Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Huna jipya mzee Mohamed zaidi ya kujinasibu na mambo madogo! mbona hujibu hoja za wakina Nyambala, Nguruvi, Mwanakijiji, Mag3...........,? sasa unakuja uwanjani na kuniita mie mvivu wa kusoma! unanitaka ni kasome kitu gani? unataka nikasome 'historical opinions' zako? au nikasome majigambo yako kuwa wewe umezaliwa Gerezani? Unataka nirudi nikasome kilio chako kuwa waislam katika nchi hii wanaonewa? Pole sana Mohamedi, umerudi jamvini bila hoja. Bora ungebaki huko ulikoamua kujificha!

Masikini ya Mungu, hata hujuwi ukasome nini? Nenda kapate elimu itayokusaidia kutoka kwenye "mambo madogo", ukishaipata urudi na "madongo".
 
wamekula za uso. Hakuna hata mmoja aliyekuja japo kujibu tu, nyumba iliyozaliwa tanu ilikuwa ya nani? Halafu wanajidai wanaijuwa historia ya wazee wa dar?

Hivi hawa wameshawahi kumsikia hata "bwa mkubwa shillingi"? Licha ya kumuona.

Wameshawahi kumsikia manilal mathuradas verani au abdulkareem karimjee? Au habib punja? Watu wenye historia ndefu dar? Wanamjuwa al marhum bwana mzee wa mchafukoge na kisha new street?

Mohamed kawaumiza sana kuwawekea mliyokuwa hamyategemei. Utakatifu muutafutie muujiza mwingine, huu wa "one man show" hauna mshiko wala hauna maana tena.

Wanaemdhania muasisi wa tanu anakiri hata jina la tanu hakutowa yeye. Anasema lilitolewa na nani?

zomba..
a.k.a mzee wa hints,,!

Please spare them for a while,go easy,,

kill them slowly..
 
Masikini ya Mungu, hata hujuwi ukasome nini? Nenda kapate elimu itayokusaidia kutoka kwenye "mambo madogo", ukishaipata urudi na "madongo".
Zomba, mwache mchochezi Mohamed ajibu hoja na maswali anayoulizwa, wewe huna hoja zaidi ya kumuharibia, unalialia tu hapa.
 
Zomba, mwache mchochezi Mohamed ajibu hoja na maswali anayoulizwa, wewe huna hoja zaidi ya kumuharibia, unalialia tu hapa.

Soma kichwa cha habari. Halafu ukajisomee, umekula ya uso, moja tu, kutoka kwa Mohamed Said, umeambiwa kasome, mie nakupa hint, anza na kichwa cha habari usianze mbali, halafu urudi na "madongo" si madogo.
 
Nothing to learn from either you or Mohamed Saidi.
 
Wamekula za USO. Hakuna hata mmoja aliyekuja japo kujibu tu, nyumba iliyozaliwa TANU ilikuwa ya nani? Halafu wanajidai wanaijuwa historia ya wazee wa Dar?

Hivi hawa wameshawahi kumsikia hata "bwa mkubwa shillingi"? Licha ya kumuona.

Wameshawahi kumsikia Manilal Mathuradas Verani au Abdulkareem Karimjee? au Habib Punja? Watu wenye historia ndefu Dar? Wanamjuwa Al Marhum Bwana Mzee wa mchafukoge na kisha new street?

Mohamed kawaumiza sana kuwawekea mliyokuwa hamyategemei. Utakatifu muutafutie muujiza mwingine, huu wa "one man show" hauna mshiko wala hauna maana tena.

Wanaemdhania muasisi wa TANU anakiri hata jina la TANU hakutowa yeye. Anasema lilitolewa na nani?

zomba, Mzee "Hints"

Unanikumbusha mbali sana.
 
Last edited by a moderator:
Bila Mohamed Said nani angejua kama Mama Maria Nyerere alikuwa kapewa mlango wa biashara na wazee wa Dar es Salaam pale mtaa wa Mchikichi, alikuwa anauza mafuta ya taa. Bahati nzuri huyu bi mkubwa bado yupo hai mnaweza kwenda kumuuliza.
 
Huna jipya mzee Mohamed zaidi ya kujinasibu na mambo madogo! mbona hujibu hoja za wakina Nyambala, Nguruvi, Mwanakijiji, Mag3...........,? sasa unakuja uwanjani na kuniita mie mvivu wa kusoma! unanitaka ni kasome kitu gani? unataka nikasome 'historical opinions' zako? au nikasome majigambo yako kuwa wewe umezaliwa Gerezani? Unataka nirudi nikasome kilio chako kuwa waislam katika nchi hii wanaonewa? Pole sana Mohamedi, umerudi jamvini bila hoja. Bora ungebaki huko ulikoamua kujificha!

G,

Wakuhurumiwa ni wewe kaka.

Mimi nasomwa sana huo ni ukweli.

Mimi DVD zangu zipo kila nyumba ya Muislam
zinasikizwa na kuangaliwa na wakubwa na wadogo.

Sina haja ya kurudia kuwa nasomwa kwenye vyuo
pamoja na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

Ila kumbuka kuwa "Mmashomvi mmoja hazuii soko."

Ningemwachia Zomba akushehereshee lakini najua
unamwogopa.

Kwa ajili hii nitakueleza mimi mwenyewe.

Huyo Mmashomvi ni wewe.
Kama wewe hunisomi ndiyo wengine hawatanisoma?

Mmashomvi mmoja akisusa kuja sokoni ndiyo soko litafungwa?

PS: Nakupa somo la bure katika taratibu za uandishi.
Weka nukta tatu kama hivi: ...
Siyo msururu.
Wenzako watakujua kuwa wewe bado.
 
bila mohamed said nani angejua kama mama maria nyerere alikuwa kapewa mlango wa biashara na wazee wa dar es salaam pale mtaa wa tandamti, alikuwa anauza mafuta ya taa. Bahati nzuri huyu bi mkubwa bado yupo hai mnaweza kwenda kumuuliza.

dah..,hili nalo ndug yangu ritz,
nilikuwa silijui,ama kwa hakika tunanufaika kwa mengi sana..!

Naomba unisaidie kunijuza kidogo,hivi big brother yericko x,ni mtoto wa ngapi wa mama maria nyerere??

Natanguliza shukran zangu za dhati..
 
g,

wakuhurumiwa ni wewe kaka.

Mimi nasomwa sana huo ni ukweli.

Mimi dvd zangu zipo kila nyumba ya muislam
zinasikizwa na kuangaliwa na wakubwa na wadogo.

Sina haja ya kurudia kuwa nasomwa kwenye vyuo
pamoja na chuo kikuu cha dar es salaam.

Ila kumbuka kuwa "mmashomvi mmoja hazuii soko."

ningemwachia zomba akushekhereshee lakini najua
unamwogopa.

Kwa ajili hii nitakueleza mimi mwenyewe.

Huyo mmashomvi ni wewe.
Kama wewe hunisomi ndiyo wengine hawatanisoma?

Mmashomvi mmoja akisusa kuja sokoni ndiyo soko litafungwa?

abadan asilani soko haliwezi fungwa..!

Njaa za mmashomvi mmoja na kususa kwake hakuwez zuia soko wala gulio kuendelea na biashara ndugu yangu..
 
Bila Mohamed Said nani angejua kama Mama Maria Nyerere alikuwa kapewa mlango wa biashara na wazee wa Dar es Salaam pale mtaa wa Tandamti, alikuwa anauza mafuta ya taa. Bahati nzuri huyu bi mkubwa bado yupo hai mnaweza kwenda kumuuliza.

Ritz,

Duka lilikuwa Mtaa wa Mchikichi karibu na nyumba ya Bi. Bahia.
 
Ulikuwa unamjuwa Abdulwahid Sykes kabla ya kumsoma Mohamed Said?

Zomba,

Kitendawili cha Abdulwahid katika historia ya Nyerere ni kuwa.
Ili ngoma ya Nyerere inoge basi shurti umfute Abdulwahid.

Tatizo kwenye historia ya Nyerere litadhihiri pale sasa utakapomleta
Abdu na kumambatanisha na Nyerere.

Maana yake ni kuwa itabidi umweleze baba yake Abdu, Kleist ambae ni
muasisi wa harakati za African Association.

Hutoishia hapo itabidi ueleze historia ya robo karne ya African Association.
Tayari hapo ushaleta mengi sana.

Sasa mpaka utakapokuja 1952 Nyerere anakutana na Abdu pale Stanley Street,
una nyaraka za kihistoria na taarifa lukuki.

Kwa msomi makini itakuwa shida kumwambia TANU kaasisi Nyerere.
Haya ndiyo yaliyokipa kitabu changu thamani.
 
Bi. Bahia huyu almaaruf kama Maalim Bahia mama'ke Ali Mzee?

Zomba,

Samahani nimekosea.

Pale Mchikichi ni kwa Mwalimu Fatina mdogo wake Mwalimu Sakina siyo
kwa Bi Bahia.

Mwalimu Fatina ni mama yake marehemu Tahia.
 
dah..,hili nalo ndug yangu ritz,
nilikuwa silijui,ama kwa hakika tunanufaika kwa mengi sana..!

Naomba unisaidie kunijuza kidogo,hivi big brother yericko x,ni mtoto wa ngapi wa mama maria nyerere??

Natanguliza shukran zangu za dhati..

THE BIG SHOW,

Julius Kambarage Nyerere amefariki kaacha watoto saba tu. Haya hapa chini majina yao wote.

1) Andrew Nyerere

2) Anna Nyerere

3) Magige Nyerere

4) John Nyerere

5) Makongoro Nyerere

6) Madaraka Nyerere

7) Rosemary Nyerere

Yericko Nyerere siyo mtoto wa Kambarage la mtoto wa Nyerere mwingine.

Ni vizuri yeye mwenyewe ndiyo aseme ni mtoto wa Nyerere yupi.
 
Last edited by a moderator:
the big show,

julius kambarage nyerere amefariki kaacha watoto saba tu. Haya hapa chini majina yao wote.

1) andrew nyerere

2) anna nyerere

3) magige nyerere

4) john nyerere

5) makongoro nyerere

6) madaraka nyerere

7) rosemary nyerere

yericko nyerere siyo mtoto wa kambarage la mtoto wa nyerere mwingine.

Ni vizuri yeye mwenyewe ndiyo aseme ni mtoto wa nyerere yupi.

nashukuru sana ndug yangu ritz..

mimi nahisi huyu yericko x,atakuwa ni mtoto wa julius mtakatifu kama alivyotamba yeye mwenyewe humu jamvini..

ama kwa hakika ni ulimbukeni wa hali ya juu kudandia nasaba ambayo huna uhusiano nayo..
 
Zomba,

Samahani nimekosea.

Pale Mchikichi ni kwa Mwalimu Fatina mdogo wake Mwalimu Sakina siyo
kwa Bi Bahia.

Mwalimu Fatina ni mama yake marehemu Tahia.

Aaah, Mwenyeezi Mungu awarehemu waliotangulia, nawaona hivi, Maalim Sakina nilikuwa sitoki kwake mtaa wa Pemba wakati wa darsa la Al-Marhum Al Faqir Ahmed Sheikh, maaruf "Sheikh Ahmed Polisi" na hapo ndipo nilipoonana kwa mara ya kwanza na Alhabib Mwinyi Baraka.

Tahia Mwenyeezi Mungu amlaze pema, nakumbuka kuna siku AlMarhum Sheikh Kassim bin Juma katokea kwake pale Mchikichi, sisi tumesimama nje Mchikichi na Lumumba miongoni mwetu alikuwepo Tahia na Amne (aliyekuja kuwa mkewe Marehem Mbaraka Mwinshehe, gwiji la mziki kutokea Morogoro,) Sheikh Kassim kama kawaida yake ya utani-utani na sauti yake ya juu akasema "Tahia na Amne kama hamkutazama jinsi mnavyokuwa warefu haraha haraka, itabidi watokee kina Unju bin Unuku wengine kuja kuwaoa nyinyi, hao wote wafupi kwenu" akimaanisha sisi.

Aaah, umenikumbusha mbali Maalim Mohamed, mitaa yangu hiyo. Furaha ilioje kuwasoma watu nnaewajuwa fika.
 
nashukuru sana ndug yangu ritz..

mimi nahisi huyu yericko x,atakuwa ni mtoto wa julius mtakatifu kama alivyotamba yeye mwenyewe humu jamvini..

ama kwa hakika ni ulimbukeni wa hali ya juu kudandia nasaba ambayo huna uhusiano nayo..

Anaweza kuwa mtoto wa Nyerere lakini siyo mtoto Julius Kambarage.

Musoma kuna Nyerere wengi tembelea sehemu za Butiama, Mkendo Kati, Makoko, Majita, kote huko wapo kina Nyerere.
 
Back
Top Bottom