Naona Mzee Mohamed anang'ang'ana kuwa AA ndio TAA na TAA ndio TANU na kwa sababu hiyo TANU ndio CCM! Kwamba huyu ni nyoka mmoja ambaye amekua akijivua na kujivika gamba jipya. Ukimwambia lete KATIBA za vyama hivi zinazolithibitisha hilo, anakwambia hakuwahi kuziona wala kuzitafuta katiba hizo!
Dhana yake hii imejikita zaidi kwenye watu na majina yao na hasa familia ya mlowezi Sykes. Kwa kuwa Sykes alikuwepo AA ilipoanza, Kleist Sykes akawepo enzi za TAA na baadae Abdu na wadogo zake wakawepo wakati TANU inaanza basi chama ni kilekile ni majina ya viongozi yanabadilika.
Historia ya vyama haiko hivo Mzee Mohamed pamoja na mapenzi yako makubwa kwa familia hii ya Sykes. Historia ya familia ndio inakuwa hivo. AA, TAA, TANU na CCM ni vyama vinne tofauti. Vilivyoanzishwa na watu tofauti, kwa nyakati, malengo na madhumuni tofauti.