Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
Na hakuna mahali ambapo Mohamed amesema kuwa alipokuwa st Joseph mfumokristo school aliwahi kubaguliwa.Ndio maana tuko hapa kuwaonyesheni kuwa ushahidi wenu ni magumashi tu. Mohamed ameshindwa kunijibu swali la Nyerere kutaifisha shule za misheni ili waislamu wapate fursa ya kusoma. Yeye hilo kwake halizungumzii kabisa. Wala hazungumzii kuwa elimu yake ameipata St. Joseph, shule ya wakatoliki. Hayo kwake hayagusi. Ukimlaumu Nyerere basi angalau mpe sifa kuwa alijitahidi kutoa fursa sawa za masomo kwa waislamu. Lakini hilo katu hamtasema kwa sababu mkisema hivyo mnamwagia maji theory yenu ya Nyerere kuwa mbaguzi wa Waislamu.
Sasa hivi yupo mstari wa mbele kuelezea mfumokristo ambao yeye mwenyewe kwa experience yake st Joseph hajathubutu kuandika hata nusu mstari wa ubaguzi aliouona.
Hataki kuongelea st Joseph maana vijana watamuuliza kwanini mtoto wa ''wazee wa Dar es Salaam'' alikwenda kusoma katika shule ya ''makafir''
Yeye yupo bize kuwakataza wenzake wasipeleke watoto kutafuta elimu inapopatikana.