Naam ndugu yangu! Lakini ngoja tuwasaidie wale ambao wameakuwa wakiamini huu utafiti uchwara wa WARSHA mbele kidogo:
Hoja nzima ya "dhulma" katika elimu inatokana na "utafiti" wa chuo kikuu kimoja tu katika Tanzania nzima. Na katika hicho chuo ni baadhi ya faculties tu zimeangaliwa. Na katika hizo ambazo hazikuangaliwa ni zile ambazo ni muhimu kwa namna ya pekee - Medicine, Kilimo na Veterinary Science. Na ikumbukwe huko kote kilichoangaliwa na majina tu. Yaani, "watafiti" wakachukua kitabu cha majina wakaanza kuangalia nani ana jina la Kikristu na nani ana jina la Kiislamu. Ambaye hakuwa na jina linaloashiria dini yake basi aliwekwa kwenye "wengine" na hata wale ambao wenye majina 'neutral' nao waliwekwa pembeni. Majina kama "Neema, Baraka, Furaha, Daudi" yanawekwa pembeni. Hili tatizo la kwanza - na ni dogo.
Tatizo la pili la "utafiti" wakina Mohammed Said na kundi lake ni kuwa unajaribu kuonesha 'systematic discrimination" katika mfumo wa elimu. Bw. Said hapo nyuma akijinukuu mwenyewe anasema hivi-kwa ujasiri wa kisomi:
Kimsingi anadai kuwa kwa kuangalia 'utafiti' wao huo walifikia hitimisho kuwa kulikuwa na 'sytem' ambayo ilikuwa 'discriminatory to Muslim Youths'. Sasa mtu anaweza kufikia hitimisho hilo kama amefanya utafiti wakutosha - wenye kuhusisha sample ya kutosha na yenye perimeters zinazoeleweka. Kwa kuangalia majina kwenye kitabu peke yake inatosha kweli?
Lakini zaidi la kuudhi ni kweli kwa kuangalia UDSM peke yake tu anaweza kufikia hitimisho la kuweza kuextrapolate his findings to the nation as a whole starting with Ministry of Education?
Mtu yeyote anayesoma takwimu na hata wanaojifunza Research 101 cha kwanza kabisa ni kuwa na sample ya kutosha. Lakini siyo sample tu bali kuna kitu muhimu sana ambacho ni "random sample". Ili uweze kupata matokeo ya kutosha katika utafiti wenye lengo la kupata takwimu fulani basi sample yako ni lazima iwe representative ya general population lakini pia iwe as random as possible. Na pale ambapo unataka kuonesha 'systematic discrimination' kama watu wa WARSHA walivyotaka kufanya basi huwezi kutumia chuo cha elimu ya juu kimoja.
Ili angalau tuweze kupima matokeo yale ni vizuri tungejua mgawanyo (distribution) ya Wakristu, Waislamu na Wengine katika elimu ya juu katika miaka hiyo ilikuwaje:
Chuo cha Uongozi Mzumbe - kilikuwa na intake ya WWW wangapi?
Chuo cha Kilimo Uyole -
Chuo cha Kilimo Morogoro (baadaye Sokoine)
Chuo cha Mifugo Tengeru
Chuo cha Mifugo Mpwapwa
Chuo cha Sanaa Bagamoyo
Taasisi ya Uvuvi Nyegezi
N.k
Na hapo hatujagusa vyuo vya Ualimu, na vyuo vingine vya elimu ya juu vya wakati huo hadi hivi vya sasa. Sasa ni akili gani inamfanya mtu achukue 'matokeo' ya chuo kimoja na kuyafanya yawe ya nchi nzima? HHivi kweli hakuna watu wenye uwezo wa kuwauliza hawa kina Mohammed Said na Warsha validity ya 'utafiti' wao? Hivi kweli hakuna wasomi Tanzania wanaoweza kudebunk this pseudo-research?
Na kweli wapo Waislamu wasomi wenye kuamini 'utafiti' huu? Msingi wa imani yao kwenye utafiti huu ni nini? NI kwa vile wamesema imefanywa na Waislamu? is that enough?