Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Teh teh teh...sio mchezo...elimu ya siku hizi inafundisha na mambo ya usultani?
 
1. kabla hatujaenda mbali zaidi aliyekujibu vibaya ni nani? bado kwanza hapa turekebishe hili jambo
2. kazi ya mungu huwezi kustaafu kwa katiba ya dini gani kama katoliki kifungu gani? (kumbuka neno kustaafu ni lako siyo langu)

mkuu wewe huwezi kuingia kwenye kanisa ndani kabisa nakuwatolea matamko wakatoliki wakati huijui katiba yao.

Naomba jibu kama Dr slaa ndiye aliekujibu vibaya, vinginevo nitakuunganisha na Mohamedi said anayemchafua hayati mwalim nyerere.

Niambie kama hayo mafundisho ya kurukia watu ndio kufuzu historia za mohamedi, Dr slaa hayupo hapa jukwanii vipi atukanwe?



Mkuu mie sijui chochote kuhusu katiba ya wakatoriki.

Kujua Dr Slaa alikuwa Padri wala haitaji kwenda shule.

Ninavyojua mie Padri ni kiongozi wa kanisa kwa wakatoriki.

Kazi Mungu hata siku moja huwezi kustaafu.
 

Siku zote mie nina utaratibu wangu ukiniuliza maswali ya kipuuzi lazima nikujibu majibu ya kipuuzi.

Wewe si mateka wa Dr Slaa kwa akili yako ilivyokuwa fupi unadhani Tanzania itatawaliwa na Padre.

mkuu achana naye huyu! ... atakupandisha jazba zisizo na lazima na kukutafutia ban! .... take him as one of those JF clowns
 
Hivi huko kwenu hamfundishwi adabu ya kutaja majina ya watu waliokuzidi umri huyu mzee ni mkubwa kuliko ww usimuite mohamed sema mzee mohamed said mbona dr slaa humuiti slaaunamuita DR SLAA

Himiza watoto wa wafamilia za Kiislamu kwenda shule za mfumo wa elimu DUNIA ili kupunguza malalamimiko yakesho ya kizazi cha elimu ya kiroho!
 
Siku zote mie nina utaratibu wangu
No one asked you, matter of fact, nobody cares.
ukiniuliza maswali ya kipuuzi lazima nikujibu majibu ya kipuuzi.
Kuna possibility wewe ndio mpuzi na sio swali uliloulizwa.
Wewe si mateka wa Dr Slaa kwa akili yako ilivyokuwa fupi unadhani Tanzania itatawaliwa na Padre.
Nafikiri u kipofu hujawahi kuona nikiwachana chademu humu ndani? Lakini why do i care to elaborate? Will it make any difference to your stupid thick skull?
 
Hivi huko kwenu hamfundishwi adabu ya kutaja majina ya watu waliokuzidi umri huyu mzee ni mkubwa kuliko ww usimuite mohamed sema mzee mohamed said mbona dr slaa humuiti slaaunamuita DR SLAA


Bokoharamu Adabu ni ipi Jina Ni Mohamedi Said au Mzee Mohamed said anapoenda benki au nje ya nchi na alipokuwa anasoma

elimu yake ya juu amekuwa akitumia lipi kati ya hayo mawili?

Narejea kejeri yako

By Boko haram

waeereze mkuu
By Boko haram



Ukishangilia mchango wa Ritz je hiyo kwako Adabu? inawezekena maana tafsiri tunatofautina.


wewe nikilaza kakojoe ukalale


By BashaDido

Kama kitabu hicho umeandika kwa ung'eng'e basi na wewe umeukubali mfumo kristo ila kama umekiandika kwa kiarabu basi
kweli wewe ni mpinga mfumo kristo....mfumo kristo ni kama maji' usipoyanywa basi utayakoga.


hujamsaidia Ritz kama ulivomshagilia akikashifu imani za watu wengine, tafadhali mzee wa adabu vipi mnawatolea matamko wakatoliki?


Amweleze nani? mwenzio anakashifu imani za watu wewe unashangilia

Bokoharam ujasili wa kuwaamulia na kuwasemea wakatoliki unatoka wapi? Nyinyi yanawahusu ya kanisani?

Naomba msaidie mwenzio kutufafanulia ili kesho mkitoa tamko tujuwe nanyinyi ni sehemu ya maamuzi ya kanisa.



By Boko haram

waeereze mkuu




Neno padri ni cheo katika kanisa katoliki na kwa imani ya wakatoliki padri haruhusiwi kuoa nasikitika kwanini umwite Dr W.P slaa padri wakati anamke/mchumba vyovyote?

b) Wewe ni mwislam vipi kujishughurisha na kanisa katoliki umepewa huo usemaji lini mkuu na mamlaka ya kuteuwa mapadri?

c) Yeye amekujibu vibaya nani? unataka kutuambia Dr W. P slaa ndiye aliyekujibu vibaya kama siyo yeye vipi umshabulie yeye?

Tanzania itatawaliwa na mtanzania yoyote awe mpagani, mkritu au mwislam kama ilivo sasa kwa kuzingatia uwezo wake.

Fahamu hakuna Cheo cha rais kama padri au shekhe kwenye katiba na katiba hairuhusu upuu huo.


Naomaba ufafanuzi mkuu wangu.
 
kulalama mda wote ni ishara ya udhaifu,itafikia mahala mtaweza kulalama hata vitu vya kipuuzi,haiwezekani kila kitu ukitizame kwa jicho la udini tu
 


mkuu Sijali

Swali la kwanza nilikuuliza Nani kwazuia waislam kuwa na Mou yao, nikasema tukimaliza tutajzdili kwanini Mohamedi analalamikia MOU ya wakristo.


Kuhusu somalia tumetokea mabali agalia hapo chini tumetokea wapi, isitoshe kama wanahistoria hatuwezi kujifungia humu ndaniya Tanzania bila kuangalia mifumo mingine, ilikuwa fair nimekariri mara kadhaa baada ya kudadisi na kuijadili somalia tutaenda nchi zingine, Syria, Libya, DRc, afghanstan nk. halafu tulinganishe na hapa kwetu. Huwezi kujifunza kwamba kunamakosa au mafanikio ukiwa umejifungia ndani ya nyumba yako. Inakupasa kutoka nje ya nyumba yako, tembea kwa majirani ujifunze halafu upime ubora wa mafanikio yako au udhaifu wako kujirekebisha. Sasa utakuwa umeelewa tunaweza kuendelea tukianzia na swali la kwanza hapo juu.

karibu mkuu wangu.




By Mohamed Said
Kitabu changu kinaitwa, ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika.''

Hakina uhusiano wowote na Somalia.
Kwa ajili hii ni vigumu kwangu kujibu maswali ya Somalia na Nyerere.





Ninakuulizen somalia na nyerere kwasababu waislam wa somalia wanamatatizo makubwa ya kijamii, kisiasa, kieliemu, afya nk

Nani mchawi maana hapa kwetu kwa mujibu wa hadithi zako ni Nyerere. (Tunaongelea matatizo ya waislamu na wanaowahujumu)

Watanzania (Waislam, wakristu pia wa imani zingine na wasio amini) wanamatatizo aghalabu si makubwa kama ya wasomali.

1. Kwanini useme waislam wa Tanzania ni hujuma za nyerere na kwanini wasiwe waislam wa somalia? kunatofauti ya uislam wa somalia na ule wa tanzania?



2. Ni mfumogani unaotawala somalia na kwanin na nani tumpe lawama kwa yanayoendelea?
 
Nimessoma tena mtiririko wa maswali yako uliyomsaili Mohamed nikagundua wewe si msomi wala mwana fikra. Unauliza alidhurika vipi na kutotajwa kw wazee fulani katika historia ya uhuru! Kwani suala ni kudhurika mtu binafsi au ni kuweka sawa historia? Mimi binafsi sintadhurika chochote kama historia haitawataja watu kama Mkwawa, Mandela, Churchil, Hitler n.k. lakini historia itakuwa pungufu.
Halafu yaelkea una mentality ya zamani unapolaumu kwa nini usalama wa taifa au security wa nchi hawamchukulii hatua Mohamed! Yaani karne hii ya 21 bado unafikiria ki-polisi polisi kwa vile mtu anatoa maoni yake juu ya historia? Ama kweli wewe bado uko maguguni. wafikiri hizi bado ni zama za wajina wako Nyerere aliyeanzisha 'the first police state in Tanzania' ambayo hadi leo inaende Amka, wakati umesogea. Haidhuru sisemi kila alichokifanya ni kibaya, kwa kweli Nyerere amefanya mengi mazuri, isipokuwa demokrasia!
Na mwishowe nanukuu: 'Somalia kuna mfumo gani unaowabana wasiendelee'
Kwanza nataka kukuambia, maana katika kutokujua kwako waona Wasomali ndio wa mwisho duniani. Actually, Wasomali are some of the most intelligent Africans, na pindi matatizo yao ya vita yakiisha, wanaweza kabisa kutawala Kenya, tanzania na Uganda!
Huku Ulaya wameshikilia biashara chungu nzima kwa muda mfupi tu, kiasi internet cafe 80% za London zamilikiwa na Wasomali. Dijui unataka kutoa ushahidi gani kuwa Wasomali kwa vile ni Waislamu hawaendelei au wanakorofishana. Kama ni vita, Liberia imekuwa vitani zaidi ya miaka 20. Liberia ni 95% Wakristo, pia Sierra Leone, DRC n.k.
Usiseme kitu usichojua na wala usichanganye maudhui- hiyo ni dalili ya ukosefu wa elimu.
 

Tangu wakati ule hadi sasa nilikuwa najaribu kuangalia movie clips kwenye youtube za Sheikh Kapungu (kwa sasa sipo Tanzania, na inshaalah siku nikirud nitatafuta hizo DVD).
Pia nimepata kuangalia clips za kwako ulipokuwa ukitoa mhadhara (nadhani ni UDSM kama sijakosea)
Kwa ufupi ni kuwa kwa video za Kapungu nilizoona, naweza kuchukua maneno yako (uliyoiita historia ya TANU ambayo Nyerere aliagiza iandikwe) kuwa 'hamna kitu'. Hamna kitu kwa sababu clips zote nilizoona (kongamano la Tabora, Kongamano la Pemba, pamoja na nyingine ambayo sikutambua ilikuwa wapi), Sheikh Kapungu anasisitiza tu kuwa nafasi zote za uongozi wa nchi zimeshikwa na wakristo (75%), na waisalmu wasiojitambua (25%) ambao wanafanya kila wanaloweza kuwadhulumu waislamu na kuwapendelea wakristo wenzao. Nimemsikiliza kote aweze kutoa vielelezo kama ushahidi lakini hajafanya hata kujaribu hivyo. Nikiangalia na jinsi mimi ninavyoona hali halisi, kwa kuangalia tu eneo langu la kazi, nimeona kuwa hoja ya Sheikh Kapungu ni propaganda tupu na zisizo na msingi.

Hata hivyo, kwenye presentation yako, nimevutiwa na jinsi ulivyokuwa unaweka ushahidi wa maandiko, na zaidi wa watu uliohojiana nao ambao inaonyesha walikuwa wanajua mambo mengi. Hata hivyo, kwa maoni yangu, hujamtendea haki mtu yeyote ambaye yuko huru na hafungamani na dini yeyote;
Je, ni kwa nini katika investigations zako hukuenda kumhoji Mwl Nyerere?
Je, Ni kwa nini katika investigations zako hukuenda kumhoji Kawawa? (inawezekana uliowahoji walikuwa na information zaidi, lakini angalau hawa wangekuwa na balancing ya namna fulani

Pia, kuna mambo ambayo nilidhani ungeweza kuyahusisha katika vitabu vyako, sina uhakika kama umeyahusisha (kwa mujibu wa mihtasari ulokuwa unatoa kwenye mhadhara ule)
Mfano, kama historia ya uhuru haiwezi kukamilika bila kutajwa harakati za waislamu, je historia hiyo itakamilika bila kutajwa harakati za wakristo (kama walikuwepo)?
Unasema, baada ya uamuzi wa busara, "Nyerere aliwaleta baadhi ya waafrika waliokuwa wamesoma kushika nafasi katika TANU, na hapo ndipo waislamu mlipopoteza nguvu zenu, na hamjazirudusha tena hadi sasa". Je, ni watu gani hao aliowaleta Nyerere, na walikuwa wapi kabla ya hapo?
Kama busara iliyotumika wakati wa kura tatu iliamuliwa ili kunusuru TANU iligawanyike kati ya waislamu na wakristo, je hawa wakristo (ambao hukuwataja katika historia hapo nyuma), walikuwa na idadi gani (au %), katika TANU, na ukiacha Nyerere, wao walikuwa na mchango gani katika kuiendesha TANU. Ni kwa nini kugomea kura tatu kungewabagua waislamu peke yao, wakati naamini hata wakristo nao walikuwepo wengi wakati ule ambao hawakusoma?

Kwa maoni yako, unadhani nini kifanyike sasa kuondoa dhana ya udini inayozidi kushika kasi Tanzania? (Kama hujashuhudia kwabahati mbaya sasa imefika mahali baadhi ya wayendaji wa serikali wanatoa huduma kwa kuangalia jina la mhudumiwa. Kwa mfano, nimekutana na case kadhaa kwenye chuo ninachofanya kazi za wanafunzi kuhisi kutotendewa haki kwa sababu ya kuwa dini tofauti na walimu wao) Haya ni mambo ambayo miaka kadhaa nyuma, kwa sisi vijana hatukuwahi kuyaona (kama yalikuwepo labda kisiri sana). Lakini, ndani ya miaka miwili iliyopita kumezuka hisia kali sana za udini miongoni mwetu. Nini maoni yako, na unadhani nini kifanyike?
 

Aaah, sasa nimekufahamu. Kwa kifupi unataka kusema matatizo ya Somalia chanzo chake ni Uislamu. Kama hapo ndipo ulipofikia upeo wa fikra zako, mimi sina la kuongeza, maana katika mjadala wowote ambao ni constructive kuna sharti zake. Kwanza, pande zote mbili zipatane juu ya misingi ya kimantiki kama vile 1+1=2. Huwezi kujadili na mtu anayesema 1+1= 3!
 
The politics of naming. Hivi udni maana yake nini hasa na nani asiyekuwa mdini?
 

Heasabu ni somo jepesi sana na bado ukweli hujitofautisaha hata kama kunamkanganyiko.


2x2=4 na 2+2 =4, 3+3 = 6 lakini 3 x 3 = 9 njia pekee ya kuujuwa ukweli ni kuthibitisha (to prove why 2x2 and 2+2 have the

same solution while contradicting the solution to 3+3 and 3X3 to be different)



mraba 2x2 jibu ni 4 na ukijulisha 2+2 jibu ni 4
[TABLE="align: left"]
[TR]
[TD]1
[/TD]
[TD]2
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
2
[/TD]
[TD]
4
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]










kumjulisha itakuwa hivi


2 + 2 = 4

( 1+1 ) + (1+1) = 4



mraba wa 3 x 3 jibu 9 siyo 9 kama ilivo kwa 2 x2 na 2+2 jibu ni 4


1

2

3

2

4

6

4

8

9



Kujumlisha 3+3 jibu ni 6 siyo 9 kama ilivo hapo chini

3 + 3 = 6

(1+1+1+1) + (1+1+1) = 6


Baada ya kuona hesabu zinavyoweza kubanisha ukweli hata palipo na mkanganyiko naomba ubainishe sintofahamu yako kwa kurejea maswali yangu tumia hesabu kama ulivo anza na hata siku moja 1+1 haiwezi kuwa 3 nawewe unafahamu hivyo

vinginevo wataalamu wa hesabu waje na taaluma tofauti katika ulimwengu mwingine sio huu.


By adolay

mkuu Sijali

Swali la kwanza nilikuuliza Nani kwazuia waislam kuwa na Mou yao, nikasema tukimaliza tutajadili kwanini Mohamedi analalamikia MOU ya wakristo.


Kuhusu somalia tumetokea mabali agalia hapo chini tumetokea wapi, isitoshe kama wanahistoria hatuwezi kujifungia humu ndaniya Tanzania bila kuangalia mifumo mingine, ilikuwa fair nimekariri mara kadhaa baada ya kudadisi na kuijadili somalia tutaenda nchi zingine, Syria, Libya, DRc, afghanstan nk. halafu tulinganishe na hapa kwetu. Huwezi kujifunza kwamba kunamakosa au mafanikio ukiwa umejifungia ndani ya nyumba yako. Inakupasa kutoka nje ya nyumba yako, tembea kwa majirani ujifunze halafu upime ubora wa mafanikio yako au udhaifu wako kujirekebisha. Sasa utakuwa umeelewa tunaweza kuendelea tukianzia na swali la kwanza hapo juu. kisha tutapitia mifumo ya nchi tofauti tofauti ilikujiridhisha na mfumo wetu.


karibu mkuu wangu. kwanini ulalamike ikiwa wewe pia umepewa fursa na huitumii.
 
Mkiambiwa ukweli mnaita Uchochezi....
Hili neno limekuwa kama ngao kwenu .....
 
Ningekuwa wewe yeriko nyerere ningeomba msamaha haraka sana kwa umbumbu huu
 

Kisa cha kumhoji Nyerere ni kisa kitamu sana.
Kwanza nikufahamishe.

Swali la historia ya TANU na uhusiano wa Nyerere na Abdulwahid kwake kilikuwa kitu nyeti.
Waliokuwa karibu na Nyerere wanalijua hili.

Si unaona hapa jinsi moto unavyowaka ninapoeleza kisa cha Nyerere na Abdu Sykes?
Hii ndiyo leo 2013.

Jiulize 1970s hali ilikuwaje.

Toleo zima la African Events (London) March/April 1988 lilikusanywa kwa kuwa lilimtaja Abdulwahid Sykes
kama muasisi wa TANU.

Wakati wa kutoa medali kabla Nyerere hajastaafu urais mwaka 1985 Mwenyekiti wa Kamati ya kutunuku medali baada ya kuona Abdulwahid hayumo pamoja na wengi waliompokea Nyerere Dar es Salaam 1952 wakawanae katika kupigania uhuru alimuuliza kuhusu hilo.

Naogopa hata kukupa habari zaidi.
Maelezo ya hapo juu yakutoshe.

Nyerere alitoa medali 3979.
Mzee wangu hata mmoja akupewa.

Abdu Sykes kaja kupewa medali katika kumbukumbu ya miaka 50 ya uhuru 2012.

Tuendelee.

Jopo la kuandika historia ya TANU la Chuo cha Kivukoni kililetewa ''notes'' za Abdulwahid Sykes
kuhusu kuasisi TANU.

''Notes'' hizo zilikataliwa jopo na Abdu Sykes akaondolewa katika kitabu.

Sasa kabla ya hapo kulikuwa na mradi wa kuandika historia ya TANU mara tu baada ya uhuru.
Nyerere akahujumu mradi kwa kuwa hakupendezewa na yeye yale yaliyokuwa akiandika Abdu.

Kutokana na hayiu mimi nikawa najua kuwa somo hili ni nyeti kwa Nyerere na sikuwa kwa kweli na haja ya kutaka kumhoji.

Lakini.
Tena narudia lakini.

Mmoja wa watoto wa rafiki yake Nyerere na vilevile ni mtoto wa rafiki yake Abdu akanambia lazima nifanye
mahojiano na Nyerere na yeye akachukua jukumu la kunipangia miadi.

Nimesubiri mpaka leo hakurudi kunipa mrejesho kaambiwa nini na Nyerere.
Na mimi hadi leo sijataka kumuuliza.

Lakini tena.
Kilipotoka kitabu Nyerere alikisoma na wengi walimuomba na yeye aandike.

Humu katika ukumbi nimeeleza khabari za Prof. Haroub Othman na Nyerere kuhusu kitabu changu.
Pitia hizo nyuzi.

Kuhusu Kawawa.
Kaandikiwa vitabu viwili.

Hamna kitu.
Kimoja ''Simba wa Vita'' nimekifanyia ''review'' magazeti yote wamekataa kuchapa ''review'' yangu.

Wanaukumbi ikiwa mtapenda naweza nikakuwekeeni hapa hiyo ''review.''

Napenda kukufahamisha sikuwa natafuta ''balancing'' yoyote.
Mimi nilikuwa naandika habari za wazee wangu.

Watu ninaowajua vizuri sana tena sana.

Sikuhitaji msaada wa mtu baki kuwaeleza au kuyaeleza yale yaliyowafika
wazee wangu baada ya uhuru kupatikana mwaka 1961.

Umeuliza habari za baada ya Kura Tatu na watu waliokuwa nje ya TANU Nyerere
akawaleta kushika uongozi.

Umeniuliza kuhusu Wakristo katika harakati za kudai uhuru.
Kanisa Katoliki Jimbo la Kusini lilikuwa linawakataza Wakristo kujiunga na TANU.

Habari nyingine ulizoniuliza tuziache.

Nakuomba soma habari hizo katika kitabu changu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…