Mwanakijiji, mimi nimemwambia
Mohamed Said kuwa wakati tunapata uhuru Desemba 9, 1961 ndio nilikuwa namalizia
Form One (darasa la kumi na mbili). Pamoja na kufuatilia sana siasa za wakati huo (hata mdahalo wa Kennedy na Nixon tuliufuatilia kama vijana wa sasa walivyofuatilia mpambano kati ya Obama na Romney) na kuwa mashabiki wa siasa si za Afrika tu bali hata Asia na Ulaya, lakini hakuna hata siku moja kwenye miaka hiyo kabla ya uhuru, niliyasikia majina ya wazee wa Gerezani anaowataja
Mohamed Said. Je wakati huo ni nani huyo alizima habari zao zisienee Tanganyika?
Miongoni mwa wanasiasa tuliowasikia ni kama Zuberi Mtemvu, Oscar Kambona, Bibi Titi Mohamed, Kasanga Tumbo, Paul Bomani na wengine wengi tu...lakini si Abdulwahid Sykes wa Gerezani, Sheikh Amir wa Unguja wala wazee wengine wa Gerezani anaowakomalia na kuwalilia. Nimekuja kuyasikia hayo majina miaka mingi tu baada ya uhuru, je ni nani huyo kabla ya uhuru alizuia habari zao na harakati zao zisiwafikie Watanganyika nje ya Dar es Salaam? Nyerere? Wakoloni? TANU? Huyu
Mohamed Said ni mchochezi tu na muongo mkubwa sijapata kuona...ukweli utabaki pale pale kwamba wakati wa kupigania uhuru Watanganyika kwa umoja wao walishirikiana bila kujali kabila zao, dini zao wala sehemu wanakotoka.
Hao wazee wa
Mohamed Said yawezekana walijulikana sana kwenye mitaa ya Dar es Salaam lakini Dar es Salaam ilikuwa na watu laki moja tu (110,000) wakati Tanganyika ilikuwa na watu milioni nane (8,000,000)