Wewe na mwalimu wako ndo mnaoangalia historia ya Tanganyika kwa jicho la Udini
Leo hamuamini baada ya miaka kumi na tano watu wanakuja kufumbuliwa macho kitabu kinageuka Ngano,ukweli unajulikana sasa kwamba:
-Si kweli kwamba mnaowaita wazee wenu walisahaulika kwenye historia
-Jengo la TANU kuna watu walifisadi
-leo utafiti mufilisi wa WARSHA umejulikana kuwa ni kiini macho tu ulitaka kujenga chuki katika jamii.
-tunajua kwamba kuna tiketi ilitolewa na Kanisa ili Mwalimu aende UN
-Tumejua kwamba Mwalimu hakuandikiwa hotuba kama mwalimu wenu alivyotaka kutuaminisha
-tunajua kuwa si kweli kwamba Mwalimu alianza Siasa alipofika Dar,ila alianza muda mrefu tu huko nyuma
-leo tunajua kwamba Mwalimu ndio aliyeleta changamoto mpya kwenye TAA na Siasa za Tanganyika wakati ule na kuibadilisha toka Chama Cha Starehe mpaka chama cha Siasa hata mnaowaita wazee wenu hili walikiri.
-tunajua kwamba hakuwabagua watu kwa Dini zao
-uongo kuhusu NECTA na SENSA,EAMWAS(kama sijakosea)...nk nk nk nk nk nk
One moment.....
-tumejua pia kwanza Mfumo Kristo ni kitu cha kufikirika tu kwasababu hata nyinyi hamjui mfumo Kristo ni nini
Yapo mengi nitarudi baadae kuongeza...
Wait....
Usisahau kwamba mwalimu wako alitaka kumdhalilisha mwalimu eti alienda sokoni hana hata senti na akapewa mia tano njiani na Mzee Mshume Kiyate na ikumbukwe kuwa kule Butiama baada ya mwalimu kuacha kazi alikuwa akilipwa Sh 600 na Kasisi Art Willie wa Maryknoll kabla ya kurudi Dar?Mwalimu wako anasema kipindi kile sh500 unajenga nyumba ya vyumba sita Kariakoo leo mnasema mwalimu alikosa senti mfukoni?(think... think...think!!)
Kwa kweli shukrani kubwa ziende kwa hawa;
Yericko Nyerere Nguruvi3 Mzee Mwanakijiji Mag3 sweke 34 Jasusi Ngongo Nyambala Son of Alaska Wimana WC,Wickama,Gwelihenzi JokaKuu na wengine wengi wa aina yao nimewasoma nimefaidika sana
Hata wewe,big show,boko boko,kadogoo,mdokoaji,ami na wengine wa aina yako hamjapuuzwa saaana mmekuwa na mchango pia tumewasoma....
Nitarudi!
Rapheri,
Hakika umeandika kwa hamaki na ukiandika kwa hamaki unapoteza mengi.
Nimeweka hapa katika siasa za wafanyakazi mambo yaliyojitokeza katika mgomo wa
makuli wa bandari ya Dar es Salaam 1947 na 1948.
Nimeeleza jinsi Abdu Sykes alivyoshiriki kama katibu wa Dockworkers Union na yote
yaliyotokea hadi kufika mapambano na mabomu kupigwa 1950 na chama cha makuli
kupigwa marufuku nana serikali ya kikoloni na baadhi ya makuli kufungwa.
Hii nililieta jamvini kwa makusudi maalum ili umuone Abdu anaingia katika
uongozi wa TAA 1950 kama katibu akiwa na turufu gani mkononi.
Ikiwa utakumbuka utafahamu kuwa uongozi wa wazee ulipinduliwa kwa juhudi za Hamza
Mwapachu, Abdu Sykes na Schneider Abdilllah Plantan na Abdu pamoja na Dk. Kyaruzi
wakachukua uongozi wa TAA Dk. Kyaruzi akiwa rais.
Uongozi huu ndiyo ulioandika ile memorandum ya Constitutional Development Committee
chini ya TAA Political Subcommittee waraka ambao uliwasilishwa kwa Gavana Edward
Francis Twining na huu waraka ukajadiliwa kwenye mkutano wa kuasisi TANU 1954 na ndiyo
uliotengeneza hotuba ya Nyerere aliyosoma UNO February 1955.
Hii kwa mukhtahsari ndiyo historia ya hotuba hiyo ya Nyerere ambayo aliisoma UNO 1955
lakini inaelekea wenzangu kuna kitu kinakuchomeni nyoyo zenu.
Hampendi historia iwe hivyo mnataka ibadilike iwe nyingine kabisa.
Si kitu.
Waliotangulia wao walifanya ujanja mmoja.
Historia ya hotuba hii hawakuigusa kabisa kwa hiyo watu walikuwa hawajui chanzo chake.
Kiasi ilisaidia maana hapakuwa na mabishano.
Sasa turudi nyuma kidogo.
Hata ilipofika 1953 katika ule uchaguzi wa 17 April kati ya Nyerere na Abdu Sykes ''track record''
ya Abdu katika TAA na katika siasa za Dar es Salaam ilikuwa ikifahamika na wengi.
Hakuna mtu aliyekuwa anamjua Nyerere ukiwatoa labda hao wenzake wa Makerere.
Kwa hakika Nyerere hakuwa na historia yoyote kuwa aliwahi kuwatia misukosuko wakoloni.
Hii ndiyo sababu katika uchaguzi ule Nyerere alishinda kwa kura chache.
Hili nalo linawachoma baadhi ya ndugu zangu.
Historia hii hawaipendi wangetaka iwe vinginevyo.
Waliotutangulia katika kuandika historia walikuwa watu ''makini.''
Uchaguzi huu haukutajwa kabisa wala jina la Abdu halikupewa uzito wowote.
Waandishi wale walikuwa wanasema Nyerere kachukua uongozi wa TAA 1953 hawataji
kauchukua kutoka mikononi kwa nani.
Mimi ndiye niliyekuja kuweka mambo sawa kwa kumrejesha Abdu Sykes katika historia
ya TANU.
Ndiyo maana unaona kadi ya TANU namba 1 Julius Nyerere, No. 2 Ally Sykes na No. 3
Abdu Sykes.
Idd Faiz aliyeratibu na kukusanya fedha za safari ya Nyerere UNO kadi yake No. 25.
Hii haikuja hivi hivi tu.
Haya hayakuja bure.
Yote hayo yana historia yake.
Rapheri,
Umeleta suala la dhulma alofanya Kleist Sykes kwa nyumba ya African Association.
Mimi ningependa kujua nini khasa alifanya.
Mimi nitatosheka na maelezo wala usitafute ushahidi kwani mie si mtu wa ubishi kauli
yako itanitosha.
Mengine nimeyaacha maana naona si muhimu sana kwangu kuyasemea.