Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
Unajua Ritz, mtu akikuambia Nyerere alikuwa Mmanda na Nkrumah alikuwa Mzanaki nawe ukakubali kuwa hiyo ni ilm mtu huyo atakuwa amekufikisha kiwango cha juu sana cha udhalili. Elimu ni maarifa siyo udanganyifu.Hazina maana kwako wengine wanachota Ilm kutoka kwa Mohamed Said.
Hivi unaamini kuwa Tanzania ni mwanachama wa commonwealth kwasababu ya mfumo Kristo. Hiyo ni Ilm kweli unayoweza kumpa kijana wako kutoka kwa Mohamed Said Abdallah Mwekapopo Muyukwa Semitungo
Hivi mtu akikwambia Nigeria ina waislam wengi barani Afirka haikushughulishi kufikiri zaidi ya hapo unameza nzima nzima bila kutafuna kwasababu ni Ilm.
Hivi mtu akikwambia Nyerere alikwenda sokoni bila kujua bidhaa zinauzwa, ni ilm kweli unayozingatia.
Hivi mtu akikuambia enrollment ya UDSM Muslims vs Christian ni 18 : 82 na kesho akaja akakumabia Muslim vs Non muslim ni 18:82 hapo utakuwa umepata ilm au umevurugwa tu kwasababu upo tayari kumeza kila kinachotupwa ukumbini.
Hivi mtu akikuambia kuwa Nyerere msomi na mwalimu aliandikiwa hotuba na kwenda kuisoma kama kasuku miaka 1950... kukiwa hakuna wasomi unaweza kuitia akilini tu kwasababu ni ilm.
Mtu akisema Darul Iman imenyimwa kibali cha kujenga chuo cha ufundi wakati Islamic foundation imepewa kibali cha kujenga misikiti 700 bado unakubali kuwa hapo pana ilm kubwa.
Leo mtu akikuambia mwaka 1981 Nyerere na BAKWATA walishindwa na Warsha, halafu mtu huyo huyo leo anakuambia BAKWATA ni vibaraka inakuingia akilini mtu huyu anasimamia wapi na je hiyo ni ilm kweli.
Kama ilm ni kuorodhesha majina ya majirani hapo sawa na hilo kila mtu ataamua lakini kama ni zaidi ya hapo vipi Tatu Said na Mwanameka wawe zaidi ya Kyaruzi na Matola.
Ilm ni maarifa na maarifa ndiyo yanampa mtu ilm. Ilm si kumeza bali kutafakari na kumeng'enya. Kumeza ni hatari maana sisi si makinda ya ndege au nyoka. Sisi si wakaa vijiweni ukituambia kitu tunatafuta ukweli wake.