Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Kwa kushindwa kwako KUJIBU HII mimi nachukulia kwanza umekubali kuwa kweli nakala iliyokuwa na story ya Mohammed Said ya jarida la Africa Events ilichomwa moto mwaka 1988.Itakuwa vile vile umekubali kuwa takwimu zilizo kwenye kitabu cha Mohammed Said zilizotokana na utafiti wa WARSHA na kutaja muslims v/s christians na muslims v/s non muslims si kasoro zinazopelekea kupuuza ukweli mwingi uliokuwa umejificha kabla uliomo kwenye historia yake.Mohamed hili jambo ni muhimu sana kwasababu wewe umeshasema ustadh Ilunga anaongea kwa niaba ya waislam. Tumekuuliza waislam wapi?
Tumekuuliza kama unakubali ile video kwavile imetolewa na mtu ''aliyetumwa'' na waislam umesema hilo huna ujuzi. Kuhusu suala la KISASI umesema waulizwe Maalumaa.
Ninapopata taabu ni kuwa wewe kiongozi wa waislam na mtu mwenye weledi wa kiwango kikubwa uliklinganisha na wafuasi wako kama huwezi kujua kuwa kauli ile ilikuwa nzuri au mbaya hadi maalumaa, sasa vipi yule mwenzangu mimi ambaye kwanza hajasoma na pili ni shabiki tu wa dini ataichukuliaje?
Je, Ilunga aliona madhara ya kaluli ile ambayo wewe unaiita utata hadi ipatiwe utaalam, je, ni muafaka kuitoa kwa mtu yoyote bila kujali athari zake? Mohamed hapo huoni kuna irresponsibility na ignorant ya kiwango cha juu sana.
Tena hiyo umeipaka rangi na kuiita ilm! Real!
Ajabu itakuja pale huko mbele mtakapozusha tena masuala haya ambayo sasa yamewashinda kuyatetea.InshaAllah tutakuwa macho kuwakumbusha.
Sasa tuje kwenye suala ambalo hapo juu umesema ni muhimu sana.
Mohammed ni mwandishi hodari wa historia na sote tunamthamini kwa hilo lakini mwenyewe anajijuwa kuwa hawezi kuchukua jukumu la maulamaa.Wewe kwa ujinga wako unataka kumuonesha kwa hadhira ya JF kuwa yeye ndiye kila kitu kwa upande wetu waislamu,hivyo kukwepa kuchukua jukumu la kujibu mambo makubwa ya ki-ilm basi ndio kila ukweli alioandika ndio umeporomoka.
Tatizo ukubwa wa elimu ya kiislamu mnaupima kwa kutumia vitabu vyenu na bado hamjaingia makraba za kiislamu mkajionea wenyewe na pia hamtaki kuamini ukweli wa historia hata iliyoandikwa na wenzenu.
Kwa mtazamo wako akina mimi ambaye ni mwalimu wa madrsa eti sijasoma.Jee umesahau ya kuwa Ulaya imesomeshwa na waislamu kama mimi kwa karne kadhaa kabla kutugeuka na kutufanyia uadui?.
Angalia Mwenzako Mwanakijiji alivyopumbaa na huu mjadala mpaka kumbukumbu hana kabisa na hajui kabisa anachokisema
Mwanakijiji pamoja na kwamba Qur'an hata chembe haijui lakini bado anajifanya ulamaa na msemaji wao kwamba Ilunga kapotosha Qur'an.Kwa vipi?.Yaani wakati mwingine nachoka kabisa; yaani katika umri wako huo hujui uovu mbele ya macho yako? Kwamba Ilunga kapotosha Qurani tena vibaya sana unasema unahitaji maulamaa wakuambie? Huu ni uvivu gani wa fikra? Ndio vijana wetu unawaambia hivi kuwa Shehe akisema kitu asihoji kiakili kama hakina mantiq?
Kama ulivyo Nguruvi,Mwanakijiji hatorudi kujibu namna Ilunga alivyopotosha Qur'an.
Kwa hapa nimeona tena jinsi Mohammed alivyowashinda kwa hekima katika huu mjadala.