Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


AMI,


Soma gazeti la Annur uone dhulma dhidi ya Waislamu na Serikali mpaka sasa haina uso wa kukanusha madai haya mazito ya Waislamu! nchi hii sijui inaelekea wapi jamani? ANNUUR 1065
 
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, kweli hukujua kuwa at some stage katika mjadala, itabidi akina Gombesugu wajitokeze? Kama alivyowahi kusema Geofrey Chaucer katika kitabu chake "The Parson's Tale" mwaka 1390...
"And ofte tyme swich cursynge wrongfully retorneth agayn to hym that curseth, as a bryd that retorneth agayn to his owene nest"
au kwa Kiingereza cha sasa zaidi ya miaka 700 baadaye...
"Curses are like young chicken: they always come home to roost."
Kulijitokeza hatari ya jahazi kuzama na hivyo kulihitajika watu wawili tu waongezeke ili namba iwe tatu,(a threesome!) Natangaza kwamba namba imetimia lakini je jahazi litaokoka?

Haya, wengine tumesema ya kwetu na sasa tuangalie book reviewers wengine waliovisoma vitabu vya Mohamed Said nao wanasemaje...Hapa Wickama katuletea vipande vya maoni ya reviewer moja kuhusiana na kitabu cha Mohamed Said alichokisoma kama hivi;

Je na huyu book reviewer naye ataambiwa aandike kitabu cha kwake?
 


Ridiculous,Very Very Ridiculous..
Yale yale ya paka wa kwenye kumbi za Ma - Bar wapenda vya bwerere,anachokifanya hapa huyu Mzee mfia dini ni kudokoa dokoa hoja ambazo yeye anaziamin anaweza kuzisimamia kukanusha yale yoote yaliyotafitiwa na kusemwa na Moh Said,tumuulize sasa,aliyonayo ni hayo tuh??mengine yaliyoandikwa na kwa rejea mbali mbali alizopewa hajaziona??
Ikumbukwe huyu ni miongoni mwa wale wanaoutumia UKRISTO Katika maandiko yake mengi,tena kwa njia ya indirect way ili kumpinga Moh Said,wenye kuling'amua hilo tumeling'amua..
Huyu ni miongoni mwa wale waliokosa busara na kumkejeli Moh Said et ya kwamba anaoga uchi na watoto wadogo,huku akijinasibisha kuwa ni Great thinker na mwandishi aliekamilika wa kuandika makala au kitabu na watu wenye akili zao wakakaa chini na kumsoma,ana maana huyu??
Na ndio kwa maana vijana wa mjini tuna msemo unaosema ukimuona Mzee kakosa busara kias na KUFIKIA HATUA YA KUVALIA SURUALI CHINI YA KIUNO DAWA YAKE KAMA UNAMUONA HATAKI KUIPANDISHA MARA BAADA YA KUMSIHI SANA NI KUIPANDISHA SURUALI ILE KWA NGUVU.,ILI KUMLINDIA HESHIMA YAKE..
A clown like Mwanakijiji cant play the part of a wise man like Moh Said,but A Wise man like Moh Said can play the part of A clown like Mwanakijiji..
Tunataka watuthibitishie uchochez wa Moh Said uko wapi??
Uchochez wake umepatikana baada ya kuyaeleza yale yaliyofichikana??
 


Whatever..
Aandike asiandike ni juu yake,lakini akiandika akafanikiwa kuishawish jamii juu ya ukweli kuhusu historia ya wale waliofichwa kwa makusudi atakuwa kafanya jambo la maana sana..
alichokifanya huyo book reviwer wako ni kama vile kutwanga maji kwenye kinu,kusema ya kwamba Moh Said kaitazama historia ya Tanganyika from Sykes family point of view ni ukanjanja wake tuh,kwani Moh Said kalificha hilo??
Moh Said kalieleza hilo wazi wazi ya kwamba yeye kaeleza historia ya wazee wake anaowafaham na alioishi nao na mchango wao katika harakati za ukombozi wa taifa hili ambazo kwa makusudi kabisa zilifichwa..
na sisi tumezipima na kuzikubali,ni maona yenu na mnaweza pia kuwa sahihi mkisema ya kwamba sisi tumekubali kwa nia ya kupigana jihad n,k n,k.,mnaweza pia kuwa sahihi,si ni mawazo na fikra zenu zinawatuma kuamini hivyo??sasa kwa nini tuwapinge,tujaalie kama Moh Said angeamua kukaa kimya na asiseme yale anayoyajua,wengine tungeyajulia wapi??
wacha tuh ukweli usemwe na watu waupime,msilazimishe watu waupinge,nyinyi andiken kile mnachokifaham na Moh Said aandike kile anachokifaham mwisho wa siku hadhira itaangalia na kuamua kuchagua upande..
 
Ridiculous,Very Very Ridiculous...
Tunataka watuthibitishie uchochez wa Moh Said uko wapi??
Uchochez wake umepatikana baada ya kuyaeleza yale yaliyofichikana??
Kwa hiyo wewe THE BIG SHOW, unakubaliana na Mohamed Said kuwa serikali ya CCM inaendeshwa kwa MfumoKristo na kuwa Mkuu wa serikali hiyo ambaye ni Jakaya Mrisho Kikwete si Muislaam safi. Katika msingi huo huo viongozi wa BAKWATA nao si Waislaam safi kwa sababu wanaendesha chombo hicho Kikafiri na katika msingi huo huo Waislaam waliopo CCM si wasafi kwa sababu wanashirikiana na makafiri.

Unajua THE BIG SHOW, mwaka 1958 walikuwepo wazee wenu waliokuwa na mawazo kama hayo hayo...waliiangalia TANU kwa misingi hiyo hiyo ya udini ila tofauti na Mohamed Said walichukua hatua, waliiacha TANU na kuunda chama cha Kiislaam (AMNUT) ili waweze kuachana kabisa na makafiri. Hata hivyo Waislaam wasio safi hawakuwaunga mkono wenzao, walibaki ndani ya TANU wakishirikiana na makafiri.

Bahati mbaya tofauti hii kati ya Waislaam safi na wasio safi bado inaendelea hadi sasa na leo Waislaam wasio safi wanaongoza serikali wakishirikiana na makafiri. Waislaam wasafi wanaunga mkono madai ya Mohamed Said kwa sababu usafi wa Muislaam na mahusiano yake na kafiri, kwa lugha ya hesabu ni indirectly proportional...unavyozidi kuwa Muislaam safi ndivyo unavyotakiwa kukaa mbali zaidi na makafiri.

Hivyo ndivyo ingetakiwa iwe lakini ajabu ni kwamba sivyo ilivyo! Mwaka 2010 Waislaam safi walihamasisha Waislaam wote bila kujali wako kundi gani kuichagua CCM. Walikubali kumchagua kiongozi yule yule ambaye kwa miaka mitano nyuma, alisimamia uendeshaji wa mfumo wa kikafiri, MfumoKristo! Na hivi leo vyombo vyote vya dola vinaendelea kuwa mikononi mwa CCM na serikali yake, vikiendelea kuwakandamiza Waislaam!

Namalizia kwa kumnukuu mwandishi Mtanzania;
 

Mag3
wewe bado hujaelewa,wale wazee walikuwa hawapiganii kuja kuisimamisha dola ya kiislam ndani ya ardhi ya tanzania,ndio kwa maana wakampa nafas julius ambae si muislam kusimama kama kiongoz na aje kuwa kiunganish kwa watanzania wote..
wangekua wanataka kuismamisha dola ya kiislam,au wangekuwa wana nia ya kupigana jihadi wangetafuta mwakilishi mwingine ambae ni muislam asimamie hoja zao..
kitu kinachozungumzwa hapa ni kugeukwa kwa baadhi ya watu na historia zao kufichwa kwa makusudi,ndipo hoja inakuja walipuuzwa kwa nini??kwa kuwa wao ni waislam??mbona hoja kuu tokea harakati za uhuru wa mtanganyika ilikuwa ni kumwondoa mkoloini??sasa kwa nini wengine wakuzwe na wengine wapuuzwe?
kwanin baadh ya upande katika nchi hii upewe nafas kama first class citizens na upande mwingine upewe kama second class citizens?najua unazijua hizo pande mbili nazozizungmzia hapa..
kwa hiyo narudi kwenye mantiq kuu,haya yanayotokea sasa na tuyaonayo yalitokea na yanatokea kwa sababu ambazo zilikuwapo na zipo tokea zamani,tatizo nyinyi hamtaki kukubali ili tuangalie suluhisho la kuganga yajayo..!
tutafikaje??oooh Moh Said mchochezii mchocheziii,,anaoga na watotooo,anaoga na watotoo,ndio nini sasa??
watu hawataacha kusema ukweli wanaofaham eti kwa kuhofia wataonekana kama ni mujahidina na watu wa madrasa au wapenda ubwabwa na wachochezi,ukweli utasemwa tuh..
Moh Said hana interests na siasa hapa,ila hawezi kuacha siasa hizi hizi ziingilie na kuathiri maisha ya wale wanaonekana kufuata mila za uislam,hiyo ndiyo hoja kuu,na iko wazi kabisa bila haya bila soni...
 




NIKIICHUKUA NUKUU YAKO HII..
Namalizia kwa kumnukuu mwandishi Mtanzania;

By Godfrey Mwakikagile
What should not be ignored or glossed over is the fact that there were people in every tribe or ethnic group, in every district, every province and every religion including African traditional religions, who fought for the rights of Africans long before TANU was formed and after it was formed. They all wanted to end colonial rule.

And they all struggled together, not as Moslems or as Christians, not as Chagas, Sukumas, Ngonis, Zaramos, Kingas, Hehes, Nyakyusas, Makndes, Matengos, Hayas, Nyasas, Digos, Pares, Bondeis, Ziguas, Sambaas, Nyaturus, Manyemas, Nyamwezis, Yaos, Lugurus, or as Gogos; they fought together as Tanganyikans who loved their country and united in their quest for freedom and independence from colonial rule.

No-one deserves more credit than others. They all deserve credit – equal credit. And they were all nationalists and patriots, not religious bigots or tribalists

Hicho ndicho hasa hata moh said anachokisimamia,kaamua nayy kuandika ili uone watu walivokajitolea kuipigania nchi hii na kujitoa kwa hali na mali ili mkoloni aondoke katika nchi hii,ila sasa cha kushangaza wakaja kufutwa bila kuenziwa kama walivoenziwa wengine eti tuh kwa kuwa wao wanaonekana kama wanalandana na uislam na waislam..
yanaposemwa hayo,wewe na majeshi yako mnakuja kusema kuwa ni uzushi na uchochezi..
 

Ukweli ni kwamba hakuna wanaonekana kama first class citizens na wale second. hizo nazo ni hisia tu na tunda la kusoma maandiko hayo. kuna jambo gani linaonesha kuwa hao wazee wanapata second class citizenship treatment? Is it constitutional? Where then? In fact these unfounded allegations are what is sinister in essence. bad treatment if any, is never to be judged or concluded by Moh himself. what he (Moh) calls the 'forgoten history of tz' kama kweli anatuletea historia au kilichosahaulika katika historia asiwe conclusive hasa na yeye mwenyewe hiyo inaonesha wazi kwamba Moh kwa kufanya hivyo at the very least is biased or religiously inclined towards his own faith while he expects a secular debate. ndiposa tunapouliza hii historia ya bongo - has it now been lowered to such standards au? Yaani mtu atuletee account ya wazee wake wanavyoiona au harakati zao akaziita historia! There is nothing special about what he is telling us here and after all these years its no news and the only perculiarity is that it cuts cross-grain with our history as we know it (on religious grounds of course). He's clearly shown a biased approach and thus continues to prove unfit to give us a fair account of events : if he will write a historical account and there are such accounts [like Howard Zinn's ~ A People's History of the United States] he has to be agnostic about what he is writing at the very least. Plus, the fact that there is already a significant amount of criticism to the subject matter itself from many here at the forum about his account of events, is very alarming and suggests mallice and were this a formal review he would face an unprecedented and insurmountable barage of serious professional sanctions from the accademic society in this country and beyond for failure to either denounce, dispell or concede on the criticism.
 

we are a 2.3bn strong over 1/3 of the world population and for 2k years christianity has been around.

**
Christianity is the predominant religion in-Europe,Russia,-the Americas, the-Philippines,-East Timor,Southern Africa,-Central Africa,-East Africa-and Oceania.There are also large Christian communities in other parts of the world, such asCentral Asia-and the-Middle East, where Christianity is the second-largest religion after Islam

source : wikipedia
 


Hahaha inabidi ukajifune mantiq; yote uliyoandika yanatoka kwenye hisia. Hayana msingi katika ukweli. Kama unaona tatizo ni serikali ipinge na kipinge chama kilichounda serikali hiyo...
 

Inaonekana hujamsoma Mohammed Said au unasoma kwa kurukaruka kama panzi kwenye mahindi yaliyokauka!
 

The Big Show,
Nani wakumwambia Jonathon Glassman kuandika kitabu?

Yeye ana vitabu na paper kadhaa kuhusu historia ya Afrika.

Glassman kila mwanafunzi wake anaeandika kuhusu Islam
and Politics pale Northwestern University moja ya kitabu
anachompa katika reading list ni kitabu changu.

Mmoja wa wanafunzi hao ni James Brenan ambae sasa
ni bingwa wa historia ya Tanganyika.
Hivi sasa anaandika kitabu cha Oscar Kambona.

Ndugu yetu hajui mengi kuhusu mimi kafunikwa na chuki.

Mimi na Glassman tumekaa ukumbi mmoja na tukamjadili
marehemu Abdulwahid Sykes ndani ya chuo anachosomesha
tena kwa mwaliko wa chuo chake.

Tukisikilizwa.

Mwisho wengi walikubaliana na mimi kuwa Abdu Sykes alikuwa
mzalendo ambae hakustahili kusahauliwa.
 

The Big Show,
Nina mengi lakini sikiza hii.

Siku kabla ya mimi kuzungumza pale University of Ohio prof mmoja
akanialika chakula cha mchana pamoja na bingwa mwingine wa historia
ya Afrika.

Waamerika wana msemo: There is no free lunch in America.
Msemo huu unaifahamu siku nyingi.

Naam.

Katikati ya chakula akanichomekea akasema: Unajua Mohamed
hapa Amerika hawezi kuja mtu na akasifia Uislam hicho ni kitu
hakikubaliki kabisa...mtu atapata shida sana.

Sikubadili msimamo wangu.
Kesho yake nikazungumza kama nilivyozoea kuzungumza.

Kidole machoni...
Yapo mengi.
 
Mwisho wengi walikubaliana na mimi kuwa Abdu Sykes alikuwa
mzalendo.
Jamani mnakasha kitu kizuri.
Leo Moddy kaamka kwa namna tofauti kabisa.
Kwanza amekubali kuwa Nyerere alijulikana TAA hata kabla ya kuonana na Abdul.
Sasa anakubali kuwa Abdul ni Mzalendo. Yaani kamweka Abdul katika nafasi yake halisi na si ile ya kumsingizia.

Thank you Mo. This is a big milestone.
 
Hahaha inabidi ukajifune mantiq; yote uliyoandika yanatoka kwenye hisia. Hayana msingi katika ukweli. Kama unaona tatizo ni serikali ipinge na kipinge chama kilichounda serikali hiyo...

Hivi kujua wanaokula vizuri keki ya taifa ni Wakirsto ni hisia tu kweli damu nzito...

Angalia "Ratio" ya Waislam na Wakirsto katika idara za serikali zote wizara mashirika ya umma toka kwa mkoloni mpaka leo wamejaa Wakirsto wengi Waislam wachache waliopo huko wanaonekana kama wanafanyiwa hisani tu.

Wewe fikra zako siku zote dhidi Waislam na mtazamo wako ni kuwa hakuna jambo baya lolote ambalo wameishafanyiwa Waislam na serikali dhulma kwako huwa wanafanyiwa Chadema tu pamoja na Maaskofu, mpaka ukafikia wakati ukatoa ushauri kwa Pengo atoe tamko dhidi ya serikali.

Nakuombea dua sana Allah hakupe umri mrefu na muda uandike kitabu cha kumpinga Mohamed Said kama ulivyosema kuwa ni kazi rahisi kuandika kitabu cha kupinga tatizo muda hauna.
 

Kwa hiyo tatizo lenu ni kuenziwa kwa wazee wenu? Tukimaliza kuwaenzi wazee wenu matatizo yenu yatakuwa yameisha? Ugomvi wenu na mfumokristo utakuwa umeisha? Mbona hamkusema hivyo mapema?
 
Kwa hiyo tatizo lenu ni kuenziwa kwa wazee wenu? Tukimaliza kuwaenzi wazee wenu matatizo yenu yatakuwa yameisha? Ugomvi wenu na mfumokristo utakuwa umeisha? Mbona hamkusema hivyo mapema?

Dogo hilo?
 
Ritz, hayo unayoyasema ni makosa na hakika hakutakuwa na suluhu ya kudumu kwa matatizo hayo kama mtazamo utabaki kama huo.

Huwezi kuniambia kuwa maofisi kuna wakristo wengi ukasahau kuwa vijijini kuna wananchi wengi wanamenyeka sawia.
Sijui kule kijijini Kibuyi karibu na Kinesi ukivuka kutoka Musoma wananchi wana afadhali gani.

Nilifika kule na sidhani kama kulikuwa na waislam zaidi ya kaya 10 katika kaya 300 siku hizo.
Ukiangalia hali za maisha ya watu ni mbaya sana pengine afadhali na kwingine.

Pili, unapoangalia maofisini unaangalia kundi dogo sana. Kwanini udhani kuwa keki ya taifa ipo katika wizara au mashirika 50 usifikirie maeneo mengine? Nimewahi kukuliza vipi mbona hatusikii idadi ya walimu na mabwana shamba, je hao hawafaidi keki ya taifa.

Ni kwa mtazamo kama huo usitegemee kuona watu wakiliangalia tatizo kutoka Magoroto, Kilwa, Mpanda au kule kwa Wamang'ati kwasababu wanadhani kuwa wakurugenzi 20 ni bora sana kuliko jamii ya watu 6,000,000 au zaidi inayomenyeka.

Ningeelewa kama mngeongelea kuwa kwanini kuna idadi kubwa ya mabwana shamba au walimu au madaktari kama siyo wauguzi n.k. Jicho lenu lipo katika ukurugenzi ambao sidhani kama una nafasi zaidi ya 100 nchini.

Kwa maana hiyo mnadhani matatizo ya waislam yataisha automatic kwa kuwa na wakurugenzi na si kuangalia tatizo na kiini chake.

Huko nyuma nimewahi kukuambia kuwa kuna shirika linatafuta Zoologist mtanzania.
Kama yupo naomba tuwasiliane naye haraka hasa akiwa mwislam ili kuhakikisha keki ya taifa inagawana vema.
Hadi leo hakuna aliyejitokeza.Nadhani ujiulize kwanza kwanini hakuna zoologist halafu ndipo ufikirie wakurugenzi.

Nimewahi kumwambia Mohamed alete majina ya Lawyers, Engineers, Doktors, Prodessor n.k.ambao wamefanyiwa hila tu.
Hakuna aliyeleta, lakini bado watu wapo pale pale kwa wakurugenzi.

Tatizo si wakurugenzi, tatizo ni namna gani wanapatikana.
Huwezi kupata wakurugenzi kutoka Kilwa ambako shule imefungwa na huko kuna asilimia 99 ya waislam.
Nadhani kuna umuhimu wa kutafuta taa ya fanusi na kuiwasha mchana ili isiaidane na jua kuangazia watu!!!

Lakini pia lazima watu waangalie mambo kwa upana wake. Hivi Wamang'ati na Wairaq pamoja na wamasai nao watasemeaje kuhusu keki ya taifa?

Tukiendelea na utaratibu huu basi ipo siku wasukuma na wanyamwezi nao watahoji keki ya taifa vipi? Maana wenyewe tu kwa idadi wanahaki ya kudai wakurugenzi na hata mawaziri. Si ndio uwezo wetu wa kufikiri ulipo!

Kitu wanachosahau watu ni kuwa wafanyabiashara wengi waliofanikiwa kwahakika ni jamii ya waislam tangu enzi.
Sijui yule jamaa yangu wa Mtimbira au kule Nyangao naye asemeje kuhusu keki ya taifa.

Keki ya taifa ni Richmond, Radar, Meremeta na dola laki moja na nusu ikwa siku bila malipo za Dowans.
Keki ya taifa ipo Dodoma pale mtu anapolipwa kwa kukaa kwenye kiti achilia mbali mshahara.
Keki ya taifa ni pesa za halamshauri zinazojenga vyumba viwili vya madarasa kwa thamani ya shule kumi.

Labda sielewi maana ya keki ya taifa lakini kama unakula na kusaza, kama unafadhili timu ya mpira huku mwingine akitafuta aspirin ya kupunguza maumivu ya njaa hilo halihusiani na keki ya taifa.

Na je sasa ni wakati watu washikwe mashati ili wasifanye biashara zao kuleta usawa na kugawana keki ya taifa.

Watu wasitafute visingizio, watafute ukweli na wakabiliane nao.Ukweli usikwepwe ueleze na kama ikibidi msaada uombwe lakini ukweli ubaki kuwa ukweli. Tatizo si wakurugenzi, narudia tatizo ni namna gani unamtengeneza mkurugenzi.

Manchester United wana timu hadi za watoto wa miaka 6 hadi 7. Hawa ndio wanaandaa 'wakurugenzi''

Kama kuna mgao wa keki, vipi mgao wa keki ya nafasi za waislam kusoma kwa msaada mbona haufuati utaratibu wa kugawana keki katika jamii hiyo hiyo inayodai keki ya taifa haigawiwi sawa sawa?

Ritz si unafahamu Afircan Muslim Agency, Islamic bank n.k wanatoa nafasi, je hujui kuna ugomvi wa kugawana''keki''

Wale waliotumwa Turkey na kwingineko kutafuta keki wangapi wamerudi na vipande na kugawia wenzao. Please please!

Kuna mahali sielewi naomba msaada, keki ya taifa maana yake nini?
 
Leo kwa mara ya mwanzo nacheka kikwetu kwi...kwi...kwiiiii...
Sasa mbona Nyerere alijifanya mzalendo zaidi kuliko Abdul Sykes!
Mfumokristo unawafanya wakristo ni wazalendo zaidi kuliko waislamu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…