Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Mkuu WildCard
umeeleza vizuri sana nadhani Hapa kuna Tatizo la uelewa au ni Makusudi tu.,

Nyerere alishalizungumza mara nyingi hilo la Waislamu kuachwa Nyuma kielimu na ndio kisa cha kuzitaifiahsa shule na mahospital ya kanisa ili viwe vya umma

Watu wanashindwaje kujua Mzee Mwinyi ndiye aliyerudisha "MfumoKristu" Tanzania, yeye ndiye aliyerudisha shule na Mahospital kwa makanisa,
na ndipo Nyerere alipokuwa anasema baada ya kuchagua mabaya yake na Kuyarekebisha basi wanayachukua yale mema na kuyafanyia marekebisho
 

Yote hayo uliyosema hakuna aliyekupinga Nyerere kalelewa na Padre mpaka katafutiwa chuo kwa kazi maalum athari za zake ndiyo hizi alizotuachia. Mbona maswali yangu unayapotezea.
 
WildCard,

Unaweza kututajia mapungufu ya Nyerere wakati wa utawala wake.
 
Last edited by a moderator:

Hapa unamsemea Nyerere wakati umekana kumsemea umeeleza jinsi alivyopambana na Waislam. Nikakuliza vipi alivyopambana na Oscar Kambona na Chifu Makwaia, ukajibu huwezi kumsemea...ha haa haa.
 
WildCard,

Unaweza kututajia mapungufu ya Nyerere wakati wa utawala wake.
Mwalimu ni mpana sana kumzungumzia. Mapungufu yake mengi aliyakiri na baadhi aliyarekebisha akiwa madarakani. Mengine yalimshinda kabisa kurekebisha kwa mfano hili la MUUNGANO. Angefuata ushauri wa Abeid Amani Karume leo hii tusingekuwa na Muungano wa matatizo kama huu.

Jingine aliwaamini sana baadhi ya watendaji wake. Akadhani wanamwelewa. Hawataiibia NCHI kama yeye alivyokuwa. Akajua UONGOZI ni dhamana. Akadhani IKULU biashara haipo. Akadhani wote wanachukia rushwa, ufisadi, wizi, na madhila mengine kama hayo. Alikosea sana.

Jingine hakutuachia taasisi na vyombo vya dola IMARA. Akadhani chama chake CCM kinatosha. Kitafanya mema na kukemea maovu. Akawa ame-"bugi" kwelikweli. Wajanja wakaivamia CCM haraka. Wakaitoboatoboa kila mahali. Ghafla tukawa na makundi na watu wenye nguvu kwelikweli kuliko CCM yenyewe.

Mapungufu ya Mwalimu mengi yalisababishwa na UADILIFU na UCHA MUNGU wake. Sheria kali kabisa zilikuwepo lakini hakuzitumia sana. Waliohukumiwa wanyongwe wengi tulibaki nao.
 
Hapa unamsemea Nyerere wakati umekana kumsemea umeeleza jinsi alivyopambana na Waislam. Nikakuliza vipi alivyopambana na Oscar Kambona na Chifu Makwaia, ukajibu huwezi kumsemea...ha haa haa.
Umenichanganya. Nilidhani ulitaka nimsemee OK. Lakini simsemei Mwalimu. Najaribu kueleza ninachokifahamu kuhusu yeye. Mwalimu amefariki hanifahamu kabisa.
 

Pamoja kuwa mpana lakini bado ana sifa ya mwanadamu lazima awe na mapungufu.

Vipi suala la uchumi na siasa zake?
 
Pamoja kuwa mpana lakini bado ana sifa ya mwanadamu lazima awe na mapungufu.

Vipi suala la uchumi na siasa zake?
Sina utaalam hata chembe kuhusu UCHUMI. Nimeanza shule ya msingi enzi za utawala wake nikaenda hadi chuoni bila kukopa wala kulipa karo. Sera hii peke yake ndio iliyotugusa watoto wa masikini wa nchi hii. Nimemaliza chuo nikakuta AJIRA inanitafuta sio mimi natafuta ajira. Wakati ule ilikuwa ni vigumu kupata chumba cha kupanga kuliko ajira!

Nilianza kumpenda Mwalimu kwa sababu hizo. Aliwezaje kuzitekeleza sera hizi mimi sijui.

Kumbuka pia kwenda shule enzi hizo ilibidi tukamatwe kwa nguvu toka kwa wazazi wetu. Hali hii iliwakumba watoto wa jamii za wafugaji na hata Waislam hasa kwa watoto wa kike.
 
Sijawahi kumsemea OK, Ritz. Yupo mke na binti yake waongeaji wazuri tu watafute hao. Sitaki kuwa kama mzee wetu Mohamed na simulizi za wazee wake na DINI yao!

WC,

Hakika huwezi kuwa na hata kama utatamani huwezi kuwa kama mimi.

Kwani we baba yako alikutana na Nyerere 1952 nyumbani kwa Abdu Sykes?

Babu yako kapigania uhuru wa Tanganyika au alikuwa mwanachama wa
African Association, Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na mwanachama
wa TANU?

Babu yako ana historia yoyote ile ambayo inaweza ikaandikwa na watu
wakasoma?

Babu yangu Salum Abdallah aliongoza General Strike ya mwaka 1947.
Babu yangu akishiriki mikutano yote ya siri ya kuasisi TANU Tabora 1953/54.

Babu yangu kaasisi Tanganyika Railway African Union 1955 akiwa rais.
Babu yangu kaongoza mgomo wa Relwe wa 1960 uliodumu siku 82.

Mgomo kama huu haujapata kutokea ndio uliomtia hofu Nyerere aogope
hapo baadae kukutana katika utawala wake na mtu kama babu yangu.

Mtu aliyewapigisha magoti Waingereza wakasalimu amri wakamwita babu
yangu kwenye meza ya mazungumzo na Waafrika wakapata haki zao zote.

Babu yangu alitungiwa mwimbo ''Ndege Mwema'' kwa ushujaa na ukarimu wake.

Vipi ikupitikie kuwa wewe unaweza kujifananisha na mimi?

Au babu yako kapata kugombana na kupingana na Nyerere katika
mambo ya utawala wa nchi?

Babu yako kawekwa kizuizini na Nyerere kama alivyowekwa babu yangu?

Sasa wewe hiyo fikra na ujasiri wa kutaka kujifananisha na mie unakujaje?

Unadhani bila ya historia hii mie ningekuwa na cha kuandikia kitabu?
Unadhani hizi view 40,000 and counting wako humu kukusoma wewe?

Usifanye haraka ya kumtaja Mohamed Said.
Jitulize na fikiri kwanza.

Mie siko humu kufanya mchezo.

Niko humu kueleza yale walofanya wazee wangu na nikiona unakejeli juhudi zao kwa
hakika nakereka.
 
Ritz
Mimi vijana wangu wawili wamemaliza degree ya kwanza mwaka 2010 na mwingine 2009. Wote mpaka sasa hawana kazi.
Wa kwangu wakikosa kazi, tunailamu serikali kwa kutokuwa na ajira za kutosha, na tunalaumu vijana wenyewe kushindwa kujiajiri.
Lakini wewe, wadogo zako wakikosa kazi, ni lazima tu wamenyimwa kwababu ni waislam si ndio?
Hapa nilipo mimi nipo katika nafasi ya kuajiri. Na katika miaka 5 nimeajiri waislam wanne waliokuwa wame-qualify. Nashindwa kabisa kukuelewa. Nilifikiri upo tofauti kidogo... Dah!
 
Last edited by a moderator:
Hee Mohamed, kumbe upo katika mashindano na si Ilm, ndiyo maana ukibanwa unakimbia maswali au hoja! Sisi tupo kwenye ilm sheikh maana kama ni shindano la! ndugu yangu labda lifanyikie ICU unapouguza majeraha.

Mohamed tutashindana nini wakati wengine tunajua Tanganyika as whole wewe unajua Tanganyika ni Tandamti, Kipata na Narumg'ombe.

Sheikh, kila ninachokuonyesha umeshindwa kukikanusha! umebaki kueleza wewe ni nani, who cares!
Mohamed uzi huu umekuvua msuli.

Mohamed unaidanganya jamii sana!Unawadanganya vijana wa kiislam na kuwafanya wawe wavivu wa kufikiri. Unawanajisi waislam, haifai sheikh! waambie watu ukweli si kuwaaambia ili uuze matole ya vitabu.

Tafuta suluhu ya matatizo, uchochezi si suluhu, chuki si suluhu wala farki haina faida.
Miaka 15 unahubiri uzushi na watu wanasoma halafu ''wakielewa'' na kujaa jazba wanakwenda kuwaambia watoto wasisome chemistry, maths na history bali waende kusikiliza kesi ya Ponda asiyejua mlango wa darasa.

Wakitoka hapo wazazi wanalalamikia NECTA! Mohamed unajua hili lakini ili uuze vitabu unafanya jamii kuwa zombie, Mohamed, Mo Muogope Mwenyezi mungu S.W.T.
Kitendo cha kushindwa kutetea hoja za kitabu chako peke yake ni dhalili kubwa sana.
Kwa atumieye chembe ndogo ya akili, hakika akisoma kitabu chako na kuhusisha na Uislam lazima ajisikie fadhaa!

Kama yupo atakayeandika kitabu ni kwasababu ya kupanua ilm si kushindana na uzushi.
Tuambie Malima alimalizana vipi na Nyerere? Othaman alijibiwa vipi na Nyerere?

Halafu ukienda Tambaza mosque au Maamur, Sheikh Mwinyi huja pale kila mara, muulize Mapinduzi ya ZNZ akufundishe siyo usubiri yatokee ukimbie kuweka kauli midomoni mwa walio mbele ya haki.

Jumbe yupo na Nasor Moyo pia waulize wakingali na kauli, ni bidaa kumwekea maneno marhum.
Marhum anaombewa mswamaha kwani yupo mbele ya haki vipi wewe upite mitaa,, miji na vijiji ukiwadhalilisha wasio na kauli.Sheik ibn Semtungo, muogope Allah!
 

CR,

Huna lingine ila ''inasemekana?''
Lete na mengine tufanye mnakasha.

Hilo moja halikidhi haja.
 
Mzee Mohamed,
Waliofanyiwa haya na Mwalimu ni wazee wako sio wewe. Wewe ulikuwa "toddler" mwaka 1953-54 wakati wa "transition" kutoka TAA kwenda TANU. Unavyosimulia ni zaidi ya Mwalimu aliyekuwepo! Miaka ile ya sitini ulikuwa sekondari na chuoni wakati wazee wako hawa wanapigania mfumoIslam uwekwe nchi hii. Hatutofautiani sana. Kuna mengi tunayafahamu na sisi ambayo wewe hauyajui. Tanganyika yako wewe ni hiyo ya Kipata kuelekea New Street. Wapigania uhuru wako wewe ni hao wazee wako wa Kariakoo. Wengi wao wakiwa ni WALOWEZI na WAKIMBIZI. Kiungo chako wewe na wao ni UISLAMU tu.
 

Nguruvi,

Nilidhani unakuja na mapendekezo ya kitabu chako cha ''kupanua ilm.''
Sijibu kila jambo hili ni maarufu.

Wala sisemi kila kitu.

Kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar weka uzi tumwage mchele kwenye kuku
wengi.

Zomba hizi huziita ofa.
Na mtu anapokuwa haichukui anakasirika.

Ati anasema inakosesha watu manufaa.
 

WC.

Umesema kweli.
Hayo yote wamefanya wazee wangu.

Nakubali na wewe yako mengi unayajua ambayo mimi
siyajui.

Kitu kimoja umenikumbusha mbali.

Hakika dunia yangu ilikuwa Kipata na New Street na
gramafoni niliyokuwa nikisikiliza nyimbo za Salum Abdallah
na Septet Habanero ya Cuba.

Nje ya hapo labda nikipanda basi la gorofa la DMT.
 
Ukweli ukidhihiri,haki huchukua nafasi yake,

Heko mohammed said kwa kuupambanua ukweli huo,mungu akubariki sana.
 
Mie siko humu kufanya mchezo.

Niko humu kueleza yale walofanya wazee wangu na nikiona unakejeli juhudi zao kwa
hakika nakereka.

Mzee Mohamed,
Wewe umemkejeli Mwalimu na kumbambikia tuhuma ngapi tena kwa vitabu na mihadhara? Unaweza kuwalinganisha nini wazee wako hawa na Mwalimu? Elimu? Uzalendo? Mchango wao kwa uhuru wa Tanganyika? Kuiunda Tanzania? Acha kujikweza mzee wewe.
 
Mohamed,
Labda unaweza kutufafanulia zaidi. Ikiwa Waislamu takriban wote walisahau vyama vyao wakampigia Muislamu mwenzao Kikwete, iweje kura za Kikwete zipungue kutoka asilimia 80 hadi 60? Hilo unalielezaje?


je Idadi ya waliopiga kura 2005 ni sawa na 2010

ukijuwa tofauti hiyo ndio utajuwa kwann zilipungua hadi kufika 60%
 

WC,

Weka kejeli zangu kwa Nyerere tuzijadili.
Hii ya kujikweza tuifatutie muda.

Nimekupa yale kukuonyesha kuwa sisi tunayo
ya kueleza katika historia ya nchi hii usijifananishenasi.
 
je Idadi ya waliopiga kura 2005 ni sawa na 2010

ukijuwa tofauti hiyo ndio utajuwa kwann zilipungua hadi kufika 60%

Ngoja tumalize moja kwanza.
Kisha tuingie huko.

Kuwa na subra ndugu yangu ili baadae
tuwe na mnakasha mzuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…