Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Mohamed Said,
..huu mnakasha ni endelevu, na ndiyo maana umefika kurasa 500+ na maelfu ya wasomaji.
..zaidi umeandika mambo muhimu sana kiasi kwamba inawalazimu wasomaji wako wakujue wewe mwandishi ni mtu wa aina gani.
..sasa katika hili zoezi la kutaka kukujua mwandishi wetu, kukujua zaidi ya jina lako, ndiyo unaona yanaibuka maswali mengine kama hii hoja ya video ya Ustaadh Ilunga.
..Kuna mahali umesema unamheshimu Ustaadh Ilunga, na kwamba ktk "darsa" lake huwezi kufungua kinywa chako. Sasa ndiyo na sisi tukauliza: hivi Ustaadh Ilunga anapomsherehesha Mwamwindi na mambo aliyomfanyia Kleruu, wewe una mtizamo gani? Je, akitoa "darsa" hilo bado utapiga goti ukiwa kimya hata kuguna ushindwe???
cc: Nguruvi3, Ritz
Joka Kuu,
Nikipita Mwanza hufika kwenye darsa zake kusoma
tafsir ya Qur'an.
Mimi namjua Sheikh Ilunga kwa darsa hili.