Kitabu cha Obama kinaelezea historia ya Tanganyika.
Leo nimeamini kuwa wewe kweli ni mzaliwa wa Gerezani na dunia yako yote uliyoijua utotoni ni Gerezani...your whole world, not only Tanganyika, your whole world was Gerezani. As far you knew, there was no world outside Dar es Salaam, no people or activity outside Gerezani!Mag3,
Ah ndugu yangu unazungumza "heart bleeding" leo tuna miaka 51 ya uhuru. Mie nimekueleza hapa habari za babu yangu Salum Abdallah 1947 kapambana na Waingereza kwenye migomo ya wafanyakazi.
Nimekuleza toka 1920s yuko na African Association. 1953 anashiriki katika mikutano ya siri kuunda TANU.
1955 anaasisi TRAU nk.nk. 1960 akiwa mwenyekiti wa TRAU kaongoza mgomo wa relwe ulodumu siku 82.
Haijatokea na haitatokea. 1964 kawekwa kizuizini. Ndugu yangu leo unataka unipe mie mjukuu wa mzalendo huyu
slogans na rhetorics za "my country!"
Try another one. Hayo mengine nawaachia wengine.
Exactly that is point.
Kusema kweli mara ya kwanza nimemsoma mwaka 2004 kidogo niingie mtegoni. Ingawa ni kweli anajua kuyaweka maandishi yake kwenye mtirriko mzuri kiasi kwamba usipokuwa makini utamkubali. Lakini kidogo kidogo nikaanza kuupata ukweli fulani kuhusu motives zake kwenye barza moja maarufu ya kahawa, hayakuwa maongezi ya wazi sana lakini niliwaelewa.
Lakini pia ndani ya JF amewekwa wazi sana ingawa ana courage ya kuzungusha maneno. Amewasomba wengi kwa miaka kadhaa hasa kutoka imani fulani japo miongoni mwao wameanza kuwa na mashaka, ndio maana utasikia "Niko hapa kutoa darsa".........Huwa nacheka sana"
Hadi hivi sasa:
Bw. Mohammed Said,
1. Ameshindwa kuthibitisha una dhulma dhidi ya Waislamu na Uislamu - kwani kuna ushahidi wa kutosha wa mafanikio makubwa ya Waislamu wa Tanzania tangu kabla ya huru hadi hivi leo. Wasomi, watendaji, wafanyabiashara, walimu, madaktari n.k
2. Ameshindwa kutoa ushahidi hata mmoja wa tendo lolote la Baba wa Taifa Mwalimu J. K. Nyerere dhidi ya Uislamu. Ila ametoa ushahidi wa kutosha wa jinsi Nyerere alivyowaheshimu Waislamu, alivyojichanganya nao na alivyoyaweka maisha yake mikononi mwao. Jinsi walivyomkarimu. Nyerere hata mara moja hajawahi kuacha kusema wema huu... ameusema kwenye kitabu chake 1985, amesema kwenye 'We Must Run While They Walk' na amesema kwenye mahojiano mengine mengi throughout his years in public service
3. Ameshindwa kutoa uthibitisho wowote kuwa Kanisa la Tanzania limewahi kuutangaza Uislamu kama ni adui na kuanza kupunguza kukua kwake. Alipodaiwa kutoa ushahidi wa nani aliwahi kutangaza hilo akamtaka Cardinal Levigerie - kutoka Algeria! Ni sawasawa na kusema tutumie maneno ya Sheh mmoja Saudia dhidi ya Kanisa halafu tuseme ndio kawaagiza Waislamu wa Tanzania!
4. Ameshindwa kuonesha kuwa lolote ambalo liliwatokea Wazee wa Kiislamu halikuwatokea wazee wa Kikristu. Kufungwa walifungwa Wakristu na Waislamu, kuwa deported wamewahi kuwa deported hata Wakristu tena Padre! Kuvunjwa kwa EAMWS na kutaifishwa kwa shule na mahospitali za Makanisa kwa Nyerere vyote vilikuwa havijali dini!
5. Ameshindwa kuonesha hata mara moja kuwa Abdulwahid Sykes katika maisha yake amewahi kumtuhumu Nyerere udini au kuonesha andiko lolote la Abdulwahid kuwa Nyerere aliukwa mdini au akiwadhulumu Waislamu.
6. Ameshindwa kuonesha kutoka kwa mlolongo wa wazee wake yeyote ambaye wakati wote wa utawala wa Nyerere hadi anang'atuka kama kulikuwa na ugomvi kati ya Nyerere na Waislamu. Mgogoro pekee ambao Nyerere ulikuwepo kwa muda mrefu mara baada ya uhuru ni makundi ya watu waliokuwa wanajaribu kudhoofisha taifa changa (sabotaging). Katika hili Nyerere hakuangalia sura. Kwa maandiko yake mwenyewe hadi katikati ya miaka ya sabini Nyerere alikuwa na mahusiano mazuri tu na wazee wake! Na Nyerere hakusahau kamwe fadhila yao kwake.
Kimsingi, kuamini simulizi la histohisia la Bw. Said ni kuamini kuwa mwezi umetengenezwa kwa jibini!
Leo nimeamini kuwa wewe kweli ni mzaliwa wa Gerezani na dunia yako yote uliyoijua utotoni ni Gerezani...your whole world, not only Tanganyika, your whole world was Gerezani. As far you knew, there was no world outside Dar es Salaam, no people or activity outside Gerezani!
- Unajua kabisa kwamba mtu wa kwanza kuwa na wazo la kuunda chombo kilichowakutanisha pamoja wafanyakazi (civil servants) ni Martin Kayamba mwaka 1922 lakini kwa kuwa hakuwa moja wa wazee wako umebakia tu kumsimanga.
- Unajua kwamba watu wa kwanza kufikiria wazo la kuunda chama cha wafanyakazi kulinda maslahi yao ni madereva wa Moshi mwaka 1927 lakini kwa kuwa hawakuwa watu wa Dar es Salaam hata kuwataja unasita.
- Unajua kwamba chama cha kwanza kuundwa rasmi kushughulikia maslahi ya wafanyakazi wa Railways kiliundwa nje ya Dar es Salaam kwenye Jimbo la Nyanda za Juu Kusini mwaka 1944 lakini mmh!
- Unajua kwamba mgomo wa kwanza dhidi ya mkoloni ulifanywa na wafanyakazi bandarini Tanga mwaka 1937 ambapo watu 250 walisusia kazi kwa siku mbili.
- Unajua kwamba nje ya vyama vya wafanyakazi vilikuwepo vyama vya wakulima vilivyokuwa hasa ndio chimbuko la hamasa dhidi ya wakoloni lakini toka lini mzaliwa wa Gerezani akalijua jembe?
Ningeweza kueleza mengi lakini kwa nini nihangaike? Wewe ulifanya utafiti halafu ukaandika vitabu; hapo nyuma niliwahi kukulinganisha na kipofu anayemgusa tembo, bahati mbaya anaugusa tu mguu na kutoka mkuku akimwelezea tembo kama gogo la mti...ndio, ndilo umbo la tembo aliloligusa, kwa nini nibishane na kipofu?
mkuu nasikia Shekhe Ilunga kakamatwa kwa uchochezi, utapona kweli?
MM,
Wala sina haja ya kukujibu hili.
Ila nakushauri usome sura mbili za kitabu cha Njozi
Mwembechai Killings.
Kitu kimoja umenifurahisha sana.
Kweli dunia yangu yote ilikuwa Gerezani tena mpaka leo.
Alfajir ikiwa nimekuja mjini nitakwenda Kipata, Mbaruku,
Livingstone maana nyakati hizo ni rahisi kupita.
Hakika hii ndiyo ilikuwa dunia yangu udogoni.
Halafu ukubwani Allah akanifungulia ulimwengu...
Alhamdulilah.
Nimemsoma Njozi vizuri sana na nimewahi kumuhoji kuhusu kitabu chake. Njozi amefanya kazi nzuri zaidi ya kutetea hoja yake. Ukimsoma Njozi utaona kuwa tatizo lake ni CCM. Yeye hakuandika ili kutetea wazee 'wake'. Yeye alishambulia moja kwa moja chama tawala na kutaja kuwa ni tatizo kwa Waislamu. CCM - kwa maoni ya Prof. Njozi - ndiyo janga kubwa kwa Waislamu. Hujajaribu hata kidogo kujenga hoja kama Njozi - not even close.
Ndio sababu ya Kitabu cha Prof. Njozi kufungiwa.
Wewe jamaa bana eti Prof. Njozi tatizo lake ni CCM umemuhoji.
Vitu vingine inabidi mtu ucheke tu humjui Prof. Njozi wewe ulimuhoji sisi tumeishi naye. Ulimuuliza kuhusu Nyerere anamchukuliaje?
Kitabu chake ninacho na nimekisoma ndiyo maana nimekuuliza ulimuhoji Prof. Njozi fikra zake kuhusu Nyerere.Mmh.. well soma Mwembechai utaona jinsi anavyoishushia lawama CCM. Lakini ni Njozi huyo huyo ambaye leo hii katika chuo cha Waislamu Morogoro asilimia 80 ya wakufunzi ni Wakristu (kwa mahojiano yake a couple of years ago). Leo unamsikia anamlalamikia Nyerere na CCM?
Hivi Ritz hujajiuliza kwanini Mohammed Said hana tatizo na CCM?
Kitabu chake ninacho na nimekisoma ndiyo maana nimekuuliza ulimuhoji Prof. Njozi fikra zake kuhusu Nyerere.
Naona unamsemea Mohamed Said kuhusu CCM ukimsoma vizuri utaona siasa zake zimeishia TANU baada ya wazee kutangulia mbele ya haki.
your mental acumen is well below par.
Z,
Kwa kawaida huwa sijibu vitu kama hivi lakini kwa kuwa inaelekea
hiyo ni moja ya nguzo zenu nitasema lau kwa uchache ili tufahamiane.
Hassan Nasralla mwanae aliuliwa katika vita na Wayahudi.
Watu wakenda nyumbani kwake kumpa pole kwa msiba ulomfika.
Ilipofika wakati wa yeye kutoa shukurani akasema kuwa siku zote
yeye alipokuwa miongoni mwao yeye akiinamisha shingo yake.
Lakini kuanzia muda ule na yeye sasa atakuwa anatembea shingo
yake iko juu kwa kuwa yeye kama wale wenzake ametoa shahidi.
Nadhani umenielewa.
La ikiwa hukunifahamu nieleze nitasherehesha Insha Allah.
Ila nataka nikueleze kitu kimoja tu.
Mimi si mwoga.
Sitishwi na vitimbi ndiyo ukaona nimeingia humu na jina langu.
Jaribu kujadiliana na kila mtu basi kwa uzuri.Kuwa kama Mohammed Said anayejibu kila mtu.Mbona najadiliana na wewe vizuri tu...?
Misitari yenye maana hii umeirudia mara nyingi sana.Umekuwa kama unaweweseka vile.Hadi hivi sasa:
Bw. Mohammed Said,
1. Ameshindwa kuthibitisha una dhulma dhidi ya Waislamu na Uislamu - kwani kuna ushahidi wa kutosha wa mafanikio makubwa ya Waislamu wa Tanzania tangu kabla ya huru hadi hivi leo. Wasomi, watendaji, wafanyabiashara, walimu, madaktari n.k
2. Ameshindwa kutoa ushahidi hata mmoja wa tendo lolote la Baba wa Taifa Mwalimu J. K. Nyerere dhidi ya Uislamu. Ila ametoa ushahidi wa kutosha wa jinsi Nyerere alivyowaheshimu Waislamu, alivyojichanganya nao na alivyoyaweka maisha yake mikononi mwao. Jinsi walivyomkarimu. Nyerere hata mara moja hajawahi kuacha kusema wema huu... ameusema kwenye kitabu chake 1985, amesema kwenye 'We Must Run While They Walk' na amesema kwenye mahojiano mengine mengi throughout his years in public service
3. Ameshindwa kutoa uthibitisho wowote kuwa Kanisa la Tanzania limewahi kuutangaza Uislamu kama ni adui na kuanza kupunguza kukua kwake. Alipodaiwa kutoa ushahidi wa nani aliwahi kutangaza hilo akamtaka Cardinal Levigerie - kutoka Algeria! Ni sawasawa na kusema tutumie maneno ya Sheh mmoja Saudia dhidi ya Kanisa halafu tuseme ndio kawaagiza Waislamu wa Tanzania!
4. Ameshindwa kuonesha kuwa lolote ambalo liliwatokea Wazee wa Kiislamu halikuwatokea wazee wa Kikristu. Kufungwa walifungwa Wakristu na Waislamu, kuwa deported wamewahi kuwa deported hata Wakristu tena Padre! Kuvunjwa kwa EAMWS na kutaifishwa kwa shule na mahospitali za Makanisa kwa Nyerere vyote vilikuwa havijali dini!
5. Ameshindwa kuonesha hata mara moja kuwa Abdulwahid Sykes katika maisha yake amewahi kumtuhumu Nyerere udini au kuonesha andiko lolote la Abdulwahid kuwa Nyerere aliukwa mdini au akiwadhulumu Waislamu.
6. Ameshindwa kuonesha kutoka kwa mlolongo wa wazee wake yeyote ambaye wakati wote wa utawala wa Nyerere hadi anang'atuka kama kulikuwa na ugomvi kati ya Nyerere na Waislamu. Mgogoro pekee ambao Nyerere ulikuwepo kwa muda mrefu mara baada ya uhuru ni makundi ya watu waliokuwa wanajaribu kudhoofisha taifa changa (sabotaging). Katika hili Nyerere hakuangalia sura. Kwa maandiko yake mwenyewe hadi katikati ya miaka ya sabini Nyerere alikuwa na mahusiano mazuri tu na wazee wake! Na Nyerere hakusahau kamwe fadhila yao kwake.
Kimsingi, kuamini simulizi la histohisia la Bw. Said ni kuamini kuwa mwezi umetengenezwa kwa jibini!
Mzee hapa umeonesha uanaume wako na hapa sunna imefanyakazi hata mtume alisema yeye na uoga ni umbali kati ya mashariki na magharibi hakuna kumuogopa kiumbe aliyepita njia mbili za mkojo si maneno yangu ni maneno ya ulamaa HASSAN AL BASSARY hawa ni wanafunzi wa maswahaba wa mtume,KIUMBE ALIYEUMBWA KWA MANII UMUOGOPE HAIJI MZEE BIG UP KWA HILO KUMKAMATA ILUNGA SIO SULUHISHO LA DHULMA NCHI HII NA MFUMO KRISTO.
Jaribu kujadiliana na kila mtu basi kwa uzuri.Kuwa kama Mohammed Said anayejibu kila mtu.
Kuchagua watu wa kujadiliana nao kuna maana gani?.Unawaogopa wengine au umeishiwa na hoja hivyo unatafuta maeneo rahisi ya kuendelea na ubishi.