Ritz, katika huu mjadala peke yake mpaka dakika hii umefikisha posti
840, mimi hata
150 sijafikisha!...mtu pekee aliyekuzidi ni huyo mchochezi, mwalimu wako
Mohamed Said, kwa posti zinazokaribia
2,000! Yaani katika siku
45 za huu mjadala amechangia mara
2000 sawa na
post mbili kila baada ya saa moja!
Sehemu kubwa ya michango yako unamtaka asimulie historia ya wazee wa Kimanyema wa Gerezani, simulizi ambazo tayari anadai ziko ndani ya vitabu alivyoandika...kwa nini usinunue tu hivyo vitabu uvisome ama kama huwezi hivyo umtumie
PM akusimulie kama vile alivyosimuliwa na wazee wake?
Mada inasema "Uchochezi wa Mohamed Said...", wewe badala ya kukaa kimya kwa sababu huna lolote jipya la kuchangia, eti unamuomba azidi kumwaga ngano zake humu, et tu Brutus? Ungemsaidia zaidi kama ungemshauri mwalimu wako ajibu maswali anayoulizwa badala ya kushabikia porojo zisizo na mshiko.
Sasa mfikishie haya maswali;
- Ni lini EAMWS iliyoanzishwa na wakuja (immigrants) na ikapata upingamizi mkubwa kutoka kwa wenye mji wakati wa kuanzishwa kwake, ilitwaliwa na hao wenye nchi (wazee wake!) kama jumuiya na mali yao?
- Ni kitu gani kilipelekea kutoelewana baina ya Waislaam wazawa na Waislaam wakuja wakati wa kuanzishwa kwa Jamaitul al-Islamiyya mwaka 1930s hadi kukawa na misikiti aina mbili...ya wakuja na ya "viroboto"?
- Kwa nini Waislaam ambao ndio wanadaiwa vinara wa harakati za uhuru na walikuwa wengi maradufu miongoni mwa waasisi wa TANU hawakumpa uongozi Muislaam mwenzao Abdulwahid Sykes badala ya Mkatoliki Nyerere?
- Na hata baada ya kumpa uongozi huku uwezo wake ukiwa haumfikii kijana wao mpendwa Abdulwahid Sykes na dai la dalili za upendeleo kwa Wakristo kuanza kuonekana wazi wazi kwa nini hawakumtosa mapema Nyerere kabla ya uhuru?
- Kwa nini huyu mchochezi anadai Mwalimu Nyerere aliwageuka Waislaam baada ya uhuru na huku ushahidi upo wazi kwamba wakorofi ambao hawakumtaka walikuwapo hata kabla ya uhuru, mfano mkubwa ukiwa AMNUT?
- Kwa nini kila serikali ya awamu ya kwanza ilipochukua hatua dhidi ya wakorofi wachache, lawama anapewa Nyerere lakini hivi sasa wakorofi wanaposhughulikiwa, hakuna anayemnyooshea kidole Jakaya Kikwete?
- Kwa nini fujo za Mwembe Chai zilizofanyika wakati wa Rais Ali Hasan Mwinyi, ambazo ndizo chimbuko la zile za mwaka 1998 huyu mdini anazifumbia macho lakini zilizotokea wakati wa Benjamin Mkapa kazishupalia sana?
- Ingawaje kwa sasa viongozi wote wa juu ni Waislaam, ni mfumo Kristo ndio unaolaumiwa kama kiini cha matatizo yetu, je mambo yangekuwaje hivi leo kama viongozi wote wa juu hivi leo wangekuwa Wakristo?
- Wakati Mwalimu anataifisha shule ili Watanganyika wote waweze kupata elimu bila kubaguana kwa misingi ya dini, ni shule ngapi za wazee wa huyu mchochezi zilitaifishwa? Ama hao wazee tayari walikuwa wamebinafsisha shule za AgaKhan na Bohora?
Mwisho natoa ombi kwa jamii yote ya JF mnaofuatilia huu mjadala...kwa kweli ni bahati ilioje tumepata fursa ya kuona jinsi uongo ukirudiwa rudiwa bila kuhojiwa, huweza kuwaathiri wengi akiwepo na huyo aliyeuanzisha. Wazee wetu walipigania uhuru si kama Waislaam au Wakristo, si kama wazawa au wakuja, si kama wapwani au wabara, si kama Wazaramo au Wahaya, Wadengereko au Wasukuma, Wamanyema au Wachaga, Warufiji au Wanyakyusa...walipigana kama Watanganyika, period.
Hivyo si ajabu kwamba hata yeye
Mohamed Said hivi sasa anaamini kwa dhati kuwa anayoyasimulia ndiyo ya ukweli, hiyo ndiyo tabia chafu ya uwongo, haimbakizi mtu pamoja na aliyeuanza! Uongo usiachwe bila kupingwa kwani wako waovu miongoni mwetu ambao watautumia huo mwanya kutugawa na kututoa katika misingi imara ya undugu na upendo uliojengeka kwa muda mrefu. Bahati mbaya tunayo serikali iliyojipa likizo, ina macho lakini haioni, ina masikio lakini haisikii...ipo kwenye usingizi mzito na viongozi wake wapo wapo tu. Ni kweli watu kama
Mohamed Said, kwenye utawala usioogopa kuchukua hatua madhubuti kwa wakati muafaka, hangedumu akipanda hii mbegu ya chuki, angeshughulikiwa na vyombo vya dola mara moja...my heart bleeds for my country!