Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Mkuu Ngongo,

Tatizo siyo Mohamed Said hebu soma kichwa cha habari cha huu uzi watu ndiyo watatakiwa wathibitishe uchochezi wa Mohamed Said.
Hivi unaweza kunifafanulia ni kwa nini Waislamu ambao wapo CCM Nyerere hawampendi na ni kwa nini JK aliyeinadi ilani ya CCM mwaka 2005 ikiwaahidi Waislamu Mahakama ya kadhi na yeye akiwa ni Muislamu na amewaruka kimanga, je kuna ajenda gani dhidi ya wasio Waislamu.
 

Tunasubiri atuletee maandiko yake. Itakuwa jambo la maana sana. Lakini katuahidi mengi humu ndio maana nashangaa kama anapo pakuanzia.
 
Zomba,

Wewe ulitaka kumkatisha tamaa si unaona tayari keshaanza ''literature review.''
Tayari atakipitia kitabu cha Kivukoni na kuangalia yalosahaulika.

Huu ni mwanzo mzuri sana.

Naam, kweli kabisa, nimeona.
 
Na ndio ukasingizia mama mgonjwa kalazwa, simu mbovu haina chaji. Umesahau?
Tusiharibu hii mada, nilikuonea huruma mwezi wa Ramadhani maana safari za msikitini zilikuwa haziishi. wacha tuendelee na mjadala huu kwanza. Bado sielewi ni kwa nini Waislamu hasa wa CCM hawampendi Nyerere lakini wanamkenulia meno JK ambaye ndiye adui wa Uislamu.
 
Hizi ndizo porojo za mitaani..alitoa amri hiyo lini na wapi?

Porojo zipi kesi ya uhaini waliokamatwa ni Bibi Titi Mohamed, Gray Mattaka, Eliya Chipaka,Prisca Chiombolo,Michael Kamaliza, viongozi hawa walihukimiwa pamoja na Oscar Kambona ambaye alikimbilia Uingereza.

Walikata rufaa na wakaachiwa huru. Wakakamatwa tena na serikali na kufungwa upya.

Wadogo zake Oscar Kambona wawili waliwekwa kizuizini bila kufikishwa mahakamani zaidi ya miaka kumi sasa ili linaitaji kujua nani aliwaweka kizuizini hawa ndugu zake Kambona.
 

Nimeipenda hapo kwenye RED... Hawa masheikh walikuwa wakifanya nini TANU? Kwa maslahi ya nani? Mapadre na wachungaji walikuwepo TANU? Mwalimu aliwaacha?
 
Mkuu Ngongo,

Tatizo siyo Mohamed Said hebu soma kichwa cha habari cha huu uzi watu ndiyo watatakiwa wathibitishe uchochezi wa Mohamed Said.

Imeshathibitishwa kwa hotuba hiyo juu ya rangi ya bluu na maelezo mengine meeeeeeeeeenggi,

Sijui ulitaka ushahidi gani uletwa zaidi ya Mohamed kuja kutetea ngano zake?
 
Last edited by a moderator:
Una maana kuliuwa na Waislamu wenye udini dhidi ya Wakristu tangu 1953 na wakarudi tena 1955 na tena hawahawa na udini wao wakarudi tena 1958 ?

MM,

Mazingira ya Dar es Salaam wakati ule yalikuwa magumu kwa Mkristo yoyote yule.
Kanyama Chiume kwenye kitabu chake ''Vituko vya Uhuru'' kaeleza hali ilivyokuwa.

Kitabu hiki unaweza kukipata Maktaba ya Chuo Kikuu.

Nyerere bila ya Abdu, Dossa, Idd Tosiri, Idd Faiz, Sheikh Hassan bin Amir na Baraza
la Wazee wa TANU chini ya Mwenyekiti wake Sheikh Suleiman Takadir uongozi wake
ungekumbwa na madhila makubwa.

Hisia dhidi ya Nyerere zilikuwapo toka 1953 kama nilivyoeleza na upeo ni pale sasa
walipotoka TANU kuunda AMNUT.

Nimeeleza haya kwa kirefu katika kitabu ikiwa unacho bora utalii.
 

Mara mama mgonjwa, mara simu mbovu, mara niliona huwezi kujibu maswali yaliyoulizwa, mara sasa nilikuonea huruma ilikuwa Ramadhan.

Waswahili hunena, mfamaji haishi kutapatapa. Watajaza waloupitia huo mdahalo.

Jee, umewahi kumsikia Mshume Kiate?
 
Haya udini wa uliosababishwa na waandishi na moh'd.. Geita watu washaanza kuchinjana
 
Hakuna mtu aliyesema kuwa Kambona muasisi wa TANU. Nimekuuliza Kambona hakuwa na cheo chochote ndani ya TANU alikuwa mwanachama wa kawaida.
 

Sicho ulichokisema mwanzoni..usihamishe magoli kama mwalimu wako hapa...
 

Kwamba baadhi ya wazee wako walikuwa wadini na wabaguzi dhidi ya Wakristu....?
 
Umeonae? Mwalimu hakuwa na utani kwa wavunja KATIBA na SHERIA za NCHI. Mwalimu na Oscar Kambona( zamani tukimwita OK) walikuwa watu wa karibu sana hata wakasimamiana NDOA.
 
Hakuna mtu aliyesema kuwa Kambona muasisi wa TANU. Nimekuuliza Kambona hakuwa na cheo chochote ndani ya TANU alikuwa mwanachama wa kawaida.

Ritz hii hapo chini inaweza kusaidia kidogo:

[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD]

TANU at New Street, 1955

In the early days the post of the Organising Secretary was always changing
hands between Mtemvu (who was TANU's first organising secretary) Denis
Phombeah, Oscar Kambona, Idd Faiz Mafongo and Stephen Mhando.

Mtemvu, being organising secretary, had the difficult task of mobilising
people to register and open TANU branches throughout the country.


[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
TANU needed about twelve thousand shillings to enable Nyerere to travel to the United Nations, New York.

The committee of Abdu Kandoro, Japhet Kirilo and Abbas Sykes had collected some funds from the provinces which were used on Ally and Phombeah's abortive trip to the Pan African Congress in Lusaka.

What was left was not enough.

Funds had to be sought from the people to enable Nyerere make the trip. John Rupia contributed more than one third of the amount. Other staunch members contributed generously, but in that formative stage TANU was poor and the amount was still beyond its ability to raise.

Realising the deficit in the funds for Nyerere's trip, Idd Faiz was requested to travel to Tanga and get more funds from there.

Mwalimu Kihere had already collected the money and was only waiting for it to be collected and to be delivered to the headquarters.

At the same time TANU received information that whoever travelled to Tanga to get the money for Nyerere's trip would be arrested on his way back. Before departure Oscar Kambona TANU General Secretary and John Rupia TANU Vice-President went to see Idd Faiz at his house in Ilala for a briefing and to wish him luck.

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

 
Umeonae? Mwalimu hakuwa na utani kwa wavunja KATIBA na SHERIA za NCHI. Mwalimu na Oscar Kambona( zamani tukimwita OK) walikuwa watu wa karibu sana hata wakasimamiana NDOA.

Juzi wewe mwenyewe umesema huwezi kumsemea Nyerere kuhusu ugomvi wao na Kambona baada ya kukuuliza. Tena ukasema mpaka anaingia kaburini hakuwahi kusema ukaniambia niwaulize watoto wake ukanitajia na majina, leo tena wewe huyo huyo anamsemea marehemu hakuwa na utani kwa wavunja Katiba.
 
Sio kweli Mzee Mohamed. Mwaka huo 1953 ndio aliochaguliwa kuiongoza TAA na baada ya miezi kadhaa TANU ikazaliwa na akachaguliwa tena kuwa Rais wake wa KWANZA. Dar Es Salaam haijawahi kuwa ngumu kwa mtu wa DINI au KABILA yoyote labda baadhi ya mitaa. Mwalimu hakuwa mgeni na siasa za TAA.

Muda huo 1953 hadi TANU inazaliwa wewe ulikuwa "toddler" kabisa. Haukuwa unajua kinachoendelea. Tusidanganyane ukubwani hivi.
 
Kwamba baadhi ya wazee wako walikuwa wadini na wabaguzi dhidi ya Wakristu....?

MM,

Sipendi kukupuuza.

Mbona hilo nimeliweka wazi kuwa kulikuwa na wazee wangu
hawakutaka Nyerere ashike nafasi ile ya urais wa TAA na
kisha TANU.

Baada ya uhuru wakati Nyerere anawaweka masheikh jela
kulikuwa na msemo maarufu Dar es Salaam, ''Haya yote
yasingetufika sama na Abdu Kleist.''

Nadhani umeridhika na majibu yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…