadri wa padri yoyete anaupataje?

3. Je kuna sifa zozote zinazoweza kumuondolea mtu upadri katika katiba ya kanisa na unaweza kuzitaja?

4. Je kunakustaafu upadri au kuacha katiba inasemaje ya wakatoriki na umri gani padri anapaswa kustaafu kama uliosema hapo juu.





Jibu Kuhusu waislam

Nani anakesha hapa kuleta hoja za mfumo kristo?, dhulma dhidi ya waislam?, Mou nk katika madai haya ungetaka nani akujibu?

a) mwislam na kama mwislam kwanini

b) mkristo na kwanini awe mkristo

tutaendelea mkuu Ritzs ukinijibu hapa, maana ndipo jibu lako lilipo.

Nifanyie uungwana kwa kujibu jibu sahihi kwa kila swali yaani mstari baada ya mstari.
 
Moja ya mambo ambayo huwa nayasoma na kuninyima raha hapa Jamii Forum ni baadhi ya wasomi kutumia vibaya elimu zao na kutumia nguvu zao zote kupotosha umma.

Katika biashara kuna aina mbili za ujasiriamali..constructive and destructive entrepreneurship Hata yule mama lishe anayeweka hamira kwenye ugali watu washibe kwa ugali kidogo naye ni mjasiriamali (destructive entrepreneurship , japo sio mjasiriamali tunayemtaka kwa maendeleo endelevu.

Kwa vigezo hivyo hivyo, msomi anayetumia usomi wake kuleta takwimu za kuonyesha wingi wa taasisi za kikristo pasipo kutuambia sababu naye ni msomi. Msomi anayetumia muda mwingi na nguvu zake zote kutafuta kila namna ya uhasi, maandiko ambayo hata kwa muktadha wake hayatuhusu watanzania lakini huyasoma na kutuonyesha kwamba ameyasoma, na mwisho kuyaleta kwetu kwa nia ya chuki naye ni msomi, ila ni bahati mbaya sio msomi tunayemtaka.

Niseme machache..Tanzania tunaelekea pabaya. Wasomi elimu zetu tunazitumia vibaya na hivyo tunaongozwa na hisia badala ya uhalisia. Maisha tunayachukulia kama mjadala (debate) tuliyokuwa tunafanya sekondari..upande unaopangwa either proposing or opposing ndio unaoutetea kwa nguvu zote, la muhimu ni upande wako ushinde.

Ebu kila mmoja wetu abadilike na kuwa mtu bora kwa ajili yake na jamii yake. Nchi hii nafasi mbona fursa ziko nyingi tu!

  • Hivi mnafurahia nafasi za juu za makampuni makubwa kuchukuliwa na wazungu, wakenya, waganda, waghana, na wanigeria leo hii miaka 51 ya Uhuru?
  • Hivi badala ya kujielimisha na kuelimisha jamii yetu kuwa bora kwa ajili ya kulinda tunu za nchi hii jibu limekuwa ni kuwashambuliana hata kwa hoja zilizo wazo na ukweli tunaoweza kutambua kwa usomi wetu?
  • Tunapoteza nguvu nyingi kulinda hoja dhaifu hata nafsi zetu zinatusuta!
  • Kwa nini huu moto wa udini tusiuanzishe dhidi ya makampuni ya madini yasiyolipa kodi na dhidi ya serikali kugawa rasilimali zetu?
  • Hivi umaskini wa nyumbani kwetu kwa sababu ya matatizo ya wazazi kutokujipanga wakati fursa zilikuwepo unasababishwaje na maendeleo ya jirani na watoto wake aliyejipanga?


Siku ujinga huu ukituondoka na kutambua tumefanya makosa itakuwa ni too late! Kupigania kushinda debate na upande wako hata kama si sahihi ni damage kubwa sana kwa ustawi wa jamii ya Tanzania. Kila nisomapo upotoshaji wa kidini huishiwa nguvu ya kufanya chochote maana naona kama wanangu huko mbeleni wataishi kwa kuulizana wewe ni mkristo au muislam? Tujifunze kwa Rwanda juu ya athari ya ubaguzi ndani ya jamii. Kuna rafiki mnyarwanda nilimuuliza kabila lake kama ni mhutu au mtusi akanijibu kwamba baada ya mauaji ya kimbari hairuhusiwi kuuliza swali hilo hadharani. Hii imekuwa kama sheria na kweli hakuniambia mbali na kwamba sote tulikuwa nje ya Rwanda. Wanyarwanda sasa ni wamoja na wanasonga mbele. Najua kwa dini itakuwa ngumu kuficha lakini hii si kitu palipo na upendo.

Niwe wazi baadhi ya michango ya GT humu inanifanya nifikirie vibaya dhidi ya rafiki na ndugu zangu wa kiislamu lakini Mungu ananipa nguvu nazidi kuwapenda zaidi. Ila, mambo haya inabidi yaishe kwani maandiko matakatifu na misaafu yanasema...mazoea mabaya hujenga tabia mbaya; pia jiweke mbali na dhambi. Haya maneno nimetohoa (paraphrase) kutoka kwenye Biblia na Kuran ili kuleta maana sawa kwa wote. Hivyo tukizoea kuongea kichuki chuki tutaishia kuishi kwa chuki.

Mungu ibariki Tanzania na watu wake. Rejesha amani iliyopotea, upendo miongoni mwetu kwani sote ni wanao. Siafiki kupeana nafasi kwa kuzingatia udini wala ukabila. Akistahili mwislamu apewe hata kama kwenye idara hiyo waliotangulia wengi ni waislam vivyo hivyo akistahili mkristo apewe hata kama waliotangulia kwenye idara hiyo wengi ni wakristo. AMINA!
 


Mkuu sijali labda wewe umeona hayo majibu.

Tafadhali tujuze walau kwa moja tu la MOU

- Nani amewazuia waislam wasiwe na mou yao? ukimaliza hilo tutakuuliza kwanini mohamed analalamikia Mou ya wakristu
 
Hahaaa daah wewe ndugu unanivunja mbavu sana, nikushukuru kwani umekuwa kitulizo tosha cha hasira yangu juu ya uposhaji wa Mohamed.
Hivi huko kwenu hamfundishwi adabu ya kutaja majina ya watu waliokuzidi umri huyu mzee ni mkubwa kuliko ww usimuite mohamed sema mzee mohamed said mbona dr slaa humuiti slaaunamuita DR SLAA
 

Mkuu mie sijui chochote kuhusu katiba ya wakatoriki.

Kujua Dr Slaa alikuwa Padri wala haitaji kwenda shule.

Ninavyojua mie Padri ni kiongozi wa kanisa kwa wakatoriki.

Kazi Mungu hata siku moja huwezi kustaafu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…