Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
Ami, naona unajaribu kupulizia manukato katika lundo la uvundo.Makosa ya aina hii huwa yanfaywa na kila muandishi na kila msemaji.Lakini kwa watu wa mfumo akifanya Mohammed Said wanakuwa wamepatia sehemu ya kuikandamiza historia halisi ya Tanzania na kutaka ionekane eti ni ngano.
Tumejaribu kukuonyesha kuwa alichofanya Mohamed si makosa madogo ni makosa makubwa kiuandishi na kiutafiti na kwamba hakufanya hivyo kwa bahati mbaya bali alikusudia.
Tuliacha hilo tukidhani somo limeeleweka, inavyoonekana sisi ndiyo tunakuwa ''victim'' wa kuonyesha ukweli kutoka katika maandishi ya Mohamed. Sasa ngoja tukuonyeshe tena kuwa makosa yale si ya kiuandishi au kitakwimu bali mwangi wake unasambaa na kuipoteza jamii.
Angalia tena jedwali hili ili tumalizie yaliyobaki.
By Mohamed Said
Table 1: Selection of Std. VII Pupils to Form I in Dar es Salaam Region 1978 to 1981
[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]Year
[/TD]
[TD]Total Selected
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]Muslims
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]% of Muslims Selected
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]1978
[/TD]
[TD]956
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]216
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]23%
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]1979
[/TD]
[TD]903
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]194
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]22%
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]1980
[/TD]
[TD]1071
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]247
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]23%
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]Year
[/TD]
[TD]Total Selected
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]Muslims
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]% of Muslims Selected
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]1978
[/TD]
[TD]956
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]216
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]23%
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]1979
[/TD]
[TD]903
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]194
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]22%
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]1980
[/TD]
[TD]1071
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]247
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]23%
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Source: Dar es Salaam City Council Department of Education
NB:In 1967 census Muslims in Dar es Salaam Region were 67% therefore the number of Muslim students in Dar es Salaam primary schools is greater than that of Christians. This should have reflected in the selection.
My take:
Mohame ameonyesha katika aya ya mwisho herufi NB. Hili ni neno la kilatin Nota bene kwa maana nota (note) bene(well) yaani inamwelekeza msomaji aliangalie jambo linalokusudiwa kwa umakini.
Kwahiyo Mohamed tayari amesharidhika na anashauri umma unaosoma uangalie aya hiyo kwa makni sana.
Mohamed anasema sensa ya mwaka 1967 idadi ya waislam ilikuwa asilimia 67% na hivyo ilitarajiwa wanafunzi wa kiislam wawe wengi kuliko wakristo na hivyo matokeo yalitakiwa yaakisi idadi ya watu.
Kwanza, Tumeshafanya sensa nyingi na ilikuwa kawaida kila baada ya miaka 10 kuna sensa. Mtafiti alitakiwa atupe sensa za karibu sana (mwaka 1977 kama nipo sahihi) na hizo za mwaka 1967 zisadie kama itabidi.
Mohamed hakueleza kwanini hakuchukua majibu ya sensa baada ya mwaka 1967 na hivyo kuwaacha wasomaji wakiwa na maswali yasiyo na majibu.
Mohamed anatakiwa afahamu kuwa population ni ''variable value'' kwamba si lazima asilimia 67 ya mwaka 1967 ibaki kama ilivyo.
Kuna uwezekano iliongezeka na kufikia 80 au kupungua na kufikia 40 kwahiyo alitakiwa kwanza apate the most recent stats.
Kufanya extrapolation ya mwaka 1967 ni sawa na mtu kupanga mipango ya maendeleo ya nchi kwa kutumia stats za 1967. Huku ni kupotosha vijana kusikoweza kuvumilika hata kidogo. Wrong! Mohamed denounce this ASAP!
Pili, hakuna ukweli kuwa ukiwa na idadi kubwa ya wananchi ni lazima idadi hiyo iakisiwe katika maMbo mengine.
Mfano, wahindi ni jamii ndogo sana katika nchi yetu lakini unapozungumzia mambo ya biashara wao wanaonekana kuwa wengi kuliko sisi wamatumbi na hivyo wingi wetu hauakisi ''matokeo ya kuwa na wafanyabishara wengi na wenye uwezo''
Mohamed alipaswa kujiuliza maswali haya
1. Je, idadi ya watoto wa kiislam iliandikishwa shule kama inavyoakisiwa katika sensa?
2. Je, walioandikishwa walimaliza darasa la saba na kufanya mtihani
3. Je, kulikuwa na ubora wa elimu katika ushindani na makundi mengine
Kwahiyo siyo kweli kuwa Quantity is directly proportional to Quality.
Inaweza kuwa hivyo endapo tu factos 1-3 hapo juu zitakuwa zimetiliwa mkazo na kufanyiwa kazi.
Wanajamvi lazima Mohamed aelewe kuwa katika matokeo ya mwaka huu kuna shule ina watoto 7 na wamefaulu 7.
Ipo shule ina watoto 28 na wamefaulu 6. Sasa kama wingi ni kigezo na wala si ubora namba hizo zinatueleza nini?
Tatu, Mohame amesema hapo juu kuwa idadi ya waislam ni kubwa kuliko watoto wa kikristo. Anachotaka kusema hapa ni kuuaminisha umma kuwa mtihani huo ulifanywa na waislam na wakristo tu. Kwamba watu wenye imani nyingine hawakushiriki. Factually wrong and serious mispresentation of scientific data.
Ndugu Ami hadi hapo nadhani unaona wazi kuwa Mohamed hakufanya utafiti wa kutafuta bali alikuwa na conclusion yake kichwani akatafuta mahali pa kuchomeka namba na matokeo yake ndiyo hayo ya kutoa vitu visivyoweza kutafsiriwa kama hivyo.
Lakini hakufanya hivyo kwa bahati mbya alifanya hivyo makusudi kwa kuweka ''sensational research'' na amefanikiwa kuwafanya watu wasome kuhusu Waialsm vs wakristo na namba zake bila kutafakari mistari yake na yaliyomo ikiwa ni pamoja na kutafuta ukweli.
Sasa upotshaji huu uliodumu kw miaka 15 unaweza kusema ni sawa na typo error. Leo wapo vijana wanahubiti data hizi bila kujua ni za kupika na wala Mohamed haonekani ku-denounce. Sasa hili ni kosa la kufumbiwa macho kweli! Hebu nishauri ndugu yangu Ami.