Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Kadogoo,
Naona bado mnaendeleza uwongo wa kumchafua Nyerere. Hakuna mahali hata siku moja ambako Nyerere alisema hakuna fikra sahihi zaidi yake. I challenge you to bring here that statement coming from Nyerere. Nyerere ameacha rekodi inayotukuka. Na hata mkijaribu kumchafua kiasi gani itakuwa kama mtu anayekimbiza kivuli chake.
 
Mwanakijiji,
Huhitaji kwenda mbali kuona matunda ya kazi aliyofanya Mwalimu. Nchini Kenya, wakati wa harakati za kupigania uhuru, kulikuwepo mshikamano mkubwa baina ya makabila kiasi kwamba Jaramogi alikubali kumwachia Kenyatta uongozi wa nchi. Lakini sote tunajua kilichotokea. Kenyatta baada ya uhuru akageuka kuwa tribal chief na kupendelea kabila lake. Nakumbuka mwaka 1973 ukipiga simu kwenye ofisi ya serikali Nairobi ama wanakujibu kwa Kikikuyu, aterere, au kama husemi Kikikuyu ni Kiingereza. Matokeo yake sote tunayaona leo. Kenya hata uchaguzi lazima ufanyike kwa tribal alliances. Na ukabila utawatafuna mpaka siku ya kiyama.
 

Mzee Mwanakijiji,

Ndugu yangu wala mie sijapata shaka yeyote kuhusu kitabu cha Mohamed Said yeye kaelezea upande wake wa wazee wake shaka ya nini.

Shaka ambayo ipo ni historia yetu ya kutafuta uhuru haipo kwa makusudi kuna watu wameondolewa kabisa.

Nadhani unamjua mwanahistoria maarufu ambaye kaandika vitabu vingi ya historia ya afrika Basil Risbridger Davidson.

Mwaka 1985 Nyerere alipokuwa anamtunukia digrii ya heshima Basil Davidson, alitoa changamoto kwa chuo kikuu cha Dar es Salaam kuandika historia ya kweli ya Tanzania.

Haya ndiyo matunda yake unayoyaona hapa jamvini tunaminyana.
 

Jasusi,

Kabla ya Nyerere ajazaliwa na kuingia kwenye siasa Tanganyika hakujawahi kutokea vita vya kikabila wala vya kidini hii hulka ya Watanganyika.
 

Kina furahisha na jinsi mnavyokimbia ukweli.

Muislamu akifanya jambo lazima mseme "KARUBUNIWA" "KADANGANYWA"
"KASHAWISHIWA"

Yote hii kulazimisha hoja. Kwasababu mnajua mkikiri waislamu wenzenu wamefanya hivi madai yenu yatakuwa INVALID.
 
Mzee Mwanakijiji,

Ndugu yangu wala mie sijapata shaka yeyote kuhusu kitabu cha Mohamed Said yeye kaelezea upande wake wa wazee wake shaka ya nini.

Shaka ambayo ipo ni historia yetu ya kutafuta uhuru haipo kwa makusudi kuna watu wameondolewa kabisa.

Usiingie kwenye mtego wa Mohammed SAid wa kujaza hyperbole kwenye hoja zake. NI watu gani wameondolewa kwenye historia? huwezi kuondoa watu kwenye historia! Kuna msemo wa Kiingereza kuwa "even God can not change the past"...
 
Whaat? inaonekana huijui historia ya nchi yako!! tumetwangana sana....

Ndiyo vizuri sasa unipe darsa lini Waislam na Wakirsto walitwangana na Nyerere ndiyo akaja kuzimisha kutwangana.

Au kutwangana kwako unakotaka kutuelezea wafugaji na wakulima. Kama ni ivyo Nyerere kashindwa kuwatuliza watu wa mkoa wake.
 
Jasusi,

Kabla ya Nyerere ajazaliwa na kuingia kwenye siasa Tanganyika hakujawahi kutokea vita vya kikabila wala vya kidini hii hulka ya Watanganyika.
Unajaribu kusema nini? Ubaguzi wa kikabila ulikuwepo. Nenda Musoma miaka ya 50-60 uelezwe. Kule tuna makabila zaidi ya 27 katika mkoa mmoja tu. Hata Kenya kabla ya uhuru hakukuwepo vita vya kikabila. Lakini tazama leo.
 
Usiingie kwenye mtego wa Mohammed SAid wa kujaza hyperbole kwenye hoja zake. NI watu gani wameondolewa kwenye historia? huwezi kuondoa watu kwenye historia! Kuna msemo wa Kiingereza kuwa "even God can not change the past"...

Mwanakijiji,
Unaongea na Ritz habari ya Mohamed Said ya nini fikra zangu nasoma vitu naelewa wala sina haja ya kutumia fikra za mtu. Hivi historia ya Kivukoni haijawasahu wapigania uhuru?
 
Unajaribu kusema nini? Ubaguzi wa kikabila ulikuwepo. Nenda Musoma miaka ya 50-60 uelezwe. Kule tuna makabila zaidi ya 27 katika mkoa mmoja tu. Hata Kenya kabla ya uhuru hakukuwepo vita vya kikabila. Lakini tazama leo.

Siyo ulikuwepo upo mpaka sasa ndiyo mkoa ambao hawezi kuendelea kwa kuendekeza ukabila unataka kunimbia Nyerere kaweza kuondoa ukabila Mara.
 
Siyo ulikuwepo upo mpaka sasa ndiyo mkoa ambao hawezi kuendelea kwa kuendekeza ukabila unataka kunimbia Nyerere kaweza kuondoa ukabila Mara.

Nikumbushe kwa sasa makabila yepi na yepi yanapigana Mkoa wa Mara
 
Mwanakijiji,
Unaongea na Ritz habari ya Mohamed Said ya nini fikra zangu nasoma vitu naelewa wala sina haja ya kutumia fikra za mtu. Hivi historia ya Kivukoni haijawasahu wapigania uhuru?

Ritz,
Nimerudi ulingoni na darsa la vuguvugu la wafanyakazi.

Nimebandika kisa cha Abdu Sykes na Waingereza 1947/48.
Naona kimyaaaaaaa!

Naendelea kusubiri.
 
Duh! hapa umepiga mfupa. Umenikumbusha kitu kimoja. Wasukuma na Wanyamwezi wangekuwa na jicho la ''sisi'' wanaweza kumchagua Rais wa nchii katika sanduku la kura.
Hiyo tu inawapa ''haki'' ya kuuliza wao vipi katika mgawanyo unaosemwa.

1.Swali ambalo nimekuwa nauliza na sipati jibu ni kuwa hivi gavana wa BoT akiwa mtu wa imani fulani, dini hiyo inafaidika na kitu gani?

2. Hivi kipi ni muhimu, serikali kutazama maeneo yenye matatizo na kuyatafutia ufumbuzi au serikali kugawa vyeo kwa watu 200.

3. Kama sasa ni wakati wa kuwa na nafasi sawa(siyo kulingana na sifa), I mean kugawana wizara(naona aibu hata kuandika nikiwa chumbani mwenyewe), vipi likiibuka kundi na kusema sasa ni wakati wale waliofanikiwa katika biashara ima wazuiwe kuendeleza biashara au watozwe kodi zaidi ili kutoa fursa kwa jamii zingine kuinuka! hilo linawezekana?

Na mwisho,wanajamvi naomba msaada kidogo wa fikra. Hivi wakati mzee Mwinyi akiwa Rais nani alikuwa katibu mkuu wa NECTA!
 
Ritz,
Nimerudi ulingoni na darsa la vuguvugu la wafanyakazi.

Nimebandika kisa cha Abdu Sykes na Waingereza 1947/48.
Naona kimyaaaaaaa!

Naendelea kusubiri.

Mohamed Said,

Karibu tena jamvini endelea kutoa darsa.
 
Ile inayoitwa socratic method uliyosema ndio utatumia kujibia ina upungufu mkubwa kwani inauona ulimwengu kama kitu kidogo kilichoanza kuwepo miaka 2013 tu iliyopita.
Mimi nimekupa sura pana ya uumbwaji wa Ulimwengu kuanzia Adam (a.s)kama Mtume mpakaYesu ( a.s) na Muhammad (s.a.w) na kwamba wote ni waislamu.Itawezekanaje mitumue waliotumwa na Mungu mmoja wawe na dini tofauti?.

Nje ya Qurani hakuna ushahidi wowote kuwa Yesu au mtu mwingine yeyote kabla ya ujio wa Uislamu alijitambua, alijua au alikuwa Muislamu).
Maelezo ya ndani ya Qur'an ndiyo ya msingi kuliko nje yake.Hata wewe hupaswi kuweka mbele porojo zako bila kuwa na maandiko.
Ikiwa ni hivyo basi hakupaswi kuwepo na ukristu
 


Insha allah Darsa hili tunalithamini sana..
 
Ami,Hebu rudi usome post yangu kwa umakini na ukiwa umetuliza akili.Mohamed anatakiwa afahamu kuwa population ni ''variable value'' kwamba si lazima asilimia 67 ya mwaka 1967 ibaki kama ilivyo.Kuna uwezekano iliongezeka na kufikia 80 au kupungua na kufikia 40 kwahiyo alitakiwa kwanza apate the most recent stats.Kufanya extrapolation ya mwaka 1967 ni sawa na mtu kupanga mipango ya maendeleo ya nchi kwa kutumia stats za 1967. Huku ni kupotosha vijana.Hapa nilitoa mfano ili kusisitiza hoja yangu kuwa Mohamed anapaswa atumie data za siku za karibuni kwakuelewa kuwa population ni kitu dyanamic as opposed to static.

Malalamiko yako kuhusu vijana wa Mohammed yamekuwa mengi

....
.... hamna lolote la maana unalosema hapa

Habari za asilimia na jumla unajidanganya unapodhani sisi hatuelewi.Hivi vitu ukiviona vinavyochambuliwa kwenye vitabu vyetu mwenyewe utashangaa.

Swali linakuja kwanini kuwepo na ongezeko au punguzo distribution population.
Kuna sababu nyingi sana zikiwemo za kijamii na kiuchumi.

-Kuna uwezekano mwaka 1967 waislam wa Dar hawakupenda kwenda mikoani na mwaka 1978 wakaenda huko...
Ikiwa hakuna sensa nyengine kuthibitisha hilo na wewe huna taarifa madhubuti juu ya kuhama waislamu basi uwezekano unaouzungumzia haukuwepo.

Uwezekano ,uwezekano,uwezekano........
Uwezekano ambao ni ukweli ni kuwa kila mwaka watu hutoka mikoani na kuhamia Dar es salaam hasa mikoa yenye umaskini zaidi inayokaliwa na waislamu wengi kama vile Lindi,Mtwara,Kigoma,Tabora,Tanga na kwengineko.
Hivyo population distribution ya Dar es salaam uwezekano wa kuwapunguzika mpaka ukajitokeza kwenye uchaguzi wa wanafunzi wa kuingia kidato cha 1 kwa 83/17 ni udanganyifu na dhulma za wazi wazi za mfumo kristo.
Ikiwa unapinga hili hupaswi kuja na maneno ya uwezekano bali utafiti wa kiwango chochote au sensa rasmi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…