Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Sasa wewe jibu, maswali niliyokuuliza, la kwanza, hapo umeona kuna library tu iliyotajwa? Halafu rudia ile post yangu ujibu mengine.

Mwenyewe ndiyo unajiona umekuja na facts? Na logic? Kwi kwi kwi teh teh teh!

Zimesharuka? Naona matusi yamepunguwa. Kuna sadaka ya darsa nilitakiwa nikupe, nilikuwa nangoja uwe swahi nikupatie sadaka yako.
 


Samahani sana brother yericko (----),, wewe ndugu yangu, nawewe unalitambua sana hilo, mimi siwez kukuvunjia heshima hata siku moja,na nilishakuambia mimi nakushukuru sana wewe kwa mjadala wako huu, hebu jiulize bila wewe kuanzisha mjadala huu mimi ningeyajua wapi kwa undani haya makubwa anayotupa mkubwa moh said?

Bila shaka nisingejua,kwahiyo watu wengi au karibia wote tunakushukuru wewe na ndugu moh said na kuwapa heshima kubwa kwa kuanzisha mjadala huu,,
najua wewe ni verified user,,ila nakuita yericko x,kwa kuwa umeshindwa kuutanabaisha ukumbi uhusiano wako na ndugu Julius, kuwa verified user tuh haitoshi yericko,,
mwenzako moh said ni verified user ila kajieleza kwa undani kuhus yeye nasi tukamfaham,ukiachilia mbali umaarufu alionao nje ya jukwaa hili,lakin hakuacha kujitambulisha,,
yericko x haiwez kufutika hadi utapojipambanua vyema tukakuelewa,,mods wanafanya kazi yao vyema tuh hadi hapa tulipofikia kwa sasa..

Julius mtakatifu ni nani yako?
 
Mohamed Said kajishusha kutoka daraja lipi? Ana nini cha mno Mzee huyu zaidi ya kujitambulisha kwa DINI yake? Mwambieni atuletee katiba ya TAA muda mfupi kabla ya haijabadilishwa kuwa TANU. Mwambieni pia atuletee katiba ya KWANZA ya TANU.
 
Mambo yalivurugikaje? Hauoni yanavyovurugika sasa hadi damu za watu zinamwagika? Mzee wewe una TANZANIA yako nyingine kabisa moyoni!
 
Mohamed Said kajishusha kutoka daraja lipi? Ana nini cha mno Mzee huyu zaidi ya kujitambulisha kwa DINI yake? Mwambieni atuletee katiba ya TAA muda mfupi kabla ya haijabadilishwa kuwa TANU. Mwambieni pia atuletee katiba ya KWANZA ya TANU.

Kuna ubaya gani kama ukizileta wewe hizo katiba tuzijadili.

Watu wapo humu kusoma kama kuna jambo unalolijua siyo vibaya kuleweka siyo kila kitu alete Mohamed Said.

Lete vitu tusome...
 
The Big Show,
Ungeanza hivi: Mimi the big show ni fulani bin fulani wewe Yericko Mwalimu ni nani yako?
 
Kuna ubaya gani kama ukizileta wewe hizo katiba tuzijadili.

Watu wapo humu kusoma kama kuna jambo unalolijua siyo vibaya kuleweka siyo kila kitu alete Mohamed Said.

Lete vitu tusome...
Nimezikosa Ritz. Kuna baadhi ya hoja humu katiba hizi zitatusaidia sana kuzipatia majibu. Kwa kuwa mzee wetu huyu wa daraja ya juu kabisa kaandika historia ya TANU na NCHI yetu atakuwa nazo tu ingawa katika kitabu chake kile alijitahidi sana kuziepuka kuzinukuu!
 
Mambo yalivurugikaje? Hauoni yanavyovurugika sasa hadi damu za watu zinamwagika? Mzee wewe una TANZANIA yako nyingine kabisa moyoni!

Tufahamishe kwa nini Chifu Kidaha Makwaia, alifungwa na Wilbard Mwanjisi kwa nini alikimbia nchi.
 
Mohamed Said kajishusha kutoka daraja lipi? Ana nini cha mno Mzee huyu zaidi ya kujitambulisha kwa DINI yake? Mwambieni atuletee katiba ya TAA muda mfupi kabla ya haijabadilishwa kuwa TANU. Mwambieni pia atuletee katiba ya KWANZA ya TANU.

Ni sifa kubwa sana leo hii mtu akajitambulisha kwa dini yake hususan Uislaam, mimi ni Muislaam na naona raha sana kuwa mimi nimejisalimisha kwa Allah na si kwa binaadam. Labda wewe umejisalimisha kwa binaadam ndiyo unaona haya kujitambulisha kwa Dini yako.

Mohamed Said anawataja wazee wake, na ndiyo ni Waislaam walivyopigania uhuru wa nchi hii, jee, wewe hilo hulipendi?

Kuna udini zaidi ya aliouonesha Nyerere kwa kuifungia kabisa EAMWS? ni taasisi ipi ya Kikristo aliifungia? kuna udini zaidi ya kuwafunga na kuwafukuza Masheikh Wakiislaam? ni mapdri wepi na wachungaji aliwafunga? kuna udini zaidi ya yeye mwenyewe kukiri kuwa analitumikia Kanisa kwanza na Taifa baadae?

Wacha wewe.
 

Sidhani kama umezikosa hata kivukoni hazipo siyo kweli.

Vipi katiba ya TANU unayo?
 

Mkuu yaani ile ya kutoa mihadhara vyuoni au una jingine? Na kuhusu tusi ni kawaida ukileta tusi unapewa tusi. ok tuendelee!!

Hivi hujui kwamba hata wale Bithers wanaosema Obama hakuzaliwa Marekani huwa wanaitwa kutoa mihadhara kwenye vyuo? Hata Julius Malema pia amewahi kuitwa kutoa mihadhara vyuoni unachokiwa kufahamu Kutoa muhadhara chuo kikuu si kutoa lecture, you are always entitled to ur facts and words. Haimaanishi usomi, ujuzi wala ujuvi.

An individual kutoka vyuo hivyo anaweza akakualika hata wewe Zomba kwenda kuzungumza chuoni audience ikiwa yeye mwenyewe na hata na mkewe.

Lakini pia kuna mihadhara unayoalikwa na chuo au department au faculty ikiwa ni sehemu ya kujifunza ziada kutoka kwa mtunzi, inventor, exceptional scholar on that particular subject etc. Hii mara nyingi huwa na kipindi cha maswali na majibu pia. Presentation yako huwa inatumwa well in advance kwa ajili ya kutoa nafasi ya watu kuipitia na kufanya utafiti kuhusu hoja zako. Hii ni mihadhara ya kisomi na fact chcking huwa ni very important.

Mihadhara hiyo hata ya zamani inawekwa mtandaoni for public consumption Sasa kwa simulizi za mwalimu wako I betcha si aina hii ya mihadhara aliyokuwa akifanya. Muulizie akupe link yeyote ya muhadhara aliotoa chuoni ulioko mtandaoni ukionyesha presentation yake na pia maswali na majibu yake.


Kwa kukumbusha tu mfano hoja ambayo ameshindwa kuiletea ushahidi usio na mashaka mpaka leo. Pg 6 katika kitabu chake "The Rise of Muslim Militancy in Tanzania 1970 - 2000"


Narudia tena ni mpaka pale watu watakapojifunza kuwa responsible for their actions kutapatikana suluhisho la hicho kinachodaiwa dhulma. Hii tabiwa ya kutafuta wachawi mtaendelea kuburudishana tu humu jamvini.
 
Nilipata kuandikiwa barua ya kifedhuli na Meneja Utumishi
wakati nipo kazini.

Huyu bwana akinichukia sana mimi.
Kisa Uislam wangu.

Katika barua ile anataka nifikishe kwake "auntheticated copies
of all my certificates."

Huyu bwana kilichokuwa kinamchokonoa ni hasad.

Alhamdulilah vyeti vilikuwa vimepangana vyema mpaka nilivyopata
katika kozi ndogo ndogo za IT.

Kwa hakika ulikuwa msururu wa vyeti uliotakata.

Huyu bwana yeye kwa cheo simfikii kwa mbali kabisa.
Ila ana kasoro moja.

Elimu yake hafifu mno ukifanananisha na yangu.
Ila na mimi cha kustaajabisha.

Elimu nzuri cheo sina nakula vumbi.

Mimi nikawa naitembeza ile barua kwa watu nauliza kwa stizai.
"Jamani hebu nisaidieni ushauri kujibu barua hii.

Huyu bwana ana kidiploma cha Mzumbe na ni Meneja Utumishi.
Mimi nyote mnanifahamu elimu yangu na sina cheo chochote.

Badala ya yeye kujishangaa vipi ana diploma tu na ni Meneja Utumishi mimi
na vyeti vyote vile sina chochote ana vibughudhi vyeti vyangu
anavitilia shaka huenda nimegushi.

Nisaidieni ndugu zangu nijibu nini?"

Salam zikamfikia kuwa Mohamed na yeye anashangaa umefikaje hapo ulipo
kwa elimu yako finyu na yeye na vyeti vyote vile mpaka vimekutisha bado yuko ubaoni.

Hata hivyo nikajibu barua ile kwa mstari mmoja nikasema,"Hivyo vyeti vipo katika jalada langu?"

Hakunibughudhi tena kwa mambo ya vyeti.

Leo tena hapa naulizwa ID ya Library of Congress.
Siaminiki.

Huenda nimezua tu lakini nikitoa kitambulisho....
 

Hapendi kulisikia Idd Faiz Mafongo, Idd Tosiri, Abdu Kandoro, Abbas Sykes, Msume Kiate, Titi Mohamed, Dossa, Aziz.
 
Mzee Mohamed usihangaike na vitu "trivial" kama hivi hasa kwa hadhi yako ya sasa. Haya yamewakumba wengi wa DINI zote. Wewe ndie uliyekuwa unamtazama mzee huyo kwa dini yake, yeye alikuwa anakutazama kama "threat" kwa nafasi yake kwa sababu ya vyeti vyako vikali ulivyovipata ndani ya mfumokristo wa elimu bila kufelishwa!

Nisaidie zile KATIBA za TAA na TANU tafadhali.
 
Mkuu wangu Mohamed Said kati ya mabandiko yako mengi pengine hili naweza kukubaliana na wewe.Sipingi kwamba Mwl Nyerere alikuwa hakosei hapana najua alikuwa na madhaifu yake mengi kama walivyo binadamu wote.Wakuu Ritz zomba Nguruvi3 Mzee Mwanakijiji Mchambuzi Mkandara... Tazameni kwa makini hiyo list ya madaktari utabaini wote ni wagalatia sasa nauliza swali rahisi sana Mwl Nyerere alikuwa akiwagandamiza wagalatia wenzake !.

 
Hapendi kulisikia Idd Faiz Mafongo, Idd Tosiri, Abdu Kandoro, Abbas Sykes, Msume Kiate, Titi Mohamed, Dossa, Aziz.
Ritz,
Unawafahamu waweka hazina waliopita wangapi wa TANU? Kwa nini Idd Faiz pekee ndie akumbukwe? Kwa DINI yake?
 
Mambo yalivurugikaje? Hauoni yanavyovurugika sasa hadi damu za watu zinamwagika? Mzee wewe una TANZANIA yako nyingine kabisa moyoni!

Wakati wa nyerere mambo yalivurugika mpaka jeshi liliasi, zikatokea vurugu maarufu "tarehe 20" au hujuwi hilo? njaa tupu mpaka watu tukawa tunapanga foleni ili tupate sukari kilo moja kwa kaya kwa wiki nzima, kila mmoja hoi bina taabani
Neema za sasa ni kama ndoto na wakati wa Nyerere. Wadanganye wasiokuwepo wakati huo. Sokoni pamekauka, wakulima hawaruhusiwi kusafirisha hata nyanya zao, mageti kila barabara kuu za mikoani eti ya kuzuwia kipindupindu. Ukibeba kikapu mgambo wanakusimamisha kukuuliza umebeba nini, wakikuta una sukari zaidi ya kilo moja lazima ujieleze. Na rushwa hizi za wazi wazi ndio zikaanzia hapo. Unataka kusema nini wewe?

Wadanganye wasiokuwepo wakati huo au wewe umedanganywa kwa kuwa hukuwepo ukadanganyika. Kaeni muusome ukweli kwa Mohamed Said, wacheni kudanganywa na kuburuzwa kama misukule.
 
Ritz,
Unawafahamu waweka hazina waliopita wangapi wa TANU? Kwa nini Idd Faiz pekee ndie akumbukwe? Kwa DINI yake?

Huyo ndiye wa kwanza na ndiye alikuwa mweka hazina wa Jammiatul Islamiya na ndiye aliyefanya safari ya kwenda Tanga kuzileta fedha zilizomuwezesha nyerere kusafirishwa kwenda New York, bado tu huuoni umuhimu wake?
 

Nimekusoma.

Sina haja ya kubishana hayo mengine kwani ni vitu vidogo sana wala
sioni fahari kusema kuwa niliingia darasani kusomesha.

Ila nitakujibu hilo jengine la mwisho.

Hapa nyumbani hali si nzuri.
Ukweli umedhihiri.

Kuna lugha imeeanza kutumika ya kufanya mazungumzo.
Ushahidi wa dhulma upo na umefikishwa serikalini.
 

Friendly fire.

Eti katika yote hayo ndiyo unakubali kwa kuwa ni wagalatia. Unanchekesha - Courtesy FaizaFoxy
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…