Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


MS, nimemsoma pia amesema hakuna cha Kiatu wala nani.
 

MM,

Uislam umekamilika.
Nikiwa na chuki nitakuwa nimekwenda kinyume na mafunzo ya Allah.

Isome historia ya uhuru wa Tanganyika ndipo utathamini wema wa
wazee wetu.

Kisha watazame Waislam walilipwa nini?

Allah anawaeleza Waislam katika Qur'an kuwa, ''Msidhulumu na wala
msikubali kudhulumiwa.''

Mimi napigania dhulma iondoke na haki itawale na haya nisemayo humu
nina ushahidi na ndiyo unaona sijapata kujificha nimeingia hapa na jina
langu kamili na haya Insha Allah nitayasema popote bila hofu.
 
MS, nimemsoma pia amesema hakuna cha Kiatu wala nani.

GG,

Hakika lipo tatizo.
Leo Mshume Kiyate mtu karim na muungwana.

Mshume aliyemvisha kilemba Nyerere baada ya
maasi ya jeshi kumtia moyo leo anatukanwa bila
hofu.

Hakika Allah amesema kweli.
 
mmh kweli wee mbaguzi.

yaani hujui kabisa hio ndio miamba na majabai makubwa sana katika kuijenga TANU?

Ama kweli umekosa fadhwila.

Baru,

Mimi msimamo wangu ni kuwa na dhana nzuri na watu ambao wanatoa jeuri.

Moja kwa moja nakwenda mbali katika makuzi kisha naja sasa nasema huenda
anasema asemayo kwa kuwa haijui historiya wa watu hawa.

Nikifika hapa najipa jukumu la kumuelewesha.

Huyu kijana inaelekea hajui kuwa Mshume Kiyate alikuwa mmoja wa wafadhili
wakubwa wa Nyerere na TANU.

Laiti labda historia ya waze hawa ingethaminiwa na ikafahamika huyu asingekuja
na kibri hiki.

Kwa ufupi ni kumuwia radhi na kumueleza.
 

Kwa mara nyingine tena, Vatican si taasisi ya kidini. Ni sovereign. Kama ni kuvunja uhusiano na Vatican basi tuvunje uhusiano na Iran na Saudi Arabia ambazo zinatawaliwa kwa misingi ya kidini.
 
Mimi napigania dhulma iondoke na haki itawale na haya nisemayo humu
nina ushahidi na ndiyo unaona sijapata kujificha nimeingia hapa na jina
langu kamili na haya Insha Allah nitayasema popote bila hofu.

Mzee Said, hupiganii dhulma iondoke; unatengeneza dhulma nyingine. Qurani inaenda mbali zaidi kwani haiishi kusema hivyo unadai. Inasema pia: Wa Jazā'u Sayyi'atin Sayyi'atun Mithluhā ۖ Faman `Afā Wa 'Aşlaĥa Fa'ajruhu `Alá Al-Lahi ۚ 'Innahu Lā Yuĥibbu Až-Žālimīna (42:40). Ni bora kupatanisha (suluhu) kuliko kulipiza kisasi. Mzee Said umefanya nini ili kuziletea jumuiya zetu hizi mbili pamoja katika kupatanisha? Ni lini umejaribu kukaa na viongozi wa Kikristu au kuwashawisi mashehe kukaa na viongozi wa Kikristu kuyaangalia madai yako? Ni lini umejaribu kutumia majukwaa unayopata kuzungumza lugha ya suluhu na upatano badala ya lugha ya utengano, kisasi na kupasha moto hisia za watu?

Mzee Said iheshimu dini yako na uwe mkweli kwa taifa lako. Usijitahidi kubomoa jaribu kujenga. Wazee wetu walifanya mema kwa pamoja, walishirikiana kwa umoja, na katika changamoto nyingi wametupatia taifa hili tulilonalo. Kwanini leo mwenzetu unajitahidi kututenganisha kwa kupotosha historia? Kwanini leo mwenzetu unaandika historia ya "Wazalendo Waislamu waliosahaulika" badala ya kuandika juu ya "Wazalendo waliosahaulika"? Of course najua jibu lako - hao wakristu siyo wazee wako! Wewe ulitaka kuandika wazee wako - Waislamu tu.

Mola akusaidie kuona dhulma unayoifanya kwa jina la kupinga dhulma. Mzee Said uondoa uovu kwa wema Qurani inasema: Adfa` Bi-Atī Hiya 'Aĥsanu As-Sayyi'ata ۚ Naĥnu 'A`lamu Bimā Yaşifūna (23:96). Ulipe uovu kwa wema; umeona dhulma mzee Said tuoneshhe katika kutenda mema. Qurani haisemi upinge tu dhulma lakini vile vile utende hisani na wema; kwa ndugu, wazazi, jirani, n.k

Mzee Said ukiona watu wanatumia Uislamu kuchoma makanisa uwe wa kwanza kulaani siyo kutafuta udhuru wa kwanini wamefanya hivyo; ukiona watu wanafanya ubaya kwa jina la Uislamu dhidi ya ndugu zao uwe wa kwanza kukataa uovu uovu huo. Vinginevyo, wewe mwenyewe unaonekana ni sehemu ya kutetea uovu huo na kuuchochea kwa jina la kupinga dhulma. HIyo siyo dini.
 
Kwa mara nyingine tena, Vatican si taasisi ya kidini. Ni sovereign. Kama ni kuvunja uhusiano na Vatican basi tuvunje uhusiano na Iran na Saudi Arabia ambazo zinatawaliwa kwa misingi ya kidini.

Jasusi,

Tanzania ndipo ilipo hapo hivi sasa.
Hakuna anaemtakia kheri mwenzake.

Tunatazamana kwa jicho baya sana.
Inatisha na inasikitisha.
 

MM,

Nitakujibu moja tu.

Muislam akitoka kwenda kuchoma kanisa
huo ni wazimu wake.

Hayo si mafunzo ya Allah wala Mtume wake
SAW.
 

Mzee Saidi hili la hansard najua limekuchoma vilivyo and I know why, ulikuwa hujawahi kuiona miaka yote hii ya kitabu chako ukijiita mtafifiti na mwanahistoria ya Tanganyika ulikuwa hujui kuhusu hii document ambayo ilikuwa ndiyo centre ya huo uhuru. What a joke???????? Kama nilivyosema mwanzo unasumbuliwa na ushindani ("trophy collecting mentallity"). Ni aibu kwa mtu wa nafasi yako badala ya kuleta hoja unaleta viroja nimekushauri hiyo waachie vijana wako.

Ngoja nikukumbushe kidogo tulikotokea ile asubuhi!!!!!!


Nikakujibu, na hoja ikiwa hansard si sawa na kujinukuu!!!!!! Lakini pia nikajibu hoja yako kwa kutoa maandiko yafuatayo nikitegemea utakuwa mtulivu upate darsa, maana wewe umeelezea uwepo wa tukio mimi nimetoa baadhi ya contents

Unayafahamu haya hapa chini????


Ukajibu kama ifuatavyo:

Nyambala,

Sijapata kuiona hiyo document.

Nitashukuru kama utaiweka yote.

Nakushukuru kwa juhudi hizi zako.

Kumbuka nilikuaga mida ile kuwa naelekea kwa kazi jambo ambalo si la kawaida humu maana it's easy unalog ou tu,

Naenda kwa kazi tuonane bidae.

ukanijibu:

Insha Allah ndugu yangu.
.

Sasa nashangaa hata sijarudi tambo zilishaanza kwa vijana wako, ni ustaarabu wa wapi huuu mzee Saidi, lakini huu ni uthibitisho mwingine kwamba una nia ovu na hivyo basi muda wowote anapotokea mtu kuweka records straight inakughafirisha sana.

Mzee Saidi unatakiwa ufahamu haya nayowakilisha wala si kwa juhudi ni mambo yapo kwa mtu yeyote if you want to know.

Kwa kusaidia tu hayo maandiko yenye ushahidi ni jinsi gani hao jamaa wa TAA wakiongozwa na Abdu Sykes walikuwa hawakujiandaa na hawana umoja zinapatikana kuanzia pg 177 ndani ya kitabu "
Voices from Tanganyika: Great Britian, the United Nations and the Decolonization of a Trust Territory, 1946-1961" by Ulrich Lohrmann. Tafuta hiki kitabu kitakusaidia sana kabla hujaendelea kujiumbua.

The last one kwa faida ya Mkanasha, wanajamvi na vijana wako "Unaweza kututajia wazee waliokuwa na Nyerere kwenye negotiating team na waingereza kuhusu upatikanaji uhuru wa Tanganyika??" Please. Maana hiyo ndiyo hasa ilikuwa nguzo ya kupatikana uhuru Dec 09, 1961. If not basi usipepese sema sijui utapewa darasa.
Inshalah tutaonana panapo majaliwa .


 

Wewe ungekuwa unajua ustaraabu na umefunzwa adabu na wazazi wako wala usingethubutu na kujaribu kumuita Marehemu Mzee Mshume Kiyate, KIATU.
 
Mkuu wangu zumbemkuu unamshangaa Mohamed Said kumlinganisha zomba mzee wa kucopy na kupesti aliyetolewa kamasi na Matola .

Ukweli ni kwamba ukitafuta vichwa vitano vya ukweli hapa JF Mkuu nguruvi yumo.Ngoja niandae list yangu Nguruvi3 Mchambuzi Mzee Mwanakijiji Jasusi Mag3 ....Mpaka hapo Ustadhi Moh na mpiga tarumbeta wake hawajaingia.Nikiandaa list nyingine ya 10 bora bado jina la zomba halitii pua kabisa labda 1000 a itategemea mnajadili nini.

Ukianzishwa mjadala wa kuisifu CCM ya Kikwete zomba anaweka akili kando anakimbilia madata ya kuchongo hata kama hayana uhalisia.Ukiijadili CCM ya Mkapa zomba atamponda ukiijadili CCM ya Mzee Ruksa zomba huyo huyo ataisifu bila kujali kipindi cha Mzee Ruksa MoU iliasisiwa na vurugu za Mwembechai atatupiwa Mrema Mwinyi hausiki kabisa ha ha ha.
Mzee wangu Mo ukifika mahali ukasifu hata visivyosifiwa unapunguza heshima yako ingawa tayari sioni kabisa.



dah!
hii kali ya mwaka. zomba ni zaidi ya Nguruvi3 ????????????????????
 
Last edited by a moderator:
Ewe Mwenyezi Mungu uzidi kumjaza Mzee huyu roho ya hekima na maarifa kama ya Nabii Suleimani.Umtembelee Mzee Mohamedi kama ulivyomgusa Sauli.Ninakuomba Baba yetu uliye mbinguni uzidi kuimarisha upendo,mshikamano na amani miongoni mwetu Watanzania.Amina.
 
Kwa mara nyingine tena, Vatican si taasisi ya kidini. Ni sovereign. Kama ni kuvunja uhusiano na Vatican basi tuvunje uhusiano na Iran na Saudi Arabia ambazo zinatawaliwa kwa misingi ya kidini.

Jasusi,

Nipe hoja za kisheria zinazosema kuwa vatican ni nchi? Nimebishana nanyie katika Memorandum of Understanding mmeshindwa kuniletea hoja za msingi nikiwauliza ni hoja gani za msingi zinazoifanya Vatican ambayo hakuna wazawa iitwe nchi? Vile vile ni hoja gani za msingi mnaweza kutuambia tofauti ya Holy See na Vatican ni ipi? Vilevile tuambiwe ni mtoto gani alizaliwa Vatican akakulia vatican akafa vatican. Vyenginevyo tuambieni huo uhusiano wa nchi mmueutoa wapi?
 

Hoja mfu kama hizi unapaswa kupeleka kwenye mihadhara na vijiwe vya kahawa. if you don't mind be friend of Google he will educate you enough than wasting our time.
 

Nini tofauti kati ya moderat and extreme muslims?
 

Unajua sisi watani wetu ni wasambaa! bila shaka wewe ni Msambaa bisha nikupe ushahidi!
 
Mkuu Jasusi asante sana kwa kisa hiki cha kusisimua sasa pata picha kama Aikael Mbowe angekuwa mzee wa Gerezani nakwambia Mzee wetu Mohamed Said angemwandika page 20 kuelezea kisa hiki kwa mbwembwe na mashamshamu ya kufa mtu.

.......
 
Hoja mfu kama hizi unapaswa kupeleka kwenye mihadhara na vijiwe vya kahawa. if you don't mind be friend of Google he will educate you enough than wasting our time.

If you say Google is your reference my friend you are one of shallowest thinker in JF I have came across with. Google really !!!!! Tell me which act of law? Which ruling? Which international law that states the characteristics that vatican has constitute a sovereign nation!!!! Otherwise mnaishushia hadhi JF ndugu.
 
Reactions: Ami
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…