Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Z,
Hiyo amani haipo tena.

Pitia nyuzi katika mnakasha huu toka tulipoanza
na maaskofu hadi uchochezi wa Mohamed Said.

Watu zaidi ya 40,000 wanafuatilia.
Si bure.

Kuna jambo zito.
sijui kwa huko mlipo, sisi huku Mlalo Lushoto amani imejaa tele, tunaheshimiana waislam kwa wakristo, tunaoleana, tunaalikana kwenye shughuli mbali mbali, tunazikana, kwa ufupi ukoo wetu umegawanyika kuwili, (waislam + wakristo)
tunarithiana bila kuangalia dini zetu, ndivyo tulivyo.
 
Z,

Jirani yako akikwambia ameona nyoka akiingia uani kwako
jibu lake haliwezi kuwa "mimi sijamuona."

Utamtafuta nyoka huku una gongo mkononi.
Hii ndiyo busara.
hapana, lazima nitamuuliza ni wa rangi gani, kama ni mweusi najua hana madhara sana kwetu ila nitamtafuta nimuue...
lakini pia kama jirani yangu ana chuki na mimi naweza sema labda kaniletea nyoka uani kwangu.
 
Z,

Jirani yako akikwambia ameona nyoka akiingia uani kwako
jibu lake haliwezi kuwa "mimi sijamuona."

Utamtafuta nyoka huku una gongo mkononi.
Hii ndiyo busara.
Mfano wako hausimami katika haya, labda kuanzia leo uukane utanzania nakujivika umangani mkuu.
 
sawa mkuu, nakutakia kheri katika hiyo dhima yako,
Mwenyezi mungu akupe wepesi na busara ya kutosha ya kuelimisha hao wanaohitaji hiyo ilimu bila kuchukiana na kuwekeana uadui kwani adui yetu sisi ni Shetani.

Z,

Wala hili si jambo la kumtakia mtu kheri.
Wala si jambo la "mtu kutaka elimu."

Dhulma imeangamiza wengi duniani.

Si kitu cha kufanyiwa istizai kuwa mimi
naishi na Waislam sina tatizonao.

Soma historia ushangazwe na yalotokea
Rwanda.

Wameijua hatari ya fitna ya dhulma kwa njia
ngumu sana.

Waislam wanatahadharisha haya kwa kuwa dalili
sasa ziko wazi.

Hii siyo ile Tanganyika ya Mufti Sheikh Hassan bin
Amir anasimama bega kwa bega na Nyerere dhidi
ya ukoloni wa Waingereza.

Hii ni nchi nyingine kabisa sasa...
Au hujasikia Waislam wakilani...Laanatullah...

"Lana ya Allah imuangukie..."

Unamjua huyu anelaniwa na msikiti mzima tena
kwenye vipaza sauti?

Hukuwa unajua haya na bado unasema unaishi
vyema na Waislam.

Usijidanganye...

Kwanini Waislam wamesema tunataka tuhesabiwe
kwa dini zetu...

Mwanza Wakristo wanakataa kula nyama iliyochinjwa
na Waislam...

Hizi si dalili nzuri.
Mwanzo wa mvua ni mawingu.

Mimi naikumbusha serikali na wananchi wenzangu kuwa
kilichotufikisha hapa ni dhulma...

Tusipuuze.

Nimekueleza haya kutoka dhati ya nafsi yangu ili ujue simo
humu kujiburudisha.

Ili wewe upate kunifahamu na unithamini ukija na mimi kwenye
mjadala ujue unakabiliana na mtu asiyefanya utani.

Ndiyo maana unaona natumia jina langu halisi ili endapo serikali
itataka ushahidi wa dhulma dhidi ya Waislam wasipate tabu kunipata.
 
Wala hili si jambo la kumtakia mtu kheri.
Wala si jambo la "mtu kutaka elimu."
hapa sijakuelewa mkuu wangu....

.......Dhulma imeangamiza wengi duniani.....
Misri? Ivory Coast? Tunisia? Iraq? Iran? Pakistani? Somalia? Lebanon?

...Si kitu cha kufanyiwa istizai kuwa mimi
naishi na Waislam sina tatizonae....
ni swala ambalo huna haja ya kuliamini, hata jina langu ni la kiislam japo mimi mkristo, nakuomba ufike Lushoto uone jinsi watu walivyooleana ama koo zilivyogawanyika (wakristo na waislam).

Soma historia ushangazwe na yalotokea
Rwanda.

Wameijua hatari ya fitna ya dhulma kwa njia
ngumu sana.
hapa nahitaji kupata ilmu kidogo juu ya yaliyotokea Lwanda, swala kule ni dhulma za kidini au Ukabila?


loh. .

hii inatokana na udhaifu wa serikali wala halina ubishi
 
Umeshindwa kulithibitishia jukwaa hili hiyo dhulma kwa waislamu, je huko utaithibitishaje ikiwa watakutaka uthibitishe?
 



Z,

Ukitaka mjadala mzuri tutulie na nchi yetu hivyo tutafaidika.

Yalowasibu Rwanda yanafanana na yanayotunyemelea sie.

Hapa ni dini.
Rwanda ni kabila.

Ubaguzi wa aina yoyote unaangamiza.
 
kaka ya said nimefuatilia sana mada hii,naomba unisaidie kwa kunijibu haya.
1.baada ya uhuru kama wewe ungepata nafasi ya kuwa rais ungefanya maamuzi gani katika elimu tofauti na alivyofanya nyerere(zingatia uwepo wa shule na vyuo vinavyomilikiwa na wakristo na uwezo mdogo wa serikali kipindi hicho kujenga shule mpya)
2.baada ya uhuru kama wewe ungepata nafasi ya kuwa rais ungefanya maamuzi gani katika afya tofauti na alivyofanya nyerere(zingatia uwepo wa hospitali zinavyomilikiwa na wakristo zilizokuwa zinatoa huduma kwa wote bila upendeleo(mf kcmc) na pia kutokuwepo na hospitali za serikali maeneo mengi ya wilaya).
3.Ungewafanyia nini waislamu katika elimu
4.Ungewafanyia nini wazee wa gerezani?
5.Pengo la elimu lililokuwepo kati ya wakristo,waislam na wasio wakristo au waislam ungefanya nini katika hili?
ningependa unijibu katika njia ya kunielimisha na pia umalizie na nini unachoamini kifanyike sasa kurekebisha hicho unachoamin.
thanx
 



Z

Jitahidini kudumisha huo udugu.
Msiruhusu fitna ya dhulma kuwatenganisha.

Asinyimwe mtu haki yake kwa ajili ya dini yake.

Mue mfano tuje kuiga kwenu.

Mengine ulosema sitayasemea kama hayo ya kurithiana
na ndoa...

Huenda hayo ndiyo siri ya "mafanikio" ya Lushoto.
 
Z,

Ukitaka mjadala mzuri tutulie na nchi yetu hivyo tutafaidika.

Yalowasibu Rwanda yanafanana na yanayotunyemelea sie.

Hapa ni dini.
Rwanda ni kabila.


Ubaguzi wa aina yoyote unaangamiza.
nani analeta huo udini mkuu?
 

Ningedumisha uadilifu.
 
Z

Jitahidini kudumisha huo udugu.
Msiruhusu fitna ya dhulma kuwatenganisha.

Asinyimwe mtu haki yake kwa ajili ya dini yake.

Mue mfano tuje kuiga kwenu.
aamina! na kwa hakika Mwenyezi Mungu atalisimamia.
maana kama ni maradhi twaugua sote na pia twapata tiba sawa, kama ni ilimu twasoma shule sawa na huduma ya maradhi na chakula na nguo kila mtu hupata kulingana na juhudi zake binafsi za kufanya kazi kwa bidii, na kama ni kazi kila mtu hupata kazi kulingana na sifa kuu ya elimu na ujuzi alionao.
 
Kiti ni kimoja Mohamed Said,anataka kumuweka kiti hicho hicho,Saidi cha Mwenyewe,Mshume Kiatu na hata wazee wa mla kodi za nyumba zomba.Kwa mila za pwani hata mkeka wanaweza kalia,lakini MS anangangania kiti-sasa tutafika????
 
Last edited by a moderator:
Ningedumisha uadilifu.
Kama ule wa Mwalimu au zaidi? Waambie Waislam kama unawapenda kweli waachane kabisa na UHAFIDHINA wa dini yao. Hata Wakatoliki walikuwa wahafidhina sana mwanzoni wakidhani kilichoandikwa kwenye Biblia ndio basi tena. Kisa cha Galileo na Wakatoliki uliwahi kukisikia?
 
mkuu embu tumegee mistari miwili tu.
 
mkuu embu tumegee mistari miwili tu.


Galileo's championing of heliocentrism was controversial within his lifetime, when most subscribed to either geocentrism or the Tychonic system.[SUP][9][/SUP] He met with opposition from astronomers, who doubted heliocentrism due to the absence of an observed stellar parallax.[SUP][9][/SUP] The matter was investigated by the Roman Inquisition in 1615, and they concluded that it could be supported as only a possibility, not an established fact.[SUP][9][/SUP][SUP][10][/SUP] Galileo later defended his views in Dialogue Concerning the Two Chief World Systems, which appeared to attack Pope Urban VIII and thus alienated him and the Jesuits, who had both supported Galileo up until this point.[SUP][9][/SUP] He was tried by the Inquisition, found "vehemently suspect of heresy", forced to recant, and spent the rest of his life under house arrest.[SUP][11][/SUP][SUP][12][/SUP] It was while Galileo was under house arrest that he wrote one of his finest works, Two New Sciences, in which he summarised the work he had done some forty years earlier, on the two sciences now called kinematics and strength of materials.[SUP][13][/SUP][SUP][14]
Nimeona niku-pastie kutoka wikipedia.[/SUP]
 
sawa mkuu, nakutakia kheri katika hiyo dhima yako,
Mwenyezi mungu akupe wepesi na busara ya kutosha ya kuelimisha hao wanaohitaji hiyo ilimu bila kuchukiana na kuwekeana uadui kwani adui yetu sisi ni Shetani.

Wala usiogope chochote Mtanzania mwenzetu! hakuna atakae kudhuru! Wewe ungana na Waislamu kudai haki TZ na amini usiamini atakae kulinda wewe na vyako si mwingine ni Muislamu! sababu sisi ni watu wa amani na mfano ni pale mauaji ya kimbari Rwanda yalipotokea, Wakristo wa kitusi walipokimbilia Makanisani kuokoa maisha yao hakuna alietoka hai! wote walichomwa moto! lakini Watusi hao hao walipokimbilia Misikitini ambayo ilikuwa ya Waislamu wengi wa Hutu walipata uslama wa kutosha!

Hivyo usiogope na Mohamed Saidi hajengi chuki miongoni mwa wa TZ bali anajaribu kutukumbusha jukumu letu la kuondoa maovu, dhuluma, uadilifu mbaya nk! Kama atanyamaza na kufumbia macho tu, basi bila shaka amani na usalama wetu hautakuwa wa kudumu kwa sababu nchi itaangamia kwa kukosa maendeleo na sababu ni zaidi ya nusu ya idadi ya raia kukosa elimu!

Mimi na wewe tushikamane kuungoa huu Mfumo kristo TZ na hapo ndipo tutapoweza kuishi kwa amani ya kweli! na mfumo kristo hauwahusu nyie wakristo wa kawaida ambao mko wengi sana bali mfumo kristo unawahusu Vigogo Makanisani, Serikali, Chama tawala, baadhi ya vyama pinzani na washirika wao Toka Ulaya na Marekani!
 

Amani sana ZUBEDA.,

AMANI SANA..
 
Ndugu yangu hakuna muislamu anaedhulumiwa katika ardhi ya Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…