Mundungus Fletcher,
Nimesoma fikra zako kwanza siyo kweli kuwa Waislam wanachaguwa mtu wa kumlaumu Waislam wanasema dhulma walizofanyiwa na Nyerere kujenga mfumo Kristo.
Achana na Mohamed Said wasome kina Smith. P. Fr. Sivalon. J, Bergen Jan Pvan, kuhusu Kanisa na Nyerere.
Angalia "Ratio" kati ya Waislam na Wakisto katika wizara zote za serikali pamoja na mashirika ya umma unadhani ili limetokea bahati mbaya chunguza huone kazi ya mfumo Kristo.
Wakati wa harakati za kutafuta uhuru Wazee wetu Wazalendo walikuwa na Nyerere bega kwa bega pitia hotuba yake hapo juu msome Nyerere anavyowaelezea Wazee wa Kiislam.
Jiulize baada ya uhuru tu Nyerere aliwakamata Masheikh na kuwaweka vizuizini na wengine kufunga jela takutajia baadhi yao kama wafuatao.
Sheikh Ali Comoriam, Sheikh Nurdin Hussein, Sheikh Hashim Haji, Sheikh Abdulkarim Abdulwahid, Sheikh Shariff Mwinyibaba, Sheikh Al Aman Maftah, Sheikh Badawiy, Mufti Hassan Bin Amir, wapo wengi sana.
Sasa jiulize hawa Masheikh kama wangekuwa na chuki na Nyerere wangekuwa naye pamoja wakati hajawa rais.
Wewe kama huoni dhulma walizofanyiwa Waislam hakuna tatizo lakini Waislam wanafahamu dhulma walizofanyiwa na Nyerere.
Naomba utukumbushe Sheikh wa South Africa aliyefukuzwa nchini.
Mkuu Ritz
Sina uhakika na takwimu sahihi za Ratio ya waislamu na wakristo kwenye mawizara lakini kweli nameobserve kwa haraka haraka kwenye sehemu nyingi makazini (both private and Public sector) wakristo wengi sana kulingana na waislamu.
But hii inamaanisha kuwa kweli ilikuwa systematic plan ya kuwajaza wakristo makazini?
Inamana haiwezekani pia ikawa hii ni matokeo ya sababu nyingine lukuki zisizo zakupangwa ambazo kwa njia moja au nyingine matokeo yake ndo haya.
Mfano hivi wakristo wakisema Zanzibar kuna mfumo Muslim ambao uko systematic kusuppress wakristo kwakutumia kigezo cha Ratio ya kila eneo waislamu kwa wakristo ni 3:1, kuanzia Uongozi, serikalini, mpka idadi ya wakazi.
Waarabu-watanzania wa hapa tanzania, 95% ni waislamu, ingawa wao ni minority katika nchi lakini ni matajiri sana kulingana na watanzania wengi, na wakitaka kuwapeleka watoto wao shule sehemu yoyotr dunia wanaweza...
Hata wahindi-watanzania wengi hapa tanzania ni wahindi waislamu, na 90% ni well off.
Je mbona hawa pia idadi yao ni ndogo sana mawizarani and yet wao ndo wanashikiria uchumi wa nchi and infact wao pia wanaendeshs hii nchi kwasababu wanapower kubwa ya kuinfluence policy ya nchi hii. ?
Umewataja masheikh walikamatwa na Nyerere, lakini na mimi nauliza je kulikuwa hakuna wakristu pia waliokamatwa katika kipindi hiko? Au utaniambia walikamatwa kuzuga tu ili isionekane ni mpango wa kuwakandamiza waislamu.
Je Nyerere aliwakamata hao Masheikh bila ya sababu? Je kams alikuwa na sababu inamana we unaona sababu ya Nyerere haina mashiko ila ya Masheikh ndo inamashiko?
Nashindwa kuelewa inakuwaje Nyerere huyu mnaesema alikuwa anatatizo na waislamu kiasi akaanza mkakati kuwakandamiza, kuchagua waziri wake wa Mambo ya ndani (kama sijakosea) muislamu ambaye baadae akaja kuwa Raisi wa inchi tena baada ya kuwa Raisi wa ZNZ.
Kwa jinsi picha nayopata ya huyo Nyerere mlivyomdisplay inamana alikuwa na nguvu kiasi kwamba angetaka Mwinyi asingekuwa Raisi, na wasingefanya lolote..
Lakini akakubali the Most Powerful person kwenye nchi awe Muislamu, mmoja ya wale wale ambao ameweka mkakati kuwakandamiza na kuhakikisha wanabakia second class citizen...
Haikuishia hapo bado aka wamentor na kuwaweka undet his wings vijana wengie wakislamu ambao wengi wao currently ndo viongozi waandamizi wa nchi...
Huyu huyu Nyerere ambaye anatatizo na waislamu ambaye mnasema ni mdini na mcatholic kwanza kabla ya yote, akakubali kuingia compromise kuwatosa Wayahudi kwa kusupport taifa la waislamu tupu Palestina...
Haikuishia hapo,
Sasa hivi viongozi waandamizi karibia wote ni waislamu, with the Most Powerful person kwenye inchi hii Raisi, hadi Mkuu wa usalama wa Taifa ni muislamu, unafikiri wajasikia kama kuna kundi la waislamu (kwassbbu haiwezekani ikawa waislamu wote kama watu Bakwata tu hawajumuishwi kwenye waislamu) linalolalamika kuna systematic dhulma against waislamu? Mbona bado mnalalamika mnaonewa, mnakandamizwa. Kams kweli kipo kweli waislamu wote hawa si wangefuta huu mtandao once and for all.
Haya matatizo kwenye mfumo yapo nchi kwetu, inatakiwa kama nchi tuyaadress na kutafuta ufumbuzi.
Lakini ukiyaangalia kikundi zaidi, hatutafika kokote na atutapata kwasababu kwenye ubishani wa imani hakuna mshindi kamwe.
Waislamu wanatakiwa wajiassemble na kukaa chini, waadress matatizo yso within wao kwao bila ya kupoint finga kwa dini nyingine ndo sababu ya matatizo yao,(kwasababu dini nyingine haitakubali kama wao ndo sababu ya hayo matatizo ambapo watarudi kwenye mabisho tena ambayo hayana mwisho) then watafute ufumbuzi wa hayo matatizo. Wafanye mikakati kama kujenga shule zaidi za kiislamu, vyuo, mahospitali na kila kitu, uone kama kuna mtu atawasumbua.
Kama wahindi wanavyofanya, wao wametengeneza kanchi kao ndani ya Tanzania ambapo wanajitegemea kwa kila kitu, wanashule zao, hospitali zao, misikiti yao, vyuo vyao, nk.
Pia nahaidi kuvitafuta vitabu Smith. P. Fr. Sivalon. J, Bergen Jan Pvan hivi nipate undani