Mohamed Said,,
i can see them,they are crying..
lakini bakora bado,mwaga facts na darsa hapa.,
tambua wanaothamin uwepo wako hapa ni wengi sana,tafadhwali tunakusihi utoe elimu hii,Allah atakulipa kheir insha allah..
The Big Show,
Unajua mimi nawaonea sana huruma hawa ndugu zangu.
Kwa hakika wazee wao hawana historia ambayo wanaweza nao
wakaiandika na ikasomeka kama historia katika kudai uhuru wa
Tanganyika.
Na hili si kosa kwani hawakuwapo Dar es Salaam ambako ndipo
palikuwa chimbuko ya yote haya nielezayo hapa jamvini.
Bahati mbaya wao kitu hiki kimejenga chuki na hasad dhidi ya
historia hii.
Kila ukiwasoma ni jeuri, kejeli, ghadhabu matusi nk.
Mimi nilikuwa nikikaa darasani UDSM na walimu wanasomesha historia
ya uhuru.
Nikiwaambia hiyo haiwezi kuwa historia ya TANU.
Mwalimu atashtuka na ataniuliza historia ya TANU ni ipi?
Hapo namfungulia habari za wazee wangu.
Namwambia Nyerere alikuja kufahamika khasa kwa watu baada ya safari
ya UNO...
Mimi nikawa nasema lile ninalolijua na kwa hakika wakawa wanatatizika sana
na majina kama ya Schneider Abdillah Plantan, Mashado Ramadhani Plantan,
Idd Faiz Mafongo, Idd Tosiri, Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir
nk.
Na nikiwaambia hawa ndiyo TANU yenyewe...
Ndipo Mwamerika mmoja akanambia nikiwa Amerika kuwa ikiwa wewe Mohamed
una uwezo wa kutunga mambo kwa kiasi cha jinsi nilivyosoma katika kitabu chako
basi wewe nakutia katika mawanda ya akina Irving Wallace.
Na huyu ni prof. wa historia ya Afrika.