Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

zomba na Ritz, mnazidi tu kumuumbua huyo mchochezi na ngano zake...ningekuwa yeye, ningewafunga LUKU, mnamharibia.

Povu la nini? Umekasirika kutajiwa uchochezi wa Lwambano? Kwi kwi kwi teh teh teh!
 


Childish mind..
Dont you think that its a right time now for you to pay a visit to your bed?
 
zomba na Ritz, mnazidi tu kumuumbua huyo mchochezi na ngano zake...ningekuwa yeye, ningewafunga LUKU, mnamharibia.

Kizuri hakiwi kizuri kama kuna kizuri zaidi.
 
Last edited by a moderator:


Kimbia haraka,nenda RIVER SIDE pale ubungo,mzee wa upako ana kusibiri akakutoe MAPEPO..
 
Childish mind..
Dont you think that its a right time now for you to pay a visit to your bed?

Yaah of coz! Now am going to my bed cons siwezi kupoteza usingiziwangu kwa kujibishana na wapuuzi kama nyinyi.

Pia napenda kurudia tena na tena mfumo kristo utawatawaleni ninyi na vizazi vyenu vyote hadi mnaingia kaburini.
 
Kulikua na kundi la wanasayansi wapatao mia moja kutoka ulimwengu mzima walikua wana mpinga mwanasayansi nguli, Albert Eistein kua anafaya Monkey science kama kejeli. Katika kuwajibu aliwaambia, ''Why a hundred scientist, only one is enough to prove me wrong'' sasa kelele za nini just prove him wrong. Haya toeni data mbadala au ombeni mdahalo nae Ndugu Mohammed Said kama kweli nyie mnazo hoja za kushindana nae.

Hebu tutajieni askofu, au padre au sister au mchungaji walioshiriki kudai uhuru wa nchi hii. Mimi ninachojua baada ya waislamu kuleta uhuru wao wakatumia kanuni za kimafia kuwasaliti waislamu ikiwemo na nyerere mwenyewe. Au mnataka ushahidi na hili. Dr John C. Sivalon na wengineo sio waislamu, ujasiri ule wa kutueleza ukweli waliupata wapi?


 
 
mods najua mpo na mtatenda haki
 

Mkuu wangu; swali hili liko at the core of the allegations za mzee wetu huyu. Hakuna kiongozi mwenye hisia za ubora wa dini, rangi, au nasaba yake ambaye hajawahi kuzisema hadharani na watu wakajua. Hitler alitukuza rangi yake -siyo sirini bali hadharani kabisa; Kina Milosevic walitukuza nasaba yao ya Kiserbia dhidi ya non-Serbs wa Serbia na Bosnia.. Idi Amin alitukuza Uafrika wake dhidi ya watu wengine wote hawa walifanya hadharani. Kaburu Botha na wabaguzi wa Deep South huko Marekani walitukuza rangi zao hadharani na haikuwa kificho.

Hakuna mtu yeyote kiongozi aliyeetukuza dini au rangi yake ambaye alifanya hivyo kwa kificho. Ahmedinajad na wenzie wote hawana siri. Hisia hii ya ubora haifikichiki kwa aliyonayo. Hata hapa unaweza kuona watu wanavyozungumza kwa ubora (superiority complex) inayotokana na dini.

Sasa, Nyerere kama kweli - NA TUMPE BENEFIT OF THE DOUBT Bw. Said...basi asingeweza kujificha kwa miaka zaidi ya 25 aliyokuwa akiongoza (miaka 31 tangu achukue uongozi wa TANU). Kungekuwepo angalau na barua, hotuba, mazungumzo ya sirini ambapo Nyerere ameusema vibaya Uislamu, au Waislamu.

Kama kuna mtu kasoma maandishi ya Bw. Said na mimi nimesoma maandishi yake mengi mno - HAKUNA MAHALI HATA PAMOJA - ambapo Bw. Said anamnukuu mzee wake YEYOTE (siyo Abdul, Rashad Ali, Dossa, Mshume Kiyate n.k) akisema amewahi kumsikia Nyerere akiutukana Uislamu, akiwakejeli Waislamu au akisema neno lolote baya kuhusu vyote viwili. HAKUNA.

Lakini jambo la pilli ambalo huwezi kuliona ni ushahidi wa aina yoyote wa agizo, amri, maelekezo yoyote ya Baba wa Taifa kwa mtu yeyote ambayo yalihusiana na kutowatendea haki Waislamu kwa misingi yoyote ile ya kidini.

Lakini la tatu ambalo kihistoria ni zito zaidi ni kuwa - HAKUNA jambo lolote ambalo Bw. Said anadai liliwatokea wazee wake wa Kiislamu ambalo halikuwatokea wazee wengine wasio Waislamu. Mfano mzuri ni uamuzi wa Nyerere kuvunja Baraza la Machifu ambao tunaweza kusema waliwakilisha watu wengi zaidi kuliko Waislamu na Wakristu. Watu wa jadi wangeweza (labda kwa haki) kudai kuwa Nyerere anawabagua katika uongozi na kuthibitisha hilo alivunja Baraza la Machifu.

Chief David Kidaha Makwaia kwa mfano alitupwa Tunduru. Kitu ambacho labda wengi hawakumbuki ni kuwa alizaliwa katika Uislamu na kukulia katika Uislamu. Alikuja kuingia ukatoliki baadaye ukubwani. Ukweli ni kuwa Waingereza walimfikiria Makwaia kama Rais wa kwanza wa Tanganyika kuliko Nyerere. Huyu amekufa juzi tu hapa (2007) lakini kwa vile hakuwa tena Muislamu basi hakumbukwi. Ana historia yake nchini lakini ni wachache sana wanajua baadhi ya mambo ambayo alifanikiwa kuyafanya.

Sasa Bw. Said ameamua kuimega historia na kutengeneza "sub-history' ambayo haifungi na matukio mengine ya historia. Anaangalia kwa jicho moja tu nalo ni la Uislamu. Sasa hili ni zuri kuvutia hisia lakini kwa mtu mwenye hekima ni lazima wahoji. Mifano miwili inatosha hapa:

Maasi ya Jeshi ya 1964 yalisababisha kamatakamata itokee; miongoni mwa watu waliokamatwa walikuwa ni mashehe na wengine wapinzani wa muda mrefu wa Mwalimu kuanzia 1958 na kabla. Sasa kama ingekuwa ni kamata kamata ya Waislamu tu basi hoja ni rahisi kujengwa lakini ni kweli walikamatwa Waislamu watupu? Kama walikamatwa na wasio Waislamu ni vipi basi kamata hiyo ionekane ni dhidi ya Uislamu unless kama wale wengine nao walishukiwa kushirikiana na Waislamu.

Tukio jingine ambalo huwa linatajwa sana ni kesi ya Uhaini ya 1969 ambapo mmojaa wa waliohusishwa ni Bi. Titi Mohammed. Kwa wengine hili lilikuwa ni dhidiya Waislamu. Ingekuwa kweli kama hawakukamatwa wengine. Lakini tuwakumbushe majina ya wale watu saba waliofikishwa mahakamani Juni 8, 1970 mbele ya Jaji Mkuu T. Georges

Bi. Titi Mohammed (Muislamu) (Muasisi wa TANU na mpigania Uhuru)
Michael Kamaliza (Waziri wa zamani wa Kazi - Mkristu)
William Chacha (Mwambata wa Kijeshi, Peking - Mkristu)
Grey Mattaka (mhariri gazeti la The Nationalist - Mkristu)
Oscar Kambona (mpigania Uhuru na Waziri wa zamani wa Ulinzi na Mambo ya Nje - Mkristu)*
John Chipaka (kiongozi wa chama cha ANC- Mkristu)
Eliya Chipaka (Kapteni wa JWTZ - Mkristu)
Alfred Mulinga (Luteni wa JWTZ - Mkristu)

* Kambona hakuhesabiwa kama miongoni mwa wale saba waliofikichwa mahakamani mwanzoni. Kambona alikuwa ameshatoroka kwenda Uingereza kabla ya kesi kuanza.

Sasa, kati ya wote hao saba ni mmoja tu Muislamu - Bi. Titi Mohammed. Lakini Bw. Said anaandika kana kwamba Nyerere alikuwa na baya dhidi ya Waislamu japo mtu angeweza kusema ilikuwa dhidi ya watu wa Kambona (wanne ya watuhumiwa walikuwa wanausiana na Kambona).

Sasa, vijana wanaosoma hapa natumaini wanapata mwanga kidogo wa kuelewa kwanini wengine tunachukulia hoja nyingi za Bw. Saiid ni za kutengeneza na zimeandikwa mahsusi kuvutia watu wasiotaka kutafuta ukweli.
 
hapo penye red
yaonekan ndipo chanzo cha kuanzisha huu 'uzi'
 
Mwanakijiji, mimi nimemwambia Mohamed Said kuwa wakati tunapata uhuru Desemba 9, 1961 ndio nilikuwa namalizia Form One (darasa la tisa). Pamoja na kufuatilia sana siasa za wakati huo (hata mdahalo wa Kennedy na Nixon tuliufuatilia kama vijana wa sasa walivyofuatilia mpambano kati ya Obama na Romney) na kuwa mashabiki wa siasa si za Afrika tu bali hata Asia na Ulaya, lakini hakuna hata siku moja kwenye miaka hiyo kabla ya uhuru, niliyasikia majina ya wazee wa Gerezani anaowataja Mohamed Said. Je wakati huo ni nani huyo alizima habari zao zisienee Tanganyika?

Miongoni mwa wanasiasa tuliowasikia ni kama Zuberi Mtemvu, Oscar Kambona, Bibi Titi Mohamed, Kasanga Tumbo, Paul Bomani na wengine wengi tu...lakini si Abdulwahid Sykes wa Gerezani, Sheikh Amir wa Unguja wala wazee wengine wa Gerezani anaowakomalia na kuwalilia. Nimekuja kuyasikia hayo majina miaka mingi tu baada ya uhuru, je ni nani huyo kabla ya uhuru alizuia habari zao na harakati zao zisiwafikie Watanganyika nje ya Dar es Salaam? Nyerere? Wakoloni? TANU? Huyu Mohamed Said ni mchochezi tu na muongo mkubwa sijapata kuona...ukweli utabaki pale pale kwamba wakati wa kupigania uhuru Watanganyika kwa umoja wao walishirikiana bila kujali kabila zao, dini zao wala sehemu wanakotoka.

Hao wazee wa Mohamed Said yawezekana walijulikana sana kwenye mitaa ya Dar es Salaam lakini Dar es Salaam ilikuwa na watu laki moja tu (110,000) wakati Tanganyika ilikuwa na watu milioni nane (8,000,000)
 
Hao wazee wa Mohamed Said yawezekana walijulikana sana kwenye mitaa ya Dar es Salaam lakini Dar es Salaam ilikuwa na watu laki moja tu (110,000) wakati Tanganyika ilikuwa na watu milioni nane (8,000,000)

Naam; na hapa ndio ugomvi ulipo. Historia ya Gerezani imekuwa ni historia ya Tanganyika nzima. Lakini siyo hivyo tu, Bw. Said kwa makusudi kabisa (na ameashiria kukubali hilo) ameamua kuwaweka pembeni wazee wengine wote walioshiriki katika harakati za Uhuru hasa kama a. Ni Wakristu (hawa hawaiti wazee wake) na b. Wako nje ya Dar (wapo wenggine wa nje ya Dar anawaita wazee wake kwa sababu ni Waislamu). Hivyo majina mengine anayataja kwa kupita tu hata kama wana mchango mkubwa sana.

Mimi matumaini yangu ni kuwa vijana na hata watu wengine ambao wametusoma toka mwanzo watakuwa wameelewa namna ya KUTOKUJENGA hoja na vile vile namna ya KUTOKUANDIKA HISTORIA. Nimepata bahati ya kusoma waandishi wengi walioandika kuhusu Tanganyika na mwamko wa Uislamu katika Tanganyika na karibu wote wametaja majina makubwa ya wakati ule katika Waislamu. Lakini hawa walitajwa zaidi katika Uislamu wao kuliko katika siasa zao.

Sasa ukiamua kuangalia kwa mwanga wa Uislamu tu utakosa mengi kwa sababu ni lazima unachoangalia kifit kwenye paradigm yako uliyotengeneza. Bw. Said kaamua kutengeneza prism ya Uislamu na hapo basi watu wote katika historia yetu wanahukumiwa kupitia hapo. Ukipingana na Sheh Amir basi uko kinyume ya Uislamu na Muislamu ukimuunga mkono Nyerere basi wewe siyo Muislamu mzuri.

Sasa hivi kwa kweli niko tempted sana kuamua kuchambua maandishi ya Bw. Said na kuyamegua megua kuyaonesha how absurd some of the claims are, and why some facts as claimed by the author have no historical bearing - and they are quite plentiful. Mimi sasa hivi wala sihitaji majibu ya Bw. Said tena kwani hana majibu hayo; ninachofanya ni kuwapa wasomaji wetu maswali wajiulize wanapomsoma.
 
Mzee mohamed saidi anafaidika yeye kwa kuwadanganya waislamu na si kweli anachosema na ancholazimisha ss pia tuamini atakavyo yy
 
Wakuu nadhani kuna jambo ambalo halijazungumziwa hapa.Kilichofanya Nyerere aende Dar ni kwasababu ndipo yalipokuwa makao makuu ya mkoloni na hata ikulu na ofisi zote na uongozi ulikuwepo Dar.

Kwahiyo wale wanaodai sijui wazee wa gerezani mimi naona ni kwamba kilichotokea ni wao kuwa wenyeji wa makao makuu ya mkoloni.

Na wanaodai kwanini asingewaondoa wakoloni akiwa Butiama wana dalili za kutoelewa vyema,na wanapotosha either kwa makusudi ama kwa bahati mbaya.
 

jmushi1
Ulikuwa wapi? Hujaonekana kwa muda sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…