Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

haaaaa!.........kumbe mnakasha unaendelea huku!.......wacha niangalie angalie isije ikawa ni ile minakasha ya wakati ule inajirudia....
 
haaaaa!.........kumbe mnakasha unaendelea huku!.......wacha niangalie angalie isije ikawa ni ile minakasha ya wakati ule inajirudia....

Karibu mkuu!
Ni marudio tu. Mengi tuliyouliza kipindi kile yanaulizwa na majibu ya mzee MS yako namna ile ile.
 
haaaaa!.........kumbe mnakasha unaendelea huku!.......wacha niangalie angalie isije ikawa ni ile minakasha ya wakati ule inajirudia....
Ni kweli, tofauti ipo lakini! maana kuna confession!
 
Kuwa na subra basi swali kaulizwa Mohamed Said. Au tayari umeishamjibia.

Sisi hatuna haja ya mazungumzo ya mitaani.
Serikali ina kila kitu chetu.

Tusubiri yote hayo yatakuwa hadhir.
 

Waislam wa fedha ndugu yangu utathubutu kuwachezea?
 
Sisi hatuna haja ya mazungumzo ya mitaani.
Serikali ina kila kitu chetu.

Tusubiri yote hayo yatakuwa hadhir.
Sasa kama ni hivyo, kwanini unaendelea kulalamika kuwa kuna uonevu unaofanywa? Hivi huoni kuwa hujaitendea haki serikali maana haina platform ya kujibu tuhuma hizi unazoeneza mitaani kule usikotaka mazungumzo ya mitaani yafanyike!
 

Sawa lakini hujawahi kumhoji; na leo mzee bado yupo hujawahi kujaribu kutafuta mawazo yake juu ya Nyerere na udini. Ila akija kututangulia sitoshangaa utaanza kutumia maneno mbalimbali kuelezea msimamo wake.



Mimi nimeingia humu kuja kueleza historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika.
Nimeingia humu kurejesha hadhi na heshima ya wazee wangu.

Lakini hili hujajaribu kulifanya na kama umejaribu basi ndugu yangu umeshindwa kwa kiasi kikubwa. Hujathubutu kuelezea historia ya 'kweli ya uhuru wa Tanganyika'. Utafanya hivyo vipi wakati unafanya kile kile unachowatuhumu kuwa Nyerere alikifanya? Unaweza kudai kuwa umejaribu kuelezea 'sehemu' ya historia ya kupigania uhuru na hapo utakuwa umekaribia kwa usahihi sana kuelezea kile unachokifanya lakini kudai umeelezea historia ya 'kweli' la hasha mkuu wangu.


Waulize Waislam.

Tunajua nini maana ya kudhulumiwa.

Tatizo ni kuwa unataka watu waamini kuwa Wakristu wa Tanzania hawajui dhulma vile vile. Unataka watu waamini kuwa Wakristu wa Tanzania wanafurahia maisha ya raha tofauti na Waislamu. Huwezi kuamini kuwa wapo Wakristu ambao hawajapata elimu, wamenyang'anywa ardhi, wamehamishwa kwa nguvu n.k chini ya utawala huu huu ambao nyie mnaulalamikia. Wakristu hawa hata hivyo yawezekana hawaoni kuwa ni ktokana na mfumo Kristu bali wanaona ni matokeo ya mfumo mbovu wa kisiasa uliojengwa kutokana na kutamalaki kwa ufisadi.

Mgogoro wa Ardhi Meru, Mgogoro wa Ardhi Usukumani, au suala la Kodi kule Upareni wakati wa Uhuru liligusa watu ambao miongoni mwao walikuwa ni Wakristu wengi tu. Na hata leo tumeshuhudia maeneo yenye Wakristu wengi - Kyela kwa mfano watu wakijiona wanadhulumiwa. Tumeshuhudia wananchi wa Rukwa huko wakilalamikia ardhi yao kuuzwa kwa wageni, tumeshuhudia Kilombero huko na sehemu nyingine nyingi tu ambapo wananchi - wakiwemo Wakristu wengi tu - wamejikuta wakihisi dhulma chini ya serikali yao lakini hawaioni hiyo kama wamelengwa wao kwa sababu ya Ukristu wao.

Utaona hata kwenye matokeo ya mitihani watoto wa Kikristu wanaofeli katika shule za Kikristu (au zenye majina ya Kikristu) hawaangalii au kudhania kuwa wamefelishwa kwa sababu ni Wakristu. Kuna vituo vya mitihani kama Dar-es-Salaam Christian Seminary ambayo mwaka 2011 ilikuwa na watoto 66 waliofeli na 24 wakiwa na Div 4, mmoja Div 2 na 3 Div 3; lakini huwezi kuwaambia watoto hawa ambao labda ni Wakristu kuwa mfumo wa elimu haujawadhulmu na kuwa wazazi wao hawajui madhara ya mfumo wa ufisadi!

Unavyozungumzia dhulma kwa Waislamu ni kana kwamba Waislamu wanaishi kwenye jamii nje ya jamii ya Watanzania. Kwamba ipo miji au mitaa ya Waislamu ambapo WAkristu hawaishi na hivyo madhara ya utawala yanawalenga Waislamu kwenye miji na mitaa hiyo. Mtaa ambao hauna maji madhara yake ni sawa sawa kwa Wakristu na Waislam wanaoishi katika mtaa huo.

Hakuna lolote ambalo unaweza kudai Waislamu wamepata katika mfumo huu wa utawala wa kifisadi ambao WAkristu hawajapata madhara yake vile vile. Madhara ya mfumo huu yanaathiri Watanzania wote bila kujali dini, rangi, jamii, au mahali. Ndio maana wengine tumeamua kupambana na mfumo huu wa kifisadi badala ya kukumbatia adui hewa wa Mfumo Kristu.

Ndio maana leo Wananchi wa Mtwara ambao walikuwa ni wapenzi wakubwa wa CCM na wengi wao wakiwa ni Waislamu wamefunguka na wanatambua mara moja kuwa adui yao siyo kanisa au Ukristu bali mfumo wa utawala wa Chama ambacho kimekuwa kipenzi kikubwa cha WAislamu. Wameanza kufunguka.
 
NIMEFUATILIA KWA KINA KINACHOJADILIWA KATIKA MJADALA HUU NA NIMEBAINI MOHAMED SAIDI YUKO SAHIHI KWASABABU YEYE ANACHOELEZA NI HISTORIA YA WAISLAM KATIKA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA NA MCHANGO WAO NA SI HIVYO TU MARA BAADA YA UHURU WAISLAM HAWAKUWA NI WENYE KUTHAMINIWA NA WALIDHARAULIWA NA HATIMAYE NYERERE AKAANZA KUTUMIKA KULIPA KANISA NGUVU HUKU AKIWAKANDAMIZA WAISLAM NCHINI TANZANIA REJEA VITABU VIFUATAVYO:-

KANISA KATOLIKI NA SIASA YA TANZANIA BARA Dr J SIVALON

THE CROSS V/S CRESCENT Mbogoni

THE MAKING OF TANGANYIKA Judith Listowell

DEVELPOMENT AND RELIGION IN TANZANIA John Vern Bergen

Soma hivyo vitabu uone nyerere anavyokiri kuwa mtumishi wa kanisa na kuchukua ahadi ya wazi kuwa atalipa kanisa lake nguvu na kuwadhoofisha waislam hivyo ni vitabu vimeandikwa nyerere akiwa hai na amefanya mahojiano na hawa waaandishi nzuri zaidi wote walioandika ni wakristo
 
kassimamari;5495692]NIMEFUATILIA KWA KINA KINACHOJADILIWA KATIKA MJADALA HUU NA NIMEBAINI MOHAMED SAIDI YUKO SAHIHI KWASABABU YEYE ANACHOELEZA NI HISTORIA YA WAISLAM KATIKA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA NA MCHANGO WAO
Mimi nimeingia humu kuja kuelezea historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika.
Hizo sentensi mbili zina maana tofauti sana labda tu kama Mohamed ana kitabu kingine alichotoa kueleze unachokisema
NA SI HIVYO TU MARA BAADA YA UHURU WAISLAM HAWAKUWA NI WENYE KUTHAMINIWA NA WALIDHARAULIWA NA HATIMAYE NYERERE AKAANZA KUTUMIKA KULIPA KANISA NGUVU HUKU AKIWAKANDAMIZA WAISLAM NCHINI TANZANIA REJEA VITABU VIFUATAVYO:-
Hebu tusaidie, kuthamiwa ilitakiwa Nyerere afanye nini?
Nyerere alitumikaje kulipa kanisa nguvu kwa kuwakandamiza waislam?
Hebu tupe undani uliomo katika vitabu hivyo japo kwa ufupi tu ili twende sambasamba usituache nyuma.

Je, ni waislam peke yao waliopigania uhuru wa nchi hii?
Kama wapo wengine, je wao walithaminiwa vipi tofauti na wenzao waislam
 
Kitabu changu sasa kina umri wa miaka15.
Hajaweza yeyote kuja na kitabu kupinga niliyosema mle.

Histori ya wazee wangu imehifadhika.
Hilo ndilo lililokuwa lengo langu kubwa.

Sikuingia humu ili nije nishinde hoja na kwa
Kweli ni lipi la kushindania?

Kitabu kinakwenda toleo la tatu.

Simlazimishi mtu kukubaliana nami.

Khiyari ni yake mwenyewe.
Kuamini au kutoamini.

Muhimu ni kuwa wale niliwapelekea
Ujumbe wako kimya.

PS🙂 Kuna post nimezifuta kwa bahati mbaya na sijui namna ya kuzirejesha mod asaidie au mwanukumbi anielekeze jinsi ya kuzirejesha.
 

Hayo maswali si ya kuuliza leo.
 

Ahsante sana.
Hivyo vitabu mashuhuri humu ukumbini.
 
Sasa kama ni hivyo, kwanini unaendelea kulalamika kuwa kuna uonevu unaofanywa? Hivi huoni kuwa hujaitendea haki serikali maana haina platform ya kujibu tuhuma hizi unazoeneza mitaani kule usikotaka mazungumzo ya mitaani yafanyike!

Neno "kulalamika" inaelekea linapendeza masikioni kwa wengi.
Hebu liunge na ulalamishi.

Utapata maana halisi.

Ukisha psta maana hiyo angalia mantiki na hilo ulokusudia.
 

Yale yale kutoka kwa wale wale!
 

Kwa bahati mbaya vitabu hivyo ninahofu hukusoma, ama umesimuliwa tu, na kama umesoma hukuvielewa kabisa,

Hakuna mstori wowote unaomnukuu Mwalimu Nyerere akikili kuwadhulmu Waislamu,

Kama ipo tuambie ni ukurasa gani wa vitabu hivyo na uuweke hapa kwa faida ya wanajamvi!
 
Neno "kulalamika" inaelekea linapendeza masikioni kwa wengi.
Hebu liunge na ulalamishi.Utapata maana halisi.
Ukisha psta maana hiyo angalia mantiki na hilo ulokusudia.
Ni kawaida yako kukimbia hoja kwa kuangalia visingizio kadha wa kadha. Wamasai wana msemo wao ''ni ngumu kumesa''

Mohamed,hivi kuna uwezekano wa mwanafunzi kutofanya mtihani halafu adhulumiwe na NECTA?
Kitendo cha padre kuchaguliwa kuongoza wizara ya elimu kilikuwa na tatizo gani katika maadili ya kiutawala
 

Kwakweli binafsi nimejitahidi sana kutafiti kile kinachoitwa dhulma kwa waislamu SIJAKIONA na hata waislamu wenyewe hawathibitishi madai hayo, wanabaki kusema TUNADHULUMIWA tu, mara kuna mfumo kristu!
 

unajua kuna vitu inatubidi kuvipuuzia tu maana ukisoma habari za MS utaumiza kichwa! Hivi yeye ameathirika vipi na mfumo kristu?
 
Waislam wa fedha ndugu yangu utathubutu kuwachezea?

Fedha inakujaje hapa. Unataka kusema wanahonga wizarani au inakuwaje? Issue si ubora wa Elimu tu ndugu yangu?
Watu wengi humu tumesoma na waislam kutoka kwenye familia zenye uwezo wa kawaida tu kama za watanzania wengi kwenye shule hizihizi za serikali lakini walifanikiwa kufauli kwa sababu ya kujituma sana kwenye masomo.
Bado una hamu ya kufungua ule uzi ili uelezee wizara ya elimu inavyowakandamiza waislam?
Mimi kama wanajamvi wengine wengi tuna hamu kubwa ya kujua ujanja wanaoufanya NECTA/Wizara ya Elimu kuwadhulumu waislam.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…