Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Mzee wangu naomba nizungumze na wewe sio kama mkristo wala muislamu bali kama mtanzania.Mzee wangu unafikiri ni kundi ilo tu unalolitaja ndio linadhulumiwa au kunyanyaswa nchi hii?

Je ni watanzania wangapi wameuwawa kwa kupigwa risasi migodini bila kujali dini zao?Je ni watanzania wangapi wamekosa fursa ya kupata elimu bora bila kujali dini zao?

Je ni watanzania wangapi wamebambikiwa kesi bila kujali dini zao?Je ni watanzani wangapi wameuwawa kwenye maandamano bila kujali dini zao?

Je ni watanzania wangapi wamefia mahospitalini kwa kukosa huduma bila kujali dini zao?Je ni watanzania wangapi wamekufa njaa sababu ya kukosa chakula bila kujali dini zao?Watanzania wangapi Mzee wangu Mohamedi wanateseka ndani ya nchi hii kwa madhila mbalimbali.

Viumbe wa Mwenyezi Mungu wangapi wamepoteza matumaini ya kuishi hapa nchini mwetu bila kujali dini zao?

Mzee wangu nakusihi sana nami nikihisihi nafsi yangu tafadhali naomba ubadilishe aina yako ya uandishi na kama ni haki basi upiganie haki za watanzania kwa ujumla wao.Usitugawe tafadhali.

Kumbuka Mtume anasema unapotaka kufanya jambo angalia mwisho wake kama ni mzuri fanya kama ni mbaya liache.Narudia tena sisi wanyonge tutapoteza kila kitu wewe mwenzetu huna cha kupoteza.Tuonee huruma watanzania wenzio.


......

Twende kazi,
Hii haimhusu Mohamed. Yeye kinachomhusu ni wale wazee wake wa Gerezani ambao historia imewasahau makusudi.

Haya ya watu kubambikiziwa kesi, watu kuuawa kwenye maandamano, kupigwa risasi migodini itamhusuje Mohamed? Kwani hao walikuwa ni waislamu wa Gerezani? Wewe nawe!
 
Mohamed Said Naona kawasahau wazawa wazaramu-na jinsi walivyokuwa forefront wa ukombozi.

"While the Wazaramo Union was gathering supporters and confronting the colonial government in the 1940s, the African Association in Dar es Salaam remained an ineffective petitioning organization, ceding political initiative to provincial branches such as Dodoma and Mwanza. Shortly after it transformed itself into the Tanganyika African Association (TAA) in 1948, the Dar es Salaam headquarters had ‘apparently collapsed entirely'.

165 The organization revived in the wake of proposed constitutional reforms in 1950, when the TAA demanded a stop to further alienation of land to immigrants, as well as to abolish ‘the imposition of Arab Liwalis' and replace them with African
kadhis"

.
 
Jasusi,

Nipe hoja za kisheria zinazosema kuwa vatican ni nchi? Nimebishana nanyie katika Memorandum of Understanding mmeshindwa kuniletea hoja za msingi nikiwauliza ni hoja gani za msingi zinazoifanya Vatican ambayo hakuna wazawa iitwe nchi?

Vile vile ni hoja gani za msingi mnaweza kutuambia tofauti ya Holy See na Vatican ni ipi? Vilevile tuambiwe ni mtoto gani alizaliwa Vatican akakulia vatican akafa vatican.

Vyenginevyo tuambieni huo uhusiano wa nchi mmueutoa wapi?

......

Mdondoaji,|
Kwenye MOU Dr Slaa alijibu na kupiga msumari malalamiko yenu kwamba serikali inagharimia hospitali za makanisa.

Kaitafute ile thread aliyojibu Dr Slaa humu JF ukajikumbushe. Kuhusu Vatican na Holy See tumia google.
 

Mdondoaji,|
Kwenye MOU Dr Slaa alijibu na kupiga msumari malalamiko yenu kwamba serikali inagharimia hospitali za makanisa.

Kaitafute ile thread aliyojibu Dr Slaa humu JF ukajikumbushe. Kuhusu Vatican na Holy See tumia google.

Dr.Slaa alijibu kama nani?
 
Mohamed Said kumbe gazeti la kwanza la mzawa lilikuwa "KWETU" au hii habari si kweli

"Meanwhile,
Kwetu, the
first African-owned newspaper was established in Dar es Salaam by Erica Fiah
in 1937, providing an important sounding board for African Association
members and fellow intelligentsia.
89 The territory's main foreign-owned
newspapers were also published in and distributed from the capital."


 
Last edited by a moderator:
Twende Kazi,

Dua yako ni nzuri sana lakini nitaiongezea mstari mmoja ndipo nami nitaitika AMIN.

''Na Mwenyezi Mungu uondoe fitna yote iliyoingizwa katika jamii yetu baada ya sisi
huko nyuma kuwa ndugu na uindoe dhulma iliyopo iipatikane haki irejeshe kwetu
mapenzi yale yaliyokuwapo baina yetu.''


AMIN.
........
na mimi naongezea ya kwangu...
''Na Mwenyezi Mungu uondoe fitna yote iliyoingizwa katika historia yetu ya Tanganyika na uhuru, ondoa kabisa histohisia za udini, dumisha umoja wetu na amani yetu.''

AAMEN.
 
Twende Kazi,

Inawezekana kwa kuwa wewe ni Mkristo ukawa
hujui madhila yanayowasibu Waislam katika elimu,
kazi na fursa nyinginezo.

Huhisi ubaguzi.
Inawezekana kabisa.

Kuna Waislam hivi sasa wako mahakamani na wako rumande Segerea.

Ni vijana wadogo walikamatwa wakitoka msikitini Ijumaa mbili zilizopita.

Wanashtakiwa kwa kosa la kuandamana.
Vijana wanamuuliza hakimu nini maandamano.

Hakimu akaeleza.

Vijana wakazema hapo tulipokamatiwa sisi wala hapakuwa na maandamano
ila tuliona watu wakiwakamata waliovaa kanzu na mimi nilikuwa nimevaa kanzu.

Kosa langu ni hilo lakini sikuwa naandamana na maandamano yenyewe hayakuwapo.

Wajerumani Vita Vya Pili Vya Dunia wanawapiga na kuwatesa Wayahudi kisha wanawauliza
hivi mnajuakwa nini tunakupigeni?

Tunajisikia raha tukikupigeni.
Hapa ndipo tulipoifikisha Tanzania.

Kuonekana na alama za Uislam unahatarisha maisha yako si njiani hata shule, vyuoni na makazini.
Katika hali kama hii nani wa kuonewa huruma?
Mohamed, tumesema sana kuwa madhaila ya elimu ambayo ni precussor ya employment wanayo waislam wenyewe.Period!

Narudia kila siku kukuambia kuwa kama huna shule hutakuwa na wanafunzi, kama huna wanafunzi hutakuwa na wataalam. Kilwa wamejengewa shule na wamekimbia shule imefungwa.

Mzee Said badala ya kwenda Kilwa kuwaeleza hatari inayowakabili katika dunia ya leo ya ushindani, yeye anawadanganya kuwa ukiitwa Mohame, Muhsin, Hafidh, Salim, Mwanameka, Tatu Said automatically una qualify kuwa Lawyer, Doctor, Mwalim au Mhasibu.

Kwa wale msiotuelewa wengine, hapa ndipo tatizo lilipo. Wenyewe wanaita escapism.
Mohamed anajitahidi kuwafurahisha watu hawaaambii ukweli, in the end anawapoteza kabisa.
Mohamed hebu tembelea madrasa zinaoendeshwa na waislam uone hali ilivyo halafu urudi kutuambia madhila.

Walimu wa madrasa wanafanya kazi za kujitolea. Hakuna mfumo maalum wa kuwatambua au kutambua kile wanachokifanya. Hakuna syllabus ni kila mmoja na lake.

Hivi kuna shida gani madrasa zikawa shule za awali, kwamba kuna muda wa dini na muda wa masomo ya kawaida.
Kawaulize wazee wa Gerezani wangapi wanajua uwepo wa madrasa achilia mbali shule n.k.
Wangapi wanajua ustadhi wa madrasa analipwa nini, maana huyu ni mwanadamu ndani ya Dar, hana shamba

Kuhusu vijana kukamatwa, tumewahi kukuambia kuwa wazo la kufunga shule ili kwenda kusikiliza kesi ya Ponda ni chafu.
Huwezi kumtambua mtu kwa vazi na wala huwezi kuuhakikishia ulimwengu kuwa vijana hao walikuwa wamesimama tu.

Unachokifanya hapa ni kutuletea maelezo ya upande mmoja kama yale ya kijana wangu anayekuja na kusema nimepigwa na rafiki yangu na baada ya uchunguzi nagundua kuwa yeye ndiye mchokozi tena mkubwa.
Sisi wazazi wenye busara ndivyo tufanyavyo na si kusikiliza na kukukurupuka tu kwa hamasa

Unapotufanya watu wazima hatuwezi kufikiri unasikitisha. Na mbaya zaidi unasema wewe ni kiongozi wa waislam.
Siku ya ijumaa shule zilifungwa mapema ili vijana wazagae mitaani na kuleta vurugu kama unavyokusudia wewe na kundi lako. Mumegeuza siku ya ibada ya ijumaa kuwa siku ya vurugu.

Haipo katika maandishi yoyote ya dini iwe Kurani, sunna au hadithi. Hili ni jambo mumelizua wewe na kundi lako la vurugu ili kuuchafua uislam. Mnazusha mambo halafu mnasingizia dini.
Ndicho tunachoueleza ulimwengu kuwa Mohamed anachochoea vijana kwenda mitaani wapambane na askari

Hata siku moja Mohamed hayupo katika maandamano, he is in the studio orchestrating chaos.
Na katika kuhakikisha kuwa anatimiza wajibu wake sasa anakuja na madai kuwa vijana wapo magereza huku alijua fika kuwa shule zilifungwa ili waandamane.

Jamani huu kama si unafiki ni kitu gani na je mwenyezi mungu anasamehe kitu hiki.
 
Mohamed Said kumbe gazeti la kwanza la mzawa lilikuwa "KWETU" au hii habari si kweli

"Meanwhile,
Kwetu, the
first African-owned newspaper was established in Dar es Salaam by Erica Fiah
in 1937, providing an important sounding board for African Association
members and fellow intelligentsia.
89 The territory's main foreign-owned
newspapers were also published in and distributed from the capital."


......

Mkuu gazeti la kwanza liliandikwa kijerumani, kuna kipande cha picha yake nimekiweka hapa, 1911 linaitwa USAMBARA lilichapwa Lushoto, (nimeshangaa babu yangu aliishia darasa la 4 lakini anajua kijerumani balaa.
 
Mkuu gazeti la kwanza liliandikwa kijerumani, kuna kipande cha picha yake nimekiweka hapa, 1911 linaitwa USAMBARA lilichapwa Lushoto, (nimeshangaa babu yangu aliishia darasa la 4 lakini anajua kijerumani balaa.

hilo la usambara nadhani lilikuwa ni mali ya wajerumani-hili kwetu lilikuwa mali ya mzalendo
 
Back
Top Bottom