Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 51,303
- 40,190
Kwa vijana wadogo ni vigumu sana kuelewa mambo yalivyokuwa huko nyuma na hivyo wanakuwa wepesi mno kumeza ngano wanazolishwa na Mohamed Said...kwa mfano, je wanajua, wakati wa mkoloni, ushindani uliokuwapo baina ya dhehebu mbali mbali za Kikristo na hasa Wakatoliki, Walutheri na Waprotestant ndio chachu iliyowezesha maendeleo makubwa kupatikana sehemu zote walizopiga kambi.
Kulikuwa na ushindani katika utoaji wa huduma za kiroho, hospitali na shule...hivyo mathalani kila moja wao alipofungua shule eneo fulani na mwenziwe alifanya hivyo hivyo kwa lengo la kutoa huduma bora zaidi. Bahati mbaya kwenye mikoa ya mwambao yenye Waislaam wengi walipata upinzani mkali kupokewa kama inavyosimuliwa hapa na Mwandishi wa historia Philemon Andrew K Mushi katika kitabu chake History and Development of Education in Tanzania, nanukuu;
Mwandishi na mtafiti Philemon Andrew K Mushi, anaendelea;
Je, Mwalimu Nyerere alirithi nini mwaka 1961 tukipata uhuru, Mwandishi na mtafiti anaendelea kutoa darasa;
After independence the new government under its leader Mwalimu Nyerere was committed to educational policies and strategies aimed at addressing the observed inequalities in education provision. The first thing Mwalimu did was to address the issue by nationalizing all mission schools to give equal opportunity to all Tanganyikans/Tanzanians and this made it possible for people like Mohamed Said to see the inside of a classroom at St Josephs...sasa shuhudieni kejeli na dhihaka zake kwa Mwalimu, kweli shukhrani ya punda ni mateke.
Hiki ni kituko cha mwaka hivi Mohamed Said na Philemon Andrew K Mushi nani anajua habari za Mwambao.
Hizi ngano walishe wenzako Mushi na Pwani wapi na wapi.
Chukuwa maneno ya hotuba ya Nyerere hapo kuhusu Wazee wa Dar es Salaam kisha mpelekee Mushi, muulize Mushi kuwa Nyerere naye alipata upinzani wakati anakwenda Mwambao.
Mwambie Mushi ajikite kuelezea habari za Machame, Kibosho, Rombo, Kishumundu, lakini siyo Mwambao.
Endelea kumeza ngano za nazi kutoka kwa Mushi.
Last edited by a moderator: