MM,
Mazingira ya Dar es Salaam wakati ule yalikuwa magumu kwa Mkristo yoyote yule.
Kanyama Chiume kwenye kitabu chake ''Vituko vya Uhuru'' kaeleza hali ilivyokuwa.
Kitabu hiki unaweza kukipata Maktaba ya Chuo Kikuu.
Nyerere bila ya Abdu, Dossa, Idd Tosiri, Idd Faiz, Sheikh Hassan bin Amir na Baraza
la Wazee wa TANU chini ya Mwenyekiti wake Sheikh Suleiman Takadir uongozi wake
ungekumbwa na madhila makubwa.
Hisia dhidi ya Nyerere zilikuwapo toka 1953 kama nilivyoeleza na upeo ni pale sasa
walipotoka TANU kuunda AMNUT.
Nimeeleza haya kwa kirefu katika kitabu ikiwa unacho bora utalii.