sawa mkuu, nakutakia kheri katika hiyo dhima yako,
Mwenyezi mungu akupe wepesi na busara ya kutosha ya kuelimisha hao wanaohitaji hiyo ilimu bila kuchukiana na kuwekeana uadui kwani adui yetu sisi ni Shetani.
Z,
Wala hili si jambo la kumtakia mtu kheri.
Wala si jambo la "mtu kutaka elimu."
Dhulma imeangamiza wengi duniani.
Si kitu cha kufanyiwa istizai kuwa mimi
naishi na Waislam sina tatizonao.
Soma historia ushangazwe na yalotokea
Rwanda.
Wameijua hatari ya fitna ya dhulma kwa njia
ngumu sana.
Waislam wanatahadharisha haya kwa kuwa dalili
sasa ziko wazi.
Hii siyo ile Tanganyika ya Mufti Sheikh Hassan bin
Amir anasimama bega kwa bega na Nyerere dhidi
ya ukoloni wa Waingereza.
Hii ni nchi nyingine kabisa sasa...
Au hujasikia Waislam wakilani...Laanatullah...
"Lana ya Allah imuangukie..."
Unamjua huyu anelaniwa na msikiti mzima tena
kwenye vipaza sauti?
Hukuwa unajua haya na bado unasema unaishi
vyema na Waislam.
Usijidanganye...
Kwanini Waislam wamesema tunataka tuhesabiwe
kwa dini zetu...
Mwanza Wakristo wanakataa kula nyama iliyochinjwa
na Waislam...
Hizi si dalili nzuri.
Mwanzo wa mvua ni mawingu.
Mimi naikumbusha serikali na wananchi wenzangu kuwa
kilichotufikisha hapa ni dhulma...
Tusipuuze.
Nimekueleza haya kutoka dhati ya nafsi yangu ili ujue simo
humu kujiburudisha.
Ili wewe upate kunifahamu na unithamini ukija na mimi kwenye
mjadala ujue unakabiliana na mtu asiyefanya utani.
Ndiyo maana unaona natumia jina langu halisi ili endapo serikali
itataka ushahidi wa dhulma dhidi ya Waislam wasipate tabu kunipata.