Twende Kazi,
Inawezekana kwa kuwa wewe ni Mkristo ukawa
hujui madhila yanayowasibu Waislam katika elimu,
kazi na fursa nyinginezo.
Huhisi ubaguzi.
Inawezekana kabisa.
Kuna Waislam hivi sasa wako mahakamani na wako rumande Segerea.
Ni vijana wadogo walikamatwa wakitoka msikitini Ijumaa mbili zilizopita.
Wanashtakiwa kwa kosa la kuandamana.
Vijana wanamuuliza hakimu nini maandamano.
Hakimu akaeleza.
Vijana wakazema hapo tulipokamatiwa sisi wala hapakuwa na maandamano
ila tuliona watu wakiwakamata waliovaa kanzu na mimi nilikuwa nimevaa kanzu.
Kosa langu ni hilo lakini sikuwa naandamana na maandamano yenyewe hayakuwapo.
Wajerumani Vita Vya Pili Vya Dunia wanawapiga na kuwatesa Wayahudi kisha wanawauliza
hivi mnajuakwa nini tunakupigeni?
Tunajisikia raha tukikupigeni.
Hapa ndipo tulipoifikisha Tanzania.
Kuonekana na alama za Uislam unahatarisha maisha yako si njiani hata shule, vyuoni na makazini.
Katika hali kama hii nani wa kuonewa huruma?
Mohamed, tumesema sana kuwa madhaila ya elimu ambayo ni precussor ya employment wanayo waislam wenyewe.Period!
Narudia kila siku kukuambia kuwa kama huna shule hutakuwa na wanafunzi, kama huna wanafunzi hutakuwa na wataalam. Kilwa wamejengewa shule na wamekimbia shule imefungwa.
Mzee Said badala ya kwenda Kilwa kuwaeleza hatari inayowakabili katika dunia ya leo ya ushindani, yeye anawadanganya kuwa ukiitwa Mohame, Muhsin, Hafidh, Salim, Mwanameka, Tatu Said automatically una qualify kuwa Lawyer, Doctor, Mwalim au Mhasibu.
Kwa wale msiotuelewa wengine, hapa ndipo tatizo lilipo. Wenyewe wanaita escapism.
Mohamed anajitahidi kuwafurahisha watu hawaaambii ukweli, in the end anawapoteza kabisa.
Mohamed hebu tembelea madrasa zinaoendeshwa na waislam uone hali ilivyo halafu urudi kutuambia madhila.
Walimu wa madrasa wanafanya kazi za kujitolea. Hakuna mfumo maalum wa kuwatambua au kutambua kile wanachokifanya. Hakuna syllabus ni kila mmoja na lake.
Hivi kuna shida gani madrasa zikawa shule za awali, kwamba kuna muda wa dini na muda wa masomo ya kawaida.
Kawaulize wazee wa Gerezani wangapi wanajua uwepo wa madrasa achilia mbali shule n.k.
Wangapi wanajua ustadhi wa madrasa analipwa nini, maana huyu ni mwanadamu ndani ya Dar, hana shamba
Kuhusu vijana kukamatwa, tumewahi kukuambia kuwa wazo la kufunga shule ili kwenda kusikiliza kesi ya Ponda ni chafu.
Huwezi kumtambua mtu kwa vazi na wala huwezi kuuhakikishia ulimwengu kuwa vijana hao walikuwa wamesimama tu.
Unachokifanya hapa ni kutuletea maelezo ya upande mmoja kama yale ya kijana wangu anayekuja na kusema nimepigwa na rafiki yangu na baada ya uchunguzi nagundua kuwa yeye ndiye mchokozi tena mkubwa.
Sisi wazazi wenye busara ndivyo tufanyavyo na si kusikiliza na kukukurupuka tu kwa hamasa
Unapotufanya watu wazima hatuwezi kufikiri unasikitisha. Na mbaya zaidi unasema wewe ni kiongozi wa waislam.
Siku ya ijumaa shule zilifungwa mapema ili vijana wazagae mitaani na kuleta vurugu kama unavyokusudia wewe na kundi lako. Mumegeuza siku ya ibada ya ijumaa kuwa siku ya vurugu.
Haipo katika maandishi yoyote ya dini iwe Kurani, sunna au hadithi. Hili ni jambo mumelizua wewe na kundi lako la vurugu ili kuuchafua uislam. Mnazusha mambo halafu mnasingizia dini.
Ndicho tunachoueleza ulimwengu kuwa Mohamed anachochoea vijana kwenda mitaani wapambane na askari
Hata siku moja Mohamed hayupo katika maandamano, he is in the studio orchestrating chaos.
Na katika kuhakikisha kuwa anatimiza wajibu wake sasa anakuja na madai kuwa vijana wapo magereza huku alijua fika kuwa shule zilifungwa ili waandamane.
Jamani huu kama si unafiki ni kitu gani na je mwenyezi mungu anasamehe kitu hiki.