Hatukuelewana Ritz. Nilikataa kumsemea Oscar Kambona. Hata Mwalimu simsemei. Karama hiyo ya kuwasemea watu wengine anayo mzee wetu Mohamed. Kaandika na kitabu kabisa na kueleza hisia zao za ndani. Mimi nasema kile ninachokifahamu kuhusu MwalimuJuzi wewe mwenyewe umesema huwezi kumsemea Nyerere kuhusu ugomvi wao na Kambona baada ya kukuuliza. Tena ukasema mpaka anaingia kaburini hakuwahi kusema ukaniambia niwaulize watoto wake ukanitajia na majina, leo tena wewe huyo huyo anamsemea marehemu hakuwa na utani kwa wavunja Katiba.
Sio kweli Mzee Mohamed. Mwaka huo 1953 ndio aliochaguliwa kuiongoza TAA na baada ya miezi kadhaa TANU ikazaliwa na akachaguliwa tena kuwa Rais wake wa KWANZA. Dar Es Salaam haijawahi kuwa ngumu kwa mtu wa DINI au KABILA yoyote labda baadhi ya mitaa. Mwalimu hakuwa mgeni na siasa za TAA.
Muda huo 1953 hadi TANU inazaliwa wewe ulikuwa "toddler" kabisa. Haukuwa unajua kinachoendelea. Tusidanganyane ukubwani hivi.
Hatukuelewana Ritz. Nilikataa kumsemea Oscar Kambona. Hata Mwalimu simsemei. Karama hiyo ya kuwasemea watu wengine anayo mzee wetu Mohamed. Kaandika na kitabu kabisa na kueleza hisia zao za ndani. Mimi nasema kile ninachokifahamu kuhusu Mwalimu
Mimi sijaridhika. Soma tena swali kisha ulijibu inavyotakiwa. Mwanakijiji kauliza hivi namnukuu: "Kwamba baadhi ya wazee wako walikuwa wadini na wabaguzi dhidi ya wakristu....?" Mwisho wa kunukuu.MM,
Sipendi kukupuuza.
Mbona hilo nimeliweka wazi kuwa kulikuwa na wazee wangu
hawakutaka Nyerere ashike nafasi ile ya urais wa TAA na
kisha TANU.
Baada ya uhuru wakati Nyerere anawaweka masheikh jela
kulikuwa na msemo maarufu Dar es Salaam, ''Haya yote
yasingetufika sama na Abdu Kleist.''
Nadhani umeridhika na majibu yangu.
Hakuna mtu aliyesema kuwa Kambona muasisi wa TANU. Nimekuuliza Kambona hakuwa na cheo chochote ndani ya TANU alikuwa mwanachama wa kawaida.
Nimeipenda hapo kwenye RED... Hawa masheikh walikuwa wakifanya nini TANU? Kwa maslahi ya nani? Mapadre na wachungaji walikuwepo TANU? Mwalimu aliwaacha?
Mimi sijaridhika. Soma tena swali kisha ulijibu inavyotakiwa. Mwanakijiji kauliza hivi namnukuu: "Kwamba baadhi ya wazee wako walikuwa wadini na wabaguzi dhidi ya wakristu....?" Mwisho wa kunukuu.
Alitimka na hakurudi tena hadi Mwalimu alipoondoka madarakani. Kwa vile OK hakuwahi kufikishwa mahakamani, tuliache hili. Turudi kwenye mada.Sasa umejuaje kama Oscar Kambona alivunja Sheria na Katiba ya nchi.
Mwalimu angefanyaje katika hali kama hii ambayo iliendelea kujirudia hadi leo?WC,
Ndiyo.
Alitimka na hakurudi tena hadi Mwalimu alipoondoka madarakani. Kwa vile OK hakuwahi kufikishwa mahakamani, tuliache hili. Turudi kwenye mada.
Msisitizo uko kwenye neno "baadhi".Na ndio hao walimkaribisha akala na kulala kwao, si ndio?
Mwalimu angefanyaje katika hali kama hii ambayo iliendelea kujirudia hadi leo?
Kitu pekee ambacho Bw. Mohammed Said ameshindwa kukionesha hadi hivi sasa japo anakidai kwa maneno ni kuwa wazee wa Kiislamu na Waislamu kwa ujumla walipigania uhuru peke yao bila ushirika wa ndugu zao Wakristu. Amejitahidi sana lakini mara zote anajikuta historia inamkatalia...
Angelikuwa na uwezo wa kufuta ushiriki wa wazee Wakristu na wasio Wakristu katika harakati za Uhuru angewafuta... angejaribu kuandika historia ya harakati zaWaislamu peke yao kupigania uhuru angejaribu
Kama Mtanzania nikitaka kusoma historia Tanganyika taipata wapi.
Kama Mtanzania nikitaka kusoma historia Tanganyika taipata wapi.
Kama Mtanzania nikitaka kusoma historia Tanganyika taipata wapi.
Tatizo ni huo ubaguzi usioonekana kwa macho ya kawaida hadi uvae miwani ya 3D. Tumesoma wote mashule hayahaya Wakristo kwa Waislam; Tumesoma wote vyuo mbalimbali; Tumetibiwa wote zahanati na hospitali hizihizi; Tumeajiriwa wote kwenye taasisi za umma; Tumegombea na kuchaguliwa wote katika nafasi na ngazi mbalimbali za uongozi wa nchi hii; Tumegawana wote pato la nchi hii; Tumesota wote vitu na huduma mbalimbali zilipokosekana.WC,
Upinzani dhidi ya Nyerere ulikuwa wa watu wachache sana na nimeshauzungumza
hapa.
Waislam waliwamudu hawa wapinzani bila matatizo yoyote na hasa baada ya ule
mkutano wa Sheikh Hassan bin Amir wa 1955 na jinsi Waislam walivyoikataa AMNUT.
Nyerere alipokuja na Kanisa Katoliki dhidi ya Waislam katika sakata la EAMWS na ile
hofu ya nguvu ya Uislam katika Tanganyika huru ikawa sasa ubaguzi si ule wa Waislam
kumkataa Nyerere.
Sasa ubaguzi ukawa ''institutionlised'' ukibebwa na serikali na Kanisa dhidi ya Waislam na
Uislam.
Ndiyo haya unayosikia leo ya mfumokristo.