Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Amma kweli, akutukanae hakuchagulii tusi, Mwinyi tumempokea wenyewe Dar., ngoja nikupe darsa dogo; Jee, unafahamu kuwa Mwinyi alikuwa anaishi nyumba ambayo sasa hivi ni bar bubu ya Pajero hapo mtaa wa Livingston? nyumbani kwa kina "Best". Na hapo katukuta (barzani kwetu hapo) tukamkaribisha kwa heshima na taadhima kama alivyokaribishwa Nyerere na Abdulwahid Sykes.
 

Hapa tunaongelea mbingu nyie mnaongelea ardhi, wapi na wapi?
 
Haiingii akilini.
 
Tatizo tunalopingana humu ni pale"WAKUJA" kuingia mjini,na kumuacha "mswahili" palepale gerezani aki mark time-wakati mwenzio ana march on-hili ndio tatizo mnalotaka ku wipe off na single blow,wakati mshaambiwa solution ni skuli

Kuna siku Maalim Mohamed Said alinitaka niwape darsa kuhusu Ihsaan. InshaAllah ntakuja nalo hivi karibuni, usiwe na haraka ntakuita kwenye darsa.
 
Last edited by a moderator:
...Na nani alomfuata mwenziwe kama sii hao wazee walomfuata Nyerere....

Hapo amma wewe husemi kweli, amma Yericko Nyerere hasemi kweli, amma Mzee Juliasi Nyerere hasemi kweli, maana Yericko kamnukuu huko juu, nnawawekea hiyo nukuu hapa chini, mkishaisoma mtujuze ni yupi ambae si mkweli kati yenu:

.
 
Soma hiyo quotation ya mkandara, kuna mahali kauliza nami nimekubaliana naye kabisa. Hivi kumbe hata kusoma na kuelewa ni tatizo kwako! samahani huwa sijibu post zako though!

Hujibu? Sasa hapa umefanya nini? Ulitumwa?
 
Nguruvi3,

Ikiwa atatokea Muislam dhalim.

Tutamshika mkono kumweleza kuwa
hivyo sivyo.
Umeshamshika mkono Sheikh Ilunga aliyetoa fatwa kwa Maaskofu? Hapa ndipo unaweza kuona ujinga uolivyotamalaki. Huyu sheikh yeye hajaua lakini amesimama katika jukwaa akihubiri na kuwaaambia weznzake waue kwa siri. Tena sababu za kuua eti ni askofu tu.
Katika Uislam imeelezwa kuua kiumbe ni kosa la namna gani sijui wanatumia Kurani ipi yarabi.

Mohamed, nenda kamshike Ilunga mkono kwanza, halafu nawe uombe watu wakushike mkono maana uadilifu wenu ni utata mtupu! in fact ni hakuna.

Huwezi kutunga kauli usizo na ushahidi nazo zikaleta farki ndani ya jamii halafu ukasema wewe ni mwadilifu, unless sijui maana ya neno uadilifu.
 
Mkandara,

Siku zote huwezi kukubali Nyerere azungumzwe vibaya bahati mbaya unakubali mfumo kristo umeletwa na Mwinyi lakini sisi Waislam tunaona mfumo kristo umeletwa na Nyerere ushahidi upo wazi.
Sawa labda nikubali aloyaleta yote haya ni Nyerere...inakuwaje wewe ni mwanaCCM chama ambacho Nyerere ndiye alikuwa kiongozi?..Nyerere yule alobadilisha kila kitu mlokitaka leo bado nyie wanachama hai tena kwa makusudi kabisa mnaendelea kukipamba..

Pili, siku zote sisi binadamu tumeumbwa kukutana na matatizo kisha tunayatafutia solution au sio?...sasa wewe baada ya kutambua hivyo kuwa Nyerere ndiye aloleta mfumo kristu, inakuwaje wewe ambaye uko CCM, rais wako muislaam, makamu muislaam na viongozi kibao waislaam mnashindwa kubadilisha mfumo mbovu wa Nyerere na kutupa kitu safi maana huyo Nyerere hayupo tena na hawezi kuja wala kuwakemea kwa mmabadiliko..

Je, huoni kwamba ni jukumu letu sisi wananchi kuwalaumu nyie mlokuwa CCM, viongozi na watawala mnaendeleza mfumo kristu na mmekuja hapa JF kwa niaba ya chama kuendeleza mfumo kristu uloasisiwa na Nyerere?..
Mkuu wangu acha hizo wewe ni zaidi ya khabari hizi za Mohammed Said ambaye anatoa malalamiko mengi lakini hana solution wakati bado mwanachama hai wa CCM na mshabiki mkubwa wa chama kile kile anachokilaani...Unamlaani Sheitan kisha unaenda yafanya yale yale tutakuelewaje?
 
umesema vizuri; nilimpigia debe si kwa sababu nilikuwa namjua. Nilichokukatilia ni hicho ulichoongeza...
Bahati yako nikwamba hakuna kumbukumbu za DHB.
Ungeona maneno yako uliyokua unayatumia mwenyewe.
Chakustaajabisha nikwamba yale tuliyokua tunayaona siku zile ndio unaanza kuyaona miaka hii nakujiunga Chadema.
Kama nilivyokuambia mwanzo, wewe ni kasuku tu!
Kujua kusema kunatoka kwa sauti za wengine nakuziiga lakini hawezi kusema unayofikiria mwenyewe.
 
Alaa mkuu wangu, haya ya kumpokea Mwinyi yametoka wapi?... mbona hata miye namkumbuka vizuri sana akija Mahiwa kuvizia mwali pale mtaani?..Swala ni vipi wewe bado mwana CCM chama ambcho ni cha Nyerere alowaanzisha mfumo kristu?
 
Alaa mkuu wangu, haya ya kumpokea Mwinyi yametoka wapi?... mbona hata miye namkumbuka vizuri sana akija Mahiwa kuvizia mwali pale mtaani?..Swala ni vipi wewe bado mwana CCM chama ambcho ni cha Nyerere alowaanzisha mfumo kristu?

Nyerere yuko wapi?
 

Siku zile mchungaji wake huyo kondoo aliyepotea alimwambia Kikwete ni chaguo la mungu.
 
Alaa si kisha kufa sasa wewe vipi bado unaendelea kuwa mwanachama wa chama chake ambacho kinatukuza mfumo kristu kwa vitendo maanake sielewi hata mnachokilalamikia wakati nyie wenyewe ndio mnaongoza nchi, huyo Nyerere hayupo tena.

Ni rahisi sana kubomowa, si rahisi kujenga. Ikiwa nyumba inayomchukuwa mtu miaka 2 kuijenga unaweza kuibomowa kwa siku moja tu, sasa piga hesabu nchi iliyobomolewa kwa miaka 44 mfululizo, itachukuwa muda gani kuijenga? Nakwambia miaka 44 kwa kuwa Nyerere 24, chaguo lake la kwanza 10, chaguo lake la pili 10.

Nchi hii ndio kwanza Kikwete kaanza kuijenga ipasavyo, kumbuka kuwa yeye tu hakuwa chaguo la Nyerere na yeye ndiye tunashuhudia akileta mabadiliko ya kweli ya utawala mpaka ya uchumi.

Hata wapigania Uhuru waliosahauliwa na Nyerere na vikaragosi vyake kwa miaka 44 tumeona wakikumbukwa rasmi kwa mara ya kwanza kwenye awamu hii ya uongozi.
 
Kujua kusema kunatoka kwa sauti za wengine nakuziiga lakini hawezi kusema unayofikiria mwenyewe.

Ungekuwa na ujasiri ungetolea mfano wa kile ambacho ninakisema ambacho wengine wamekisema...(narudia kikasuku)...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…