NAKUSHUKURU SWEKE KWA HOJA ZAKO ZENYE TIJA.
LAKINI NINA UHAKIKA TUPO WOTE KWENYE MWANZO WA MJADALA HADI SASA,MAJIBU YA HOJA ZAKO YAPO HUKO NYUMA,TENA YAMEFAFANULIWA VEMA TUH,JARIBU KUPERUZI NA KUONA UNDANI WA SUALA HILO.,KWANI SISI TUNA SHIDA NA NYERERE?HAPA TUPO KATIKA KUZUNGUMZA YALE YALIYOFANYWA KWA MAKUSUDI NA KUPOTOSHWA,NA SIO KWAMBA TUNA CHUKI BINAFSI NA NYERERE LA HASHA,
HOJA ZETU ZISIHUZUNISHWE NA CHUKI BINAFSI.
Maneno yako hapo kwenye blue yanakinzana na ya Mohamed Said. Mzee wetu tumetoka naye mbali sana tangu zile nyuzi za makala zake za miaka 50 ya uhuru lakini hatupati ufafanuzi na uthibitisho kwenye mambo mengi anayomtuhumu Nyerere badala yake anatupa mabandiko ya vitabu na papers zake.
Mimi kwenye suala la elimu kwa kweli ningependa kupata ufafanuzi zaidi maana mtu akikunyima elimu kwa makusudi ni kwamba amekufanyia dhulma kubwa sana.
Mohamed Said ameendika tangia nchi hii inapata uhuru mpaka pale Kighoma Malima aliteuliwa kuwa waziri wa elimu, wizara hiyo ilikuwa inaongozwa na wakristu tu. Anasema ilifikia mpaka wakati padre/mchunguji aliongoza wizara hiyo. Teuzi hizo za wakristu zilikuwa na lengo la kuwakandamiza waislam kielimu na kuwapendelea wakristu na ndiyo maana (kwa mtazamo wa MS) Kighoma Malima alipoingia wizarani akakutana na madudu mengi.
Kuna siku nimemuuliza hivi hawa mawaziri wote waislam(Juma Kapuya,Maghembe, Shukuru Kawambwa) waliotumikia hiyo wizara ya elimu baada ya Malima hawayaoni hayo madudu tena wakati huu vitu vipo wazi zaidi? Hakunipa jibu la maana. Yeye Mohamedi said anajua dhulma hiyo kushinda waziri muislam anayetumikia wizara hiyo.
Ni huyuhuyu Shukuru Kawambwa aliyeacha kazi zake na kwenda kupokea maandamano yenu(wanafunzi waislam) Kidongo chekundu kuhusiana na ile issue ya wanafunzi wa ndanda. Na aliwaahidi atalishughulikia lile tatizo. Lakini nadhani ni naibu waziri wa elimu wakati huo Kassim Majaliwa(Muislam) ndiye aliyeivalia njuga issue ile na mwisho wake wote tunajua kilichokuja julikana.
Ni huyuhuyu Shukuru Kawambwa aliyetoa ufafanuzi mzuri tu kwenye vyombo vya habari kuhusu majibu ya Islamic Knowledge yaliyokosewa.
Sasa inashindikana vipi kwa huyu muislam kuona dhulma wanayofanyiwa waislam kwenye wizara yake? Anatumikia Kanisa?
Si mnaswali naye misikitini huyu?
Jamani tuwe wakweli. Leo hii ukifeliswa ni rahisi sana kujua umeonewa au la kwa sababu mitihani huwa inabaki pale wizarani kwa muda kuruhusu watu ku appeal na hivyo mitihani yao kuangaliwa upya. Mkuu muulize mohamed said anajua nini kuhusu jinsi mtihani invyosahihiswa mpaka kufikia kutolewa matokeo.
Binafsi kama angeniletea cases za wanafunzi kadhaa za waislam walioonewa na baada ya kuappeal wakapata matokeo mazuri zaidi, ningemuelewa. Au aniletee cases kadhaa za wanafunzi wa kiislam waliofaulu lakini hawakuchaguliwa kuendelea na masomo nitamuelewa.
Lakini asituambie tuamini tu.
By
Mohamed Said
Sweke.
Kwanini tubishane?
Ikiwa wewe unaona hakuna dhulma na wengine ipo
kuna haja gani tuzunguke katika hilo?
Kila mtu abaki na msimamo wake.
Tuiachie historia pindi mwaka itatuamua.