Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Ami, naona unajaribu kupulizia manukato katika lundo la uvundo.

Tumejaribu kukuonyesha kuwa alichofanya Mohamed si makosa madogo ni makosa makubwa kiuandishi na kiutafiti na kwamba hakufanya hivyo kwa bahati mbaya bali alikusudia.

Tuliacha hilo tukidhani somo limeeleweka, inavyoonekana sisi ndiyo tunakuwa ''victim'' wa kuonyesha ukweli kutoka katika maandishi ya Mohamed. Sasa ngoja tukuonyeshe tena kuwa makosa yale si ya kiuandishi au kitakwimu bali mwangi wake unasambaa na kuipoteza jamii.

Angalia tena jedwali hili ili tumalizie yaliyobaki.

By Mohamed Said
Table 1: Selection of Std. VII Pupils to Form I in Dar es Salaam Region 1978 to 1981
[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]Year
[/TD]
[TD]Total Selected
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]Muslims
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]% of Muslims Selected
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]1978
[/TD]
[TD]956
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]216
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]23%
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]1979
[/TD]
[TD]903
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]194
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]22%
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]1980
[/TD]
[TD]1071
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]247
[/TD]
[TD="bgcolor: transparent"]23%
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Source: Dar es Salaam City Council Department of Education

NB:In 1967 census Muslims in Dar es Salaam Region were 67% therefore the number of Muslim students in Dar es Salaam primary schools is greater than that of Christians. This should have reflected in the selection.

My take:
Mohame ameonyesha katika aya ya mwisho herufi NB. Hili ni neno la kilatin Nota bene kwa maana nota (note) bene(well) yaani inamwelekeza msomaji aliangalie jambo linalokusudiwa kwa umakini.
Kwahiyo Mohamed tayari amesharidhika na anashauri umma unaosoma uangalie aya hiyo kwa makni sana.

Mohamed anasema sensa ya mwaka 1967 idadi ya waislam ilikuwa asilimia 67% na hivyo ilitarajiwa wanafunzi wa kiislam wawe wengi kuliko wakristo na hivyo matokeo yalitakiwa yaakisi idadi ya watu.

Kwanza, Tumeshafanya sensa nyingi na ilikuwa kawaida kila baada ya miaka 10 kuna sensa. Mtafiti alitakiwa atupe sensa za karibu sana (mwaka 1977 kama nipo sahihi) na hizo za mwaka 1967 zisadie kama itabidi.
Mohamed hakueleza kwanini hakuchukua majibu ya sensa baada ya mwaka 1967 na hivyo kuwaacha wasomaji wakiwa na maswali yasiyo na majibu.

Mohamed anatakiwa afahamu kuwa population ni ''variable value'' kwamba si lazima asilimia 67 ya mwaka 1967 ibaki kama ilivyo.
Kuna uwezekano iliongezeka na kufikia 80 au kupungua na kufikia 40 kwahiyo alitakiwa kwanza apate the most recent stats.
Kufanya extrapolation ya mwaka 1967 ni sawa na mtu kupanga mipango ya maendeleo ya nchi kwa kutumia stats za 1967. Huku ni kupotosha vijana kusikoweza kuvumilika hata kidogo. Wrong! Mohamed denounce this ASAP!

Pili, hakuna ukweli kuwa ukiwa na idadi kubwa ya wananchi ni lazima idadi hiyo iakisiwe katika maMbo mengine.
Mfano, wahindi ni jamii ndogo sana katika nchi yetu lakini unapozungumzia mambo ya biashara wao wanaonekana kuwa wengi kuliko sisi wamatumbi na hivyo wingi wetu hauakisi ''matokeo ya kuwa na wafanyabishara wengi na wenye uwezo''

Mohamed alipaswa kujiuliza maswali haya
1. Je, idadi ya watoto wa kiislam iliandikishwa shule kama inavyoakisiwa katika sensa?
2. Je, walioandikishwa walimaliza darasa la saba na kufanya mtihani
3. Je, kulikuwa na ubora wa elimu katika ushindani na makundi mengine

Kwahiyo siyo kweli kuwa Quantity is directly proportional to Quality.
Inaweza kuwa hivyo endapo tu factos 1-3 hapo juu zitakuwa zimetiliwa mkazo na kufanyiwa kazi.

Wanajamvi lazima Mohamed aelewe kuwa katika matokeo ya mwaka huu kuna shule ina watoto 7 na wamefaulu 7.
Ipo shule ina watoto 28 na wamefaulu 6. Sasa kama wingi ni kigezo na wala si ubora namba hizo zinatueleza nini?

Tatu, Mohame amesema hapo juu kuwa idadi ya waislam ni kubwa kuliko watoto wa kikristo. Anachotaka kusema hapa ni kuuaminisha umma kuwa mtihani huo ulifanywa na waislam na wakristo tu. Kwamba watu wenye imani nyingine hawakushiriki. Factually wrong and serious mispresentation of scientific data.

Ndugu Ami hadi hapo nadhani unaona wazi kuwa Mohamed hakufanya utafiti wa kutafuta bali alikuwa na conclusion yake kichwani akatafuta mahali pa kuchomeka namba na matokeo yake ndiyo hayo ya kutoa vitu visivyoweza kutafsiriwa kama hivyo.

Lakini hakufanya hivyo kwa bahati mbya alifanya hivyo makusudi kwa kuweka ''sensational research'' na amefanikiwa kuwafanya watu wasome kuhusu Waialsm vs wakristo na namba zake bila kutafakari mistari yake na yaliyomo ikiwa ni pamoja na kutafuta ukweli.

Sasa upotshaji huu uliodumu kw miaka 15 unaweza kusema ni sawa na typo error. Leo wapo vijana wanahubiti data hizi bila kujua ni za kupika na wala Mohamed haonekani ku-denounce. Sasa hili ni kosa la kufumbiwa macho kweli! Hebu nishauri ndugu yangu Ami.


Variability ya population lazima iwe na sababu zilizoainishwa.Ikiwa 1967 waislamu walikuwa ni 67% unadhani ni nini kiliwapunguza mpaka tuseme 40%.Ikiwa hakuna tukio la kimaafa au namna nyengine yenye kupimika basi hilo la kupunguzika mpaka 40% statistically haliaminiki.
Kwa maana hiyo maswali yako mengine na shutuma zote zinazofuatia bila kujibika swali hili hayana mashiko.
 
Jasusi,

Nakutajia haya machache tu ambayo wakurugenzi wake ni Wakirsto.

LAPF, TANESCO, TTCL, TBC, TANAPA, NCAA, TPA, BOT, TCRA,

Nikuongeze yapo mengi mtafanya tuangalie ratio sasa.
Vipi NECTA ambako katibu mkuu wake analindwa kimfumo asiondoke
 
Mwalimu wangu wa Falsafa alifundisha kitu kimoja sijakisahau (kati ya mengi nisiyoyasahau) alisema fallacy mojawapo ya watoa hoja ni kile alichokiita "pseudo-obviousness" yaani mtu anaamini watu wote wanauona au wanapaswa kuuona ukweli ambao uko 'wazi kabisa'. Mtu anayesema hivyo mara nyingi hana ushahidi. Kwa mfano, mtu akisema ukienda Moshi utakuta Wachagga wengi wanafanya biashara basi kuna ubaguzi dhidi ya watu wa makabila mengine na ukimuuliza atakuambia "we huoni Wachagga walivyolundikana hapo?" au mtu aende Zanzibar na kusema "Zanzibar kuna ubaguzi sana wa watu wa dini nyingi kwa sababu Waislamu wamelundikana kila mahali".

Sasa, Ritz na wengine wamejiaminisha kuwa 'ubaguzi' ni wingi. Kwamba ukienda mahali ukakuta watu wa kabila moja ni wengi basi mara moja ni ubaguzi. Yaani wanaondoa uwezekano mwingine wowote (bila hata kujaribu kuona kama una ukweli) na kubakia na 'ubaguzi' peke yake. Anapoenda kwenye ofisi na kuuliza Mkurugenzi anaitwa nani hapa wakakuta "John Paul" basi kichwani kengele zinazolia ni "mfumo Mkristu". Lakini akisikia anaitwa "Omar Rajab" hawezi kuhisi upendeleo wa kidini!!

Na hili mtu anafikiria ni la kiakili. Ukikuta jina la Mkristu kwenye ofisi ya serikali basi ni udini (mfumo Kristu) na ukikuta jina jingine lolote basi hakuna mfumo Kristu. Mawazo ya namna hii matokeo yake ni kuwa mtu anatembea kichwani anasikiliza majina; akikuta jina la Kikristu anajiambia "Mfumo" akikuta jina la Kiislamu anajiambia "ndugu yangu huyu anastahili". Hivyo, Wakristu katika mawazo yao hawastahili kushika nafasi, hawapaswi kugombea nafasi yoyote na mahali popote watakapoomba basi waangaliwe kama Waislamu nao wameomba na kama wameomba basi Mkristu asichukuliwe achukuliwe Muislamu (a sort of affirmative action).

Tatizo ni kuwa watu hawajui kuwa mara nyingi discrimination inafanywa na jamii ya watu wenye nguvu. Sasa tuendelee hapa nitaonesha kwa kutumia mantiq kwanini hoja ya dhulma dhidi ya Waislamu haina msingi katika ukweli; ni hoja tu ya kihisia.




Ritz kwa vile unaonekana unaamini kweli kabisa Waislamu wanadhulumiwa na kuonewa na 'mfumo Kristu" naomba unisaidie jibu hili - utakuwa ni mlolongo wa maswali kwako na tutaendelea kwa kadiri unavyoyajibu.

1. Taasisi gani au zipi ambazo zina Wakristu wengi na katika nafasi zipi?

Mzee Mwanakijiji,

Unauliza taasisi zipi zimejaa Wakirsto na nafasi zipi.

Nimekuwekea hizo Wizara na Mashirika ya umma nafasi zote nyeti mpaka makarani watu wa mapokezi ni
Wakirsto.

Wewe ni mwandishi wa habari fanya utafiti wako kwenye ili lakini bahati mbaya akili yako haitaki kukubali kama Waislam wanafanyiwa dhulma.

Jamaa yako Jasusi, naye anasema jamaa yake alifanyiwa dhulma NSSF kutokana na dini yake.
 
Last edited by a moderator:
Vipi NECTA ambako katibu mkuu wake analindwa kimfumo asiondoke

Ami,

Mzee Mwanakijiji,

Haoni dhulma wanazofanyiwa Waislam lakini anaona dhulma wanazofanyiwa Chadema.

Tafakari kisha chukuwa hatua.
 
Sio kutojua tu. Hatuamini shutuma zenu. Nyerere was a nationalist. Aliweka level play field kwa Watanzania wote bila kujali kabila, rangi au dini. Shutuma zenu bado hazina mashiko. Try again.
Kutokuamini ni jambo jengine lakini hivyo vitu vipo na ushahidi umetolewa.
Ikiwa nyinyi hamuamini wengi wetu tayari sasa kazi yenu ni kutubadilisha tusiamini kama mtaweza.
 
Hakuna ushahidi wowote wa dhulma dhidi ya Waislamu Tanzania; zipo tuhuma zinazotolewa lakini hakuna mtu ambaye ameweza kuthibitisha uwepo wa dhulma. Watanzania wa dini zote wanapata matatizo yale yale kwenye ajira, elimu, maisha na waliofanikiwa nao wamefanikiwa katika dini zote.
Sisi tunaona ni ushahidi kwani tuhuma za muda mrefu bila majibu na wa kujibu yupo mzima wa afya inakuwa ni kweli hana jibu la kutoa tu.
Shutuma miaka yote tangu uhuru hakuna tume ya kushughulikia na serikali ipo unadhani itakuwa ni uongo?.
Nilikupa mfano wa mwari anavyoozeshwa kwa kukaa kwake kimya na mtuhumiwa anavyofungwa kwa kushindwa kujitetea.
 
Ongezea,

St Augustine
Acheni husuda ya ajabu nyie watu.. hiki ni chuo cha Kikristo kabisa, Kipo chini ya kanisa lakini angalia watoto wakiislamu wanavypota elimu pale. Nenda kafanye utafiti uone kama wanabaguliwa kwa ajili ya Uislamu wao.

Ongezea,
Mfano Christmas unakuta miti kila mahali, maua na kwaya zinaimbwa katika ofisi za umma je vp hapo???
hehehehe.. kwahiyo krismasi kushelekea kumbe ndo moja ya dhulma yenyewe... Mbona iddi hatuendi makazini. na wengine ni wakristo....
 
Hatujapunguza speed, ni majukumu tuliyonayo. Utatuona tu.

Isitoshe, ushasema wewe si mwana historia, na Mohamed Said kaandika historia, kwa hilo inakubidi ukae usome na kuijuwa historia ya kweli.

Nyerere ni dikteta na mdini wa ukweli nani asiyelijuwa hilo?

Sijaona hata moja lilioneshwa mpaka sasa la kuonesha "uchochezi wa Mohamed Said kwa wapigania uhuru wa Tanganyika na Zanzibar" kama mada ilivyodai. Jee, wewe umeliona?

Hata mmoja mpaka sasa hajaja na hoja yenye hizo shutuma, naona watu wanakuja na maswali yasiyo na kichwa wala miguu.

Hizo video za Nyerere unazosema zipo, Yericko Nyerere mpaka sasa kashindwa kutuwekea aliyoahidi atatuwekea kama ushahidi. Au hukupitia hayo?

Mimi sijaja kudhibitisha kama Mzee Saidi ni mchochezi, ila nimekuja kuona ushahidi wa dhulma kwa Waislamu.

ambayo sijaona mpaka sasa..... ila bado nasubiria
 
Mzee Mwanakijiji

Ni hitimisho zuri na sahihi.
Yeyote atakayedai kuwa kuna dhulma dhidi ya waislam, hawezi kuleta ushahidi nje ya maandiko ya Moh Said, Njozi na vitabu vya akina Sivalon wanavyovitaja. Dhulma gani hiyo ambayo kuonekana kwake mpaka kwa vitabu tu? Tena vitabu vyenyewe vinmeandikwa "inasemekana..."

Kwenye maisha ya kawaida huku mtaani kila observation ina maelezo yake:
"Wahindi wengi wamefanikiwa biashara kwa sababu wana umoja na wanainuana kwenye mitaji".
"Fulani na fulani wana utajiri wa kurithi kutoka kwa babu yao ambaye alikuwa jambazi."
"Ukoo ule wanapenda shule na wamesoma sana"
"Wakinga, wapemba na Wachaga wanafanikiwa kibiashara"
"Wale jamaa hawathamini shule, wanapenda sana ufugaji na uwindaji"

Watu ninao wa-refer kwenye statements hizo wanaweza kuwa wa dini yoyote. Na sijawahi sikia kuwa fulani kafanikiwa kwa sababu ya ukristo wake au kashindwa maisha kwa sababu ya uislam wake.

Kwa kweli hakuna ushahidi wowote huku mtaani wa dhulma dhidi ya waislam. Shida na raha sote tunazipata. Waislam wanadhulmiwa kwenye maandiko tu ya Moh Said.
Wewe ndio mpuuzi wa mwisho kwenye huu mjadala.
Yaani huamini maandiko kwenye vitabu?.
Ukija huku mitaani waislamu tunasema umoja na maendeleo yetu huwa havisimami kwani vinahujumiwa na mfumo kristo.
Hata hao wahindi na wachaga wakisimama na uislamu wao basi pia nao watahujumiwa.
Hukumbuki Ngano ya Bakhresa ilivyochomwa moto baada ya uchaguzi uliomweka madarakani Mkapa?.
 
Vitabu vimeisha mikoani watu wanavitaka watu wanataka vitabu vya Mohamed Said huu uzi ni promo tosha wakumshukuru ni Yericko kuanzisha huu uzi.

Wewe endelea kujifariji na kujiliwaza unajua ni raha sana na inapendeza kumsoma mtu ambaye unamfahamu.

Bahati mbaya maandishi yenu hayana uzito wowote kutokana mnaondika mmejificha kwa majina ya bandia.
Kwani jina la Ritz ni verified?
 
Katika kujenga hoja zako jaribu kufanya tafiti kwanza kabla ujaandika.

Umeipata wapi kuwa Palestina ni taifa la Waislam watupu hivi unajua kama Palestina kuna Wapelestina Orthodox, Jehovah Witnesses, Baptists, Anglicans. jewish, Catholics.

Unajua historia ya Bethlehem?
Soma historia ya Palestina kuna Mameya wengi tu Wakiristo kuna mabalozi wengi tu Wakirsto kuna balozi wa Palestine nchini Urusi alikuwa Mkirsto, meya wa Bethlehem Mkisto.

ngoja nitumie Inchi yenye Waislmu wengi...(Dominated by Muslim Majority)..

Turudi kwenye munakasha wetu. Unatoa mfano wa Zanzibari kwa hiyo Tanganyika Wakirsto walikuwa wengi kuzidi Waislam ndiyo maana Ratio inaonyesha Wakirsto ni wengi kwenye wizara za serikali na mashirika ya umma.

Hata kama waislamu wangekuwa wengi, kutokua wengi katika sehemu za kazi na mashuleni kuna sababu nyingi tu lakini dhulma si moja wapo...

Vipi kuhusu muamko wa elimu maeneo yalikuwa yanakaliwa na waislamu? kama pwani, lindi, mtwara?????
 
Mdondoaji,

Mashirika ya umma yapo zaidi ya 200 mengi yamejaa Wakisto watupu wao wanamuangalia Dau NSSF.

Juzi Mkristo alikuwa bosi TBS kafanya ufisadi wa kutisha Muhando wa Tanesco hakuna cha Chadema wala Mkirsto yeyote alipiga kelele.

Wao na Dau tu.
Sio bule we utakuwa na matatizo.
 
Nguruvi3,

Sijui kama unajua hijabu ni nini Mama Theresa alikuwa anavaa mtandio au ushungi tu lakini siyo hijabu.

Waislam hawafanyi makosa kunasibisha kofia na dini yao Muislam kuvaa kofia ni Sunna.

Halafu unatakiwa uelewe siyo kila kitu mtu akikisema basi kaambiwa na Mohamed Said vitu vingine vipo wazi kwa macho tu hivi kujua kuwa Wakiristo wamekamata ajira nyingi serikalini na kwenye mashirika ya umma mpaka uambiwe na Mohamed Said.

Kwa hiyo unataka kutuambia matatizo ya shule za Kilwa na Al Hassan Mwinyi ndiyo yamesababisha Wakirsto wawe wengi Wizara ya Elimu, Wizara ya Afya, Wizara ya Miundombinu, Wizara ya Ulinzi, Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya Mambo ya Ndani, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara zote.

Mashirika ya Umma yamejaa wafanyakazi Wakirsto achalia mbali Wakurugenzi.

Nenda TANAPA, BOT, TCRA, TBC, TBS, TANESCO, BIMA, ITCL, TCCL, na mengine haya yote kuwajaza Wakirsto unadhani limefanyika kwa bahati mbaya Mfumo Kirsto.

Uwa mnanifuarahisha sana mnataka tuwe tujadili matizo ya shule za Kilwa na Mtwara lakini hata siku moja amtaki kujadili kwa nini Wakirsto wameodhi ajira serikalini na kwenye mashirika ya umma.
Kwani mwenye kuteua hao wkurungezi ni nani? Au ni pengo?
 
Vipi NECTA ambako katibu mkuu wake analindwa kimfumo asiondoke
Na shukulu kawambwa nae analindwa na mfumo asiondoke?
Vipi hoja za mbatia, na nasari, kuhusu elimu na necta zilivyo chinjiwa baharini.
 
ngoja nitumie Inchi yenye Waislmu wengi...(Dominated by Muslim Majority)..



Hata kama waislamu wangekuwa wengi, kutokua wengi katika sehemu za kazi na mashuleni kuna sababu nyingi tu lakini dhulma si moja wapo...

Vipi kuhusu muamko wa elimu maeneo yalikuwa yanakaliwa na waislamu? kama pwani, lindi, mtwara?????

Umeishajiuliza kwa nini iwe Pwani, Lindi, Mtwara.

Vipi muamko wa elimu kwenye hizi nchi zenye Waislam wengi.

Malaysia, Singapore, Egypt, Bahrain, Oman, Indonesia, Brunei, Saudia Arabia, Kuwait, Turkey, Jordan, Iran, Qatar, Pakistan.

Hata Tanzania kwenye Waislam wachache tunawazidi muamko wa elimu au unaonaje.
 
Kuna kitu kimoja ambacho wanaolia "dhulma" wanadhani Watanzania hawakijui sana. Wakati wa Nyerere kama kuna kitu kilikuwa kinapigwa vita sana ni kile alichokiita "undugunization" yaani kwa neno la kimombo "nepotism". Tafsiri moja ya nepotism inasema ni "patronage bestowed or favoritism shown on the basis of family relationship, as in business and politics".

Sasa undugunization ulianza kwa kasi baada ya kuanza kuwa na kada ya watumishi wa umma wasomi ambao wameanza kushika nafasi. Kwa kiasi wale waliopata nafasi kidogo walianza kuwaingiza wana familia wao kwenye hizo ajira. Kama Baba alikuwa meneja wa Benki basi mtoto wake akigraduate naye anatafutiwa kazi benki; hii ilikuwa kweli kwenye polisi, na ilikuwa kweli kwenye ajira nyingi sana. Na kwa kadiri watu walivyozidi kupata nafasi za juu ndivyo nao walivyozidi kuwaingiza ndugu zao kwenye ajira na hawakufungwa na ofisi zao kwani waliweza kuwaunganisha na marafiki zao kwenye kada nyingine. Hivyo, mtu anaweza kuwa yuko Ikulu lakini mtoto au jamaa yake akaunganishwa kupata kazi Benki Kuu, au taasisi nyingine.

Lakini hili halikuishia tena kwenye undugu wa damu likawa limeingia hata kwenye undugu wa "kijiji kimoja"; ambapo hapa utakuta watu ambao wanatoka kijiji kimoja (hata kabila moja) wanadai undugu na kuombeana msaada. Hivyo, mtoto atatoka Tarime na kwenda kwa 'mjomba' Arusha ambaye ni afisa wa JWTZ ambaye atamtafuta kazi kujiunga na jeshi. Matokeo yake utakuta watu wa kabila moja nao wakiwa wamejazana sehemu fulani.

Huu undugunization ndio kwa kiasi kikubwa sana umekithiri na sijui kama kuna Mtanzania ambaye hana ndugu au jamaa aliyenufaika na kumfahamu mtu fulani. Lakini katika maana yake pana zaidi huu 'undugunization' ulifika hadi kwa marafiki. Watu waliosoma pamoja wanasaidiana na marafiki wanapeana nafasi na hata kwa watoto wao. Kwa mfano, mtu ambaye ni Mkristu mwenye tafiki Muislamu anaweza kuombwa na rafiki yake kumtafutia "binti" yake ajira na akafanya hivyo. Yule binti ataingia kwenye ajira na hakuna mtu ataweza kuona upendeleo kwa sababu aliyeingia ni Muislamu na kaingizwa na Mkristu (au kinyume chake).

Hili unaliona hata kwenye teuzi mbalimbali. Mtu Muislamu anaweza akamteua mtu Mkristu ambaye anaweza asiwe na uwezo sana lakini watu wasione "upendeleo" kwa sababu wamefungwa na kuangalia dini tu. Ukiniuliza mimi kitu kinachowanyima watu nafasi kuendelea katika ajira siyo "dini" hasa bali 'undugu" ambapo pamoja na nepotism sasa kuna 'cronyism' yaani 'thepracticeoffavoringone'sclosefriends,especiallyinpoliticalappointments.'

Mfano mzuri sana wa haya mawili ni nafasi za ajira kule BoT ambao tuliona majina ya watoto wa vigogo yakijazana na kupeana nafasi mbalimbali. Sidhani kama kuna mtu anaweza akasema wale walipewa upendeleo kwa sababu ya dini zao. Na hivi karibuni tumeona pia kwenye viwanja vilivyouzwa kule Kigamboni ambapo wanasiasa na watumishi wakubwa serikalini wamepewa viwanja hivyo kwa kufahamiana na wahusika.
Ukisikia ngano basi ndiyo hiyo hapo juu.Angalia Nguruvi alivyoandika
MMM unaposema ume discredit ''utafiti'' naona wapo wanaoweza kutoa benefit of doubt ku-sooth nafsi zao.
Mimi nasema ni NULL AND VOID.

Tumejifanya mazumbu kuku na kukubali kuzijadili kama zilivyo, hata katika uzumbu kuku wetu wa kujifanya, Mohamed ameshindwa, nasema failed to stand and defend a single line. failure! Mo failed misereably to defend his own research methodology and findings scientifically.

Halafu bado anatumia neno research. Please tumia neno jingine ili researchers wasipate nausea.
Miaka 15 analisha vijana wetu ngano hii! Jamanani jamani ! eh mola.

Hilo la Kawawa linachekesha kweli. Hivi 1982 Kawawa alikuwa VP!
Alichokifanya ni kitu kinaitwa ''sensational news'' kwamba watu washtuke kuwa aliyekuwepo alikuwa VP.

Ni kile kile cha kuonyesha namba 18 Vs 82 huku akibadili maudhui ya ''reseach'' kila uchao.
Mara 18: 82 Muslim vs Christian, mara 18:82 Muslims vs Non Muslims. Ilimradi kuamsha hisia tu.

Ni kile kile cha hotuba ya karne ya Rehani Waikela ambayo nakala yake haipo duniani lakini tunaambiwa alisimama na kutaka kumbaraza Nyerere kwa bakora. Ushabiki ni kitu kibaya sana hasa kwenye intellectual discourse.
Mimi nikamuahidi Nguruvi kama hivi

Nakuahidi kwa uwezo wa Allah nitakuletea alipodefend chapters za uongo wenu.Nitakapokuletea uwe tayari kuchagua tusi la kujitukana mwenyewe.Naona Nguruvi utaalamu kidogo wa statistics unataka kukupa kiburi na kufru.
Jibu la ngano ya Mwanakijiji lipo kwenye paragraph chache alizozinakili Mohammed Said katika kitabu chake kama hivi
Kwenye kitabu cha Developement and religion in Tanzaia cha Bergen uk365 alimnukuu mwalimu Nyerere akisema
" I am a layman but I try to do what I can and will not go against my own church.I want to give the church a better chance here.Tell the bishops that I have established in TANU a department of political education and have put a Lutheran minister in charge;he was not a greater politician. I selected him because of his strong faith"

Sasa hiyo ngano yako Mwanakijiji ya udugunization imeanzaje?.
 
Mdondoaji, kwanza naomba nirejee hoja yako ya ''waswahili;;. Nadhani unakosea kama wengi wanavyokosea kwa kudhani kuwa neo waswahili ni waislam.

Coincidentally watu wanaoongea kiswahili na hakika waliokisambaza ni waswahili (Sahel) ambao wengi wao wametokea kuwa waislam. Ndio maana mswahili hakawii kumwiga afande rire rimekuja ri aresti na wengine nao kusema huyo ni mswahili.

Mimi katika nyuzi hii nimetumia neno ''wamatumbi'',sikumaaanisha wamatumbi bali sisi waafrika.
Mtu aweza sema mnyamwezi akimaanisha Mtanzania. Hiyo ni misemo tu kama tunavyosikia watu wakisema ''aah waswahili bwana, nimemwambia aje saa 3 anakuja saa 6'' hao wanaoongea hivyo wote si waislam.

Ni makosa hayo hayo waislam wanayafanya kwa kudhani kuwa kofia za baraghashia ni Uislam.
Hayo ni mavazi tu na hayana hati miliki wala si alama za dini kama baadhi ya watu waliokosa hoja wanavyodai.

Mama Theresa wa Culcata alikuwa navaa hijab, je alikuwa miwslam? Kuvaa vile alidhihaki uislam?
Haya ni matatizo ya ufahamu tu vinginevyo hilo siyo suala kabisa!

Nikirudi katika nukuu yako, hakika nawe umejikuta katika mtego wa Mohamed.
It's unfortunate Mdondoaji! kwasababu sikudhani unaweza kunasa katika mtego mbovu na dhaifu kama huo.
Sorry. I have to be honest with you

Nashangaa sana unajenga hoja kuwa kuna wakristo ni wengi IFM na PPF.
Vipi kwanini usiangalie kuwa Walimu wengi ni wapi, Mabwana shamba wengi ni wapi, madaktari na wauguzi wengi ni wapi, mavetenari wengi ni wapi n.k.Kwanini mnadhani nafasi ni benki kuu, NSSF, PPF na IFM ni muhimu zaidi ya sehemu nilizozitaja

Ukiangalia shule nyingi za sekondari achilia mbali za msingi za waislam, tatizo lililopo ni ukosefu wa walimu.
Shule ya Al Hassan Mwinyi mwaka 2010/2011 ilikuwa na wanafunzi 250 na walimu wawili.

Hili ndilo tatizo na wala si mkuu wa Faculty IFM. Utapataje mkuu wa faculty kama mtoto hakufaulu huko nyuma?

Mohamed amechota akili za watu kudhani kuwa ukiwa na wakurugenzi 50 katika uwiano wa 0.5 basi matatizo ya waislam yamekwisha. Anawaaminisha watu kuwa ukiwa na mawaziri 20 kati ya 40 basi inflation imeondoka kwa waislam.
Sasa moto umepamba tunakutana na hoja za IFM na PPF

Watu wamefunga macho kabisa kutambua kuwa Kilwa Shule imefungwa kwa wanafunzi kukimbia, jicho lipo kwa Wakurugenzi watatu au wanne IFM.

Huu ni mwendelezo ule ule wa fikra za kuwa Mwanerongo ilikuwa na shule ya kiislam na sasa imerudi nyuma kwasababu EAMWS haikuruhusiwa kujenga chuo kikuu.

Watu wenye fikra hizi za ajabu hawajui kuwa kule kule Mwaneromango sasa hivi wakazi wanafukuzwa na ardhi inaporwa na wawekezaji. Hawana habari kabisa kwasababu jicho lao lipo katika kutafuta ubaya wa wakristo na wala si ubaya wa mfumo wa utawala au madhila wanayopata watu.
Hilo halishughulishi vichwa vyao wao wanashughulika kuandaa data za udanganyifu.

Mohamed daah! kaiharibu jamii ipasavyo. Ni kwa fikra zake kuna mtu hapo nyuma kasema NECTA ni kigango cha kanisa na imeshawahi kuongozwa na Padre. Nimamuuliza Padre aliyeongoza NECTA alikuwa nani na lini, masikini hana jibu.
Sababu kubwa ni kula ngano ya Mo kama ilivyo, haichukui nukta ukimpeleka kwenye kona hana hoja.

Watu wamemeza ngano na data mbichi sasa hivi wanazunguka wakiazima majenereta huko vijijini kuelezea ushahidi wasiojua kuwa wamelaghaiwa. Kasema Mohamed mwenyewe kuhusu majenereta.
Leo tunamuuliza vipi mwenzetu kuhusu utafiti kulikoni ! anasema ni makosa ya kibinadamu.

Bado watu hawajaona tu! Sad

Nguruvi3,

Labda nikuulize swali jengine kwanini kama sote Tanzania ni Sahel na tunajijua sisi ni waswahili kwanini baadhi yetu tuitane majina ya Mdondoaji ni mswahili yule wengine tuitane kwa majina Mdondoaji au Nguruvi ni mswahili but Mdondoaji asiitwe mswahili?

Nimekupa mfano wa taasisi za serikali sio wakurugenzi wawili au watatu bali ni wote ni wakristo na usifikiri nimetoa mfano huo hakuna waislamu walio na safi hawafai kuwa katika nafasi zile hapana bali dhambi ya udini imetawala katika nafasi zenu na hivyo mnaona ni sawa tu waislamu wakandamizwe.

Sasa inapotokea kwenu nyie mnalalama kama vifaranga vichanga huku kiunafiki mkijua nyie mmekuwa mkiyafanya hayo takriban every single day.

Na kwenye maandishi haya mekundu basi mshauri nduguyo Jasusi kuwa yule ndugu yake kama alisoma St. Kanumba basi asilalamike akikosa kazi NSSF maana yule mwenye qualification za juu ndie aliyepata.

Acheni kudharau waislamu mkuu, wasomi wapo wengi sana na wanaongezeka kila siku ondokeni na mfumo huu wa udini utatumaliza shauri zenu.
 
Mdondoaji
Sina definition rasmi ya mswahili. Siku moja nilikuwa na wamalawi kwenye conference na wakatu-refer watanzania wote kama waswahili- sidhani kama walimaanisha sisi ni waislam. Siku nyingine nimemsikia mtu akisema "Obama yule, mbona mswahili tu?" Siku nyingine nilikuwa mtaa wa mkendo pale Musoma. Ni hapo peke yake nilipomsikia mama mmoja akisema waswahili huku akimaanisha waislam. Mara nyingine nimewaskia watu wakimsema padre pekupeku (mzungu) pale morogoro "Yule padre mswahili tu, anaongea kiswahili kama sisi"
Na mara kadhaa mtu asiye muaminifu au asiye timiza ahadi au asiejali muda, wote hao nimeskia wakiitwa waswahili hata kama ni viongozi wa makanisa.

Je kwa hapo nitatoa definition gani ndugu yangu?

Inawezekana kijana wako alichelewa kwenye interview, jamaa wakasema ana mambo ya kiswahili, yeye akajishuku kuwa ni kwa sababu ya uislam wake.

Mkuu,

Nanren kwanza wewe na Nguruvi mnielewe mie sina ugomvi wala chuki yeyote na mtu ila msimamo wangu ni tuwe fair na huo msimamo unatokana na principles zangu za kuamini hii dunia yetu sote awe mwislamu, mkristo, asiye na dini na kadhalika.

Napata tatizo katika jamii yetu ya watanzania tukianza kubaguana wenyewe kwa wenyewe. Ndio kwasababu hiyo nimemuuliza Nguruvi sasa kama sote sisi Sahel (Waswahili) iweje neno mswahili litumike kuwatambua watu fulani hapa Tanzania? Sio hilo tu mtu anaweza kupewa jina la Mswahili likinasibishwa na sifa mbaya je huo sio ubaguzi?

Labda nikupe mfano UK kulikuwa na neno linaitwa Paki likimaanisha wapakistani wote but this word paki was used by white british wakirefer to as a racist word. Serikali ya Uingereza imelipiga marufuku kutumika na ukikamatwa ukilisema neno hilo unaenda jela miezi 6 au kulipa fine. Sasa kwa mtazamo jina Paki halina tofauti na Pakistani na tafsiri ya nje ni Pakistani. Lakini likichambuliwa kwa tafsiri ya ndani Paki means jitu shamba lilitokea pakistani.

Je hili neno Paki lina tofauti gani na Mswahili au lile na kuitwa watu toka Tanganyika kule Zanzibar (Machogo au Watwana)?
 
Back
Top Bottom