Mohamed,
Ubunge unagombewa. Haugawanywi. Kwa hiyo kama kuna makosa hapa tuwalaumu raia wote wa Tanzania wakiwemo
Waislamu, kwa kuwachagua 75% ya wabunge wa Kikatoliki. Hilo moja. Kitabu cha Bergen hakijawahi kupigwa marufuku. Hiyo nitairudia mpaka unithibitishie vinginevyo. Na kama kilipigwa marufuku miaka 20 iliyopita, kama unavyodai, basi kilipigwa marufuku na serikali iliyoongozwa na Muislamu, Ali Hassan Mwinyi, jambo ambalo haliingii akilini. Nimesema kitabu cha Njozi kilipopigwa marufuku ilitangazwa. Tutafutie Gazette ambamo serikali ilitangaza kupiga marufuku kitabu cha Bergen. Najua ni suala dogo, lakini hivi viuongo vidogo vidogo vikiunganishwa pamoja huleta picha tofauti kabisa. Pia kitabu cha Sivalon mimi nina nakala ya 2001. Naomba uninukulie Sura, kwa sababu ukiniambia ukurasa, kwangu ukurasa 49 ina "Mafundisho ya Maaskofu wa Tanzania," yakielezea barua ya maaskofu inayozungumzia "amani na maelewano."