Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Nashawishika kukwambia kuwa juhudi za kanisa katika harakati za Ukombozi zipo na zimetukuka, japokuwa hazisemwe wala kulalamikiwa!

Ukitaka nikushuishie ushiriki wa kanisa nitakushushia bila chembe, na utashangaa kwakuwa hukuwahi kusikia hayo!

Nakuomba kwa faida ya wana ukumbi tushushie ili tuone kanisa lime fanya nini?
 
Mkuu Mohamed Said, usione kimya, nipo nje ya ofisi natumia simu, nikitulia kwenye kompyuta nitakupa ushiriki wa kanisia kwenye uhuru wa nchi hii hadi uhuru kamili!
 
Mohamed Said kitabu chako si ungekiita "Mein Kempf" kingejulikana kimataifa zaidi maana sioni tofauti,wewe unazungumzia christian conspiracy chenyewe kilizungumzia jewish conspiracy-the end result what happened next the world had to face germany,wewe unatakawaislam wawakabili wakristo in the name of kutaka usawa-someday history itakuhukumu as the harbringer of a distabalised tanzania
 
Last edited by a moderator:
Kweli wewe kichwa chako KIGUMU.



Sasa nakuomba uwe mstaarabu, sawa?

Swadakta, katika quote hiyo uliyotumia, kuna sehemu imetukana Bibilia, kama ulivoitukana Qur-an na kusema kuwa ina makosa mingi ya kihesabu?

Au kwenye hiyo quote, kuna sehemu amesema lolote kuhusu Kanisa takatifu?

Mjadala unaendelea uzuri, wewe unataka kuupotosha. Mada hapa ni kuwa kaka yetu Yeriko anam "challenge" mzee wetu Mohamed Said. Tusijaribu kuanzisha mjadala mwengine. Kama unataka mjadala wa kuanza kukosoana dini, hapa si pahali pake. Anzishe thread kwenye sakafu husika, tujadiliane huko.

Mbona kaka/dada unakua mgumu kuelewa a simple premise as that?

Nawasilisha
 

Sasa kaka huji na hoja. Weka hoja mbele kama anavyofanya kaka yetu Yeriko, mzee wetu Mohamed Said ajibu. Ndivo mjadala unavokwenda.

Au pia hilo ni gumu?

Nawasilisha
 
Last edited by a moderator:
“Serikali haitavumilia vurugu wala ukabila kwa namna yoyote ile…. Mwaka 2012 vurugu zenye sura ya kidini zilianza kujitokeza ila sasa nasema kwamba hatutazivumilia kwa namna yeyote ile, inatosha,” alisema Rais Kikwete.
Mungu atuweke hai .Nina uhakika kukamatwa kwa Ponda and co na jinsi maandamano waislam yalivyodhibitiwa utayaandika kama ulivyoandika wakati wa Mwinyi. Ila kama angekuwa rais Mkristo madarakani ungeandika kama nilivyo highlight hapo chini kwenye paper yako. Kimsingi unasukumwa na chuki ya kidini tu . Hautoki nje ya hapo.
In an operation on Easter Friday afternoon a group of young Muslims like well trained commando squad moved swiftly
 
Mohamed Said, wimbi la mbele,

..hivi mnaweza kutuletea vitabu vya van Bergen na John Sivalon ambavyo mara nyingi mmekuwa mkivinukuu?

..nadhani ili mjadala huu uweze kupendeza tunapaswa na kuviona vitabu hivyo ambavyo mnadai vina ushahidi wa uonevu wa Mwalimu Nyerere dhidi ya Waislamu.

..kama kuna tatizo mnaweza kuwasiliana na Maxence Melo au moderator kuona taratibu gani zitumike vitabu hivyo vifike hapa kwa ajili ya mjadala wetu.

cc: Nguruvi3, Mzee Mwanakijiji, Companero, Jasusi
 
Last edited by a moderator:

Kitabu cha Bergen hakipatikani madukani kwa sasa.
Lakini John Sivalon kitabu chake kinapatikana Msikiti
wa Mtambani Kinondoni.

Bei yake ni shs: 2,000.00.

Yoyote akitakae akanunue pale.
Ila muhimu Waislam wamefikisha kila kitu serikalini.

Hakuna ambacho hakijulikani.
Serikali imekuwa kimya.

Walichofanya ni kukifungia kitabu cha Dr. Njozi ''Mwembechai
Killings.''

Lakini wakakiruhusu cha Dr. Mbogoni ''The Crescent and the Cross.''
Ambalo kimechukuliwa kama jibu kwa Dr. Njozi.

Haya ndiyo mambo ya serikali yetu.
 
jokaKuu,
Kitabu cha John Sivalon ninacho. Hakuna mahali popote pale alipoandika kuwa Nyerere alipendelea wakristo. Aliandika kitabu kuelezea mchango wa kanisa lake katika political transformation ya Tanzania. Sasa wenzetu wamekitumia na kupotosha makusudi kuwa ni ushahidi wa jinsi kanisa Katoliki lilivyoshirikiana na Nyerere kuwabagua Waislamu. Ukitaka siku moja pitia hapa nikuazime ukakisome mwenyewe. cha Van Bergen nimewahi kukisoma lakini kwa sasa sinacho. Nimekitafuta Amazon wakasema kiko out of print. Lakini Mohamed anatafsiri kuwa kilipigwa marufuku Tanzania. Si kweli.
 

Rais anasema tu.
Wenye kuvumilia ni sisi Waislam.

Sisi hatutoi vitisho kwa mtu.
Tunaomba wasaa tu tuzungumze na serikali bayana na watu wasikilize.

Umma ndiyo utakaokuwa muamuzi nani anaedhulumiwa.

Hapa nimejitahidi sana na kwa lugha ya kiungwana kueleza hali ya Waislam
na historia yao.
 
Mohamed Said, Jasusi,

..kitabu cha Sivalon sijakiona kabisa, kitabu cha Van Bergen unaweza kusoma pages chache on the internet.

..sasa bila kuwa na vitabu hivyo viwili ni vigumu sana kuweza kushiriki mjadala wa mahusiano ya Mwalimu Nyerere na Kanisa.

..kwa upande mwingine nadhani kitabu cha Van Bergen kimemuelezea Mwalimu Nyerere kama mtu aliyepigania haki za wa-Tanzania wote, na mara nyingine hata kufikia kukwaruzana na Maaskofu.
 
Last edited by a moderator:

Soma Sivalon uk. 49 (Ndanda, 1992) anazungumzia kuhusu mgawano wa viti katika Bunge.

Anasema Wakatoliki wanahodhi 75% ya viti vyote. Vilivyobaki wamegawana Wakristo
wa madhehebu nyingine na Waislam.

Sivalon uk 37 anazungumzia kuhusu njama za Kanisa Katoliki dhidi ya Uislam na kuuita Uislam
ni adui wake...

Kuhusu kupigwa marufuki Bergen.
Wahusika wako kimya.

Hawajajibu sasa takriban miaka 20.
Wao huwa kimya wanakuachieni nyie muwajibie ingawa nyinyi siyo mliotuhumiwa kwa dhulma.
 
wakati wakutaifisha shule na taasisi mbalimbali waislamu walipotrza shule,vyuo,hospitali nk ngapi na wakristo walipoteza ngapi?
 
Mohamed Said,

..mbona Van Bergen naye anadai kuwa Wakristo walikuwa wanalalamika kwamba wananyimwa uongozi ktk Tanu?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Jokakuu,

Nimesoma maelezo ya Mohamed Said kuhusu Mshume Kiyate alivyomkirimu mwalim hadi kumpa pesa, chakula n.k.
Mohamed akaenda mbali zaidi na kusema Ditopile alipoelezea mchango wa Kiyate, Magazeti yalipotosha kwa kusema alimdhalilisha Nyerere kwa maneno ''kulishwa''. Hapa Mohamed anatuambia kuwa kuna kusoma habari na kupotosha habari kunakoweza kutokea. Fair enough!

Ukisoma maelezo ya vitabu tuhumiwa utaona kilichotokea ni kuchukua baadhi ya mistari na kupoteza dhana nzima.
Sina maana kila kinachosemwa hakikuandikwa, ninamaanisha kuwa kuna sehemu imechukuliwa sentensi tu na kuacha maudhui ya aya nzima. Sina hakika kama hakuna upotoshaji kama ule aliofanyiwa Ditopile.

Lakini pia lazima watu wasome vitabu vya ngano za Mzee Said kwa kufahamu kuwa yapo mambo yaliyokuwa pre-determined kuandikwa na hivyo hutafutiwa eneo tu.

Ukisoma majibu kwa Yericko Nyerere kuhusu Mshume Kiyate, Mohamed ameelekeza tuhuma zake kwa Nyerere hasa pale anapodai kuwa kulikuwa na zipo hujuma za jina lake kutopewa mtaa. Kwamba Nyerere alifanya hivyo kama sehemu ya dharau na chuki kwa wazee wake.

Anachosahau Mohamed ni kuwa Tangu Uhuru, madiwani wa jiji la Dar es Salaam kwa asilimia zaidi ya 80 hadi sasa ni Waislam wakiongozwa na Mameya Waislam tena wazee wake akina Kitwana Kondo, Sykes, Abouu n.k.
Hakuna kumbu kumbu kama walifanya chochote na kuzuiwa zaidi ya wao kuwa sehemu ya mabadiliko ya majina kama UWT/Bibi Titi n.k. Why Nyerere na sio madiwani? Kwanini Moshi waenzi watu wao Dar washindwe? Ni kosa la nani!

Mfano huu ni kuonyesha kuwa yapo mazingira yaliyoandaliwa ili kujenga mazingira yenye ushahidi usiokuwepo.
Hapo ndipo ''vitabu husika'' huelezwa kwa undani kwasababu kuna mstari mmoja au miwili inayoweza chomolewa na ku-fit the purpose.

Fikiria hivi, mambo yote yaliyotokea kati ya 1954 hadi 1985 yalimhusu Nyerere kama mtu. Leo Mohamed anasema serikali ikae na Waislam iongee nao kuhusu tatizo. Kwanini Waislam wasitake kukaa na Mwinyi, Mkapa au Kikwete bali serikali.
Lini mambo ya taifa yametoka kwa mtu na kuwa serikali? Mbona huko nyuma haitajwi serikali anatajwa Nyerere na kwanini leo hatajwi Kikwete inatajwa serikali.

Nitamwelewa kama atasema hivi, Waislam wanataka kukaa kitako na Kikwete kuelezea kadhia yao wasikilizwe.
Asiishie hapo tu, ni lazima na ni wajibu wa mtu anayetafuta suluhu kuweka kila kitu mezani.
Mohamed hawezi kutuambia kuna kadhai lakini hatuambia anafikiri suluhisho ni nini.

Hii ni kwasababu tayari ameshajenga mazingira ya ''wasikilizwe'' na wala si kusikilizwa bali kutekelezewa.
Hiyo ndio pre-determined condition ambazo zinashangaza ndani ya masimulizi na ngano za mzee wetu.

Ametoa madai kitabu kimepigwa marufuku, hajaeleza ni tamko la nani na lini! Ameshauriwa viwekwe hapa anatoa bei ya vitabu! Yote haya ni kwa kujua kuwa vitabu hivyo vikitua jamvini kwa wale wasiovisoma awali au waliosoma kwa ushabiki, ngano inaweza kuchukua mweleko mpya kabisa.
 
Mohamed,
Ubunge unagombewa. Haugawanywi. Kwa hiyo kama kuna makosa hapa tuwalaumu raia wote wa Tanzania wakiwemo
Waislamu, kwa kuwachagua 75% ya wabunge wa Kikatoliki. Hilo moja. Kitabu cha Bergen hakijawahi kupigwa marufuku. Hiyo nitairudia mpaka unithibitishie vinginevyo. Na kama kilipigwa marufuku miaka 20 iliyopita, kama unavyodai, basi kilipigwa marufuku na serikali iliyoongozwa na Muislamu, Ali Hassan Mwinyi, jambo ambalo haliingii akilini. Nimesema kitabu cha Njozi kilipopigwa marufuku ilitangazwa. Tutafutie Gazette ambamo serikali ilitangaza kupiga marufuku kitabu cha Bergen. Najua ni suala dogo, lakini hivi viuongo vidogo vidogo vikiunganishwa pamoja huleta picha tofauti kabisa. Pia kitabu cha Sivalon mimi nina nakala ya 2001. Naomba uninukulie Sura, kwa sababu ukiniambia ukurasa, kwangu ukurasa 49 ina "Mafundisho ya Maaskofu wa Tanzania," yakielezea barua ya maaskofu inayozungumzia "amani na maelewano."
 
HOJA YA UBUNGE HUGOMBEWA HUJAITIZAMA KWA MLINGANYO SAHIHI...!

UTARATIBU WA UPATIKANAJI WA MPIGIWA KURA UNAFAHAMIKA NCHI HII TOKEA ZAMA NA ZAMA.

NAOMBA NISEME :nono:

:nono::nono::nono::nono:
 

Hayo yote uliyosema yana mantiki.

Kwa mtazamo wa juu kwa hakika viti vinagombewa na kama Waislam hawatakiwi na watu wapiga kura wanawapenda Wakatoliki vipi uwalaumu Wakatoliki?

Ni ukweli kuwa hapana popote pale panapoonyesha kitabu cha Bergen kimepigwa marufuku.
Nk. nk. nk.

Ukiwa si Muislam hakika utakuwa katika hali ya kushangazwa na kila kitu.
Hiyo ndiyo kawaida ya jamii iliyosalimika na dhulma.

Lakini hali huwa nyingine kwa wale wanaodhulumiwa.
Anaefaida matunda atatoa kejeli, atatoe matusi nk.

Yule anaedhulumiwa atajitahidi sana kueleza ukweli akitegemea ataeleweka.

Lakini hapa JF sisi tunafanya kama ''academic exercise.''
Waislam na serikali tunaelewana.

Serikali inajua yote tunayowalalamikia.

Muda si mrefu Insha Allah tutafika mahali tutazungumza bayana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…