Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Pata darsa kuhusu tunayofundishwa sisi, uelewe kwanini tunakushangaa na kukuonea huruma:

Qur'an 49:13
Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari.
zomba
Acha hizo.
Sio ninyi mnaodharau watu wa bara na kutuita watu wa kuja, na kuwa hatujui kiswahili?
Sio ninyi sometimes hata kwenye dini yenu mnaona mzanzibari lazima anaijua zaidi kuliko mmanyema wa Kariakoo, na Mmanyema wa kariakoo anaijua zaidi kuliko mmnanyema wa kigoma na Congo? Mpaka mmesababisha inferiority complex ya wadini wa bara wanajilazimisha kuwa ni waswahili wa Dar, ili tu muwakubali? zomba, hebu pitia posts zako hapa jinsi zilivyojaa maneno makali, hata kuhusu marehemu... Hayo mnafundishwa na Quran? Give me a break meeeeeeen!
 
Last edited by a moderator:
nashukuru sana kwakuamua kupasua jipu la mzee mohamed mwenye kisirani asichokijua sababu yake!

Tena washukuru serikali hii ya kikwete (ya kikristo) inawabeba na kuwaacha waendelee kupiga umbeya usio na dawa kila kukicha!

Wanashindwa kuhimiza watoto wao waende shule lakini wanaweweseka kila uchao kudai wanaonewa, ukiwauliza wapi mnaonewa wanabaki kutoa mapovu tu bila jibu la msingi!

yericko x,
mimi nadhan kwa sasa ungeamua kujisimamia ww mwenyewe kuliko kukaa na kusubiri back up za ndugu zako,haitakusaidia hata kidogo..

Kadir muda unavozid kwenda ndivo jins unavozid kusikitisha na kutia huruma kwa hoja zako..
 
G,

Wakuhurumiwa ni wewe kaka.

Mimi nasomwa sana huo ni ukweli.

Mimi DVD zangu zipo kila nyumba ya Muislam
zinasikizwa na kuangaliwa na wakubwa na wadogo.

Sina haja ya kurudia kuwa nasomwa kwenye vyuo
pamoja na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

Ila kumbuka kuwa "Mmashomvi mmoja hazuii soko."

Ningemwachia Zomba akushehereshee lakini najua
unamwogopa.

Kwa ajili hii nitakueleza mimi mwenyewe.

Huyo Mmashomvi ni wewe.
Kama wewe hunisomi ndiyo wengine hawatanisoma?

Mmashomvi mmoja akisusa kuja sokoni ndiyo soko litafungwa?

PS: Nakupa somo la bure katika taratibu za uandishi.
Weka nukta tatu kama hivi: ...
Siyo msururu.
Wenzako watakujua kuwa wewe bado.
Nje ya hapo DVD zako hazina nafasi, kwani hazina maarifa zaidi ya uchochezi na udini.
 
zomba
Acha hizo.
Sio ninyi mnaodharau watu wa bara na kutuita watu wa kuja, na kuwa hatujui kiswahili?
Sio ninyi sometimes hata kwenye dini yenu mnaona mzanzibari lazima anaijua zaidi kuliko mmanyema wa Kariakoo, na Mmanyema wa kariakoo anaijua zaidi kuliko mmnanyema wa kigoma na Congo? Mpaka mmesababisha inferiority complex ya wadini wa bara wanajilazimisha kuwa ni waswahili wa Dar, ili tu muwakubali? zomba, hebu pitia posts zako hapa jinsi zilivyojaa maneno makali, hata kuhusu marehemu... Hayo mnafundishwa na Quran? Give me a break meeeeeeen!

Kukuita wakuja ni sifa, kwani sio wakuja kweli? na kukukwambia Kiswahili hujui ni sifa, msome Nyerere kwenye post namba 1 anavyojisifu kuwa alipokuja Dar akakutana na wazee wa Dar alikuwa hata Kiswahili vizuri hakijuwi. Kama si sifa ni nini hiyo? alikuwa anajitukana au anajisifu?

Hutotusikia sisi kukutukana kukuita "koko", koko ni neno linalotumika kwa mbwa na si binaadam. Tafadhali sana, huu ni mjadala tu, usipandishe hasira kiasi hicho, si vyema.
 
Yericko mdogo wangu,

Hebu punguza jeuri.

Nilishapata kusema humu ukumbini kuwa kwa sisi watu wa pwani
kunywa kahawa katika barza ni mila yetu kama nyie kukutana katika
sehemu za kunywa ulevi.

Unywaji kahawa kwetu ni ''art'' khasa hata vile vikombe ikiwa umenikuta
nyumbani nkakukaribisha na nikatoa na halwa...

Utapenda.

Mantiki inabaki palepale kuwa maeneo hayo ni makazi ya Ngano tu!
 
Kukuita wakuja ni sifa, kwani sio wakuja kweli? na kukukwambia Kiswahili hujui ni sifa, msome Nyerere kwenye post namba 1 anavyojisifu kuwa alipokuja Dar akakutana na wazee wa Dar alikuwa hata Kiswahili vizuri hakijuwi. Kama si sifa ni nini hiyo? alikuwa anajitukana au anajisifu?

Hutotusikia sisi kukutukana kukuita "koko", koko ni neno linalotumika kwa mbwa na si binaadam. Tafadhali sana, huu ni mjadala tu, usipandishe hasira kiasi hicho, si vyema.

Haya mkuu zomba. Ila hapa koko - Swahili-English Dictionary
inaonesha wazi kuwa "koko" can mean "wild" or "unconventional".
So it can apply to anything -mbwa, binadamu, mzungu, mwarabu, kugetemeana na maana unayoitaka (wild au unconventional).
Kiswahili kinakua ati, hakipo kariakoo tu. Na sisi wa bara tumo...
 
Last edited by a moderator:
Kukuita wakuja ni sifa, kwani sio wakuja kweli? na kukukwambia Kiswahili hujui ni sifa, msome Nyerere kwenye post namba 1 anavyojisifu kuwa alipokuja Dar akakutana na wazee wa Dar alikuwa hata Kiswahili vizuri hakijuwi. Kama si sifa ni nini hiyo? alikuwa anajitukana au anajisifu?

Hutotusikia sisi kukutukana kukuita "koko", koko ni neno linalotumika kwa mbwa na si binaadam. Tafadhali sana, huu ni mjadala tu, usipandishe hasira kiasi hicho, si vyema.

Haya mkuu zomba. Ila hapa koko - Swahili-English Dictionary
inaonesha wazi kuwa "koko" can mean "wild" or "unconventional".
So it can apply to anything -mbwa, binadamu, mzungu, mwarabu, kugetemeana na maana unayoitaka (wild au unconventional).
Kiswahili kinakua ati, hakipo kariakoo tu. Na sisi wa bara tumo...
 
Last edited by a moderator:
Pata darsa kuhusu tunayofundishwa sisi, uelewe kwanini tunakushangaa na kukuonea huruma:

Qur'an 49:13
Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari.
Zomba kwa hili uko juu yaani hii aya wakiisoma vizuri bila ushabiki watafaidika sana na watajua ukweli uko wapi BIG UP KEEP IT UP
 
Mohamed Said
Wewe na Harith Ghassany ni kama magazeti ya uhuru na mzalendo. Muelekeo mmoja tu. In fact ulimsaidia kumpa story zako za uongo alizoingiza kwenye kitabu chake. Wote mna chuki kwa Nyerere, ila yeye anamchukia zaidi kwa suala la muungano. Wewe unamchukia Nyerere kwa sababu babu yako aliwekwa ndani kwa u-radical wake. Ghassany ni mwarabu koko ambaye hakupenda utawala wa kisultani kupinduliwa, na anachukia waarabu kuhusishwa na biashara ya utumwa na yeye katika ujanja wake (kama wako) ametumia kuzifanya chuki zake ziwe pia chuki za waislam. Nyie wote wawili ni wajanja wajanja wa kutumia mambo ya ukweli mengi, na kupandikiza hisia zenu hasi ndani ya hayo mambo ili hisia hizo zionekane kama sehemu ya ukweli na wakati huo huo, lengo lenu la kuigawanya jamii likifanikiwa.

Kwa hiyo mtu hawezi kutafuta kitu cha kukupinga kutoka kwenye kitabu cha Ghassany, na hali kadhalika mtu hawezi kumpinga Harith Ghassany (kama gazeti la uhuru) kwa kutumia maandiko yako Moh Said (kama gazeti la mzalendo). Ni wale wale tu...

N,

Sawa sisi ni Uhuru na Mzalendo.
Kuna mtu alinambia kuwa nyie ni watu wa chama fulani.

Mimi si mtu wa kuambiwa neno nikaamini hapo hapo sasa dalili zinaanza kujitokeza.
Ala kumbe Uhuru na Mzalendo hawana maana.

Hivi wewe umejua lini hili?

Sasa fungua uzi mpya tujadili.

Ungelijua uungwana wa Harith na ukoo wake wa Waafrika pamoja na yeye mwenyewe
ungejuta kumtukana.

Nitakuonjesha kidogo.

Bibi yake Harith ni Mmanyema mweusi tiii Biti Tambwe na babu yake ni Muarabu wa Zanzibar
mwenye asili ya Kiomani.

Zanzibar walikuwapo wasichana wa Kiarabu lakini babu yake Harith alianguka kimapenzi na
msichana wa Kimanyema Mwafrika kama Waafrika wanavyokuja.

Posa zikenda na ndoa ikafungwa.
Ndiyo leo tuna huyu mjukuu Harith Ghassany.

Baba yake Mzee Ghassany alisoma Oxford pamoja na Mwinyibaraka.
Nikimjua Mzee Ghassany wala sikuuona huo Uarabu wake na kafanya kazi serikalini hadi alipostaafu.

Nikikutana na Harith huniimbia nyimbo za Kimanyema alizofunzwa na bibi yake.
Nyimbo hata mie sikupata bahati ya kuzijua.

Sasa mnapambana na kizazi hiki ambacho hakijaathiriwa na propaganda za Wamishonari na huku Bara
ngano zenu za Waarabu kutesa Waafrika.

Ndiyo hii Zanzibar ya leo inayodai uhuru wake.
 
Haya mkuu zomba. Ila hapa koko - Swahili-English Dictionary
inaonesha wazi kuwa "koko" can mean "wild" or "unconventional".
So it can apply to anything -mbwa, binadamu, mzungu, mwarabu, kugetemeana na maana unayoitaka (wild au unconventional).
Kiswahili kinakua ati, hakipo kariakoo tu. Na sisi wa bara tumo...

Kwa hiyo baba'ko na mama'ko wakati wanakukaripia kwa kukukanya unawaita baba'ko "baba koko" na mama'ko "mama koko" ndio Kiswahili kikuavyo hivyo? au sivyo unavyotaka kusema, sasa huo u "wild" wa Dr. Harith uko wapi? unaweza uonesha kwa kuufungulia nyuzi?, ili tusiharibu mada ya Yericko Nyerere? inayo mlemea vibaya sana, maana mpaka sasa kila anazoleta anakula knock out.
 
Back
Top Bottom