Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Hebu nipe vipengele vya kisheria nilivyouliza hapo mwanzo je kisheria Vatican nchi??? Naona kati yangu mie na nyie msomi anaweza kujitambua mwenywe.
 
Joka,Mimi na wewe tunakwenda vyema.Nakuomba ukizungumza na mimi tuache habari ya Sheikh Ilunga.Tujikite katika yale ambayo mimi nina ujuzinayo na wewe wayajua.
Mohamed, tuliangalie hili la Ilunga kidogo ili tuzidi kwenda vyema.

Hebu tuangalie hii habari kwa ufupi halafu tujiulize kama unasababu za kutojua au kutokuwa na ujuzi na yale ya Ilunga Huyu ndiye ameaminiwa na ''waislam'' kuwazindua kuhusu Mfumokristo.
Katika maandiko yako mengi sana yakiwemo ya hoja hapa JF, mara nyingi umeelezea moja kwa moja jinsi mfumokristo unavyofanya kazi.

Na hakika maana halisi ya kazi zako ni kueleza kuhusu mfumo huo na jinsi waislam wanavyoonewa na kufanywa raia daraja la pili(nina nukuu ya maneno hayo) kutokana na mfumokrsito.

Sasa iweje usiwe na ujuzi na mfumokristo ''waislam'' waliomtuma Sheikh Ilunga kuueleza ambao wewe umekuwa kinara wake katika kuuonyesha kwa maneno na takwimu?

Tutawezaje kutenganisha mfumokristo anaoongelea Ilunga na ule unaojadiliana nasi hapa kila siku?
 
Naona unawalisha wenzako ngano za nazi...ha haa ha.Akukuuliza kuhusu bei ya hotuba ya Nyerere pale TBC?Akukuuliza wewe ni mtoto wa ngapi wa Julius Kambarage?
 
Mdondoaji;6013872] Na unaposema hili sio issue tunarudi kwenye maswali ya Former president Aboud Jumbe kuwa ikiwa Tanzania haina dini then why tuna uhusiano wa kibalozi na Vatican?
Mdondoaji, naomba msaada kidogo. Hii kauli ya Jumbe sijaielewa vizuri.
1. Je, Jumbe alimaanisha nchi ikiwa na uhusiano na Vatican tayari inaondoa maana ya ''..Haina dini''
au
2. Tanzania kuwa na uhusiano na Vatican tayari ni kielelezo cha kuwa na dini nadhani hapa ni Ukristo.

Ahsante
 

Nguruvi,
Kama ni Sheikh Ilunga na Mfumokristo hilo naweza tukazungumza sana.

Nilichosema sina ujuzi ni suala la kisasi kama alivyoeleza Sheikh Ilunga.

Kwa kweli mimi niliandika kuhusu tatizo hili zaidi ya miaka 25 iliyopita
lakini neno nililotumia mimi lilikuwa ''Christian Lobby.''

Ahlan Wasaalan.
Tunaweza kuanza Insha Allah.

Nakusubiri.
 
Mdondoaji,
Acha uwongo. Mimi si Katoliki lakini najua fika kwamba kanisa halipewi kodi na serikali ya Tanzania kila mwaka. Makanisa hayalipi kodi kote duniani kwa mujibu wa kanuni ya separation of church and state. Sasa lini kodi yako imelipwa kwa kanisa Katoliki? Ndivyo mnavyoeneza chuki miongoni mwa waislamu kwa kuwadanganya kuwa serikali inalipa makanisa. Shame!
 

Kwa hiyo Mwanakijiji akitoa points zinakuwa pumba. Na wewe unapotoa pumba zinakuwa points. Now I get it!
 
He who praises rain has been rained on...
 
Mohamed Said,

Naomba kukuuliza hivi ulitumia muda gani kukamilisha kazi ya kuandika kitabu chako "Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes"
 
Kwani pengo hana haki ya kulalamika?Ila wenye haki ya kulalamika ni mashehe tu? Leo mnaona wenye haki ya kuchinja nnchi ni waislama kwa sababu zipi? Kila raia wa nchi hii ana haki ya kulalamika katika jambo ambalo kwake anaona hana maslahi nalo kama waislam wanavyolalamikia, mou ni haki yao na pengo ni haki yake kulalamika.
 

Kama kweli wewe ni Muislamu, unamuamini Mungu yupi? na Mtume gani? na tufanye kazi zipi? ziko wapi? wewe ni mwajiri nikuletee Waislamu 5 tu wanaotafuta kazi tena wana shahada za Chuo kikuu utawapa kazi?
 
Mohamed Said,

Naomba kukuuliza hivi ulitumia muda gani kukamilisha kazi ya kuandika kitabu chako "Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes"

Ritz,

Takriban miaka 10 au zaidi maana kulikuwa na writing and rewriting.

Kazi kubwa ilochelewesha kitabu ni publishers walikuwa wanaogopa
yale niliyoandika.

Ndipo kikenda kuchapwa Uingereza.
 
Ritz,Takriban miaka 10 au zaidi maana kulikuwa na writing and rewriting.Kazi kubwa ilochelewesha kitabu ni publishers walikuwa wanaogopayale niliyoandika.Ndipo kikenda kuchapwa Uingereza.
Mohamed Said,Umefanya kazi kubwa sana kuna mtu yeyote aliyekusaidia kwenye Faharasa.
 
Mkuu nguruvi,Wewe ni kiboko kwa engo unazomweka mzee wetu ni balaa.Hapa haonewi mtu ni hoja kwa hoja, tatizo la mzee wetu asifikili anaojadiliana nao wote ni wale wa ndiyo mzee anakosea sana. we ni noma.

Mgashi,
Mimi ndiye Maalim hapa.

Mimi ndiye ninaetoa darsa.
Nasomesha.

Nguruvi anauliza maswali baada ya kunisoma.
Usisahau hilo.

Hapa nimetoa kazi nilizoandika kwa mkono wangu
zilizochapwa kwenye majarida kadhaa ndani na nje
ya Tanzania hata hesabu yake siijui.

Tulia kwenye jamvi utanijua Insha Allah.
 
Ritz,

Takriban miaka 10 au zaidi maana kulikuwa na writing and rewriting.

Kazi kubwa ilochelewesha kitabu ni publishers walikuwa wanaogopa
yale niliyoandika.

Ndipo kikenda kuchapwa Uingereza.

Kwanini wanaogopa kuchapicha vitabu makini huku wanaruhusu kuchapisha vitabu vyenye picha za kihuni na maadili ovu? Mohamed Said,
Ktk makala yako nimeona umemtaja Shekh Salim Hamis aliechaguliwa ktk Mkutano wa Chuo kikuu kuratibu mabadiliko ktk Baraza la kudhibiti Waislamu Tanzania (Bakwata)! namkumbuka sana Shekh Salim na Katibu wake Mohamed aliekuwa mjumbe wa Press Club! jee, wako hai? pia nakuomba utupe kisa cha Marhum Kighoma Ali Malima kuhama CCM mwaka 1995!
 

Sawa, lakini hayo ni maoni ya aina moja tu; mtu mwingine anaweza (kwa kuangalia facts zile zile) kufikia hitimisho tofauti na kumwasha msomaji aamue mwenyewe. Sasa kujibu hoja zako nyekundu wacha na miye nikupatie toka Wikipedia huko huko:


Lakini tunaweza kwenda mbali zaidi kutoka huko huko Wikipedia:


Kumbe utaona kuwa 'territory' ya Holy See ambayo yenyewe ndio sovereign ni Vatican City State. Lakini hata bila ya kuwa na territory imewahi kuendelea kuwa sovereign!
Na unaposema hili sio issue tunarudi kwenye maswali ya Former president Aboud Jumbe kuwa ikiwa Tanzania haina dini then why tuna uhusiano wa kibalozi na Vatican?

Swali la jumbe kwa namna limekosewa; kama ana maanisha kuwa ni kwanini tuna Uhusiano wa Kibalozi na Holy See jibu liko wazi - tuna mahusiano na serikali ya Kipapa ambaye ni mkuu wa Vatican City. Serikali hii ndiyo Holy See.

Kuna bwana/bibi ameniuliza swali ati nchi gani za kiislamu ambazo hazina uhusiano na Vatican labda nimtajie Saudi Arabia, Afghanistan, Brunei, Somalia, Oman. Pia kuna zisizo za kiislamu pia hazina mfano China, North Korea je una swali jengine?

Jibu lako ni partially true; kuna mahusiano ya karibu kati ya Holy See na nchi hizo zote ukiondoa kuweka mahusiano rasmi ya kibalozi. Hili si jambo geni; nchi kutokuwa na mahusiano ya kibalozi haina maana haiitambui ile nchi nyingine kuwa ni nchi au kuwa hakuna mahusiano mengine ya karibu chini kidogo ya yale ya Ubalozi. Marekani haina balozi Cuba wala Cuba haina balozi Marekani lakini nchi hizo hazina mahusiano? Well..

Angalia na hapa:


Utaona ni nchi tano tu duniani ambazo hazina KABISA mahusiano yoyote (katika level yoyote) na Holy See - hizi ni Bhutan (sidhani kama wana ubalozi Tanzania au sisi kwao), Maldives, North Korea, China na nchi ambazo hazijatambulika Rasmi (kama Somaliland n.k)

Sasa, nchi zaidi ya 180 zina mahusiano ya kibalozi na Tanzania nii mojawapo. Hawa wote wametambua na wanatambua nafasi ya Holy See licha ya maswali ambayo unayo na ambayo labda wengine walishauliza. Nchi hizi zote hazijakosea. Tanzania haijakosea. Na nchi hizi zote haina maana zimebadilisha dini zao (Saudi Arabia bado ni ya Kiislamu, Malaysia bado ni ya Waislamu, Falme za Kiarabu bado ni nchi ya Kiislamu, Bahrain bado ni nchi ya Kiislamu, Misri bado ni nchi ya Waislamu wengi, Kuwait bado ni nchi ya Kiislamu hujasikia wameanza kusali Rozali!; Pakistan bado ni nchi ya Waislamu wengi hujasikia watu wanaandamana ati Pakistan sasa imegeuzwa nchi ya Wakatoliki!

Kuendelea na hoja yako hii jinsi ilivyo kunaonesha ni kutokutaka kujua au kukubali ukweli hata kama unakutumbulia macho. Nchi 180 (za Kikristu, Kiislamu, Sekula, Orthodox n.k) zimetambua Holy See kama entity ambayo ni nzuri kuwa nayo na mahusiano ya Kibalozi. Nchi 80 kati ya hizo zina mabalozi wa kudumu Vatican! Vatican yenyewe ina mabalozi zaidi ya 100 kwenye nchi hizo. Sasa, kusema ati kwa vile tuna Uhusiano wa kibalozi na Vatican (Holy See) basi Tanzania imekuwa nchi ya Kikristu ni kutokujua, kutokupenda kujua na kuwa mgumu kujua.

Sasa unaweza usipende hili kwa sababu Holy See inawakilisha Kanisa Katoliki (serikali ya Kanisa Katoliki chini ya Papa) na hili linakukwaza lakini wewe kukukwaza haina maana halipo. Mwenyewe umeona mabadiliko ya Papa tu dunia nzima inapeleka waandishi zaidi ya 5000 kufuatilia; it is not about the church my friend, it is about history of Western Civilization. Nchi hizi za Magharibi nyingi zimechota katika elimu, tamaduni n.k kutoka kwa Kanisa Katoliki. Utambue kuwa Kanisa Katoliki limekuwa ni sehemu ya utawala wa nchi za Magharibi kwa karibu miaka 1000.

Sasa una haki ya kuchukia uwepo wa Ubalozi wa Holy See na kile inachosimamia; unaweza kabisa kuona huu ni upendeleo lakini hili peke yake halibadili ukweli kuwa uongo. Kuendelea kubishania hili ni kujaribu kupigana na ukuta wa historia. Na wakismama watu kama wewe kuzungumza kwa mamlaka ya kisomi ati hawatambui Holy See au sovereignty ya Vatican City watatuabisha sisi wengine.
 

Wewe endelea kutoa darasa lakini darasa lako linachambuliwa na kuoneshwa kuwa ndani yake kumejaa ulaghai wa maneno, upotoshaji wa historia na jaribio dhaifu la kufuta mchango wa kipekee uliotukuka na usio na mfano wa Baba wa Taifa katika harakati za Uhuru. Darasa lako Maalim, linatolewa darasa na watu wanatusoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…